Wednesday, December 24, 2014

MERRY CHRISTMAS WADAU....

Nachukua nafasi hii kuwatakia sikukuu njema ya Christmas. Let us celebrate responsibly!

Nimekuwa kimya kidogo sababu ya majukumu fulani, ila yote ni kukusanya nguvu ili kuleta mabadiliko kwenye blog yetu pendwa ili mwaka ujao tuanze kuwa more serious.

Katika siku hii ya leo, wewe mdau nakuombea furaha, amani, utulivu na usherehekeaji mwema.

Nawapenda sana!

LAURA PETTIE
BLOGGER!

Thursday, December 18, 2014

UREMBO NA LAURA:... KUONDOA MAKUNYANZI USONI KWA TANGO NA NYANYA.


Tumeshukuru Mungu!

Kwa mara nyingine tena  tunakutana hapa kusoma makala hii ya UREMBO na Laura. Ni jambo la kipekee kwa kweli. Mwaka umekuwa mgumu sana huu!

Haya siku ya leo nakuletea tiba ya kuondoa makunyanzi usoni. Kuna vijana, ni vijana tu wala uzee haupo karibu leo wala kesho lakini wana mikuno usoni Ashakum si matusi utasema ngozi  ya goti! 
kuna makunyanzi ya paji la uso, ya pembeni ya macho, chini ya macho, kwenye mistari ya tabasamu na hata kidevuni.

Makunyanzi, kuna umri unafika hayaepukiki, ndio vile umri umeenda. Ulaya uko wanafanya mpaka upasuaji wa kunyoosha ngozi. Ila kwako wewe kijana tu hapana!....narudia hapana huna haki ya kuwa na makunyanzi kabisaaaaa!!

Makunyanzi yanaletwa na mambo mengi mno. Seli zilizochoka usoni na hazijaondolewa, Mwili hauna maji ya kutosha, lishe yako ni duni, una stress, na kuna makunyanzi mengine wanasema ni ya kigenetic tu au namna unavyoukunja uso wako… lakini hii haimaanishi usipambane nayo. Mwenzangu uso mchovu mwisho ukooo mjini kila mtu softi tachi hahahahaa! sasa wewe wa wapi hapa mjini?

Tunaishi mara moja katika maisha haya ya duniani, kwanini usijipende tu, ukajihudumia na ukajifurahia kujiona ukipendeza, ukiwa na ngozi ya kuvutia tena kwa kutumia mambo ambayo hayana gharama kabisa. 

Wakati mwingine tunakosa umaridadi na mvuto si kwa kuwa hatuna pesa za kumudu gharama za mahitaji ila hatujipendi au tunaendekeza uvivu tu wa kuandaa hiki na kile ili kuuleta umaridadi. na wakati mwingine nyuso zinakosa mvuto kwa kuwa tunatumia vipodozi visivyo sahihi vyenye kemikali.

NJIA ZA KUONDOA MAKUNYANZI USONI

Zipo njia nyingi sana. Kuha mafuta, krimu, vidonge, upasuaji na kadhalika. Ila mimi nitakupa njia moja ya kiasili ya kuondoa makunyanzi.
MAHITAJI….
1. TANGO

2. NYANYA


JINSI YA KUFANYA….

1. Osha yango lako, kata kipande likiwa na ganda lake. Usimenye!

2. Hicho kipande kitwange kwenye vile vinu vidogo ya jikoni au saga

3. Osha nyanya yako na ukate nusu , yale maji maji ya ndani ya nyanya yakamulie kwenye Tango ulilosaga AU wakati unatwanga tango au kusaga tupia kipande cha nyanya, kidogo tu

4. Osha uso na kausha kwa taulo safi…nasisitiza sana kutumia vitu visafi kukausha uso. Maana kuna wakati rashes zako zinatokana na taulo tu unalotumia. Labda limepigwa sana vumbi hapo unapolining’iniza au hujalifua siku mbili tatu. Taulo la uso ni kitu cha muhimu sana kufuliwa mara kwa mara jamani.
Ukishaosha. Paka mchanganyiko wako kuzunguka uso mzima

5. Kaa kwa nusu saa hadi saa nzima. Ukipata sehemu yenye upepo itakauka haraka sana


6. Ikishakauka, wakati wa kuondoa. Chovya vidole kwenye maji na usugue ule mkauko polepole. Nasisitiza polepole jamani…. Hasa sehemu zile zenye mikunjo.

7. osha uso wako na maji safi, na sabuni unayotumia kisha kausha uso na uuache upigwe na upepo kidogo kabla hujapaka chochote

Fanya hivi kadiri unavyoweza iwe kila siku, iwe mara  mbili au tatu kwa wiki. Ni wewe tu na juhudi zako ila lazima makunyanzi yataondoka ama kupungua saaaaana. Utapata ngozi f’lani ng’aavu maana nyanya inang’arisha uso.


TUKUTANE TENA PANAPO MAJAALIWA….

Thursday, December 4, 2014

UREMBO NA LAURA:.... BIDHAA NA BEI ZAKE NA NAMNA YA KUVIPATA



Nikiwa sina kipodozi chochote usoni.... hapa ni baada ya 
kufanya facial treatment yangu mwenyewe nyumbani.

