Wednesday, January 14, 2015

MEKONI....UGALI, DAGAA MCHELE ZA NAZI KWA TEMBELE



Kama ilivyo ada…leo tena tuko mekoni. Na wala tusipoteze muda.
Mlo wetu wa leo ni UGALI, DAGAA  MCHELE  za nazi na TEMBELE. Hapo penye ugali unaweza ukaweka wali au hata ndizi za kupika wewe tu upendacho.

TUANDAE UGALI…
Japo najua wengi tunajua kuusonga ugali ila huwezi jua labda wapo wasiojua kuusonga ugali. Acha tuelekezane tu.

-          Bandika sufuria lako la maji ya ugali yachemke

-          Koroga unga mimina kwenye maji…usikoroge mwepesi sana wala mzito sana

-          Sasa uji uchemke, wengine stage hii wanaisha tu basi para para nguna hilo mezani
-          Uji ukichemka vizuri hata ugali utatoka poa

-          Anza kusonga sasa polepole ukiongeza unga… kama sio mjita au msukuma (hahahahaaaa samahani lakini) lazima utataka ugali mwepesi hivyo usimimine unga mwiiingi utashaa!

-          Songa ugali wako mpaka uone unga umepotea na ugali umeshikamana au nati nati sana
-          Usiwaishe kutoa jamani…songa hata dakika tano hivi huku ukiuacha acha jikoni uive. Aibu ukitenga ugali mbichi mezani au ukute unakula mbichi kila siku ila hujui tu
-          Mwisho ipua na utenge kwenye chombo chako.

-          Wengine hunyunyuzia chumvi wakati wa kukoroga uji wa ugali ili kuupa ladha kidogo… kama nakuona ulivyoshangaa hahahahaa
-          Ugali tayari


TUANDAE DAGAA MCHELE

Mara nyingi hawa huwa tunawanunu wameshakaangwa
Wanauzwa kwa mafungu, ni dagaa fulani wana nyama nyama na ukubwa wake unazidi dagaa wale wa mwanza.... 
sehemu wanazouza samaki wa kukaanga mara nyingi utakuta pia wanauza hawa dagaa mchele.

MAHITAJI
- Kitunguu
- Kitunguu swaumu
- karoti
-nyanya za kawaida
-Nyanya ya kopo/ pakti
- binzari masala/ royco/ curry powder/ Onga  au chochote unachotumia
- pilipili manga
- Iliki
- Nazi
-Chumvi
- Hoho...hii ni ukipenda
na dagaa zako


Jinsi ya kupika
- tia sufuria yako kwenye moto, weka mafuta kidogo... kuna watu wanadhani kupika vizuri ni kujaza mafuta
weka kidogo ya kukaangia vitunguu...binafsi sipendi chakula chenye mafuta mengi

- weka vitunguu vyako sasa...geuza geuza usisubiri vikabadilika saana
- weka karoti zako....inapendeza ukikata ndefu ndefu
- geuza geuza hapo kisha tia nyanya kisha hoho
- weka kitunguu swaumu.... tuelewane kwanza kitunguu swaumu mimi huwa natia baada ya kuweka nyanya  maana sipendi viungue kwenye mafuta nakosa ile ladha yake na harufu yake tulivu

- weka nyanya ya kopo kidogo inaongeza uzito wa mchuzi na ladha
- haya sasa geuza wakati unatia viungo vyako kama ni Royco na binzari masala, iliki na hiyo pilipili manga.
- usiweke manga nyingi kama si mpenda ladha ya pilipili...weka kidogo tu...ila usiache kuweka bwana haiwashi pilipili mbuzi anhaaaa!

- hivi viungo ulivyoweka vitafanya mkorogo wako wa nyanya uwe mzito 
-usiharakie kuweka maji.... ponda ponda nyanya zilainike labda uwe umesaga

- pesti ukishikana kabisa yaani nyanya unaona ziko rojoooo weka maji kiasi kupata chuzi zito kama roast hivi
- weka dagaa zako sasa na uzigeuzie humo

Funika dakika mbili tatu... kama unatumia gesi itakuwa inachemka
- usisahau chumvi mwenzangu!

Likichemka ongeza nazi pole pole huku ukigeuza kwa kiasi unachotaka.
-kama ni mchuzi mwingi au roast flani hv wewe tu na uamuzi wako na idadi ya watu wako
Au kama una watoto basi mchuzi lazima mwenzangu si unawajua watoto kwa mchuzi....otherwise weka tui lako zito utengeneze roast tu.

- igeuze tu mpaka utaona inachemka...dakika mbili zinatosha
zima jiko ila endelea kugeuza geuza mpaka utaonamchuzi umetulia uko softiii

- Dagaa zako tayari

TUMALIZIE TEMBELE

- kuna watu tembele wanaiona kama mboga duni saaana
Wanakosa uhondo kwa kweli..
Ukishachambua vizuri

- Osha tembele lako...wengine wanalianika juani... mie huwa naenda nalo moja kwa moja tu bila kuanika
- Tia sufuria motoni
- weka mafuta ya kutosha...linataka mafuta hili mwenzangu la sivyo utalichukia
ukalalamike matembele so mazuri kumbe upishi wako duni!
- tia kitunguu chako
- geuza geuza kisha tia nyanya zako na ya pakti kidogo
- weka royco kidogo
- nyanya zikiiva weka tembele lako

-Ligeuze hapo mpaka linywee
weka maji kidogo mnooooo na kisha funika
- sio unafunika unatoka unaenda kubadili chaneli za TV....utaunguza!
- unakuwa hapo hapo unalichungulia kama limeiva
- ukiona bado unaongeza tena maji kidogo...kidogo

usimimine pwaa litadoda!
utaona tu linanywea zaidi ndio linaiva
mwisho mwisho kamulia kipande cha ndimu au limao
- geuza dakika mbili tatu

tayari!


Weka mezani....  kama hutakipenda hiki chakula
Baaasi mwenzangu nimekushindwa...wazungu wamejilamba vidole iwe wewe sasa hahahahahaaa

natumaini umemeza hata mate

MCHANA MWEMA!!

No comments:

Post a Comment



Snowfall Widget for Blogger


Snowfall Widget for Blogger