24
‘Kuna nani uko?’ Pamella akauliza akihamisha uso toka kule
alikokuwa akitazama na kumuangalia Meddy ambaye naye aliurudisha uso wake
haraka usoni pa Pamella.
‘Mmh nadhani ni Dodo amengusha kitu uko jikoni’ Meddy akajibu
akijibaraguza kwa kumsingizia paka wake.
Pamella akashusha
pumzi kwa nguvu kiasi cha mabega yake kuinuka juu na kuteremka chini sambamba
na pumzi ile. Akajivuta kinyonge na kuketi sofani na Meddy naye akiketi kando
yake huku mara kadhaa akigeuka na kutazama kule uliko mlango wa kuingilia
jikoni. Ni kama hakumini Jerry angetulia uko aliko bila kuzua kashi kashi
nyingine.
‘Tatizo ni nini Pam?’ Meddy akauliza akijaribu kujituliza
mwenyewe na kurudisha mazungumzo katika mstari. Pamella akamtazama Meddy kwa
huruma mno, uso wake ulionyesha hali ya kukata tama
‘Jerry…’ akatamka taratibu akilaza shingo yake uoande mithili
ya mtoto anayejitetea mbele ya mzazi wake huku akibetua mabega yake na kutikisa
kichwa kulia na kushoto.
‘Amekufanyaje?’ Meddy akadakia huku pia akigeuza tena shingo
yake na kutazama kule jikoni. Wasiwasi ulimjaa kwa kiasi Fulani akijua wazi
Jerry alikuwa anasikia kila walilokuwa wakizungumza
‘Hivi Jerry ni mtu wa kumpa mwanamke simu apokee nikimpigia?’
Pamella alilalamika
‘Ehh!... nini?’ Meddy akashangaa, uso ukijenga matuta kadhaa
na kisha kutoweka ghafla
‘Nimempigia simu Jerry asubuhi ya leo na simu imepokelewa na
mwanamke’ Pamella akajieleza na Meddy akajikuta akiguna na kurudisha kichwa
chake nyuma kidogo katika namna ya kushangaa zaidi.
Asubuhi hiyo alikuwa
na Jerry, ni mwanamke gani alikuwa amepokea simu ya Pamella? alijiuliza hili
swali kichwani na asipate jibu la haraka
‘Mbona mimi nimeongea naye asubuhi….ulimpigia saa ngapi?’
Meddy akazungumza akishangaa kwani alizungumza na Jerry asubuhi sana akihisi
Pamella alikuwa akitafuta cha kumlaumia Jerry.
‘Muda mfupi tu uliopita’ Pamella akajibu na kule jikoni Jerry
aliipapasa mifuko ya suruali yake na kuachama mdomo kwa mshangao.
Simu yake ilikuwa imebaki kwa Sindi! Akakumbuka alipoipokea
simu ya Meddy hakuirudisha simu mfukoni, aliitupia kwenye kochi ili achomekee
shati. Akauma meno kwa tukio lile la kukumbuka kuwa aliisahau simu yake kule
kwa Sindi!
Meddy akawa kama mtu asiyeelewa kitu!
‘Hivi hizi dharau za ghafla ghafla zinatoka wapi?’ Pamella
akahoji kwa uchungu
‘..labda alikuwa mbali na Simu na Sindi akapokea simu yake’
Meddy akamtetea Jerry
‘Tangu lini amekuwa opareta wa Jerry?’ Pamella alihoji
kimamlaka zaidi na Meddy akamkata maini
‘Tangu wawe wapenzi….huwezi jua wamekubaliana nini’
Pamella akacheka kwa dharau akisahau huzuni yake
‘Jerry is mine!....He is mine?... angekuwa Clarita sawa sio
ile takataka isiyojua tofauti ya mkoba na pochi…excuse me!...’ Pamella akatamba
na asijue Jerry mwenyewe alikuwa akimsikia
‘Twende mbele turudi nyuma Pam…wewe si una Petrick… Jerry ana
nafasi gani kwako hapo?....au ulitaka awe anakulilia kila siku…na umburuze
unavyotaka?’ Meddy akampasulia ukweli ambao Pamella aliumeza kwa kiburi
‘Patrick ni Patrick na Jerry ni Jerry…. mimi ndio najua nani
nampenda na kwanini….Jerry loves me….na mpaka sasa sidhani kama anaweza
kujishusha heshima na ku’date na kitu kama Sindi….kina nini kile kitoto?...
uzuri hana, elimu hana, pesa hana, exposure hana… kwa Jerry ninayemjua mimi
kumkataa mwanamke kama Clarita sababu yangu na kisha kumchkua Sindi ni sawa na
kunitukana matusi yote makubwa duniani….that will never happen!’ akajiaminisha
mwenyewe!
