Sunday, December 20, 2015

KUHUSU HADITHI YA SINDI

....Wapenzi wasomaji wangu

Nasikitika sana kuwa imebidi niikatishe kutokana na feedback kuwa ya kuvunja moyo.
Siku zote kwa Mwandishi, feedback ni kitu kinachomuhamasisha kufanya kazi kwa bidii zaidi lakini pia ni kitu kinachompa mwongozo wa kujitathmini.

kwa hadithi ya Sindi, nimesikitika sana kuwa pamoja na kazi kubwa ya kuwaburudisha. Feedback yake haikuwa ya kuvutia hata chembe. Kuandika page 15 na mtu akazisoma na kupita kimya kimya  hata comment hata kushare au hata like inaamisha hakuvutika na ulichoandika, hivyo basi badala ya kuendelea kupoteza nguvu zaidi nikaona niirudishe kabatini mpaka hapo nitakapoona kuna mabadiliko.

Kwa sasa, nimeileta NAHIYARI MAUTI kama zawadi ya kufungia mwaka wa wasomaji.
Sijui Feedback ya hii ila kwa kuwa ni zawadi sina neno..

Poleni sana kwa wale wachache mno waliojaribu kunisupport waziwazi ila ndio hivyo imenipasa kuchukua hatua hii.


Niwatakie usomaji mwema!

Laura Pettie!

Tuesday, December 1, 2015

HAPPY NEW MONTH…MAMBO 6 NINAYOKUKUMBUSHA!


Mpenzi msomaji!

Tunauanza mwezi mpya… mwezi wa mwisho wa mwaka…mwezi wa  likizo kwa wengi na mwezi unaojulikana kama mwezi wa sikukuu. Christmas na Mwaka mpya  ni wiki chache zijazo. Ni jambo la kumshukuru Mungu sana kuwa mimi na wewe mpaka dakika hii tupo hai na kwamba pamoja na changamoto zote za kidunia na kiimani bado tungali hai tukipewa nafasi nyingine ya kunyoosha njia zetu na kurekebisha hapa na pale. Tunasema Asante Mungu!

Kama ilivyo ada tunapouanza mwaka, wengi wetu huwa tuna zile New Year’s  Resolutions!.... mipango ya mwaka  mpya kwa mwaka mzima. Na sasa tunapoelekea kuumaliza mwaka tunapaswa kukaa chini na kutazama ni yapi tumeweza kuyatimiza na yapi yamekwama na kwa sababu zipi. Kwa ujumla ni wakati wa kujitathmini kwa kina na kujiandaa kumalizia yaliyokwama na pengine kupanga mengine mapya.

Yawezekana yapo tuliyoyapanga  lakini kutokana na sababu za maana na zisizo za maana kama uzembe na kukata tamaa basi tumeshindwa kuyatimiza. Si busara kuyatupa mbali na kutafuta mapya, ni vema tujitathmini ni kwa vipi mambo haya hayakutimia ili kuyajua kwa undani madhaifu yetu na kuyafanyia kazi.

Kwa kuuanza mwezi nina neno kwako msomaji! Mambo haya SITA  nimeona ni mazuri tukiyafanyia kazi wakati tunapoelekea kuumaliza mwaka.

Friday, November 27, 2015

UREMBO NA LAURA... TUZUNGUMZIE SCRUB!!


Tuzungumzie SCRUB!
Scrubbing ni njia mojawapo ya kusafisha ngozi kwa mtindo wa kusugua kwa kutumia mikono au vifaa maalumu ukiwa umepaka aina yoyote ya scrub uipendayo na inayoendana na ngozi yako.

Scrubbing ni nzuri na muhimu kwa ngozi aina zote na kwa watu wote, wanawake na wanaume! Mambo ya wanaume kuwa na ngozi mvurugo imechoka kama ngozi ya goti na michunusi hujui hata ubusu wapi it is  so 90’s!.... mwanaume usafi na kujijali bwana anhaaa! Uso unaonekana uso hata  Bae anaona raha kukuweka kwenye wallet jamani  hahahahahaaa!! Joke!

Tukija kwa wanawake, usafi wa uso sio kuung’ang’aniza uso  uwe mweupe. Nope!..kwa hiyo hiyo rangi uliyonayo ufanye uso uwe na rangi moja tulivu. No madoa, no chunusi,  no harara. Uso hata ukifuta vipodozi bado utajiamini kuwa una uso msafiiii!!

Yote haya haya hayaji bila kushughulikia uso wako!!.... Kwenye meza yako kusikosekane Scrub au wale wa mabafu ya peke yao. Scrub isikosekane kando ya sabuni. Ni kitu muhimu hiki sio cha kukosa kwa watu wanaojijali.

