Wednesday, March 5, 2014

SINDI.... na LAURA PETTIE (59)

59


Meddy aliiona hatari  iliyokuwa mbele yake, haraka akanyanyuka na kumfuata Nadina kule alikokuwa akijirudisha kinyume nyume. Akamdaka na kuamua kumrudisha chumbani haraka sana. Huku sebuleni Jerry Agapella alikuwa bado katika bumbuwazi fulani lakini akili yake haikufanya kazi haraka na kutambua maneno aliyoyatamka Nadina yalikuwa ni jina la mtu aliyeshikilia robo tatu ya furaha yake.


Meddy akamtembeza Nadina taratibu akimrudisha chumbani alikokuwa. Akamketisha kitandani na yeye kuketi kwenye  kile kiti alichoketi usiku uliopita akimtazama Nadina.
‘Tulia kwanza…’ akamsihi Nadina aliyekuwa bado katika ile hali ya kushtuka
‘…nitakwambia kila kitu Nadina kwa sasa tulia kwanza…’Meddy akausisitizia wito wake akimtazama usoni Nadina ambaye hakuitikia chochote kuonyesha alimuelewa au lah!

Kwa wasiwasi Meddy akanyanyuka na kutoka mule chumbani, akarejea sebuleni na kumkuta Jerry amesimama akionekana bado kutoelewa chochote
‘who is she?’ akauliza kwa shauku
‘Nadina!’ akalitaja jina lake akijua wazi Jerry angelielewa haraka kuwa alikuwa ni nani na ikawa hivyo.

Jerry akaonyesha mashangao wa wazi usoni pa Meddy, alimshangaa haswa!
‘Hivi uko sawa kichwani?... nina mashaka na utimamu wa akili zako Meddy’ Jerry akaongea akimtazama Meddy katika namna isiyoeleweka
‘Kwanini?!’ alishangaa na kuuliza kwa wakati mmoja
‘huwezi kuokota Malaya wa danguroni ukamleta kuishi naye ndani ya nyumba… hivi unawaelewa hawa viumbe au huwa unawasikia tu juu juu… nilidhani ni mtu unayemnunua na kustarehe na kuachana hapo hapo…hiki nini sasa?’ Jerry aliuliza kwa ghadhabu kana kwamba Meddy alikuwa ameingiza huyo Malaya ndani ya nyumba yake.

‘Najua ninachofanya Jerry…angalau mara moja katika maisha yako heshimu maamuzi yangu juu ya huyu binti’ Meddy akajitetea na kuzidi kumshangaza Jerry
‘Sikuelewi…’ jerry akampinga
‘…na sidhani kama nataka kukuelewa katika hili, hawa ni watu hatari sana kwa michongo ya wizi na mauaji sijasemea maovu yao mengine humo danguroni…hujisikii hata kinyaa…come on…Meddy!’ bado alizidi kupingana naye na Meddy akashusha pumzi na kumtazama Jerry.

Alizisikiliza kashfa za Jerry kwa umakini mkubwa na akitamani sana kumwambia kuhusu Sindi lakini akaona angelileta kizaazaa kingine kisicho na ulazima, akatulia tu

‘…nadhani baada ya wiki utakuja kuniambia unajutia huu uamuzi uliouchukua sasa’ Jerry akakamilisha kauli yake na kuondoka akimuacha Meddy amesimama pale kama nguzo mpaka alipoamua kugeuka na kuelekea kule chumbani alikokuwa Nadina. Akamkuta amejikunyata kitandani, akiwa mbali kimawazo.

‘Kwanini alimfanyia vile Sindi… kwanini?... alikuwa msichana mwenye roho ya kipekee kustahili unyama aliomfanyia’ Nadina alilalamika na kumuachia viulizo vingi Meddy
‘Sijui ulichosikia kuhusu Jerry… lakini nataka kukuhakikishia kuwa Sindi ndiye mwanamke aliyewahi kumfanya Jerry afikirie kujiua’ Meddy akamduwaza Nadina
‘…Baada ya kumfikisha kwenye madanguro?’ Nadina akadhihaki na kumfanya Meddy amueleze kwa kina stori nzima ya Jerry Agapella na Sindi Nalela.

