Friday, November 27, 2015

UREMBO NA LAURA... TUZUNGUMZIE SCRUB!!


Tuzungumzie SCRUB!
Scrubbing ni njia mojawapo ya kusafisha ngozi kwa mtindo wa kusugua kwa kutumia mikono au vifaa maalumu ukiwa umepaka aina yoyote ya scrub uipendayo na inayoendana na ngozi yako.

Scrubbing ni nzuri na muhimu kwa ngozi aina zote na kwa watu wote, wanawake na wanaume! Mambo ya wanaume kuwa na ngozi mvurugo imechoka kama ngozi ya goti na michunusi hujui hata ubusu wapi it is  so 90’s!.... mwanaume usafi na kujijali bwana anhaaa! Uso unaonekana uso hata  Bae anaona raha kukuweka kwenye wallet jamani  hahahahahaaa!! Joke!

Tukija kwa wanawake, usafi wa uso sio kuung’ang’aniza uso  uwe mweupe. Nope!..kwa hiyo hiyo rangi uliyonayo ufanye uso uwe na rangi moja tulivu. No madoa, no chunusi,  no harara. Uso hata ukifuta vipodozi bado utajiamini kuwa una uso msafiiii!!

Yote haya haya hayaji bila kushughulikia uso wako!!.... Kwenye meza yako kusikosekane Scrub au wale wa mabafu ya peke yao. Scrub isikosekane kando ya sabuni. Ni kitu muhimu hiki sio cha kukosa kwa watu wanaojijali.

Kuna watu ni waoga wa kuscrub kwa kuhofia kuwa kuscrub kunachubua ngozi. Nataka nikutoe hofu kuwa,  Kuscrub hakuchubui ngozi isipokuwa aina ya scrub unayotumia ndio inayoweza kukufanya ujichubue. Ni kama mafuta au losheni, ukitaka ya kukubadilisha rangi yapo na ukitaka ya kukuacha na rangi yako yapo. Chaguo ni lako!

Zipo scrub za kisasa na scrub za kutengeneza nyumbani
Zipo Scrub za uso na scrub za mwili au vyote kwa pamoja

FAIDA ZA KUSCRUB


-          Kuscrub kunaondoa seli zilizokufa kwenye ngozi na kukuletea ngozi mpya kwa juu. Ukishamaliza kuscrub utasikia tu ngozi ya uso imekuwa laini.
-          Kuscrub kunaondoa uchafu uliondani zaidi kwenye ngozi. Tunaosha uso kwa  maji na sabuni  na pengine tuna cleanse lakini kuscrub ni usafi wa ndani  zaidi kwa kuwa tunasugua ngozi
-          Kuscrub kunaondoa makunyanzi ambao yanaletwa na jua kali, uchovu na stress. kwa wanawake kuna makunyazi yanakera kwamba hata ukipaka poda unaona haikai vizuri mpaka usilibe zaidi ndio unajiona uko sawa!
-          Kuscrub kunazuia vipele kwa wanaume wanaoshave na hata vipele vile vinavyokuja kwa wanawake wanapokaribia siku zao, kuna wale wenye mapele makubwa kwenye mashavu. Scrub inayoendana na ngozi yako ni tiba kubwa sana.
-          Kuscrub  mwili kunachangamsha mwili na kuongeza vema mzunguko wa damu mbali na kuiacha ngozi yako ikiwa saaaafi.
-          Kuscrub kunafifisha madoa meusi na hatimaye kuyaondoa kabisa
-          Kusrub kunapunguza uwezekano wa kupata chunusi kama huna
     -  Kuscrub kunaondoa sugu.... Kama una sugu miguuni au kwenye viwiko vya mkono...we tafuta scrub uapply kila baada ya siku tano uone zitakavyoanza kufifia fasta....ukiwa mvumilivu unatengeneza mwenyewe tu nyumbani  scrub kama vile sukari, baking soda na mafuta nazi. una mix kisha unasugu sehemu yenye sugu kama nilivyokwambia. utakuja kuniambia!

MUHIMU

wanja tu ndio uliopita usoni ila uso uko fresh kama ulivyo
no poda no lotion. ngozi inapumua LOL!

