Thursday, January 22, 2015

UREMBO NA LAURA... PEDICURE AT HOME !!


Kama nilivyoahidi kuleta njia ya namna ya kusafisha miguu nyumbani na ndio hii hapa nakuletea leo
Wapo wanaokwenda saluni kuosha miguu na wapo ambao kwa namna moja ama nyingine wanashindwa kwenda kupanga foleni saluni kusubiri kuosha miguu.

Leo nakuletea njia ya kuosha miguu nyumbani mara mbili kwa mwezi, kwamba unaosha wiki hii unasubiri wiki nyingine inapita... kisha unaosha tena kwa staili hii.

Hii si kwa wanawake tu, hata wanaume wanaweza kufanyiwa haya na wenzi wao kama sehemu ya kuimarisha mahusiano yao. Usione tabu kumfanyia mwenzio pedicure home mbona sio kazi sana!

Sasa hebu tuangalie nini cha kufanya

1. ONDOA RANGI KWENYE KUCHA ZAKO...



Nail polish remover na pamba vinahusika hapa. ondoa rangi yote uache kucha chako zikiwa safi. Kama unazikata kucha zako zikate na ulinganishe kulingana na urefu unaotaka. ondoa vinyama nyama kando kando ya kucha kwa kifaa maalumu nadhani unavijua au wembe safi na mpya...toa uchafu chini ya kucha na kama kucha zimefubaa sana zisugue na ule msasa

Wednesday, January 21, 2015

MEKONI.... MAPISHI YA SOSEJI NA MAYAI




Huu ni mlo wa chap chap...

MAHITAJI
Soseji idadi unayotaka
mayai 2/3
nyanya 1
kitunguu 1
majani ya mint kiasi
pilipili manga
hoho nusu
chumvi

JINSI YA KUPIKA
1. Pasua mayai yako kwenye bakuli safi yachanganye

2. kwenye hilo hilo bakuli  kata kata soseji zako saizi unayopenda

3. katia hoho kidogo

4. katia vitunguu vyembamba

5. katia nyanya ziepuke mbegu za nyanya

6. nyunyuzia pilipili manga na chumvi

7. dondoshe vijani vichache vya mint

8. vichanganye kwa pamoja

9. weka kikaangio jikoni na mafuta kiasi

10.  mimina mchanganyiko wako

11. ukaushe vizuuuri kama unavyokausha yai

MLO WAKO TAYARI!!

UKIPENDA 
unaweza ukakata kipande ukakiweka katikati ya vipande viwili vya mkate
sukumia na chai ya rangi ya viungo, juisi, chai ya maziwa, soda...etc


TUONANE JUMA LIJALO!!




Thursday, January 15, 2015

UREMBO NA LAURA....USAFI WA MWILI WA MWANAMKE....




Kama ilivyokuwa mwaka jana kila alhamisi tuna makala ya urembo hapa… na kabla ya yote hebu tumshukuru Mungu kwa wema wake kwanza kwa kutuumba wanawake na kisha akatuweka hai mpaka sasa halafu akatupa nafasi ya kusoma hata hii makala unayoisoma.

Nakuita mwanamke!...nakuita binti…nakuita hapa tuelezane machache kuhusu usafi wetu kwa ujumla. Wanasema usafi ni hulka ya mtu ni kweli lakini ukiamua kuwa msafi hushindwi…na kwanini ushindwe! Nitagusia mambo 15 ambayo kuhusu usafi wa miili yetu maana urembo na usafi ni kama kobe na jumba lake haviachani!

Hebu tuanze…

1. USAFI WA NYWELE

Utatia aibu kama utasukia weaving lako wiki mbili hadi nne na usiwe umepitisha maji kichwani… haijalishi uko wapi ila kukaa na nywele wiki nne pasi kuosha ni UCHAFU bibi!!... toa nywele bandia hizo…au fumua mzigo wa yebo yebo huo uoshe kichwa kama huwezi kuosha zikiwa kichwani…watu wanaweza wasikwambie ukweli ila pembeni ukapewa cheo cha yule dada mchafu maana huwa zinanuuuuka acha!!