Meddy akacheka na kutikisha kichwa. Tambo za Pamella Okello zilimuacha
hoi mno, alitamani sana amwambie ukweli wa hali halisi ulivyo lakini akaona
ilimpasa kukaa kando na kuwa mtazamaji asiyefungamana na upande wowote.
Pamella Okello, akalikata tabasamu la Meddy kwa kubadili
maongezi ghafla.
‘Fiona amekuja kuniona leo asubuhi’ akatamka kwa utulivu kama
mtu aliyetaka aeleweke na hakueleweka.
‘Nini?...Fiona?!’ Meddy alitoa macho na Pamella akaitikia kwa
kutikisa kichwa juu chini
‘Anataka nini?’ Meddy sasa alibadili mkao na kumtazama
Pamella kwa wasiwasi kana kwamba jibu la Pamella lingemlipulia mbali. Hali ile
ya hamaniko haikumtokea peke yake. Jerry kule jikoni alikaribia kujigonga
kwenye mtungi wa gesi wakati akiisogea zaidi baada ya kulisikia jina la Fiona.
‘Sio anataka nini…just uliza amegundua nini?... yule mwanamke ni pacha wa shetani Meddy…hisia
zangu zilikuwa sahihi… ndiye aliyesuka mipango yote ya kumuua Jerry’ Pamella
aliongea kwa kujiamini
‘Pamella!’ Meddy aliita kwa mshangao, ni kweli walikuwa
wakifanya utafiti wa chini chini lakini Meddy hakuwahi kukubaliana na Pamella
kuwa Fiona anahusika. Hakuiona sababu ya Fiona kufanya vile. Meddy alikuwa
upande wa Jerry wakiamini Mzee Agapela ndiye hasa aliyetaka kumuua Jerry sababu
ikiwa ni ugomvi wao ukiwa juu ya Jerry kumtongoza Fiona.
‘Trust me Meddy!...’ Pamella akasisitiza na Meddy akajikuta
akigeuza shingo na kuchungulia kule jikoni huku akijua wazi Jerry alikuwa na
hali gani uko aliko.
‘Amekwambia nini?’ Meddy akataka kujua kwa undani
‘Amemuona Jerry akiwa na gari langu…na nahisi ni ile wiki
tuliyotibuana maana ndio gai alilokuwa anatumia….’ akajieleza naye uso ukionekana
kujaa wasiwasi
‘Mungu wangu!....’
Meddy akakosa la kuongeza
‘Nilisema siku ile….Jerry anatakiwa atulie na afanye
uchunguzi akiwa mafichoni… you guys mkaona naingilia uhuru wake…. na ile
takataka isiyojua kinachoendelea ndio inayomfanya azurure ovyo hali akijua it
is too dangerous out there…stupid!’ Pamella akaongea kwa mtindo wa kufoka akiwa
amemuacha Meddy anamtazama na wala sielewe anachoongea. Hofu yake ilikuwa kubwa
mno, aliiona vema hatari iliyokuwa mbele yake!
888888888888888888888
Wiki moja baadaye….
Magari matatu makubwa ya kisasa yaliyofanana yaliongozana
barabarani yakitokea eneo la uwanja wa ndege. Kila aliyekuwa kando ya barabara
aligeka kuyatazama hali wale waliokuwa katika magari yao walitoa vichwa nje
kushangaa magari haya yaliyokuwa yameongozana. Msafara ule usio rasmi ulikuwa
unaelekea Oysterbay muda huo wa saa kumi
jioni.
Dakika arobaini na tano baadaye msafara huo ulisimama katika
nyumba moja ya kisasa na geti kufunguliwa. Mwanaume wa makamo, mwenye kimo cha
kutosha, mweusi ti mwenye sura nzito kidogo iliyojaa umakini usioeleweka
aliteremka baada ya kufunguliwa mlango na msaidizi wake.
Alisimama na kuitazama nyumba ile iliyokuwa mbele yake huku
akitabasamu na kutikisa kichwa juu chini mara kadhaa kuashiria kuridhishwa na
hali aliyoiona. Mzee yule akifuatiwa na wasaidizi waliokuwa na mizigo pamoja na
mkewe aliyekuwa kando yake waliingia ndani na kupokelewa na mwanamke mtu mzima
aliyekuwa amevalia sare za wasaidizi katika nyumba ile.