-          Paka kitu chenye moisturizer baada ya kuscrub kama unahisi ukavu usoni
-          Usiscrun kila siku. Jiwekee ratiba ya  kufanya hivi mara moja kwa wiki au hata kwa mwezi kulingana na hali ya ngozi yako
-          Tumia scrub inayoendana na ngozi yako, hili ni jambo la muhimu sana ambalo watu wengi wanalipuuzia. Ukiielewa ngozi yako hutoscrub na vitu visivyoendana na wewe. kwa mfano scrub ya Asali + Olive Oil + Sukari ile ya brown hii ni kwa ajili ya watu wenye ngozi zenye mafuta... halafu kuna scrub ya machicha ya nazi, hii ni kwa watu wenye ngozi kavu..... ukidakia dakia vitu bila kujua nini ni nini kwa ajili ya nini.... ndio unaibuka na michubuko au chunusi zaidi au mpauko wa haja halafu unaipondea scrub kumbe umekosea mwenyewe!
-          Usitumie nguvu sana kuscrub ngozi ya uso. Ngozi ya uso ni kitu sensitive sana, ni ngozi tofauti na sehemu nyingine mwilini mwako, ndio maana unaweza kupaka kitu mkononi ila ukikiweka usoni inakuwa balaa
-          Mfanyie Scrub mwenzi wako kama sehemu ya kumfanyia usafi na kuboresha mahusiano yenu. Eeeh Mscrub bwana yako apunguze kiguu na njia kwenda saluni.

UTUMIE NINI KUSCRUB
Hii ni ya mwilini...tena vinauzwa 1500/= tu! kwa wamachinga

Tumia mkono kama hasa usoni na mikononi
unaona sugu zinavyotolewa

huwa vinauzwa kwenye kimfuko
hiki cha kuscrub, cha kufunga kichwani na dodoki laini bei cheee!


kuna scrubber za umeme pia

scrubber za uso


AINA ZA SCRUB
zipo nyiiiingi mno sana sana sana

Hii ni nzuri sana na niliitumia zamani sana
Ilikuwa the best scrub ever!





Zipo special za wanaume kama hii ADIDAS!

Zipo za kutengeneza nyumbani pia ambazo nikipata nafasi nitakuwekea hapa
Ni rahisi na very cheap!

MIMI BINAFSI

Natumia scrub ya chumvi…. Ni scrub moja nzuuuuri sana na imetengenezwa kiasili. Ni scrub ya chumvi iliyochanganywa na manjano na pia ninayo iliyochanganywa na mmea wa mzambarau... naweza kuitumia mara moja kwa mwezi lakini napenda matokeo yake maana katika kipindi hiki cha joto naweza nisipake losheni siku mbili na usigundue kitu kabisaa!

ZAIDI YA YOTE ZINGATIA HAYA....
Kupata ngozi nzuri siri kubwa ni kunywa maji mengi kwa kadiri uwezavyo.... drink a lot of water dear and yes! utapata adha ya kukojoa mara kwa mara  lakini ni pale mwanzo baadaye utaona poa tu lakini kiafya utakuwa umepiga hatua kubwa sana maana maji mngi ni dawa ya mambo mengi mwilini ikiwemo UTI inayosumbua wanawake wengi. Maji ni dawa isiyo na gharama ambayo inawashinda watu wengi sana. 

See you again!
Laura!

5 comments:

  1. Laura huku ni burudan zaid kwakwel...nilijaribu kufanya scrub jaman nikaharibika uso sijui wale hawakujua aina ya ngoz yangu jaman nilichukia loh..... hiyo ya chumvi naitaka ntaipataje sasa

    ReplyDelete
  2. Asante kwa darasa zuri.numeipenda hiyo scrub ya chumvi nitaipataje?

    ReplyDelete
  3. Ooh yeah Uzi umetulia nimeelewa umuhimu wa scrub mara nyingi nimekuwa nikiona kama scrub ni mambo ya kike tu kumbe No. Hata sisi boy tunsuhtaji nao.

    ReplyDelete
  4. Kabla ya kuscrub mwili unatakiwa uwe umelowa au mkavu tuu

    ReplyDelete



Snowfall Widget for Blogger


Snowfall Widget for Blogger