Wednesday, January 14, 2015

HEBU PITA ZAWADI SALON... HAPO KINONDONI MANYANYA


Haya wenzangu wapenda mambo mazuri mazuri kwa gharama nafuu kabisaaaa na unapata huduma stahiki na hela yako nakuletea hii sehemu ambayo ukikosa kwenda na ukalalamika urembo gharama basi hujitendei haki mwenzangu.

ZAWADI SALON...ipo kinondoni manyanya barabarani kabisaaaa yaani ukishuka kituoni uhitaji bodaboda wala bajaji na kama una usafiri wako basi ni kutoka nje ya njia kuu na utakuwa umefika...unaona raha hiyoooo!!

Kama unatokea Moroko basi unamwambia konda akushusha kituo cha manyanya....unavuka barabara utaona yadi ya magari mwisho wa ukuta wa yadi utaona frame zimepangana....fremu ya pili ndio ilipo Zawadi Salon!

Kama unatokea kariakoo badi upande huo huo ndio ilipo Saluni....


KWANINI UCHAGUE ZAWADI SALON....
1. Mmiliki ndio mhudumu wako akisaidiana na mtu mwingine hivyo tegemea huduma safi kabisaaa maana bosi ndio anakuhudumia.

2. Dada ni mkarimu mnoooo...yaani anavyokupokea utajisikia huru sana...sio unaingia saluni wahudumu wanakunyali na senti zako kama wanakuhudumia bure!...na biashara huria hii ya nini manyanyaso kwa hela yako!

3. Bei zako ni affordable mnoooo kulingana na huduma zake.... rasta za elfu 25 au 40 unajiangalia unatamani kumuongezea pesa!

4. Ukimpigia simu kuuliza kitu au kuweka miadi unampata haraka sana na atakujibu vizuri...hana nyodo dada wa watu.... yupo kwa ajili yako.... tena ukimtafuta mwambie ulipotoa contact zake ni  kwenye blog ya Laura Pettie....na punguzo utapata!

5. Rasta, weaving zipo hapo hapo saluni kwa bei nafuu mnoooo.... maana anajua anahudumia pia watu wa kipato cha kati....unaenda na pesa zako unachagua rasta zako au weaving... unalipia unasukwa!

6. Ana mkono mwepesi sana!...yeye na mhudumu wake.... unakaa kitini hata sugu za  makalio hazijaanza kuuma mwenzio yuko robo tatu ya kichwa!

7. Yupo wazi siku zote.... unaweza ukapigia ukaongea naye kuhusu kuweka miadi ya kusuka kama utamuhitaji akufuate basi utaongezea gharama kidogo.... na anakuhudumia!!

Mwisho!..... anapamba MAHARUSI... anapamba hata watu wenye mitoko ya hapa na pale.... inahusu kwenda harusini na uso ule ule unaokwenda nao kazini...mmmmmh! kwa ubahili gani sasa unashindwa kupendeza siku moja moja kwa maisha haya haya bwanaaaa!...bei zake zinashikika kabisa kama mimi naziweza wewe utashindwa nini jamani hahahahaaa... hebu tumuunge mwanamke mwenzetu!!


Tena unakuwa huru kumwambia hapa hivi hapa vile na anakusikiliza vizuri... unatoka saluni roho kwatuuuuu na umependeza!!


BAADHI YA KAZI ZAKE NDIO HIZI......

HEBU ZICHEKI....!


MEKONI....UGALI, DAGAA MCHELE ZA NAZI KWA TEMBELE



Kama ilivyo ada…leo tena tuko mekoni. Na wala tusipoteze muda.
Mlo wetu wa leo ni UGALI, DAGAA  MCHELE  za nazi na TEMBELE. Hapo penye ugali unaweza ukaweka wali au hata ndizi za kupika wewe tu upendacho.

TUANDAE UGALI…
Japo najua wengi tunajua kuusonga ugali ila huwezi jua labda wapo wasiojua kuusonga ugali. Acha tuelekezane tu.