Watu wengi wamekuwa wakiuliza wapi watapata hiki na kile katika zile bidhaa za asili ninazohimiza kutumia katika makala za urembo na Laura. Leo nakuwekea hapa baadhi ya vitu, bei zake na namna ya kuvipata.

Nimekuwa nikisisitiza sana matumizi ya vitu asilia kwa kuwa kwanza havina madhara kabisaaa! labda uwe na allergy na kitu, vinginevyo sijawahi kuwa disappointed.  

Pili vinapotibu tatizo hutibu taratibu ila kwa ufasaha na  matokeo ya matibabu yako hudumu kwa muda mrefu. Gharama zake ni nafuu sana  na utaweza kuzimudu  hata kipato kikiyumba ati! Lol!

Hivi kwanini usijivunie rangi yako, kwanini usiiboreshe rangi yako tu pasipo kuibadili?... kwanini usitafute muonekano wako wa kipekee!... hizi kemikali tunazo hangaika nazo mwisho wa siku tunapata chunusi za ajabu ajabu na kuungua uso zinapokukataa halafu unaanza kuhangaika tena kutatua tatizo kwa kemikali zaidi...Pheeew! Haya tusikilizane mwenzangu!

TUANZE NA BAADHI YA VITU VYA  FACIAL TREATMENT

1. CHUMVI BODY SCRUB



Hii ni scrub yenye mchanganyiko wa chumvi na manjano…. Ni nzuri sana, nakuhakikishia ubora wake kwa vile ninaitumia pia. Ni laini na unapomaliza kuitumia unasikia kabisa mwili unabaki na hali ya ulaini wa kuvutia na unapoitumia kila mara kuna mng’ao fulani unaupata. Namaanisha unatakata sio kuchubuka!

Kuna wakati uso unakuwa na weusi ambao sio wa asili, weusi uliofifia au kufubaa, au weupe uliochujuka. Chumvi Body Scrub  inakuondolea hali ya kufubaa. Ni uitumie tu kila baada ya siku mbili kusafishia uso wako. Kwa wale wavivu wa kuosha uso after make up au kupaka paka facial kila mara…nafasi ya facial hadi weekend hii  ni booonge la msaada!

Au kichunusi kikianza tu wakati wa kuoga chukua kidogo  sugulia hapo, baaasi kesho ukiamka unaona kinaanza kupotea siku inayoafuata hakipo! na hubaki na doa hata!

MATUMIZI: unaweza kuitumia kila siku mwilini kama utapenda kuitumia mwilini, au  ukaitumia kila baada ya siku mbili usoni.  Unachovya kidogo unalowesha uso kisha unamassage kwa mtindo wa kuzungusha maduara usoni. Inaua chembechembe  hafifu za uso na kuuweka uso wako fresh kabisa. Unaosha uso wako na sabuni yako baaaaasi umemaliza!
Inafaa wanaume na wanawake.

BEI: ni Tsh. 15,000 tu! 
Utakaa nayo sana tu

2. UNGA WA LIWA

Kuna liwa hii nyeupe...tunaita liwa ya Comoro

Kuna Liwa hii ya Brown

Liwa hukausha chunusi, liwa hutibu chunusi…

Ipo liwa ya kawaida nyeupe na ipo liwa ya kahawia. pia ipo nyekundu ambayo kwa sasa imeniishia...
hii nyekundu huwa naichanganya na poda ya kawaida. 
Aisee! inakupa poda yenye rangi nzuriiiii sana hasa kwetu weusi!

MATUMIZI:  unachukua unga wa liwa kidogo unachanganya na maji ya Liwa au maji ya Rose unapata uji mzito kidogo. Unapaka usoni unaacha ikaukie kwa nusu saa hadi saa nzima. Kisha taratibu unachovya vidole kwenye maji na kumassage uso ili kulainisha ile liwa iliyokauka. Fanya taratibu tu usiwe n haraka ya kuindoa kwa kusugua kwanguuuuuvu. Hapana!

Ukimaliza osha uso wako vizuri na sabuni yako uache uso upumue kidogo hata dakika 10 hivi  kabla ya kuanza purukushani za make up!
BEI: ni Tsh. 5,000 tu!


3. UNGA WA DENGU


Unga wa Dengu kwa kiingereza unaitwa Gram flour au Besan yaani una majina lukuki…hebu google uone faida zake kama huniamini.
Kwa wale wenye chunisi ngumu, hii ni kiboko yao na mbali na kuondoa chunusi kali, pia hung’arisha uso sana tu!

MATUMIZI: Chukua unga wa dengu changanya na manjano na maji ya liwa kama huna maji ya liwa basi weka maji ya limao fresh… pata uji mzito kisha paka usoni. Kaa nao nusu saa hadi saa nzima. Kisha taratibu unachovya vidole kwenye maji na kumassage uso ili kulainisha ule mchanganyiko uliokauka. usiparuze mchanganyiko kwa nguvu

BEI: Tsh. 5000 tu


4. SINGO WAKAWAKA

Monday, December 1, 2014

PERUZI YA ENZI.... HABIBI YA NOUR EL AIN BY AMR DIAB NA LYRICS ZAKE!!



Mambo ya kiarabu!..... unaambiwa viuno viuno... mapigo mapigo sasa pata na maana yake
unaachaje kuupenda huu wimbo ati!

