MWANAMKE NYWELE HASA ZIKIWA ZAKO MWENYEWE HAHAHAHAAA!!
Watu wengi wanadhani kuwa na nywele ndefu za asili, nzuri na
zinazopendeza ni kitu kisichowezekana kwa mwanamke wa kisasa au kuwa na nywele
za asili ni ushamba au kutokuwa mrembo.
Dhana hii ni potofu kabisaaa!... unaweza kuwa na nywele zenye
dawa au nywele bandia za kusukia na bado ukashindwa kuzitunza vizuri na
ukaondoa mvuto wako.
Sikatai kwamba kuna wakati tunahitaji mambo ya ziada
kichwani ili kupendeza lakini pia si vibaya mara kadhaa ukaziachia nywele zako
halisi na ukajiletea muonekano tofauti kabisa!!
Kutunza nywele za asili si kazi ndogo na hasa unapotaka ziwe nywele
zenye afya na zinazovutia. Nywele za asili huleta muonekano wa mwanamke
anayejiamini kwelikweli.
Binafsi nina nywele za asili nikimaanisha hazina dawa kabisa….
ingawa pia huwa ninasukia weaving au kuvaa wig pale ninapotaka muonekano
tofauti lakini mara nyingi kichwa changu huwa huru. Leo ningependa kushea pamoja nanyi njia mojawapo ninayoitumia kutunza
nywele zangu.
1. OSHA NYWELE ZAKO KWA MAJI YA UVUGUVUGU
kwa shampoo
unayotumia… huwa inasaidia kuondoa mafuta mafuta na uchafu unaoshikana na
nywele hasa kwa vile huwa tunamaliza hata wiki mbili pasipo kuosha nywele…. Wengine
wenye nywele za asili huogopa kuziosha mara kwa mara kwa kuhofia zitasinyaa na kuwa fupi
hahahahaaa… hapana ndio unazisafishia njia ziwe ndefu zaidi…. Osha tu mara kwa
mara usiogope…. Ukishaosha suka nywele za uzi zinasaidia kunyoosha au tumia
hand dryer kukaushia…kariakoo kuna mpaka Tsh. 35,000/= tu hilo hand dryer…. Kama unanunua nguo ya elfu 40,000/=
utashindwa kweli kuwa na hiki kifaa??? Sema tu hujakipa kipaumbele lakini ni
kifaa muhimu mwanamke mwenye kuzipenda nywele zake kuwa nacho
Shampoo ya mayai iko smoooooth
2. CHUKUA YAI NA UTOE KIINI PEKEE….
Mimi niliamua kuweka kiini na ute wake… lakini vizuri
ukitumia kiini pekee
3. ONGEZA ASALI VIJIKO VITATU VYA CHAKULA
4. VURUGA MCHANGANYIKO WAKO
5. PAKAA NA UVAE KOFIA YA KUFUNIKA
Unaweza tanguliza mfuko wa plastic ile miyeusi kisha ukavaa
kofia na kufunga lemba kwa juu ili kupata joto zaidi…. Njia hii ni bora kuliko
moto mkali wa saluni.
excuse my nails heheheee!!...
6. KAA NA KOFIA KWA SAA MOJA AU ZAIDI.
7. OSHA NA MAJI YA UVUGU VUGU NA SHAMPOO… zikitakata zikaushe kwa taulo na paka mafuta
ya maji kwanza…. Hii inasaidia kuondoa ukavu wa nywele. Mi natumia Olive oil
for hair
unaweza tumia mafuta ya nazi au yoyote ila ya maji ni mazuri baada ya kuosha
Zikishakauka vizuri…paka mafuta kwenye ngozi na umassage
kichwa kwa dakika kadhaa…utahisi tu ngozi ya kichwa iko fresha kabisaa.
Mafuta ninayotumia kwa sasa
nina aina mbili hii aina ya kwanza...ni mazuri sana kwa kweli
Kupata mafuta kwenye ngozi kunasaidia sana kuondoa ukavu
kwenye kichwa na hata mba si rahisi kukuvamia. Ukipuuzia ukapata mba kuzitibu
mba ni kazi sana na huwa zinazuia ukuaji wa nywele itakiwavyo.
Zilikatika sana pembeni ila now zinarudi faaaasta sana...
Furahia nywele zako na jisikie farahati kurock your natural
hair mara moja moja!!... sio kila siku una fake hair kichwani Lol!!.... jiamini
unaweza kuzilinda na kuzitunza nywele zako mwenyewe na zikawa na mvuto..
Njia hii pia hata walioweka dawa na nywele ni dhaifu
wanaweza kuitumia.
Unaifanya treatment hii mara mbili kwa mwezi inatosha
kabisaaa au hata zaidi kulingana na nafasi yako.
Zipo treatment zingine pia
kama ya kutumia mtindi ambayo ni nzuri mnooo imesaidia kunijazia nywele…. Tukutane tu kila jumatano
hapa uwanjani!!
natumaini umeambulia kitu... Mwanamke nywele shost!!
No comments:
Post a Comment