-          Bandika sufuria lako la maji ya ugali yachemke

-          Koroga unga mimina kwenye maji…usikoroge mwepesi sana wala mzito sana

-          Sasa uji uchemke, wengine stage hii wanaisha tu basi para para nguna hilo mezani
-          Uji ukichemka vizuri hata ugali utatoka poa

-          Anza kusonga sasa polepole ukiongeza unga… kama sio mjita au msukuma (hahahahaaaa samahani lakini) lazima utataka ugali mwepesi hivyo usimimine unga mwiiingi utashaa!

-          Songa ugali wako mpaka uone unga umepotea na ugali umeshikamana au nati nati sana
-          Usiwaishe kutoa jamani…songa hata dakika tano hivi huku ukiuacha acha jikoni uive. Aibu ukitenga ugali mbichi mezani au ukute unakula mbichi kila siku ila hujui tu
-          Mwisho ipua na utenge kwenye chombo chako.

-          Wengine hunyunyuzia chumvi wakati wa kukoroga uji wa ugali ili kuupa ladha kidogo… kama nakuona ulivyoshangaa hahahahaa
-          Ugali tayari


TUANDAE DAGAA MCHELE

Mara nyingi hawa huwa tunawanunu wameshakaangwa
Wanauzwa kwa mafungu, ni dagaa fulani wana nyama nyama na ukubwa wake unazidi dagaa wale wa mwanza.... 
sehemu wanazouza samaki wa kukaanga mara nyingi utakuta pia wanauza hawa dagaa mchele.

MAHITAJI
- Kitunguu
- Kitunguu swaumu
- karoti
-nyanya za kawaida
-Nyanya ya kopo/ pakti
- binzari masala/ royco/ curry powder/ Onga  au chochote unachotumia
- pilipili manga
- Iliki
- Nazi
-Chumvi
- Hoho...hii ni ukipenda
na dagaa zako

Friday, January 9, 2015

DARASA...TUJIFUNZE KIFARANSA - 2

Ijumaa nyingine tena...tunarudi darasani tena au sio!

Kwanza Bonjour!.... itikia......
Comment ca va?.... itikia....

Haahahaaa i hope hujasahau kitu Lol...
haya leo tujifunze namba....
kama somo lolote lile, kifaransa nacho kinahitaji wepesi wa kukariri...huwezi jua lugha bila kukariri baadhi ya mambo. kuna baadhi ya watu hujiaminisha kuwa ni wazee sasa au watu wazima na hakuna haja ya kujifunza kitu kipya.... hii si sahihi hata kidogo!

una kila haki ya kujua mambo mapya na ukayafurahia bila kujali umri wako. umri usikuzuie kuichangamsha akili yako jamani na kukuza upeo wako... utajisikiaje anakuja mtu anayeongea kifaransa ofisini kwako angalau unaweza kumwambia Bonjour Monsieur naye akajibu bonjour...ukamjulia hali akasema ca va bien!.... urafiki unaanzia hapo na kuna maksi unajiongezea kwa kujua salamu za mataifa mbalimbali... usibaki nyuma nyuma saaana LOL!