Niliupenda hata kabla ya kujua maana yake...
nangojea tu pale habibiii habibiii habibiii hahahahahaaaa
Hebu twende sambamba na Amr kwanza...
tupunguze uchovu wa kazi

Habibi ya nour el-ain
Ya sakin khayali
Aashek bakali sneen wala ghayrak bibali

Habibi, Habibi, Habibi ya nour el-ain, aah
Habibi, Habibi, Habibi ya nour el-ain
Ya sakin khayali


Agmal aouyoun filkone ana shiftaha ...
Allah aalake allah ala sihraha
Aoyonak maaaya ...
Aoyonak kifaya ...
Tinawar layali


Habibi, Habibi, Habibi ya nour el-ain, aah
Habibi, Habibi, Habibi ya nour el-ain
Ya sakin khayali

Kalbak nadani wkal bithibini
Allah aalake allah
Tamentini

Maaak elbidaya ...
Wkoul elhikaya ...
Maaak lilnihaya

Habibi, Habibi, Habibi ya nour el-ain, aah
Habibi, Habibi, Habibi ya nour el-ain, aah
Aah ... Habibi ... Habibi ... aah



ENJOY!!

Friday, November 28, 2014

UREMBO NA LAURA:.... DETOX WATER NA FAIDA ZAKE MWILINI....


Kwa rehema za Mwenyezi Mungu. Natumaini wasomaji wangu mu  wazima… kuwa tu na ule uzima ni jambo la kushukuru Mungu.

Leo nawaletea hiki kitu kinaitwa kuondoa sumu mwilini… ninaposema sumu simaanishi sumu kama ile ya panya… La hasha! Nazungumzia sumu, hizi takataka za mwilini.

Unajua na hii milo yetu tunayokula si ajabu tu kujisikia ovyo ovyo kila siku na ukapanga foleni kumuona dokta na ukaambiwa huna hata malaria. Lakini ndio mwili haueshi uchovu na maradhi yasoeleweka! 

Na hospitali hizi za siku hizi hawawezi kukuacha ukatoka bila kupewa dawa!...
Sasa hii kudetox mwili kwa maji , ndio kama kuupunguzia mwili kadhia na kuuimarisha. Nyumba inakarabatiwa seuze mwili, tena mwili wa binadamu! Hii si yakukosa ndugu yangu!

Zipo aina nyingi za detoxification…. Zipo dawa za vidonge, zipo dawa za hali ya kimiminika hasa kwenye bidhaa za Forever living na GNLD… zipo detox diet, na detox  ya maji ambayo mimi ndio nitaizungumzia maana ni nafuu mnooooo na rahisi sana kutengeneza!

Kwanza tujue DETOX WATER NI NINI?


Huu ni mchanganyiko wa maji na virutubisho kadhaa (matunda etc) vyenye nia ya kuusafisha mwili na mifumo yake. Ni kinywaji murua kabisa, chenye ladha  fulani tulivu na chenye manufaa makubwa mwilini mwako kuliko unavyofikiria.

FAIDA ZA DETOX WATER

1. Hukupa nguvu (energy)… ile hali ya kuhisi kuchoka choka bila sababu  hupotea kabisaaaa

2. Huondoa ‘sumu’ mwilini. Tunajua mwili hujisafisha kwa kutoa taka kupitia jasho n.k lakini unapodetox mwili unaondoa hata zile taka ambazo kwa namna moja ama nyingine hazikutoka ipasavyo. Yaani kama ni usafi basi ndio umeamua kuchukua brashi sabuni na maji… full kutakata!!

Tuesday, November 25, 2014

HAPPY BIRTHDAY MAMA YANGU!!.





Dear Mom,
Sijui hata nianzie wapi jamani...
Now i know there’s no bond quite like that between mother and child. 
You know me in ways no one else ever will. You also see in me all the things I can still become and continue having faith that I can do and be whatever I want, no matter what my age.
You are my biggest fan, my mentor, my confidant, my hero, my turn-to person when my world comes crashing down and the first person I call to tell when things are going great.
The comfort that comes from our friendship, the confidence that your faith in me instills, and your unquestioning support of whatever I do, is irreplaceable. The kind of there-for-me that you are is the very essence of what makes a great mother. I wear your unconditional love and support around me like a big hug every single day.
I am so blessed to have you in my life. I’ve probably said it before …. you are my angel on earth. Thank you for always, always being at my side and having my back. No one is in my corner quite the way you are. I treasure you, mother, and love you more than life itself.
You are an amazing soul ever ready to learn something new, always open to differing opinions, and so compassionate and kind. You have always taught by example.
I hope you break 100 with good health and a strong mind. There’ll never be a day in my life when I won’t need you. I’m here for you too. Please remember that.
Happy, Happy, Happy Birthday, mom. You make the world a better place.
Love you always, I mean alwaaaaays mom!!
your daughter
LAURA PETTIE
NB. ni siku kama ya leo mwaka jana nilivunjika mguu!... from there life was never the same again... but i'm still thankful to God!!

Saturday, November 22, 2014

10 MINUTES WITH GOD!...WATEULE WA BWANA





Wateule wa Bwana karibuni mezani pake, njoni, Bwana awaalika enyi wenye moyo safi x 2

Amewaandalia, leo, karamu takatifu, njoni mwili na damu yake chakula safi cha roho x 2
  1. Kwanza tujitakase, nafsi zetu wenyewe, tukishakutakata, tujongee meza yake.
     
