Thursday, November 6, 2014

UREMBO NA LAURA:.....JINSI YA KUKABILIANA NA WEUSI KWAPANI!!

K


Habari zenu wasomaji wangu!
Kama kawaida leo tunakutana tena ulingoni…. Katika kuwekana sawa hapa na pale kwenye masuala ya urembo masuala ya usafi na kadhalika! Mradi kwa gharama ndogo tu unabaki msaaafi kabisa na mwenye furaha tele! Team kubana matumizi hahahaha!

Leo nataka kugusia suala la makwapa kuwa meusi. 
Inakera sana!... hasaaa linapokuja suala la kuvaa nguo ya kukata mikono. Yaani unakosa kujiamini. Tena  basi uwe kwenye kadamnasi ambapo unatakiwa kupunga mikono hivi…ni zaidi ya shughuli!... unashindwa hata kujimwayamwaya mwenzangu aiiii kisa tukwapa tweusi!

Kuwa na kwapa jeusi sio ugonjwa, sio dhambi lakini mwenzangu linapunguza maksi kiasi fulani…. Halafu kwanini uwe na lami makwapani wakati njia tele za kuondoa na kuzuia zimejaaaa!!

Kwanza tuangalie sababu za makwapa kuwa meusi!
1. Unyoaji…. Wembe unachangia sana kuwa na makwapa meusi…ile puruuu puruuuu aaah mwenzangu lazima kwapa lidate hahahahaaa…. Hapo umetia vijisabuni kidogo unashave kwa nguuuuvu ili kwapa libaki jeupe mpaka mtu nje anaweza uliza jamani kuna usalama uko? anhaaaa!!

2. Deodorant:… unaroll deodorant  wiki ya kwanza…ya pili..ya tatu…unaona mabadiliko kwapani we umo tu!.... kipodozi chochote kikionyesha hali ya kukukataa hata kama ni siku mbili tatu…KIACHE!! Ukijitia una uchungu na hela yako utagharamamika zaidi ya hizo ulizotoa kwenye kutibu matokeo, unapaka deodorant unasikia  kwapa linawaka moto jamani bado umo tu! yahusu!

3. Magonjwa… hapa sitaingia sana maana sina utaalamu huo ila ndio hivyo kuna wakati hali hiyo inaletwa na ugonjwa ulionao na utagundua hili kama njia zingine zote zikidunda.
Haya sasa ndio tushapata kwapa jeusi...tufanyeje?

NAMNA YA KUKABILIANA NA  KWAPA JEUSI
1. LIMAO NA SUKARI


Hii njia ya kwanza iliyo bora kabisa na nyepesiiii
Kata kipande cha limao kichovye kwenye sukari, tena ile ya brown ndio nzuri zaidi.
Sugua kwapa lako kwa mtindo wa kuzunguka. Taratibu tu ila hakikisha unasugua eneo zima. Usikamue limao wewe sugua tu…majimaji  yatatoka yenyewe.
Acha kwa dakika 10-15 kisha osha makwapa yako vizuri kwa sabuni yako ya kila siku.
Fanya hivi asubuhi na jioni mpaka uone weusi umeondoka na lazima uondoke.
Faida yake ni kuwa Limao litaondoa pia harufu ya kwapa, na katika kipindi hiki usipake deodorant yoyote.



2. BAKING SODA


Narudia ni Baking Soda au sodium bicarbonate…. Sio BAKING POWDER! Usinichanganyie maarifa ukaumua kwapa hahahahaaa…  mara nyingi tunaitumia kwenye maandazi. Baking Soda ni tofauti kabisa na Baking powder!!

Hii unaweza kuitumia kwa staili mbili.
Ya kwanza:….. unachanganya kidogo na maji unapata uji mzito  kisha unapaka kwenye kwapa. Unaacha kwa dakika 15-20…kisha unaosha. inafaa siku upo tu nyumbani na khanga ya moja kifuani.

Ya pili…. Unachanganya baking soda na maji kidogo… inakuwa nyepesi kidogo kisha unachovywa pamba unapaka kwenye kwapa. Mfano ile Asubuhi  unatoka. Unakaa nayo siku nzima.
Baking Soda sio tu inaondoa harufu na weusi, bali pia inaondoa hali ya kuvuja jasho…. Unakuta mdada unaloa jasho mpaka blauzi inabaki na alama….. Naaaasty!!


3. UNGA WA LIWA NA MAJI YA ROSE


Ni moja ya vitu vinavyosaidia sana kuondoa weusi makwapani. Unachanganya kidogo tu na kupakaa kisha kaa nayo kwa dakika 15, halafu osha kwa maji baridi.


4. MAFUTA YA NAZI

Kuna mafuta ya nazi feki pia, mi nilishakumbana nayo. Sasa ukipata mafuta ya nazi halisi. Ukishashave unapaka kidogo eneo la makwapa hasa usiku. Mafuta ya nazi unaweza kutumia hata kule mapajani kama kuna weusi. Kila baada ya kuoga unajipaka. Hakikisha tu kwapa ni safi muda wote unapopaka. haya mafuta yatasaidia hata tuvipele tusitoke... kwa ushauri wangu tafuta yameandikwa Minara! ni mazuri kweli.


