Ya kwangu hayoooo mkononi
yenye majina ya kizungu hayoooo!!...na mmea wake huo hapo nyuma
Nadhani niihamishie alhamisi hii makala ya Urembo na Laura.
Maana naona Jumatano huwa inakuwa na mambo mengi mno.
Yote kwa yote, natumaini kwa uwezo na kudra za mwenyezi Mungu mu wazima. Tuendelee sasa!
Leo nakuletea Mafuta ya mchaichai. Sidhani kama huufahamu huu
mmea wa mchaichai. Wengi wetu tunautumia kuungia chai. Na Majani yake si mageni
kwetu. Ni mmea wenye harufu na ladha nzuri sana. Wakati mwingine hutumika kama
kiungo kwenye chakula na kwenye mapishi, tumia kumarinate kuku kabla hujamchoma au kumkaanga utapenda na roho yako!
Sasa haya ndio mafuta yake pia. Ni mafuta mazuri mno na kwa mtu
yoyote anayejipenda, haya mafuta ni wajibu kuwa nayo. Ni mafuta yenye matumizi
mengi kwa wakati mmoja
1. KUKUZA NYWELE ZILIZOKATIKA
Kuna wakati unaweza ukajikuta ukitumia hiki na kile tena kwa
gharama kubwa saaaana ili kuzuia kukatika kwa nywele au kuhangaika kuzikuza.
Mafuta ya mchaichai ukiyachanganya na mafuta ya nazi
(coconut oil) au mafuta ya Mzaituni (Olive Oil). Nakuhakikishia ni treatment nzuri
sana ya nywele zako.
Unachotakiwa kufanya ni kumimina mchanganyiko wako kiganjani
na kusugua kichwani kwa muda wa dakika mbili hadi tano. Kisha funika kichwa kwa
kofia yako au funga mfuko wa plastic. Kaa nayo nusu saa hadi saa nzima. Kisha osha
na shampoo yako.
Kwenye shampoo napo wengi tunakosea, tunatumia shampoo za
nywele kavu wakati nywele zenyewe kavu basi ukitoka kuosha unywele umekakamaa
wenyewe tunadhani ndio zimetakata kumbe ndio tunakaribisha kukatika kwa nywele.
Wakati mwingine, ongeza matone kadhaa katika conditioner
yako unapotaka kusteam nywele. Matokeo utaniambia!
2. KUFANYIA MASSAGE
Kuna watu wakisikia massage wanadhani ni kazi moja ngumu
saaana kama kupasua miamba Lol!... massage ni kuchua… inawezekana unajisikia
maumivu mahali, uchovu nk.. mafuta haya ni mazuri kwa shughuli hiyo. Kwa aina
dada wenye waume na wapenzi haya ni moja kati ya mafuta unayopaswa kuwa nayo
ndani mwako.
Usiyapake peke yake yachanganye na mafuta ya Olive au nazi pia yapo mafuta ya massage hii topic nyingine sasa. hapa chukua vijiko
vinne vya mafuta ya nazi, weka kimoja cha mafuta ya Mchaichai
Weekend nzima mara uko vikoba, sijui wapi mara wapi na wapi…hupati
hata siku moja na au muda ukamfanyia mwenzio hata message ya miguu jamani?....
aaah! Shoga, maisha ndio haya haya usimpet pet mzee leo mkiwa na furaha
unangoja mpaka mkishachokana au?...
hivi
ndio vionjo vyenyewe sasa na yalivyo na harufu nzuri…. Wallah asiposhukuru basi
ana roho ya jiwe ukilikalia yallaaah! ukilibeba yallaaah!! Na si yeye tu unaweza
kumuomba hata yeye akufanyie massage!... usione massage centre zinaibuka tu
kama uyoga kuna raha uko weee hahahahaaa!