  2. Karibuni mezani, Bwana awaalika, kwenye karamu yake, enyi wenye moyo safi.
     
  3. Na tule mwili wake, na tunywe damu yake, ndicho chakula bora, cha roho zetu karibu.
     
  4. Tusipokula mwili, na kunywa damu yake, tunazinyima roho zetu neema zake Bwana.




ENJOY!!

Friday, November 14, 2014

UREMBO NA LAURA:.....JE WAZIJUA CHARGER PLATES??


hiyo sahani ya chini, rangi ya pink ndio inaitwa Charger Plate!

Kuna vitu ambavyo wengi wetu tunaviona tu katika sherehe au mialiko majumbani mwa watu lakini hatuvijui vizuri, si kwa majina wala kazi zake. Moja ya vitu hivi ni hizi sahani paaaana zinazoitwa ‘Charger Plates’

 Unazijua? au unaziona tu kwenye picha?.... hahahahaaaa!!...
Najua mnazijua bwana ila kwa wale wenzangu na mimi ambao kuna mambo ya kisasa na nini na nini yanapita kushoto kwa kasi wakati sisi tuko kulia…ndio hivi tunaelezana ili mwisho wa siku usije ukabeba Charger  Plate ukaenda kupakulia  chakula ohooo!!

MATUMIZI YA CHARGER PLATES
1. MAPAMBO

Sahani hizi pana mara nyingi huwa mapambo. kuna umaridadi fulani unaletwa na hizi sahani unapotumia kupambia meza yako wakati wa mlo. Yes! unaweza kuzitumia hata nyumbani
Mfano unawageni wako, basi unazitumia kupamba meza na hakika
utajizolea maksi tele za umaridadi.

Katika sherehe Charger Plates zinaweza kuendana na rangi ya Party. Hebu angalia hiyo picha hapo juu uone rangi nyekundu ilivyoendana na rangi nyekundu kwenye viti!
classy!....

Thursday, November 6, 2014

UREMBO NA LAURA:.....JINSI YA KUKABILIANA NA WEUSI KWAPANI!!

K


Habari zenu wasomaji wangu!
Kama kawaida leo tunakutana tena ulingoni…. Katika kuwekana sawa hapa na pale kwenye masuala ya urembo masuala ya usafi na kadhalika! Mradi kwa gharama ndogo tu unabaki msaaafi kabisa na mwenye furaha tele! Team kubana matumizi hahahaha!

Leo nataka kugusia suala la makwapa kuwa meusi. 
Inakera sana!... hasaaa linapokuja suala la kuvaa nguo ya kukata mikono. Yaani unakosa kujiamini. Tena  basi uwe kwenye kadamnasi ambapo unatakiwa kupunga mikono hivi…ni zaidi ya shughuli!... unashindwa hata kujimwayamwaya mwenzangu aiiii kisa tukwapa tweusi!

Kuwa na kwapa jeusi sio ugonjwa, sio dhambi lakini mwenzangu linapunguza maksi kiasi fulani…. Halafu kwanini uwe na lami makwapani wakati njia tele za kuondoa na kuzuia zimejaaaa!!

Kwanza tuangalie sababu za makwapa kuwa meusi!
1. Unyoaji…. Wembe unachangia sana kuwa na makwapa meusi…ile puruuu puruuuu aaah mwenzangu lazima kwapa lidate hahahahaaa…. Hapo umetia vijisabuni kidogo unashave kwa nguuuuvu ili kwapa libaki jeupe mpaka mtu nje anaweza uliza jamani kuna usalama uko? anhaaaa!!

2. Deodorant:… unaroll deodorant  wiki ya kwanza…ya pili..ya tatu…unaona mabadiliko kwapani we umo tu!.... kipodozi chochote kikionyesha hali ya kukukataa hata kama ni siku mbili tatu…KIACHE!! Ukijitia una uchungu na hela yako utagharamamika zaidi ya hizo ulizotoa kwenye kutibu matokeo, unapaka deodorant unasikia  kwapa linawaka moto jamani bado umo tu! yahusu!

3. Magonjwa… hapa sitaingia sana maana sina utaalamu huo ila ndio hivyo kuna wakati hali hiyo inaletwa na ugonjwa ulionao na utagundua hili kama njia zingine zote zikidunda.
Haya sasa ndio tushapata kwapa jeusi...tufanyeje?

NAMNA YA KUKABILIANA NA  KWAPA JEUSI
1. LIMAO NA SUKARI


Hii njia ya kwanza iliyo bora kabisa na nyepesiiii
Kata kipande cha limao kichovye kwenye sukari, tena ile ya brown ndio nzuri zaidi.
Sugua kwapa lako kwa mtindo wa kuzunguka. Taratibu tu ila hakikisha unasugua eneo zima. Usikamue limao wewe sugua tu…majimaji  yatatoka yenyewe.
Acha kwa dakika 10-15 kisha osha makwapa yako vizuri kwa sabuni yako ya kila siku.
Fanya hivi asubuhi na jioni mpaka uone weusi umeondoka na lazima uondoke.
Faida yake ni kuwa Limao litaondoa pia harufu ya kwapa, na katika kipindi hiki usipake deodorant yoyote.