Mzee akaingia na kuikagua sebule yake huku akitabasamu kisha
akakifuata kiti na kuketi, wakati huo wasaidizi wakikimbizana huku na kule.
wengine wakiingiza mizigo na wengine wakihakikisha hali ya usafi pale alipoketo
bosi wao ili mradi kulikuwa na pilika pilika. Mzee huyu alikuwa Mzee Okello!
‘Pamella yuko wapi?’ Mzee akauliza na mkewe akichungulia
kordoni kana kwamba angemuona huyo Pamella. Yule mama mtu mzima akainamisha
kichwa chini kama mtu aliyekosa jibu kwa wakati ule.
‘Sijui nimesikika?’ Mzee Pamella akakazia swali lake
‘aahm…Pam… amehama hapa’ Yule mama mtu mzima akamung’unya
maneno lakini alisikika vizuri tu.
Mama yake Pamella akamtazama mumewe, na mumewe akamtazama
mfanyakazi wake katika namna ya kutomuelewa
‘Amehama?!... binti yangu anaondoka nyumbani anatangatanga
nje na nyie mpo tu humu ndani…. hamniambii?...kwa hiyo mnaishi wenyewe tu humu
ndani’ Mzee Okello akauliza jibu na yule mtumishi akaitikia kwa kichwa
akionyesha woga utadhani yeye ndiye aliyemuahamisha huyo Pamella.
‘Gadna!....Gadna!’ Mzee Okello akapaza sauti na kumuita
mfanyakazi wake ambaye pia ni dereva wake. Gadna akafungua mlango na kuingia
ndani
‘Naam Mzee’ akaitikia wito, akiwa kasimama kwa heshima mbele
ya bosi wake
‘Two hours from now…nataka kumuona Pamella humu ndani…. and
you…’ akamuonyeshea kidole yule mtumishi mtu mzima na kumatzama kwa sekunde
kadhaa
‘…you are fired!’ akatamka kwa sauti kali na kusimama. Mama
wa watu akaduwaa na hapo hapo akaweweseka na kutetemeka akimtazama Mzee Okello
alivyokuwa akiiacha Sebule na kupandisha ngazi kuelekea chumbani.
Mama Pamella akasimama pia na kumatazama yule mama mtu mzima
kwa huruma. Ni kama vile hakuwa na mamlaka wala maamuzi ya kubadili hali ile.
Akasikitika na kumfuata yule mtumishi akamkumbatia. Kazi ndio ilishapotea!
8888888888888888888888
Sindi Nalela alikuwa chumbani kwake akimalizia kukunja nguo
alizotoka kuanua na kuzitia katika sanduku. Akachukua shuka moja na kutandika
kitandani huku akitikisa kichwa chake na kuonekana kuufurahia muziki uliokuwa
ukisikika redioni. alitabasamu mwenyewe na kuufuatisha hali akizunguka kile
kitanda na kuchomekea shuka.
Wakati akivalisha kava za mito ya kulalia, mlango
ukafunguliwa na Jerry akaingia na kimfuko chake cha Rambo kikiwa na fungu la
mchicha na samaki waliofungwa kwenye
kipande cha gazeti.
‘Umewahiiii…’ Sindi akamtania akiachana na mto wa kulalia na
kwenda kumpokea Jerry.
‘Hebu washa feni aisee…joto kweli’ Jerry akalalamika na Sindi
akamuwashia Feni iliyokuwa imesimamishwa kando ya kitanda.
Wakati akiketi kitandani akagundua pazia jipya lilikuwa
linaning’inia mlangoni
‘Umenunua pazia jipya?’ akamhoji Sindi aliyekuwa anachota
maji kwenye wenye ndoo na kumimina kwenye sifuria
‘Lile lingine lilikuwa baya…’ akajitetea akitabasamu
‘hili bdio baya sasa dah…’ Jerry akambeza na sindi akachota
vijimaji kwenye mkono na kumrushia Jerry pale kitandani. Jerry akayakwepa
akicheka.
‘unataka maji ya moto sana?’ Sindi akamuuliza akiajiandaa
kwenda nje kuyachemsha kwa ajili ya Jerry.
‘kwanza hata usichemshe kama naoga saa hizi …kuna joto mno’
Jerry akatoa wazo na Sindi akarudi kuyamimina maji kwenye ndoo
‘Basi ngoja nikuchotee kisimani hapo’ Sindi akataka kutoka
tena
‘Njoo kwanza bwana…’ Jerry akamshika mkono na kumvutia pale
kitandani
Sindi akamkalia Jerry kwenye paja huku mkono wake wa kulia
ukizunguka mgongoni na kutulia bega la kulia la Jerry na mkono wa kushoto
ukivitumbua tumbua vijiupele pajini mwa Jerry. Mahaba juu ya mahaba!