5. BADILI MTINDO WA KUSHAVE….

….WAX: Hii unaweza fanya mwenyewe ingawa sikushauri maana ni mtindo wa kutia sukari ya moto… kama huna utaalamu utababua makwapa wallah!...nenda  kwa wataalamu kwenye saluni ufanyiwe waxing. Kama unaona aibu…basi tafuta Wax special zilizo tayari kabisa unapaka tu na kubandika na kubandua. Ni kind of expensive kidogo na inauma sio siri lakini ni bora kuliko wembe mwenzangu!

…. SHAVER MACHINE: tumia shaver sio wembe mkavu mkavu… kuna watu unakuta ghafla ana mtoko, anajitazama makwapa anaona vinyweleo vileee… anaamua kuchukua wembe kuviparaza kavu kavu… wee! Ndio unapanda weusi hivyo taratibu… Shave kwa kufuata utaratibu jamani….
Lowesha hiyo sehemu kwa sabuni nyingi, au cream maalumu kwa kushevia… tumia shaver yako kuanzia juu kwenda chini…kufuata namna vinyweleo vinavyoota…. Usiparuze kwa nguvu kwa kutaka kung’oa zooote haraka haraka ndio unaumiza ngozi na vipele vitafuata…be gentle with your skin shaaa! ukiona mtu anakaa bafuni saa nzima usifikiri kuna hesabu anakokotoa..usafi bibi!!

….. VEET and the like: tumia cream kama veet. Ni nzuri sana. Huacha makwapa malainiiiii masafiii. Tatizo la veet zipo feki pia tena nyingi tu ambazo ukitumia zinaleta weusi pia kwa vile hazilainishi vinyweleo itakiwavyo hivyo unapotumia ile tupa yake ya kunyolea inabidi utumie nguvu kidogo kukwangua ngozi sasa hapo unategemea nini jamani?.... Pata Veet halisi aisee utajipenda makwapani.


6. CHAGUA MANUKATO YANAYOFAA

Usilazimishe kutumia deorodant kama unaona hazikupendi. Kuna Mist zinanukia vizuri tu. Pakaa Mist yako na perfume yako basi yatosha!... na kama u mpenzi wa deodorant tafuta zilizopoa kidogo kulingana na ngozi yako. Na ukiipata jaribu kustick kwenye hiyo hiyo pasipo kubadili badili sasa! maana kuna watu kila deodorant anataka, kila anayoikuta anapaka... mrad tashtiti tupu!


7. KUNYWA MAJI MENGI…

Mwili unapokosa maji ya kutosha jasho huwa zito aisee. Wengi wetu tunapuuzia sana unywaji wa maji kwa kuona ni kazi ngumu sana. Tunasahau mwili unahitaji maji zaidi kuliko tunavyofikiria. Kuna wakati mwili unapokosa maji ya kutosha kichwa kinauma, mdomo utoa harufu mbaya, choo ukosekana, mwili huisi uchovu, mkojo utoa harufu mbaya na huwa wa njano sana… sasa vipi kuhusu makwapa hali ni hiyo hiyo jasho linalotoka linakuwa si la kawaida. Utaacha kupata weusi makwapani?

Kunywa maji kila unapopata nafasi, kunywa maji angalau lita moja kwa siku kama lita 2 na zaidi zinakushinda ila jitahidi unywe maji mengi. Ni dawa nan i vizuri kiafya!!

Zipo njia nyingi zaidi lakini natumaini hizi pia zitakusaidia kwani ni njia ambazo nina uhakika nazo zaidi kwa vile nimeshazitumia hapa na pale mimi binafsi na watu wa karibu.

NB: Unapotumia vitu vya asili usitarajie matokeo ndani ya siku mbili tatu… jipe mwezi mmoja hadi mitatu kuisha kwa tatizo. Uzuri wa njia za asili ukishatibu tatizo ni nadra tatizo kurejea, ni nadra saaana kupata matokeo negative, ni gharama nafuu mnooo na unatumia pasipo wasiwasi kuwa nikimaliza nitapata wapi pesa za kugharamika tena na mwisho unabaki na urembo wa asili. Ni kitu cha kujivunia!!

NATUMAINI UMEPATA CHOCHOTE CHA MAANA KWA SIKU YA LEO.


Wale wenye ushauri, maoni na mapendekezo njoo Facebook inbox au tumia namba ya whatsapp iliyopo eneo la mawasiliano.

MBAKI SALAMA!!

4 comments:

  1. Yaani we dada nimekupenda bure jamani. Asante saaana

    ReplyDelete
  2. hey na baking soda inaweza toa pimples kweli

    ReplyDelete
  3. Hiyo ya baking soda unaeza kufanya kila siku?

    ReplyDelete



Snowfall Widget for Blogger


Snowfall Widget for Blogger