Monday, November 3, 2014

PERUNZI YA ENZI....AZALAKI AWA BY GATHO BEEVANS WITH LYRICS!



Sijui hata nilichokumbuka...basi tu nimejikuta naimba huu wimbo leo saaana!
Halafu naimba kiitikio tu tena ninavyojua mwenyewe hahahahaaa
chezea kilingala!
ila nimekumbuka mbaaaali kweli dah!...twende kazi sasa!

Azalaki awa
Pembeni na nga
Esika akeyi ekaboli nga na yé

Ye na bembo na ndako mosika
Distance na kati ye ngambo ngai na ngambo

Tango mususu soki na kanisi ndengué oyo tozalaki epesi nga kobanga
Moto na lingi akoma mosika
Natondi na ba souvenirs na motema
Na lela na nani ?, na salako nini ?, na kende ko wapi ?
Nakomi se ko banza ngai moko

Azalaki se awa
Se awa
Cherie a keyi nayé
Alobaki na ngai akozonga
Se awa
Ngako na zelaka yé


Azalaki se awa
Se awa
Cherie a keyi mosika
Alobaki na ngai akozonga
Se awa
Suka se okoya

Thursday, October 30, 2014

UREMBO NA LAURA:....MAFUTA YA MCHAICHAI (LEMONGRASS OIL)

Ya kwangu hayoooo mkononi

yenye majina ya kizungu hayoooo!!...na mmea wake huo hapo nyuma

Nadhani niihamishie alhamisi hii makala ya Urembo na Laura. Maana naona Jumatano huwa inakuwa na mambo mengi mno.

Yote kwa yote, natumaini kwa uwezo na kudra za mwenyezi  Mungu mu wazima. Tuendelee sasa!

Leo nakuletea Mafuta ya mchaichai. Sidhani kama huufahamu huu mmea wa mchaichai. Wengi wetu tunautumia kuungia chai. Na Majani yake si mageni kwetu. Ni mmea wenye harufu na ladha nzuri sana. Wakati mwingine hutumika kama kiungo kwenye chakula na kwenye mapishi, tumia kumarinate kuku kabla hujamchoma au kumkaanga utapenda na roho yako!

Sasa haya ndio  mafuta yake pia. Ni mafuta mazuri mno na kwa mtu yoyote anayejipenda, haya mafuta ni wajibu kuwa nayo. Ni mafuta yenye matumizi mengi kwa wakati mmoja

1. KUKUZA NYWELE ZILIZOKATIKA

Thursday, October 23, 2014

UREMBO NA LAURA:.... JINSI YA KUPAKA WANJA WA KISASA!!


Nyusi ni sehemu ya urembo wa mwanamke... namna unavyozitengeneza nyusi zako unaweza pata muonekano wa kuvutia au ukawa kichekesho pia. Maana unakutana na mtu nyusi zimekaa rafu mpaka basi au ndio vile zimechongwa kipashkuna mno hahahaha... ama ndio uso unakuwa kama anazomea hivi...mradi hekaheka tu!

Unaweza kumpa pole mtu ukijua ana huzuni kumbe walaaa nyusi zimekupa wrong infomesheni!!

Sasa kabla hatujapakana wanja hebu tuone vitu muhimu vya kuwana navyo au kufanya. Hii ni kwa hohehahe wenzangu wanaotaka kupendeza ila ndio wanaona kuna vitu havikamatiki!... unaweza punguza bajeti ya mboga nyumbani hivi hivi...lakini sio sababu usiwe mrembo jamani. tubanane tu humu humu!

1. Tinda nyusi zako unavyotaka wewe.... binafsi sijui ni mazoea au ni nini...huwa nazichana nyusi kurudi chini... kiasi kwamba sasa hivi zinaota kueleke chini LOL!...so nazitrim mwenyewe kwa chini... vyovyote utakavyotinda au kutindwa mradi ziwe kwenye shepu fulani ya kueleweka

2. Kuwa na vifaa !.... wanja sasa hivi unauzwa kila mahali kuanzia 10,000 mpaka 25,000 kulingana na aina ya wanja, quality, brand etc!
kwa wale wenzangu na mimi ambao we cant just use tarakimu 5 za hela  kwa ajili ya wanja tu... basi nunua wanja wa kawaida tu!

WANJA.... 
unaweza kuwa na huu wa penseli au mwingine
Bei yake hata 5,000 haifiki!

Sunday, October 19, 2014

10 MINUTES WITH GOD... LULU BY MTONI EVANGELICAL CHOIR!!




Yesu nipeleke kule kwa baba nikaishi naye kule mbinguni kwenye mji wa lulu na milango ya dhahabu
Yesu nipeleke kule kwa baba nikaishi naye kule mbinguni kwenye mji wa lulu na milango ya dhahabu
Oooooh.. Oooooh lulu..
Ooooh... Ooooh lulu
Ooooh Lulu...
Iko mbinguni
Ooooooh.... mmmmm...
Kweli ndani ya Yesu, Kuna raha ya ajabu isiyo na mwisho
kweli jamani mmmmmmm!
Yesu nakuomba nipe nguvu nikutumikie humu ulimwenguni kabla ya siku zangu hazijaisha..
Yesu nakuomba nipe nguvu nikutumikie humu ulimwenguni kabla ya siku zangu hazijaisha..
Oooooh... Ooooooh Lulu...
Ooooh... Oooooh Lulu
Oooooh Lulu...
iko mbinguni  
Ooooooh.... mmmmm...
Kweli ndani ya Yesu, Kuna raha ya ajabu isiyo na mwisho
kweli jamani mmmmmmm!