Kuna watu ni waoga wa kuscrub kwa kuhofia kuwa kuscrub kunachubua ngozi. Nataka nikutoe hofu kuwa,  Kuscrub hakuchubui ngozi isipokuwa aina ya scrub unayotumia ndio inayoweza kukufanya ujichubue. Ni kama mafuta au losheni, ukitaka ya kukubadilisha rangi yapo na ukitaka ya kukuacha na rangi yako yapo. Chaguo ni lako!

Zipo scrub za kisasa na scrub za kutengeneza nyumbani
Zipo Scrub za uso na scrub za mwili au vyote kwa pamoja

FAIDA ZA KUSCRUB

Sunday, November 22, 2015

LELETI KHUMALO a.k.a SARAFINA



Leleti Khumalo a.k.a SARAFINA


cover la movie ya Sarafina

Wakati nakua moja ya filamu zilizopata kuvuma utotoni mwangu, ilikuwa filamu ya SARAFINA!
Nilipoiona kwa mara ya kwanza, nilitamani kuwa kama Sarafina, nilitamani kuigiza, kuimba na kucheza kama yeye. 

Nilitamani kuwa mdada jasiri kama Sarafina!... nadhani sikuwa peke yangu katika hili,  Sarafina aliwagusa maelfu ya watoto na  vijana katika namna ya pekee na wapo watu wazima ambao filamu hii ilikuwa bora kwao na kila mtu alikuwa na sababu zake za kuipenda filamu ya Sarafina.

Leo nimemkumbuka mhusika mkuu Leleti khumalo almaarufu kama SARAFINA! Nikaamua tu kudodosa ni wapi alipo, ni nini anafanya, na kitu gani kinaendelea maishani mwake. 
Tiririka nami!

TUMJUE SARAFINA KWA KIFUPI….


Alizaliwa March 30 mwaka 1970 katika mji mdogo ujulikanao kama Kwamashu, kaskazini mwa Durban, nchini Afrika kusini. Mugizaji huyu ana asili ya Zulu. Baba yake Sarafina alifariki wakati Sarafina akiwa na miaka mitatu na kumuachia mama yake mzigo wa kuwatunza Sarafina ndugu zake watatu. 

Sunday, November 1, 2015

IJUE HALLOWEEN NI NINI NA IMETOKA WAPI....


Chimbuko la Haloween na Laura Pettie.
Kwanza niwatakie heri ya mwezi mpya wa Novemba! nimerudi kublogua kwa kudonyoa donyoa tu. Tuendelee!!

Ni sherehe inayofanyika usiku wa Oktoba 31 kila mwaka! Unapoitafuta maana halisi ya sherehe hii utakutana na maana nyingi zikiwa na mrengo tofauti tofauti.

Kubwa ni  kuwa chimbuko la Halloween ni sherehe ya kipagani iliyokuwa ikifanywa na watu waitwao wacelts miaka 2000 iliyopita. Wacelts kwa miaka ya leo wanatajwa kuwa ni watu wa Ireland, Scotland, Brittany, Wales na kadhalika kwa kuwa chimbuko la lugha ya celts iko ndani ya mataifa haya.

Saturday, September 12, 2015

UREMBO NA LAURA: .....J4 - JIPENDE, JITHAMINI, JIAMINI, JIVUNIE WEUSI WAKO!!!!


Haya jamani mpo wana kona ya urembo na Laura?

Kama umepata nafasi ya kujumuika nasi hapa, ukaisoma makala hii,  basi tuna kila sababu ya kumshukuru Mwenyezi Mungu!

Leo nataka kuongea na akina dada weusi… weusi tiiii kama mimi ambao bado hawajajikwangua au ndio wanafikiria kujikwangua. Anti wewe ni mzuri tu, …..na weusi wako huo ulionao…..unaweza kuendelea kuwa mzuri hivyo hivyo ulivyo!

Kuna watu wanadhani kuwa mweupe ndio kuwa mzuri, ndio kuwa mrembo, ndio kuwa mlimbwende! HAPANA!!.... si kweli! Hata ukiwa na weusi wako huo huo ulionao bado unaweza kuamua kujiweka katika namna ya kuvutia na ukavutia. Siku zote vile utakavyosimama mbele za watu ndivyo watu watakavyokuchukulia…. Ukijiamini watu  nao watakuamini pia!!

Nimepaka wanja na Lip Balm tu!.... 
usoni hata poda ya kawaida  haijapita

Katika pitapita zangu mitandaoni, hivi karibuni nimegundua kumekuwa na ongezeko la bidhaa za kujichubua. Tena wauzaji wakisifia kabisa kuwa unakuwa mweupee, unatakata, unakuwa na rangi f’lani amazing n.k kana kwamba kuwa mweusi ni laana au uchafu!

Huwa nasikitika sana ninapoona feedback ya bidhaa hizi kwenye picha ambapo  mtu aliyekuwa na weusi wake mzuri tu amekuwa mweupe na ndio anasifiwa kuwa amependeza na amekuwa mzuri.

