Saturday, September 12, 2015

UREMBO NA LAURA: .....J4 - JIPENDE, JITHAMINI, JIAMINI, JIVUNIE WEUSI WAKO!!!!


Haya jamani mpo wana kona ya urembo na Laura?

Kama umepata nafasi ya kujumuika nasi hapa, ukaisoma makala hii,  basi tuna kila sababu ya kumshukuru Mwenyezi Mungu!

Leo nataka kuongea na akina dada weusi… weusi tiiii kama mimi ambao bado hawajajikwangua au ndio wanafikiria kujikwangua. Anti wewe ni mzuri tu, …..na weusi wako huo ulionao…..unaweza kuendelea kuwa mzuri hivyo hivyo ulivyo!

Kuna watu wanadhani kuwa mweupe ndio kuwa mzuri, ndio kuwa mrembo, ndio kuwa mlimbwende! HAPANA!!.... si kweli! Hata ukiwa na weusi wako huo huo ulionao bado unaweza kuamua kujiweka katika namna ya kuvutia na ukavutia. Siku zote vile utakavyosimama mbele za watu ndivyo watu watakavyokuchukulia…. Ukijiamini watu  nao watakuamini pia!!

Nimepaka wanja na Lip Balm tu!.... 
usoni hata poda ya kawaida  haijapita

Katika pitapita zangu mitandaoni, hivi karibuni nimegundua kumekuwa na ongezeko la bidhaa za kujichubua. Tena wauzaji wakisifia kabisa kuwa unakuwa mweupee, unatakata, unakuwa na rangi f’lani amazing n.k kana kwamba kuwa mweusi ni laana au uchafu!

Huwa nasikitika sana ninapoona feedback ya bidhaa hizi kwenye picha ambapo  mtu aliyekuwa na weusi wake mzuri tu amekuwa mweupe na ndio anasifiwa kuwa amependeza na amekuwa mzuri.

Uzuri ni vile unavyowaza wewe na unavyojichukulia! Miaka  fulani nikiwa mtoto  mdogo nilikuwa na rafiki yangu aliyekuwa mweupe sana……. Namna alivyojipenda na kujisifia kila mara  kuhusu rangi yake alikaribia kunifanya niamini mimi sikuwa na rangi nzuri hata kidogo hata hivyo kila nilipojitazama niliipenda rangi yangu pia.
Ni mweusi lakini mzuri tu!!

Nilitaka kuanza kuamini weupe ni uzuri mpaka siku moja tukiwa wawili mbele ya watu fulani, mtu mmoja akasema kwa sauti…Laura usije ukajichubua baadaye baki hivyo hivyo una rangi nzuri sana! Rangi adimu! Mweusi anaweza kuwa mweupe lakini mweupe hawezi kuwa mweusi!

Kumsikia mtu akiisifia ngozi yangu kulinipa kujiamini sana, na sasa ndio nikagundua watu wengi wanasikia watu wakisifia weupe wanadhani weupe ndio uzuri  (kama mimi nilivyokuwa nasikia rafiki yangu akijisifia sana)…..kwa kuwa ni nadra kwao kusikia mtu akiwasifia kwa ngozi zao nyeusi (kama mimi nilivyosifiwa)….


Wakati naingia usichana, mama yangu aliniambia kila mara usije ukajichubua baki hivyo hivyo huoni mimi nilivyo mzuri tu (mama yangu ni mweusi pia)… kumsikia mama akisema hivi kulinijaza ujasiri zaidi na leo naweza kumwambia mtu yoyote mweusi BAKI HIVYO HIVYO ULIVYO HUONI MIMI NILIVYO MZURI TU HAHAHAHAAAAA!!
Ni mweusi Ti! na bado ni mzuri tu
na anajikubali mpaka weupe tumemkubali!

Yaani unakuta mtu kajichubua ana sugu balaaa, mwingine mashavu yameungua….mwingine mpaka ndevu zimemtoka… mkorogo umembabua miguu yaani unamtazama unamhurumia maana badala ya kuwa mrembo anakuwa kituko kwelikweli…. Mwingine mweupe kama karatasi yaani mpaka unajiuliza yote haya juu ya nini jamani?

Anyway, unawezaje kutunza  ngozi yako nyeusi na ikavutia?
MAMBO 10 YA KUZINGATIA


1. KUNYWA MAJI MENGI…. Kunywa maji kadiri uwezavyo, Uvivu wa kunywa maji unachakaza ngozi na badala ya kuitibu watu hukimbilia makemikali kuing’arisha kinguvu wakati kumbe maji ni dawa nzuri sana!.... najitahidi lita 1 hadi mbili kila siku! ukiona hayana ladha weka vionjo kama limao kwa mbali au ndimu.

2. Safisha ngozi yako kwa vitu visivyo na kemikali, pendelea vitu natural hata kama ni vya kizungu ila vyenye ingredients natural…. Mfano usoni napenda sabuni ya Liwa, zile natural kabisa au zile zinazofungwa kwenye cover ya kahawia zimeandikwa sandwool soap bee and flower!

3. Tumia vipodozi vinavyoendana na ngozi yako…. Poda, foundation etc viwe vya ngozi yako vitakupa muonekano mzuri sana.

4. Kula chakula bora hususani matunda na mbogamboga usisubiri uandikiwe na daktari

Thursday, September 3, 2015

UREMBO NA LAURA:......LIP SCRUB YA SUKARI NA VASELINE!



Jamani mpooooo!!
Leo tunaongelea utunzaji wa lips zetu ukizingatia kipindi cha baridi ndio hiki.... Haipendezi mwanamke kuwa na lips kaavu, zina mipasuko,  sio soft yaani not smooth not kissable hahahahahaa!

Yaani kuna watu asipopata lipshine dakika tu hutotamani lips zake kwa namna zilizopauka pasuka
au unakuta mdomo una zagamba anafanya kuzing'ata kwa meno, ukiuliza ooh baridi oooh upepo...ooh leo sijapaka lipshine...sasa ndugu yangu hata ukitaka kumkiss babe utakuwa unawahi lipshine kwanza?

Hebu uko!...

Kama unavyotunza uso wako, Lips pia zina matunzo yake tena mepesiiii
Hata dakika tano humalizi!! unabaki na lipsi flani laini ukiongeza na lipshine yako mashallaaaaah! 
Uhitaji nguvu nyingi kuonekana mrembo!
Maaaana

Lips ni kiungo kingine kinachoongeza urembo usoni mwa mwanamke yeyote
Hapa nakuletea namna ya kuscrub lips zako kwa sukari na mafuta ya Vaseline


Lips zangu hizo bila chochote.... na kibaridi hiki na upepo  sijapaka chochooooote kwa masaa kadhaa
ndio hivyo unaona zimeweka michirizi kwa mbaaaali.

FAIDA ZA KUSCRUB LIPS



Snowfall Widget for Blogger


Snowfall Widget for Blogger