ENJOY!!

Wednesday, October 15, 2014

UREMBO NA LAURA:...NAMNA YA KUJIFUNZA 'GELE'... LEMBA LA KINAIJA!! (PICHA NA VIDEO)

Wengi wetu tumeona namna fasheni inakoelekea!
kufunga gele kumeshika chati sana japo fasheni ilikuwepo kitambo tu.
Leo ngoja nikupe hatua kwa hatua za namna kulifunga GELE 

unaweza kukosea hapa na pale lakini nakuhakikishia ukitulia unaweza kugeuka mtaalamu hivi hivi hahahahaa.... ni wewe tu na utundu wako katika kujifunza

HATUA YA 1

kunja kitambaa chako kwa staili hii... vitambaa vya kufungia gele shurti kiwe kikavu kidogo
kikunje hivi ili ule mwanzo kwa lemba uwe smooth pale mbele.  au pia unaweza kunja ikaribie nusu ya kitambaa chako

HATUA YA 2
linganisha pande zile za mwisho zilingane... yaani ukikiweka kichwani sio huku kurefu kule kufupi
Ni kulingane...kwamba ukianza kufunga mstari unaogawa katikati uwe katikati ya uso...sijui umenielewa heheheee...ualimu wito ujue!

Monday, October 6, 2014

SHOUT OUT TO WYNJONES KINYE!!- ASUBUHI ITAFIKA!!



Kuna muziki wa midundo...na kuna muziki wa maneno!
Kivipi?.... ni mara ngapi umesikiliza nyimbo za kikongo ukajikuta unajitikisa tu pasi kujua ni nini kinaimbwa!.... ni mara ngapi umesikiliza wimbo ukajikuta unabonyeza kitufe kurudisha nyuma kidogo ili upate kufaidi ubeti fulani wa wimbo huo?

This is what am talking about!.... Asubuhi itafika ni wimbo wa maneno... Kinye is talented...kuanzia sauti mpaka mpangilio wa tungo zake... ni kati wale vijana wachache wanaofanya muziki kama sehemu ya hobby lakini naamini akiamua kukaza ndula huyu anakwenda sawa na AY!!

Mjini hapa promo tu ila tukisema tufuate talent... kuna talent nyingi sana kama hizi na moja wapo ikiwa hii.... huu sio wimbo wake wa kwanza anazo kadha wa kadha....

kwa leo hebu tulia kidogo ujipe nafasi ya kumsikilia Kinye!... 
Hapo ulipo kama kuna kikwazo unapitia...kama kuna mtihani unakuelemea msikilize Kinye anavyokwambia Asubuhi itafika!!

Hongera sana Kwa kazi nzuri kama hii.... Maaaaan ! una sauti mwana! unayo haswaaaa!! endelea KUITIMIKIA SAUTI YAKO!!

Sunday, September 28, 2014

10 MINUTES WITH GOD!! - SAYARI BY AMBASSADORS OF CHRIST



Ni moja kati ya nyimbo za dini ninazozipenda sana
Hauchoshi...kuna ujumbe murua na hakika huwa najisikia kubarikiwa sana ninapousikiliza
Kuna lyrics zake ila kwa sababu ya haraka niemshindwa kuzipost

Napenda kukukumbusha tu kuwa pasipo kujali ugumu wa tatizo unalopitia... pasipo kujali vikwazo unavyopitia.. pasipo kujali machozi ambayo umeshalia... pasipo kujali faraja ilivyo mbali kuifikia... Mungu wetu ni Mungu mwenye upendo anakuona...anakusikia... atakujibu!
USIKATE TAMAA yawezekana umeikaribia faraja!

panapo maajaliwa!
ENJOY!!

Wednesday, September 24, 2014

UREMBO NA LAURA......TREATMENT YANGU YA NYWELE ZA ASILI

MWANAMKE NYWELE HASA ZIKIWA ZAKO MWENYEWE HAHAHAHAAA!!

Watu wengi wanadhani kuwa na nywele ndefu za asili, nzuri na zinazopendeza ni kitu kisichowezekana kwa mwanamke wa kisasa au kuwa na nywele za asili ni ushamba au kutokuwa mrembo.

Dhana hii ni potofu kabisaaa!... unaweza kuwa na nywele zenye dawa au nywele bandia za kusukia na bado ukashindwa kuzitunza vizuri na ukaondoa mvuto wako.

Sikatai kwamba kuna wakati tunahitaji mambo ya ziada kichwani ili kupendeza lakini pia si vibaya mara kadhaa ukaziachia nywele zako halisi na ukajiletea muonekano tofauti kabisa!!