kukurahisishia kazi
Hili hapa chini ni jedwali la namba na namba zinavyoandikwa na kutamkwa
0
zéro
[zay-ro]
1
un
[uh]
2
deux
[duhr]
3
trois
[twa]
4
quatre
[katr]
5
cinq
[sank]
6
six
[sees]
7
sept
[set]
8
huit
[weet]
9
neuf
[nurf]
10
dix
[dees]
11
onze
[onz]
12
douze
[dooz]
13
treize
[trez]
14
quatorze
[katorz]
15
quinze
[kanz]
16
seize
[sez]
17
dix-sept
[dee-set]
18
dix-huit
[dees-weet]
19
dix-neuf
[dees-nurf]
20
vingt
[van]
21
vingt et un
[vant-ay-uh]
22
vingt-deux
[van-duhr]
23
vingt-trois
[van-twa]
24
vingt-quatre
[van-katr]
25
vingt-cinq
[van-sank]
26
vingt-six
[van-sees]
27
vingt-sept
[van-set]
28
vingt-huit
[van-weet]
29
vingt-neuf
[van-nurf]
30
trente
[tront]
31
Trente et un
[tront ay-uh]
32
Trente-deux
[tront-durh)
33
Trente-trois
[tront-twa)
34
Trente-quatre
[tront-katr)
35
Trente-cinq
[tront-sank)
36
Trente-six
[tront-sees)
37
Trente-sept
[tront-set)
38
Trente-huit
[tront-weet)
39
Trente-neuf
[tront-nurf)
40
quarante
[karont]
41
quarante et un
[karont-ay-uh]
42
quarante-deux
[karont-deux]
43
quarante-trois
[karont-twa]
44
quarante-quatre
[karont-katr]
45
quarante-cinq
[karont-sank]
46
quarante-six
[karont-sees]
47
quarante-sept
[karont-set]
48
quarante-huit
[karont-weet]
49
quarante-neuf
[karont-nurf]
50
cinquante
[sank-ont]
51
cinquante et un
[sank-ont-ay-uh]
52
cinquante-deux
[sank-ont-deux]
53
cinquante-trois
[sank-ont-twa]
54
cinquante-quatre
[sank-ont-katr]
55
cinquante-cinq
[sank-ont-sank]
56
cinquante-six
[sank-ont-sees]
57
cinquante-sept
[sank-ont-set]
58
cinquante-huit
[sank-ont-weet]
59
cinquante-neuf
[sank-ont-nurf]
60
soixante
[swa-sont]
61
soixante et un
[swa-sont-ay-un]
62
soixante-deux
[swa-sont-dur]
63
soixante-trois
[swa-sont-twa]
64
soixante-quatre
[swa-sont-katr]
65
soixante-cinq
[swa-sont-sank]
66
soixante-six
[swa-sont-sees]
67
soixante-sept
[swa-sont-set]
68
soixante-huit
[swa-sont-weet]
69
soixante-neuf
[swa-sont-nurf]
70
soixante-dix
[swa-sont-dees]
71
soixante-et-onze
[swa-sont-ay-onz]
72
soixante-douze
[swa-sont-dooz]
73
soixante-treize
[swa-sont-trez]
74
soixante-quatorze
[swa-sont-katorz]
75
soixante-quinze
[swa-sont-kanz]
76
soixante-seize
[swa-sont-sez]
77
soixante-dix-sept
[swa-sont-dee-set]
78
soixante-dix-huit
[swa-sont-dees-weet]
79
soixante-dix-neuf
[swa-sont-dees-nurf]
80
quatre-vingts
[kat-ra-van]
81
quatre-vingt-un
[kat-ra-vant-uh]
82
quatre-vingt-deux
[kat-ra-van-dur]
83
quatre-vingt-trois
[kat-ra-van-twa]
84
quatre-vingt-quatre
[kat-ra-van-katr]
85
quatre-vingt-cinq
[kat-ra-van-sank]
86
quatre-vingt-six
[kat-ra-van-sees]
87
quatre-vingt-sept
[kat-ra-van-set]
88
quatre-vingt-huit
[kat-ra-van-weet]
89
quatre-vingt-neuf
[kat-ra-van-nurf]
90
quatre-vingt-dix
[kat-ra-van-dees]
91
quatre-vingt-onze
[kat-ra-van-onz]
92
quatre-vingt-douze
[kat-ra-van-dooz]
93
quatre-vingt-treize
[kat-ra-van- trez]
94
quatre-vingt-quatorze
[kat-ra-van-katorz]
95
quatre-vingt-quinze
[kat-ra-van- kanz]
96
quatre-vingt-seize
[kat-ra-van- sez]
97
quatre-vingt-dix-sept
[kat-ra-van- dee-set]
98
quatre-vingt-dix-huit
[kat-ra-van- dees-weet]
99
quatre-vingt-dix-neuf
[kat-ra-van- dees-nurf]
100
cent
[son]

1000 - Mille
10,000 - Dix Mille
100,000 - Cent Mille
1,000,000 - Un Million
1,000,000,000 - Un Milliard


Wednesday, January 7, 2015

MEKONI....JINSI YA KUKAANGA NYAMA YA NG'OMBE!