Kwa dakika nzima Nadina alimtolea macho Meddy kana kwamba yale aliyoyasikia yaliingia na upepo ganzi na kumgandisha akili. hakuamini! hapana alimiani lakini hakuelewa, hapana yawezekana alielewa lakini hakuamini. kichwa kikamzunguka kama tiara!

ukauhisi uchungu, uchungu kuwa anayezungumziwa sasa yu marehemu, akaumia na akajikuta tu akilengwa na machozi.
‘Kwanini asingekuwa wazi tu… kuficha kwake kumemsaidia nini sasa… amekufa… Sindi amekufa na mtoto wake… Sindi amekufa kwa mateso sababu mtu mmoja na tamaa zake alitaka kummiliki huku akificha Siri… Sindi wangu..Sindi ajmani’ Nadina akalia na kulia, akalia sana kiasi cha kumfanya Meddy amkumbatie kwa nguvu kumbembeleza.
888888888888888888888888

Annie na mdogo wake Rebecca wako bustanini wakistaftahi kwa mapocho pocho ya kuvutia huku jua la asubuhi hiyo likiwagonga na kuwarutubisha kwa vitamini za kutosha. Halikuwa jua kali la kuumiza na vile kulikuwa na upepo ulioleta baridi kidogo, jua lile lilileta raha ya kipekee.
‘Mna ukaribu gani na Santina?’ Annie akauliza mara baada ya kushusha kinywaji chake
‘tumemlea Annie…kwangu mimi Santina ni kama Pamella tu.. wamepishana mwaka mmoja au miezi tu…’ Rebecca akajibu akigeuka nyuma na kuwatazama Pamella na Santina waliokuwa wameegemea gari wakiendelea na maongezi

‘Mmmh!... unazijua tabia zake vizuri?’ Annie akadadisi
‘’Mtoto anayejiheshimu na kuheshimu wengine… kwake mimi ni mama…nimemlea huyu binti Annie…what’s wrong?’ Mama Pamella akauliza akianza kupata wasiwasi juu ya yale maswali ya dada yake Annie.

‘nilitaka kujua malezi yako yakoje… ukaribu wake na Okello siuelewi’ Annie akaweka wazi bila kumung’unya na kumfanya Pamella acheke kwa sauti
‘mtake radhi binti wa watu…. Kwa Okello, Santina ni kama binti yake na ukizingatia alikuwa mtoto pekee wa marehemu rafiki yake… sioni ajabu wao kuwa karibu… mi sio mama wa kuchukia watoto kwa vile sio wangu… usimfikirie vibaya mtoto wa watu’ Rebecca akatetea na Annie akashusha pumzi taratibu na kumkazia macho Rebecca

‘Nikikwambia anaweza kutembea na Okello?’ Annie akamtega mdogo wake ambaye alitabasamu na kucheka kabisa
‘…Naweza kukufungashia mabegi yako nikakutimua kabla ya harusi, Pamella amemzidi Santina mwaka mmoja tu… ni sawa ni kuniambia Okello anatembea na binti yake… Annie, pamoja na yote unayojua kuhusu mimi na Okello…huna ruhusa ya kumtusi mume wangu!’ Rebecca akajibu akiondoa tabasamu ili kuonyesha alimaanisha alichoongea. Annie akapiga funda la juisi na kumtazama Santina kule alikokuwa amesimama.

‘Meddy??...Meddy huyu huyu?!’ Pamella alishangaa baada ya Santina kumweleza naman meddy alivyompokea kwa hasira na majibu ya ovyo
‘Yeah! Meddy huyu huyu… aisee nilitamani niyeyuke pale restaurant… sijui nilichomkosea mpaka amenibadilikia hivi’ Santina akalalamika
‘Una uhakika hukumfanyia chochote kabla ya kuondoka’ Pamella bado hakuelewa
‘Nina uhakika Pam…. alikuwa rafiki yangu wa karibu’
‘Najua na ndio maana nashangaa’ Pamella akadakia
‘…from nowhere baada ya kulala na mimi usiku ule kesho yake jioni nikamtafuta na matatizo yakaanzia hapo… alianza kunikwepa kabisaa baada ya mwezi ndio hakutaka hata kuniona wala kuongea na mimi… miaka miwili imekatika na unaenda wa tatu… Pam… Meddy bado hataki kupatana na mimi huku kosa silijui’ Santina akahuzunika na Pamella akamhurumia