Kutunza nywele za asili si kazi ndogo na hasa unapotaka ziwe nywele  zenye afya na zinazovutia.  Nywele za asili huleta muonekano wa mwanamke anayejiamini kwelikweli.
Binafsi nina nywele za asili nikimaanisha hazina dawa kabisa…. ingawa pia huwa ninasukia weaving au kuvaa wig pale ninapotaka muonekano tofauti lakini mara nyingi kichwa changu huwa huru. Leo ningependa kushea pamoja nanyi njia mojawapo ninayoitumia kutunza nywele zangu.

1. OSHA NYWELE ZAKO KWA MAJI YA UVUGUVUGU 
kwa shampoo unayotumia… huwa inasaidia kuondoa mafuta mafuta na uchafu unaoshikana na nywele hasa kwa vile huwa tunamaliza hata wiki mbili pasipo kuosha nywele…. Wengine wenye nywele za asili huogopa kuziosha mara kwa mara kwa kuhofia zitasinyaa na kuwa fupi hahahahaaa… hapana ndio unazisafishia njia ziwe ndefu zaidi…. Osha tu mara kwa mara usiogope…. Ukishaosha suka nywele za uzi zinasaidia kunyoosha au tumia hand dryer kukaushia…kariakoo  kuna mpaka Tsh. 35,000/= tu hilo hand dryer….  Kama unanunua nguo ya elfu 40,000/= utashindwa kweli kuwa na hiki kifaa??? Sema tu hujakipa kipaumbele lakini ni kifaa muhimu mwanamke mwenye kuzipenda nywele zake kuwa nacho
Shampoo ya mayai iko smoooooth

2. CHUKUA YAI NA UTOE KIINI PEKEE….

Mimi niliamua kuweka kiini na ute wake… lakini vizuri ukitumia kiini pekee

3. ONGEZA ASALI VIJIKO VITATU VYA CHAKULA


4. VURUGA MCHANGANYIKO WAKO



5. PAKAA NA UVAE KOFIA YA KUFUNIKA
Unaweza tanguliza mfuko wa plastic ile miyeusi kisha ukavaa kofia na kufunga lemba kwa juu ili kupata joto zaidi…. Njia hii ni bora kuliko moto mkali wa saluni.
excuse my nails heheheee!!...


6. KAA NA KOFIA KWA SAA MOJA AU ZAIDI.
7. OSHA NA MAJI YA UVUGU VUGU NA SHAMPOO…  zikitakata zikaushe kwa taulo na paka mafuta ya maji kwanza…. Hii inasaidia kuondoa ukavu wa nywele. Mi natumia Olive oil for hair

unaweza tumia mafuta ya nazi au yoyote ila ya maji ni mazuri baada ya kuosha

Zikishakauka vizuri…paka mafuta kwenye ngozi na umassage kichwa kwa dakika kadhaa…utahisi tu ngozi ya kichwa iko fresha kabisaa.

Mafuta ninayotumia kwa sasa 
nina aina mbili hii aina ya kwanza...ni mazuri sana kwa kweli

Kupata mafuta kwenye ngozi kunasaidia sana kuondoa ukavu kwenye kichwa na hata mba si rahisi kukuvamia. Ukipuuzia ukapata mba kuzitibu mba ni kazi sana na huwa zinazuia ukuaji wa nywele itakiwavyo.

Zilikatika sana pembeni ila now zinarudi faaaasta sana...


Furahia nywele zako na jisikie farahati kurock your natural hair mara moja moja!!... sio kila siku una fake hair kichwani Lol!!.... jiamini unaweza kuzilinda na kuzitunza nywele zako mwenyewe na zikawa na mvuto..
Njia hii pia hata walioweka dawa na nywele ni dhaifu wanaweza kuitumia.
Unaifanya treatment hii mara mbili kwa mwezi inatosha kabisaaa au hata zaidi kulingana na nafasi yako.

Zipo treatment zingine pia  kama ya kutumia mtindi ambayo ni nzuri mnooo imesaidia kunijazia nywele…. Tukutane tu kila jumatano hapa uwanjani!!
natumaini umeambulia kitu... Mwanamke nywele shost!!

PERUZI YA ENZI:.....TAGO MAGO BY KAOMA DANCA



Huu wimbo nilikuwa naupenda sana ila sasa kuuimba ikawa shughuli
nilikuwa nangoja kuitikia tu Tago Mago ...eho ehooo 
Halafu naudansi mpaka basi!!
Leo nikaukumbuka nikasema kwanini nisiwakumbushe na nyie 
You remember it!!

ENJOY!!

Wednesday, September 17, 2014

UREMBO NA LAURA.... TREATMENT YANGU YA USO MARA MBILI KWA WIKI

MWANAMKE RECEPTION!!... shepu hata mbuzi anayo Lol!
Haya wasomaji wangu za siku tele?.... maana kuonekana humu imekuwa kama kuwinda mkia wa kobe…nadra nadra lakini ndio vile mishughuliko na mihangaiko mkono uende kinywani kunafanya nashindwa kuwa active inavyotakiwa… Mniwie radhi tu na kama hivi siku nikitulia basi tunapeana ya hapa na pale. Sasa kila jumatano tutapeana vijitip vya urembo vya hapa na pale.