‘Nimekuletea zawadi’ Jerry akainua uso na kumwambia Sindi
ambaye tabasamu lake lilitosha kumfanya Jerry ajisikie bukheri wa afya
‘Zawadi gani..’ Sindi akauliza akiiuma uma midomo yake.
Jerry akaufungua ule mfuko na kutoa kibahasha cheupe.
akampatia Sindi ambaye aliutoa ule mkono wake wa kulia mgongoni mwa Jerry na
kuifungua bahasha. Akatoa nguo ya ndani nyeupe. Sindi akacheka na kujiinamia
akizidi kucheka
‘Yaani unafanya kazi uko huku unawaza kuninunulia chupi
khaaa…’ Sindi akatania
‘Yaani hata nikiwa wapi akili yangu inakuwaza tu… nakuwaza
tu…’ Jerry akajibu naye akianza kumpapasa Sindi kimahaba.
Sindi Nalela alishaingia mtegoni, hakutamani kukutana na
Nyanza tena. Si kwamba hakumpenda, bali hakujua angemtazamaje na angemwambia
nini kuhusu ahadi ya kuwa wake peke yake. Ngome aliyomuahidi ilishabomolewa.
Alitembea na hatia moyoni mwake lakini pia moyo huo huo ulifunguka kwa kasi ya
ajabu na kumpkea Jerry Agapela! akimpenda maradufu ya alivyompenda Nyanza!
8888888888888888888
Kijijini aliko Nyanza Mugilagila, maisha yalikuwa yanaendelea
pamoja na yote yaliyotokea. Nyanza alikuwa akimalizia kibarua chake cha kulima
na taratibu alisimamisha jembe na kutuliza macho ule upande ambao jua lilikuwa
linazama. Alitulia vile akilitazama lile jua kana kwamba alitaka kulipa salamu
zimfikie Sindi popote alipo.
Moyo wake ulikuwa na maumivu, moyo wake ulikuwa na hekaheka
kila siku iliyoenda kwa Mungu. Akainama na kupinda mgongo kumalizia kazi yake.
Wakati akifanya yote haya Alma rafiki kipenzi wa Sindi alikuwa amesimama nyuma
ya mti mkubwa akimtazama Nyanza kwa huruma. Roho yake ilikuwa inataka kufanya
jambo ambalo alihisi lingemletea ahueni. Alitaka kumwambia Nyanza ukweli wa alipoenda
Sindi Nalela!
Akajishauri pale nyuma ya mti kwa dakika kadhaa kisha
ataratibu akajitokeza mbele ya Nyanza ambaye wala hakuwa na habari naye.
Aliendelea kulima huku akimsifu Mungu kwa nyimbo za mapambio. Alma akapiga
hatua za kutetemeka na kumfuata Nyanza. Alitaka kusema yote jioni bila kujua
zahma ambalo angelizua!
Wakati Alma akitaka kukiri, Huku mjini Wazee wawili walikuwa
simuni wakizungumza na bila kujua wake zao walikuwa wamebanisha mahali kila
mmoja mahali pake wakiwasikiliza.
Mke wa Okello alikuwa akimsikiliza mumewe kwa kuibia hali
kadhLIKA Fiona Agapela alikuwa amebanisha mlangoni akimsikiliza Mzee Agapela.
‘Jerry hawezi kuwa mfu…. come on…. harusi ya kifahari
niliyonayo kichwani haiwezi kufutika kwa kitu cha kufikirika’ Mzee Okello
alizungumza kwa kujiamini
‘….na hatuwezi kumpa Pamella matumaini kwa kuongea naye
kuhusu ndoa wakati hatujui alipo Jerry…. it is not that easy kukubali my son is
still safe and sound…. it os hard Okello!’ Mzee Agapella aliongea kwa uchungu
akishusha pumzi.
Fiona aliyekuwa akisikiliza alitoa macho na kuduwaa pale
mlangoni. Haya yalikuwa mapya mno masikioni mwake.
….. MAMBO NDIO YAMEANZA KUCHANGANYIA....
dada una kipaji keep it up! frm salehe masoud wa ilala n tha'ts ma really name
ReplyDeleteAsante sana Salehe....nimefurahi mno kujua nimerunga hadithi kwa jina la mtu anayeexist kabisa kiukweli hahahahaaa...pengine siku itakapotakiwa kuwa movie...itabidi uchukue nafasi ya huyu Salehe...i hope unajua kuigiza!!
ReplyDeletei will do ma bst
Delete