Wednesday, October 15, 2014

UREMBO NA LAURA:...NAMNA YA KUJIFUNZA 'GELE'... LEMBA LA KINAIJA!! (PICHA NA VIDEO)

Wengi wetu tumeona namna fasheni inakoelekea!
kufunga gele kumeshika chati sana japo fasheni ilikuwepo kitambo tu.
Leo ngoja nikupe hatua kwa hatua za namna kulifunga GELE 

unaweza kukosea hapa na pale lakini nakuhakikishia ukitulia unaweza kugeuka mtaalamu hivi hivi hahahahaa.... ni wewe tu na utundu wako katika kujifunza

HATUA YA 1

kunja kitambaa chako kwa staili hii... vitambaa vya kufungia gele shurti kiwe kikavu kidogo
kikunje hivi ili ule mwanzo kwa lemba uwe smooth pale mbele.  au pia unaweza kunja ikaribie nusu ya kitambaa chako

HATUA YA 2
linganisha pande zile za mwisho zilingane... yaani ukikiweka kichwani sio huku kurefu kule kufupi
Ni kulingane...kwamba ukianza kufunga mstari unaogawa katikati uwe katikati ya uso...sijui umenielewa heheheee...ualimu wito ujue!



HATUA YA 3
Kiweke kichwani sasa

HATUA YA 4
pishanisha nyuma uko...usifunge butu aah aah pishanisha tu
kaza kidogo  lemba liake sawa
shika uko nyuma au mtu akushikie visiachane
chagua upande mmoja nyooka nao kuja mbele kama hivyo


Leta mpaka hapo nyuma...unaona eeeh 
au umepotea Lol!

HATUA YA 5
kunja zile layers au zile ngazi unazotaka hapo mbele ukiwa bado umeshikilia
unakunja chache tu...utanyoosha zaidi mbele ya safari








MTIRIRIKO WOTE HUU JAMANI
HUJAELEWA TU!.... Leta fimbo khaaaa!! hahahahaaa

HATUA YA 6



HATUA YA 7

HATUA YA 8

HATUA YA 9

Unanyoosha vizuri sasa na kuweka lemba unavyotaka lisimame

HATU YA MWISHO
KAZI IMEISHA!!

HAPA CHINI NAKUWEKEA NA VIDEO 
AMBAYO ITAKURAHISISHIA KAZI KABISAAAAAA
USIPOELEWA KWENYE VIDEO BASI JAMANI


BINAFSI NIMESHAJARIBU NA NIKAJIFUNGA FRESH TU!!
baada ya kuhangaika kidogo lakini ikatoka poa kabisa

next time tukutane kwenye wanja sasa hahahahaaa

panapo majaaliwa!!

SOURCE: BOFYA HAPA

No comments:

Post a Comment



Snowfall Widget for Blogger


Snowfall Widget for Blogger