Mpo wasomaji wangu?
Haya tunaendelea na mapya ya mwaka mpya… kila jumatano tutakuwa na kipengele cha MEKONI… meko kwa Kiswahili ni jikoni na kama nilivyoahidi kulete burudani mbalimbali basi kila jumatano tukutane kwenye safu hii ya Mekoni.

Kinachotufungulia safu yetu ya kwanza ya mwaka ni JINSI YA KUKAANGA NYAMA YA NG’OMBE.

Ukaangaji nyama unasumbua watu wengi tu.  Wapo wasiojua kabisaaaa na wapo wanaojitahidi hapa na pale lakini ndio nyama inatoka ngumuuu kama kipande cha jiwe Lol… wapo pia mafundi wa kukaanga na akikukaangia lazima ulambe sahani… twende kazi sasa! 

Mwaka huu usipijua kupika vizuri baaasi tena!

Ukaangaji nyama hauna kanuni moja. Zipo kanuni nyingi tu za kukaanga nyama na ikatoka poa kabisa, laini na tamu. Mi nakuletea njia mojawapo.

MAHITAJI... itategemea na kiasi unachotaka  kupika
- Nyama

- Kitunguu swaumu

- Kitunguu maji

- Tangawizi... menya na uitwange, au isugue iwe laini

- Limao/ ndimu/ vinegar

- Chumvi

- Binzari ya pilau/ binzari masala/ curry powder/ meat masala na vingine unavyopenda

- Pilipili manga


- Mafuta kiasi cha kutosha

Friday, January 2, 2015

DARASA:....TUJIFUNZE KIFARANSA na Laura Pettie


Heri ya mwaka mpya msomaji!

Haya sasa Mwaka mapya na mambo mapya. Laura Pettie Blog sasa itakuletea kipengele cha darasa kila siku ya ijumaa. Lengo la kipengele hiki ni kujifunza mengi kuhusu Lugha na tamaduni za wenzetu. 

Kama ambavyo Motto wa blog yetu  ni ‘KUISHI NI KUJIFUNZA’….  Hivyo tunakuletea darasa la utu uzimani ili upate kupanua upeo zaidi na ujifunze zaidi…  Mnasemaje wadau? LIWEPO AU LISIWEPO? Mkiona halifai tutaliacha hakuna tatizo!

KWA KUANZA DARASA LEO. TUNAANZA NA LUGHA YA KIFARANSA…

Tutajifunza salamu na maneno machache ya kuanzia… ukitoka hapa lazima uwe nusu mfaransa hahahahaa. Kifaransa ni lugha ya mahaba. Raha sana ukiijulia na ukitaka kuifurahia basi upate bahati ya kuwasikia watangazaji wanaotumia kifaransa wakibubujisha maneno yao haraka haraka… utawapenda! moja kati ya watu walionivutia nijifunze kifaransa ni mwanadada Angelique Kidjo! wakati ule akitangaza tuzo za Kora...

Utasema wana mafua hivi, halafu kama wanabembeleza kisha kama wanakazia maneno halafu haoooo wanateleza tena. Ni lugha inayokadiriwa kuzungumzwa na watu karibu milioni 338 ulimwenguni!... wanasema ni lugha ya tatu barani ulaya baada ya kiingereza na kifaransa.

Kifaransa ni lugha rasmi Katika baadhi ya nchi za Afrika na hivi dunia imekuwa kama kijiji kimoja. Si haba ukijua lugha tofauti tofauti. Wala huitaji kuwa mtaalamu kile  cha kuombea maji kinatosha kabisaaa!

Tunanze na salamu kwanza na maneno madogo madogo...kisha nitakuwekea na namna ya kutamka ili kukuwezesha kujifunza matamshi wewe mwenyewe. twende kazi.




Snowfall Widget for Blogger


Snowfall Widget for Blogger