Tuesday, August 13, 2013

SINDI....NA LAURA PETTIE (35)

35


Fiona Agapella alimeza mate kwa juhudi zote wakati akijaribu kujiweka sawa kumpokea Mzee Okello. Macho yake yalicheza kulia na kushoto katika namna ya kutafuta utulivu wa nafsi. Akameza tena mate kwa juhudi kiasi cha kufanya koo lake lididimie ndani kwa nguvu kidogo. Alihamanika!

Sunday, August 11, 2013

SINDI.....NA LAURA PETTIE (34)

34

Jua la saa nne asubuhi lilikuwa kali kiasi cha kufanya waliokuwa juani kukunja nyuso zao na  wengine kutafuta vivuli. Pilika pilika za hapa na pale zilishaanza na vurumai za jumatatu zilishika kasi kila kona. Sindi alikuwa uani akifua nguo zake na za Jerry.

Kulikuwa na ukimya mkubwa uani hapo kutokana na wapangaji wengi kutokuwepo asubuhi hiyo. Akiwa ameketi kwenye stuli yake aliendelea kufua taratibu  shati alilokuwa nalo mkononi huku akiimba wimbo alioutoa kwa sauti ya miguno tu na kutikisa kichwa.

Monday, August 5, 2013

SINDI....NA LAURA PETTIE (33)

33


mke wa Mzee Okello, mama wa Pamella alikata simu na kusimama akiwa kama mtu aliyetaka kupayuka kitu kwa sauti ya juu na asiweze. Mdomo ulikuwa aukiwayawaya huku macho yakipepesuka na kutembea huku na kule. Mchecheto!

Akalazimika kujiweka sawa pamoja na mchecheto ule ili binti yake aliyekuwa anaingia pale dukani asigundue hali aliyokuwa nayo.

Thursday, August 1, 2013

MGENI WANGU:....MHADHIRI WA SAUT BW. ROBERT MKOSAMALI

Leo mgeni wangu ni Mhadhiri wa chuo kikuu cha St. Augustine University of Tanzania, bwana Robert Mkosamali. Pasi kupoteza muda karibu utiririke na mtiririko wa maswali  toka kwa Blogger wako Laura Pettie…. Karibu sana!
MHADHIRI WA SAUT
BW. ROBERT MKOSAMALI

Laura Pettie Blog: Kwa maneno matatu tu, unamwelezeaje Robert Mkosamali?
Robert Mkosamali:     Haahaaa! Ninaweza kumwelezea Robert J. Mkosamali kama mtu simple, straight forward na hardworking!

Laura Pettie Blog:  Kitu gani kilikuvutia kujiunga na tasnia ya habari? Is there any motivational story behind?
Robert Mkosamali:      Kitu kilichonivutia kuingia katika tasnia ya habari ni umaskini uliokithiri wa watanzania hasa wale wanaoishi katika mikoa ya pembezoni. Mikoa hii mbali ya kuwa katika hali ngumu ya maisha ilikosa waandishi wa habari ambao wangeweza kuelezea matatizo ya watu walio ndani ya mikoa hiyo na hivyo kuifanya serikali iweze kuchukua hatua.

Nakumbuka miaka ya 1993 kulikuwa na mfumko wa wakimbizi mkoani Kigoma lakini kwa bahati mbaya maisha ya watu wa Kigoma yalionekana kuwa duni kuliko hata yale ya wakimbizi kutokana na mashirika mengi ya kimataifa ........



PERUZI YA ENZI....LORD'S PRAYER SONG IN SARAFINA MOVIE




I LOOOOVE THE DANCE UWIIII..... 
Our father
Which art in heavenHallowed be thy nameThy kingdom comeThy will be done on earthAs it is in heaven
And forgive us our trespassesAs we forgive those who trespass against usAnd lead us not into temptation
But deliver us from evilFor thine is the kingdomAnd the powerAnd the glory, forever, amen

ENJOY!



Snowfall Widget for Blogger


Snowfall Widget for Blogger