Tuesday, May 14, 2013

FILAMU: The gods must Be Crazy 1..... Cocacola ikaleta balaa nyumbani kwa bushman


N!XAU GCAO COMA..... The starring himself
hii ni mwaka 2003...mwaka aliofariki


TUMJUE KWANZA N!XAU
N!xau (matamshi yake mpaka leo ni utata but wanasema linatamka Gcao Coma, maana unaita kisha unashangaa, (huo mshangao ni silabi inayotamka kikao) halafu unamalizia na jina…what a name!...tried to make mine L!?ura Lol!). N!xau alizaliwa mwaka 1943 lakini inasemekana yeye mwenyewe alikuwa hajui umri wake halisi. Alizaliwa uko Tsumkwe, nchini Namibia akitokea kabila la San ambalo ndilo kabila linalojulikana kama Bushmen, jamii ya wafugaji wanaoishi maisha ya ujima. 

 wana sema etiiii alifanana saaana na Usher Raymond 
hahahahahaaa



Kabla ya kuingia katika ulimwengu wa filamu, ulimwengu wa kisasa uliojaa teknolojia na mambo mengine ya kizungu. N!xau alikuwa mkulima, na katika maisha yake hakuwahi kutembelea miji mikubwa yenye magari na majumba ya ghorofa. Alizoea kuona nyumba za nyasi kijijini kwao, alikuwa amekutana na wazungu watatu tu lakini kali kuliko zote ni kuwa hakuwa anaijua thamani ya pesa, kama vile alivyoigiza kuzitupa pesa katika filamu yake…na katika maisha yake halisi N!xau hakuithamini pesa kwani alikozaliwa na kukulia, jamii yake haikujua pesa ni ina thamani gani.

Pato lake la kwanza katika filamu yake ya kwanza The Gods must be crazy lilipotea tu bila kufanya chochote, lakini baada ya kusaidia kujua anaweza kufanya nini kwa kutumia pesa anayopewa. N!xau alifanya makubwa na hapo ndipo akaanza kunegotiate mamilioni ya pesa kwa ajili ya kucheza filamu za hao jamaa!….! kumbe hizi mbio za kukimbizia haya makaratasi a.k.a  kazileta mzungu..ona sasa mbio haziishi duniani!
N!xau alicheza filamu zipatazo saba…. The Gods Must Be Crazy (1980),  The Gods Must Be Crazy II (1988), Kwacca Strikes Back (1990), Crazy Safari (1991), Crazy Hong Kong (1993), The Gods Must be Funny in China (1994) na Sekai Ururun Taizaiki (1996)
Aliianza kazi ya uigizaji mwaka 1980 na kuhitimisha rasmi mwaka 1994 ingawa mwaka 1996 alishiriki filamu ambayo hakuwa muigizaji mkuu (lead actor).

Alipomaliza kazi yake ya kuigiza, N!xau alirejea Namibia akajenga nyumba ya matofali aliyoiwekea umeme na maji, akarejea katika ukulima sasa akimiliki ng’ombe kadhaa na mashamba, pia alikuwa na gari ambalo aliajiri dereva wa kumuendesha. Pamoja na kupata upeo wa namna ulimwengu wa upande wa pili ulivyo, N!xau alijifunza kunywa pombe na kuvuta sigara, mambo mabaya aliyoyapata katika utandawazi.

July 1, 2003 N!xau alifariki dunia. Msemaji wa Mimosa films ambao ndiyo watengenezaji wa The Gods Must be Crazy alisema katika taarifa yake kuwa N!xau alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kifua kikuu (Tuberculosis) na kwamba siku ya tukio aliondoka na kwenda kuwinda lakini hakurejea. Familia yake ilipomtafuta kwa siku kadhaa ilimkuta akiwa amelala porini na tayari akiwa ameshakufa.

N!xau aliacha wake zake watatu na watoto 12.



FILAMU YENYEWE SASA....
Nadhani wengi tunaijua hii movie aisee…. imaigiziwa Botswana ila na kampuni toka South Africa
Starring akiwa mnamibia mkulima wa jamii ya Bushmen

kama utaiangalia mwanzo mwisho bila kucheka, mwenzangu tafuta hospitali wakacheki kama bandamo yako bado ipo… ni stori yenye pande tatu….
1…. N!xau au Xi kama anavyojulikana katika movie. Siku moja rubani anadondosha chupa ya cocacola toka angani na Xi analiona tukio hili. Kwa kutokujua chupa ni nini anaipeleka kwa jamii yake uko kijijini. Kufika ule chupa inaleta mzozo mkali na mifarakano maana kila mtu anataka atumie…huyu anatwangia….yule anasagia basi tafrani
hizo kazi za chupa....kwenye movie utacheka ufe.....

Ukoo unakaa na kuamua kuirudisha chupa kwa miungu(uko ilikotoka) ili kuepusha mifarakano zaidi. Xi anatumwa akaitupe mwisho wa dunia na safari inaanza….

2. …kuna biologist anaitwa Andrew Steyn (Marius Weyers) hahahahaaaaa acha nicheke kwanza maana the man is real fuuuuuunnnny kha!....huyu jamaa bwana na aibu zake anatumwa kumpokea kate Thompson (Sandra Prinsloo)….uwiii the whole safari balaaa… unakumbuka wakati anafungua geti la mpaka….au wakati wanafukuzwa na viboko ule usiku hahahahahaaaa…..acha hiyo alipompelekea viatu vyake darasani kule LOL!!!.... sijamsahau Mpudi rafiki wa Andrew…. huyu quote yake moja iliniacha hoi nab ado ipo kichwani I know how to marry them. Nobody knows how to live with them” 
hahahahahaaa ndio safari inaanza.... hata nusu ya vituko bado
 Andrew ni balaaa....halafu no kazeeka basi kawa tofauti kabisaaa

3. ….kundi la waasi likiongozwa na Sam Boga (Michael Thys). Wakateka wanafunzi na mwalimu Kate,  hapo wameshafanya mauaji kwenye kikao cha Rais na mawaziri kisha wakakimbilia porini. Wakawaburuta wanafunzi mpaka uko porini na kuamrisha waletewe chakula la sivyo wanateketeza kila kitu….
Sam Boga na kundi lake.... Kuubwa la maadui

kuna matukio ya kuchekesha sana humu ndani…. lets catch some funniest moments….


Nilicheka mpaka kichwa kinauma....





.......'amai vachauayaa amai chauyaaa...woya woya woyaa' lol! sijui lugha gani hii ila dah! 
mie huo ugali unaopikwa hapo najiuliza tu ni wa mtu mmoja
hahahahahaaa....

na  Movie inafikia tamati pale Xi anapofanikiwa kufika katika hili korongo
akiamini kuwa ni mwisho wa dunia...Xi anaitupa ile chupa na kurejea kwake
Apokelewa na familia yake na kuanza kuwasimulia vimbwanga vya wazungu na watu wa mjini

HOPE UMEBURUDIKA KIDOGO EEH...
UKARELAX!

1 comment:

  1. nimeipenda hii kona ya filamu keep it up!

    ReplyDelete



Snowfall Widget for Blogger


Snowfall Widget for Blogger