Nilishasema na narudia kusema USO bwana ndio mapokezi yako… hasa kwetu sisi wanawake. Haijalishi umeolewa au lah! Haijalishi u kigoli au kikongwe… kupendeza uso ni haki ya kila mtu aliyehai…

Leo nitakuletea mambo ninayoyafanya mimi kuuweka uso wangu katika hali ya usafi…hali ya kupendeza hali ya kung’aa… yaani uso ukiwa shwari unakuwa na confidence f’lani mwenyewe kuliko mwenye uso wenye makorokoro.
Kujichubua sio kupendeza wala weupe sio kupendeza… unaweza baki na rangi yako na bado ukapendeza sana tu. Mwanzo nilikupa hints za jumla jumla tu leo nakupa hatua kwa hatua…twende kazi!!
1. OSHA USO KWA  MAJI SAFI NA SABUNI.
Mimi natumia sabuni ya Liwa kuoshea uso… ni sabuni nzuri sana aisee, inazuia harara za ovyoovyo na inapunguza mafuta kwenye ngozi kwa wenye chunusi hii inawafaa sana…. Baada ya kuosha nakausha uso kwa taulo safi sio tena unajifutia khanga yoyote uliyotundika hapo chumbani… utatoa uchafu na kuingiza uchafu hapo!
hapa sijapata chochote ni nimetoka kuosha uso na kuufuta.
Sabuni ya Liwa ninayotumia

2. Nina mchanganyiko wa liwa na manjano… nachukua kidogo nachanganya na maji au wakati mwingine nachanganya na maji ya liwa. Iwe uji mzito sio majimaji… hapana!... ni kidogo tu. Paka usoni taratibu kwa kusambaza kama unazungusha maduara hivi. Paka uso mzima
Huu ndio mchanganyiko wenyewe... 
unaweza chukua manjano na unga wa liwa unamix mwenyewe

Uji mzito mzito.. hapo nishaukwangua nikapaka

3. Naacha kwa nusu saa tu… au hata dakika 15 hivi zinatosha mradi ikaukie usoni…. Kisha taratibu sugua uso kuondoa yale makapi kapi yaliyoganda. Sugua taratibu sio paruuu paruuu…ngozi ya uso iko sensitive na ikibidi chovya mkono kwenye maji kisha chua taratibu kama dakika moja hivi… ukizunguka uso mzima
Haya mchanganyiko huo usoni
nikatulia nusu saa nzima... nasoma gazeti... naperuzi hapa na pale

4. Uso utabaki na mlaini na ule unjano njano… sasa osha kwa sabuni yako tena kuondoa kabia ule mchanganyiko. Utasikia tu uso unabaki msafi kwelikweli.

Baada ya kusugua takataka zote

5. ukishakausha uso…chukua pamba chovya kwenye cleanser yako… yangu mimi ndio haya maji ya liwa. Nayatum ia kusafishia uso badala ya cleanser zile za kizungu. Sikudanganyi ni nzuri mno aisee.  Safisha mpaka pamba inabaki nyeupeee
Picha ya maji ya liwa.

Haya ndio maji ya Liwa.... nachanganyia na manjano na liwa
na pia nasafishia uso


Mwisho…. Kama unapaka lotion paka kidogo sana saaana… kama ni cream yako paka kidogo sana au unaweza usipake kitu kama upo tu nyumbani na huendi kokote. Nashauri ufanye hivi ukiwa huna safari ili ngozi ipumue kidogo kama masaa mawili hivi ndio uukandike poda. Mimi natumia hii cocoa butter. Napaka kidogo sana kwa vile uso wangu una mafuta.
Hii ndio nabrashia usoni... ni unapaka kidogo nasisitiza kidogo mno
hasa kwenye nyuso za mafuto... hii ni kama unataka kupaka poda usoni ili utoke
kama uso hautaki mafuta kabisaa basi usipake kitu! na kama ni usiku usipake kitu kabisaa
Baada ya shughuli nzima
Uso ukiwa muruaaaaa!! 

Hii treatment naifanya  mara mbili tu ila unaweza ongeza ukipenda ni wewe tu… urembo unataka juhudi, usafi, uvumilivu hasa kwa matumizi ya vitu vya asili lakini nakuhakikishia uso ukibadilishwa na vitu vya asili hutajuta wallah…. Ni kitu permanent uso hauwezi kuvamiwa na sugu wala chunusi za ajabu ajabu. Na treatment kama hizi hata wale wa wageni wa kila mwezi wakija hawauchafui uso kiasi uuchukie ni kipele kimoja kimoja tena kidooogo sana sio nundu hiyoooo!

Natumaini umepata kimoja cha kukusaidia hapo… upende uso wako jamani… utunze kwa kadri unavyoweza ndio mapokezi hayo mwaya !!! ukishafanya hivi kumbuka zile sheria nilizokupa mwanzo...utakuwa na uso msafi utashangaa mwenyewe!!





Monday, August 25, 2014

PERUZI YA ENZI.... SOLEMBA BY JUWATA JAZZ NA LYRICS JUU

Ni wimbo wa kitambo sana lakini kama kawaida old is gold
Nimejikuta tu naukumbuka sana leo na kuuimba
nikaona niwakumbushe na wale wapenda za kale

ENJOY!!

#MCM.... KENNY ROGERS!

I LOVE THIS OLD MAN TO BITS!!


Alifanya upasuaji wa uso... things didnt go well but.... 
I love him either way Lol!

My favorite Photo!




Snowfall Widget for Blogger


Snowfall Widget for Blogger