Uzuri ni vile unavyowaza wewe na unavyojichukulia! Miaka  fulani nikiwa mtoto  mdogo nilikuwa na rafiki yangu aliyekuwa mweupe sana……. Namna alivyojipenda na kujisifia kila mara  kuhusu rangi yake alikaribia kunifanya niamini mimi sikuwa na rangi nzuri hata kidogo hata hivyo kila nilipojitazama niliipenda rangi yangu pia.
Ni mweusi lakini mzuri tu!!

Nilitaka kuanza kuamini weupe ni uzuri mpaka siku moja tukiwa wawili mbele ya watu fulani, mtu mmoja akasema kwa sauti…Laura usije ukajichubua baadaye baki hivyo hivyo una rangi nzuri sana! Rangi adimu! Mweusi anaweza kuwa mweupe lakini mweupe hawezi kuwa mweusi!

Kumsikia mtu akiisifia ngozi yangu kulinipa kujiamini sana, na sasa ndio nikagundua watu wengi wanasikia watu wakisifia weupe wanadhani weupe ndio uzuri  (kama mimi nilivyokuwa nasikia rafiki yangu akijisifia sana)…..kwa kuwa ni nadra kwao kusikia mtu akiwasifia kwa ngozi zao nyeusi (kama mimi nilivyosifiwa)….


Wakati naingia usichana, mama yangu aliniambia kila mara usije ukajichubua baki hivyo hivyo huoni mimi nilivyo mzuri tu (mama yangu ni mweusi pia)… kumsikia mama akisema hivi kulinijaza ujasiri zaidi na leo naweza kumwambia mtu yoyote mweusi BAKI HIVYO HIVYO ULIVYO HUONI MIMI NILIVYO MZURI TU HAHAHAHAAAAA!!
Ni mweusi Ti! na bado ni mzuri tu
na anajikubali mpaka weupe tumemkubali!

Yaani unakuta mtu kajichubua ana sugu balaaa, mwingine mashavu yameungua….mwingine mpaka ndevu zimemtoka… mkorogo umembabua miguu yaani unamtazama unamhurumia maana badala ya kuwa mrembo anakuwa kituko kwelikweli…. Mwingine mweupe kama karatasi yaani mpaka unajiuliza yote haya juu ya nini jamani?

Anyway, unawezaje kutunza  ngozi yako nyeusi na ikavutia?
MAMBO 10 YA KUZINGATIA


1. KUNYWA MAJI MENGI…. Kunywa maji kadiri uwezavyo, Uvivu wa kunywa maji unachakaza ngozi na badala ya kuitibu watu hukimbilia makemikali kuing’arisha kinguvu wakati kumbe maji ni dawa nzuri sana!.... najitahidi lita 1 hadi mbili kila siku! ukiona hayana ladha weka vionjo kama limao kwa mbali au ndimu.

2. Safisha ngozi yako kwa vitu visivyo na kemikali, pendelea vitu natural hata kama ni vya kizungu ila vyenye ingredients natural…. Mfano usoni napenda sabuni ya Liwa, zile natural kabisa au zile zinazofungwa kwenye cover ya kahawia zimeandikwa sandwool soap bee and flower!

3. Tumia vipodozi vinavyoendana na ngozi yako…. Poda, foundation etc viwe vya ngozi yako vitakupa muonekano mzuri sana.

4. Kula chakula bora hususani matunda na mbogamboga usisubiri uandikiwe na daktari

Thursday, September 3, 2015

UREMBO NA LAURA:......LIP SCRUB YA SUKARI NA VASELINE!



Jamani mpooooo!!
Leo tunaongelea utunzaji wa lips zetu ukizingatia kipindi cha baridi ndio hiki.... Haipendezi mwanamke kuwa na lips kaavu, zina mipasuko,  sio soft yaani not smooth not kissable hahahahahaa!

Yaani kuna watu asipopata lipshine dakika tu hutotamani lips zake kwa namna zilizopauka pasuka
au unakuta mdomo una zagamba anafanya kuzing'ata kwa meno, ukiuliza ooh baridi oooh upepo...ooh leo sijapaka lipshine...sasa ndugu yangu hata ukitaka kumkiss babe utakuwa unawahi lipshine kwanza?

Hebu uko!...

Kama unavyotunza uso wako, Lips pia zina matunzo yake tena mepesiiii
Hata dakika tano humalizi!! unabaki na lipsi flani laini ukiongeza na lipshine yako mashallaaaaah! 
Uhitaji nguvu nyingi kuonekana mrembo!
Maaaana

Lips ni kiungo kingine kinachoongeza urembo usoni mwa mwanamke yeyote
Hapa nakuletea namna ya kuscrub lips zako kwa sukari na mafuta ya Vaseline


Lips zangu hizo bila chochote.... na kibaridi hiki na upepo  sijapaka chochooooote kwa masaa kadhaa
ndio hivyo unaona zimeweka michirizi kwa mbaaaali.

FAIDA ZA KUSCRUB LIPS



Snowfall Widget for Blogger


Snowfall Widget for Blogger