Na uzuri wake ni kwamba husaidia kuondoa maumivu ya misuli,
kwa hili hata mimi shahidi ya haya mafuta. baada kukaa kwenye foleni wiki nzima...kupandia daladala dirishani... kukaa ofisini masaa... kusimama kituoni masaa...aaaah! massage muhimu bwanaaa!
3. KWENYE MAMBO YETU YALE
Hapa nashindwa kufunga vizuri maana ni Public lakini
mchaichai ni moja ya mafuta ambayo huamsha ashki, huondoa harufu mbaya hasa kipindi umemaliza maliza kusindikiza wageni wenye makoti mekundu, namna ya kufanya siwezi andika hapa hahahahahaaaa.... haya na huku
chini pia huponya fangasi na kurutu kurutu vamizi za hapa na pale.
Hata ukishafagia
barazani kwako ili kuepuka vipele na nini na nini unachovya pamba kwenye
mafuta, kidogo tu kisha unasugulia
sehemu fagio lilikopita. Unabaki msafiiii, unanukiaaa, mlainiiii yaani
utajipenda mpaka ushangae.
4. KWENYE NGOZI.
Humu yamo pia… una losheni yako au cream yako unapaka mwili,
basi unafanya kumix hivi kidogo tu. Kama umewahi kusikia kitu kinaitwa moisturizer
kwenye vipodozi basi mafuta ya mchaichai ni moisturizer ya asili kabisaaa. Na hayatoi
jasho.
AU Maji ya uvuguvugu, dondoshea matone ya mafuta halafu loweka miguu yako humo dakika 45. Kisha sugua
gaga lako sasa. Kama una harufu mbaya, ama fangasi, au magaga ndio yanaanza
lazima utoke softiiii!...kama ndio mzee wako aiii huwezi pata kashfa babe yake
anuka miguu ati hahahaaa!
5. KWENYE MAGONJWA
Mapunye, fangasi nk. Mafuta ya mchaichai ni dawa. kuna wakati
watoyo wanakuja na mapunye toka shule uko, wakati mwingine minyoo tu inakuletea
fangasi au ndio mambo ya kujaribisha mitumba… unatoka na ugonjwa wa ngozi hapo au utangotango….
Basi hii Unasugua kwenye tatizo kila siku, na baada ya wiki lazima uwe umepona
labda kama tatizo ni kubwa la kuhitaji vipimo vikubwa. Lakini hizi fangasi za
kawaida tu…. Hii mwisho wa matatizo!
MATUMIZI YAKE NI MENGI MNO
HAYA NI MACHACHE TU!
NB: Cha kukumbuka sasa ni kwamba
haya mafuta usipopewa feki, hayo niliyokwambia hapo juu yanatekelezeka na utagundua
unayahitaji tu hapa na pale.
Kikubwa kumbuka
ni makali kidogo hivyo kuna watu wachache ambao wana ngozi sensitive yaani wale
ambao akipaka kitu chochote kigeni rashes zinamtoka…
kama wewe ni mmoja wapo: fanya hivi chukua paka
shingoni, mkononi, au kwenye hairline (mstari wa mbele wa nywele) kaa nayo kwa
saa 14…unaweza paka asb jioni ujicheki…kama hakuna chochote kilichotokea basi
na ngozi poa na utayatumia bila shida yoyote
NATUMAINI NIMEKUONGEZEA UJUZI
FULANI!!
yaani we dada jamani unaelezea vizuriiiii mpaka nimecheka. asante sana nimepata kitu cha maana kweli. niliyaona mahari nikawa sijui matumizi yake
ReplyDeleteWe call it miracle oil!!! Thank you for sharing.
ReplyDeleteLita moja ni tsh ngapi
ReplyDeleteAsante Sana kwa kweli nimepata faida kubwa ya mafuta ya mchaichai Mungu akubariki.
ReplyDeleteNasikia yanaondoa visunzua ni kweli?
ReplyDeleteSamahani kipenz mafuta ya mchai chai nayapataje
ReplyDelete