Saturday, June 29, 2013

SINDI....NA LAURA PETTIE (23)

23

kwa uso uliojaa mashaka vile vile, Pamella aliukorokochoa mlango wa chuma na kuufungua huku akiusukumia mbele kule alikosimama Fiona. Sasa wakatazamana uso kwa uso, paji kwa paji hali Fiona akijaribu kujenga tabasamu ambalo hata hivyo halikudumu usoni pake.

Tuesday, June 18, 2013

SINDI....NA LAURA PETTIE (22)

22
Pamella Okello alijikuta akiiachia simu idondokee mapajani mwake pasipo kujitambua. Mikono ikalala juu ya usukani kiuchovu huku macho yake yakitembea taratibu mule ndani ya gari na asielewe kila alichokitazama. Mdomo wake uliokuwa wazi ulidhihirisha bumbuwazi lililomtembelea ghafla kwa wakati ule.

 Taratibu akashusha pumzi na kufumba macho katika namna ya kuumeza ule ujumbe aliousoma kama mtu anayemeza kaa la moto. Akatulia hivyo kwa sekunde kadhaa pengine akitaka kuiweka sawa akili yake ama tu alitaka kupingana na kile kilichosomwa na macho yake.


Thursday, June 13, 2013

SINDI....NA LAURA PETTIE (21)

21
Sindi Nalela alitulia vile alivyojikunyata kwa sekunde kadhaa akibana pumzi na kukisubiria kipigo pasipo kukipata, utulivu ule ndio uliomfanya aisikie ile harufu ya pombe ambayo Jerry aliitoa kupitia pumzi na jasho lake.

Taratibu akainyanyua kichwa na kumtazama Jerry usoni, akianza kuondoa mikono yake kichwani na kubaki ameduwaa baada ya kugundua Jerry mwenyewe hakuwa hata akimtazama. Alikuwa ameinamisha kichwa chini akionekana kuwayawaya na kusumbulia kihisia.

Saturday, June 8, 2013

PERUZI YA ENZI:...RUPEEEEEEN TEMPTED TO TOOOOOUCH!




Huu wimbo yaani kama unataka kujaribisha nguo ya kuvaa kesho na unaona uvivu jaribu tu ....kuupiga huu wimbo kama hujajaribu kabati zima na kwenda kuazima kabati la mwingine pia

...the song is forever doooope yeyiiiiii



.....And de way that you twist and turn your waist
Leaves me wanting, leaves me yearning
Leaves me feelin for a taste


Before the end of the night
I wanna hold you so tight
You know I want you so much
And I'm so tempted to touch
Tempted to touch, tempted to touch
Little woman, man I need you so much
Tempted to touch, tempted to touch
Little woman, man I'm inside your clutch

SINDI....NA LAURA PETTIE (20)

20

Jua la asubuhi lilishachomoza, pilika pilika za hapa na pale zilishaanza na kuifanya siku kuwa vurumai za kutosha. Ilikuwa Ijumaa na kama ilivyo ada watu wengi walikuwa wakijiandaa kupumzika siku inayofuata.

Sindi Nalela aliamka asubuhii akiwa mnyonge mno. Alikuwa amekumbuka kwao bambali na hayo alikuwa amemkumbuka Nyanza mno. Kuna kitu kama majuto kilikuwa kikimpitia kila sekunde ya asubuhi hii.

Sunday, June 2, 2013

SINDI....NA LAURA PETTIE (19)

19
Patrick Mazimbwe alisimama akiwatazama binadamu hawa wawili kama viumbe vilivyotokea sayari nyingine. Alijikuta akitaka kuzungumza na kunyamaza kwa wakati mmoja na pengine alitamani hata kuimba ila ndio kwa wakati ule mifumo ya fahamu ilishatawanyika kila mfumo na njia yake, akabaki mwenyewe tu na akili za kukodoa macho. Kufumania kipaji si kila mtu anahimilia vishindo!



Snowfall Widget for Blogger


Snowfall Widget for Blogger