Thursday, October 23, 2014

UREMBO NA LAURA:.... JINSI YA KUPAKA WANJA WA KISASA!!


Nyusi ni sehemu ya urembo wa mwanamke... namna unavyozitengeneza nyusi zako unaweza pata muonekano wa kuvutia au ukawa kichekesho pia. Maana unakutana na mtu nyusi zimekaa rafu mpaka basi au ndio vile zimechongwa kipashkuna mno hahahaha... ama ndio uso unakuwa kama anazomea hivi...mradi hekaheka tu!

Unaweza kumpa pole mtu ukijua ana huzuni kumbe walaaa nyusi zimekupa wrong infomesheni!!

Sasa kabla hatujapakana wanja hebu tuone vitu muhimu vya kuwana navyo au kufanya. Hii ni kwa hohehahe wenzangu wanaotaka kupendeza ila ndio wanaona kuna vitu havikamatiki!... unaweza punguza bajeti ya mboga nyumbani hivi hivi...lakini sio sababu usiwe mrembo jamani. tubanane tu humu humu!

1. Tinda nyusi zako unavyotaka wewe.... binafsi sijui ni mazoea au ni nini...huwa nazichana nyusi kurudi chini... kiasi kwamba sasa hivi zinaota kueleke chini LOL!...so nazitrim mwenyewe kwa chini... vyovyote utakavyotinda au kutindwa mradi ziwe kwenye shepu fulani ya kueleweka

2. Kuwa na vifaa !.... wanja sasa hivi unauzwa kila mahali kuanzia 10,000 mpaka 25,000 kulingana na aina ya wanja, quality, brand etc!
kwa wale wenzangu na mimi ambao we cant just use tarakimu 5 za hela  kwa ajili ya wanja tu... basi nunua wanja wa kawaida tu!

WANJA.... 
unaweza kuwa na huu wa penseli au mwingine
Bei yake hata 5,000 haifiki!






BRASHI
hizi zinauzwa kwa pamoja ila pia unaweza kuta sehemu wanauza moja moja
ukipata moja kati ya hizo ndogo ndogo sio mbaya... 
Bei yake ni kuanzia 10,000-20,000 kwa brush zote kwa moja moja sijui

Brashi zinasaidia kuapply Concealer na kusawazisha pamoja na kuchana nyusi


ukikosa hizo
tafuta hata hii... inaitwa brow brush 

kuna hivi vitana vidogooo... wengine mpaka miswaki wanatumia
hahahahaaa chezea urembo wewe!

Hiki sasa ndio kitakuletea munekano muruaaaa 
na kingo za nyusi zinataonekana vizuri kabisa
hakikisha unachagua concealer inayoelekeana na ngozi yako
hii pichani Bei yake ni 10,000 tu!!...na ni nzuri mnoooo

kuna wakati sijisikii kupaka concealer basi natumia huu wanja hapa
kuupaka taratibu sehemu ninazo paka concealer... halafu nasawazisha kwa kidole
Najua sio kitu prefessional but HUH!...nikishapaka utajua basi hahahahaaaa
uzuri wa wanja ni uhitaji brush za kisasa kiviiiile unatumia kidole kisafi kusawazisha


HATUA hizo hapo




HAPA CHINI NIMEKUWEKEA VIDEO KABISAAAAA... zinaonyesha hatua zote
Ukishindwa useme umeshindwa wapi....
Sio dhambi kuwa mrembo jamani

hii ni ule wanja wa kuchovya.....





Hii ni wanja wako wa kawaida tu!....

NATUMAINI UMEJIFUNZA KITU!!

No comments:

Post a Comment



Snowfall Widget for Blogger


Snowfall Widget for Blogger