Wednesday, September 17, 2014

UREMBO NA LAURA.... TREATMENT YANGU YA USO MARA MBILI KWA WIKI

MWANAMKE RECEPTION!!... shepu hata mbuzi anayo Lol!
Haya wasomaji wangu za siku tele?.... maana kuonekana humu imekuwa kama kuwinda mkia wa kobe…nadra nadra lakini ndio vile mishughuliko na mihangaiko mkono uende kinywani kunafanya nashindwa kuwa active inavyotakiwa… Mniwie radhi tu na kama hivi siku nikitulia basi tunapeana ya hapa na pale. Sasa kila jumatano tutapeana vijitip vya urembo vya hapa na pale.

Nilishasema na narudia kusema USO bwana ndio mapokezi yako… hasa kwetu sisi wanawake. Haijalishi umeolewa au lah! Haijalishi u kigoli au kikongwe… kupendeza uso ni haki ya kila mtu aliyehai…

Leo nitakuletea mambo ninayoyafanya mimi kuuweka uso wangu katika hali ya usafi…hali ya kupendeza hali ya kung’aa… yaani uso ukiwa shwari unakuwa na confidence f’lani mwenyewe kuliko mwenye uso wenye makorokoro.
Kujichubua sio kupendeza wala weupe sio kupendeza… unaweza baki na rangi yako na bado ukapendeza sana tu. Mwanzo nilikupa hints za jumla jumla tu leo nakupa hatua kwa hatua…twende kazi!!
1. OSHA USO KWA  MAJI SAFI NA SABUNI.
Mimi natumia sabuni ya Liwa kuoshea uso… ni sabuni nzuri sana aisee, inazuia harara za ovyoovyo na inapunguza mafuta kwenye ngozi kwa wenye chunusi hii inawafaa sana…. Baada ya kuosha nakausha uso kwa taulo safi sio tena unajifutia khanga yoyote uliyotundika hapo chumbani… utatoa uchafu na kuingiza uchafu hapo!
hapa sijapata chochote ni nimetoka kuosha uso na kuufuta.
Sabuni ya Liwa ninayotumia

2. Nina mchanganyiko wa liwa na manjano… nachukua kidogo nachanganya na maji au wakati mwingine nachanganya na maji ya liwa. Iwe uji mzito sio majimaji… hapana!... ni kidogo tu. Paka usoni taratibu kwa kusambaza kama unazungusha maduara hivi. Paka uso mzima
Huu ndio mchanganyiko wenyewe... 
unaweza chukua manjano na unga wa liwa unamix mwenyewe

Uji mzito mzito.. hapo nishaukwangua nikapaka

3. Naacha kwa nusu saa tu… au hata dakika 15 hivi zinatosha mradi ikaukie usoni…. Kisha taratibu sugua uso kuondoa yale makapi kapi yaliyoganda. Sugua taratibu sio paruuu paruuu…ngozi ya uso iko sensitive na ikibidi chovya mkono kwenye maji kisha chua taratibu kama dakika moja hivi… ukizunguka uso mzima
Haya mchanganyiko huo usoni
nikatulia nusu saa nzima... nasoma gazeti... naperuzi hapa na pale

4. Uso utabaki na mlaini na ule unjano njano… sasa osha kwa sabuni yako tena kuondoa kabia ule mchanganyiko. Utasikia tu uso unabaki msafi kwelikweli.

Baada ya kusugua takataka zote

5. ukishakausha uso…chukua pamba chovya kwenye cleanser yako… yangu mimi ndio haya maji ya liwa. Nayatum ia kusafishia uso badala ya cleanser zile za kizungu. Sikudanganyi ni nzuri mno aisee.  Safisha mpaka pamba inabaki nyeupeee
Picha ya maji ya liwa.

Haya ndio maji ya Liwa.... nachanganyia na manjano na liwa
na pia nasafishia uso


Mwisho…. Kama unapaka lotion paka kidogo sana saaana… kama ni cream yako paka kidogo sana au unaweza usipake kitu kama upo tu nyumbani na huendi kokote. Nashauri ufanye hivi ukiwa huna safari ili ngozi ipumue kidogo kama masaa mawili hivi ndio uukandike poda. Mimi natumia hii cocoa butter. Napaka kidogo sana kwa vile uso wangu una mafuta.
Hii ndio nabrashia usoni... ni unapaka kidogo nasisitiza kidogo mno
hasa kwenye nyuso za mafuto... hii ni kama unataka kupaka poda usoni ili utoke
kama uso hautaki mafuta kabisaa basi usipake kitu! na kama ni usiku usipake kitu kabisaa
Baada ya shughuli nzima
Uso ukiwa muruaaaaa!! 

Hii treatment naifanya  mara mbili tu ila unaweza ongeza ukipenda ni wewe tu… urembo unataka juhudi, usafi, uvumilivu hasa kwa matumizi ya vitu vya asili lakini nakuhakikishia uso ukibadilishwa na vitu vya asili hutajuta wallah…. Ni kitu permanent uso hauwezi kuvamiwa na sugu wala chunusi za ajabu ajabu. Na treatment kama hizi hata wale wa wageni wa kila mwezi wakija hawauchafui uso kiasi uuchukie ni kipele kimoja kimoja tena kidooogo sana sio nundu hiyoooo!

Natumaini umepata kimoja cha kukusaidia hapo… upende uso wako jamani… utunze kwa kadri unavyoweza ndio mapokezi hayo mwaya !!! ukishafanya hivi kumbuka zile sheria nilizokupa mwanzo...utakuwa na uso msafi utashangaa mwenyewe!!





2 comments:

  1. mama nashukuru kwa maarifa, lakini hizo manjano na liwa huku kwetu sijaziona kabisaaa,naweza kutumia nini mbadala?

    ReplyDelete
  2. uko maeneo gani mpendwa! Unaweza kutumiwa kokote ulipo na hao wauzaji au nenda sokoni ulizia manjano utapata tu... kama meshawahi sikia binzari ya manjano ndio hiyo... tafuta unga wa dengu pia ni mzuri ukikukubali. Uko mkoa gani?

    ReplyDelete



Snowfall Widget for Blogger


Snowfall Widget for Blogger