Thursday, September 23, 2010

USILIE SANA...KILA JAMBO LINA SABABU....

Mambo yamekuwa mengi na ndio maana sipati ule wasaa ufaao katika kukumbushana hapa na pale. lakini hii si kwamba ndio nimeitupa hii blog yangu hapana. Ni kama hivi leo nimerudi tena...

Jamani katika maisha kuna wakati unaweza kupitia machungu ya aina yake yanayoweza kukufanya uanze kuhisi aidha una mikosi na kama ndio wale wa kuamini vya mizizi unaweza kumaliza waganga wa mtaa na mkoa kama si nchi ukihangaika na mavumba na mafusho na usipate ahueni hata ya kudanganyia.

wengine ndio pa kumkufuru Mungu kuwa hayupo, na wengine wenye imani zao ndio pa kushukuru kwa yaliyotokea.

Kwangu mimi, kila jambo hutokea kwa sababu, na unapoona matatizo yanakukabili jua Mwenyezi Mungu mwenye rehema zote anajua shoda zako na anajua unaweza kuubeba huo mzigo.
Usilie sana!

Ipo njia, ipo nafasi, yupo mtu, anayeweza kukuinua. Jitokeze na ulikabili tatizo lako kwa kadri ya uwezo wako. ukifumba masikio pale yanapokuja ya kukurudisha nyuma, na kufungua moyo na masikio pale yanapokuja ya kukuinua!

Adui yako ni wewe mwenyewe, hakuna atakayeweza kukuangusha bila kumruhusu akuangushe.

Futa machozi, mwambie Mungu Asante nae atakutua Mzigo alionao


Alamsiki!

Tuesday, August 17, 2010

Ni kukumbushana tu....!


Wengi wetu tunajaribu kwa kadiri tunavyoweza kuyatafuta maisha, kupambana nayo kwa kila hali ili mradi tu mwisho wa siku ukamate kitu kinachoitwa PESA...

Ni halali ya binadamu kuhaingikia maisha lakini halali hii isihalalishe kusahau utu wetu... katika mambo kama misiba, sherehe au mikusanyiko yoyote yenye nia ya kukutanisha watu kiuungwana!

Utatengwa!
Maisha ni watu ndugu yangu... pesa ni chachandu tu ya kuongeza utamu wa maisha

Monday, May 3, 2010

Haya Yote ni Maisha!

Katika safari ya maisha kila mmoja ana majaaliwa yake hapa duniani,tumezidiana urefu, uzuri, mali na vyeo lakini kipo kimoja kubwa kinachotuweka pamoja, kitu hiki ndicho hasa kinachotufanya sisi tuitwe binadamu bila yale yooote yanayotutofautisha.
Si masikini si tajiri, si mzuri si mbaya si mweusi si mweupe wote kwa pamoja tunamtumainia MUNGU MMOJA!!
Wakati wewe mwenyezi mungu akikujaalia afya na furaha kuna wengine wapo katika huzuni na mateso makali, ni wajibu wetu kuwakumbuka, kuwasaidia hata kwa kile kidogo alichokubariki mwenyezi mungu!
Umesaidia wangapi?
FUNGUA MKONO WAKO UMSAIDIE MWENZAKO...!
PAMOJA!


Snowfall Widget for Blogger


Snowfall Widget for Blogger