‘baada ya hii mihangaiko ya harusi nitamafuta niongee naye… Meddy ni mtu poa sana… mwenye roho ya hurum mno…nashangaa kusikia ameyafanya haya!... relax Santina lazima ipo sababu na labda kuna kutokuelewana juu ya kitu… akikisema tutajua wapi pa kuanzia…kwa sasa mpe distance tu ukizidi kumfuata ndio atakuumiza vibaya zaidi’ Pamella akamshauri mwenzie na wakati huo mama yake akinyanyuka toka kule alikokuwa na kuwafuata pale walipokuwa wamesimama, alikuwa na simu mkononi
‘Santina dear…baba yako anataka kuongea na wewe…’ Rebecca alimpatia simu Santina ambaye alisita kidogo ila haraka akajikuta akiipokea na kusikiliza

‘Acha huu utoyo Santina please!.... jibu meseji zangu na upokee simu zangu kwa simu’ Mzee okello aliongea kwa sauti ya kubembeleza
‘Haya nitafuatilia baba’ Santina alijibu kitu tofauti ili kuwazuga Rebecca na Pamella waliokuwa wanamtazama wakitabasamu. Akaikata simu na kumrudishia Rebecca

‘Kuna tatizo?’ Rebecca akauliza
‘Hapana mama…ni… kuna… kuna fomu za malipo ya chuo natakiwa kujaza na kusaini haraka’ akadanganya na wakamuelewa
‘…usome mwanangu, na ukimaliza tu… kuna nafasi ya kazi inakungoja…’ Rebecca akampa moyo kuhusu kusoma na asijue mwenzake alikuwa nje uko akilea mimba na sasa mtoto anayeaminika kuwa wa Mzee Okello.

Santina akajitabasamisha na kushukuru huku Pamella akimtazama kwa upendo. ni Annie tu ndiye aliyemtupia jicho la wasiwasi toka kule kule bustanini.
8888888888888888888888

ofisini kwa Dennis Mazimbwe, Dennis anamtazama Fiona kwa jicho kali kidogo huku bibiye akiwa na tabasamu tele usoni.
‘Long time no see…’ Fiona akaongea kwa bashasha huku mwenzake akitikisa kichwa kwa kuona dhihaka ya wazi toka kwa Fiona

‘Sema kilichokuleta ofisini kwangu…nina msururu wa kazi na sina muda wa kupoteza tafadhali’ Dennis akaongea kwa jazba za chini chini
‘…ning’oe kwa gurugota basi unitupe nje kama unaweza!...hahahahaaa’ Fiona akafanya utani akicheka kabisa na asijali ile hali ya kukasirika aliyonayo Dennis

Dennis hakujibu kitu wala utani haukuondoa ndita chache zilizokuwa soni pake muda ule
‘…okay, ni kuhusu Kristus’ Akaweka bayana shida yake na Dennis wala hakumjibu kitu chochote. Alimtazama tu kana kwamba alitaka aongee na kumaliza shida zake zote
‘…hapokei simu zangu, hajibu text zangu, na nyumbani amemkatalia mlinzi nisiingie’ akaendelea kujieleza

‘Sasa mimi nikusaidie vipi?’ Dennis akauliza kwa dhihaka za chinichini
‘nikutanishe na Kristus’ akatamka haraka sana
‘…kakae getini kwake umvizie akiwa anatoka ama anarudi… huo ndio msaada pekee nilionao… samahani nina kazi za kufanya’ akataka kumtimua Fiona kwa kumuonyesha mlango wa kutokea

Fiona akamtazama Dennis kwa kituo, jibu lile halikumfurahisha hata chembe. Akataka tu kumtibua Dennis
‘yeah kazi lazima unazo sana ndio maana mkeo anazunguka usiku na wazungu wenzake kwenye mahoteli…mume umejifungia humu unalea kazi nyingi…’ akasema akitabasamu na kunyanyuka
‘na wewe uko mahotelini usiku ulikuwa na nani?’ Dennis akauliza kikawaida kama vile ile kauli ya Fiona haikumshtua

‘Muulize mkeo jana usiku tulikuwa wapi …’ Fiona akatamka kwa kujiamini kana kwamba alikomuona huyo mkewe dennis kulikuwa na mambo ya ajabu na aibu. taratibu akaokota mkoba wake na kumtazama dennis
‘See you around!’ akaaga na kuondoka pasipo kuangalia nyuma wala kungoja maswali zaidi ya Dennis ambaye hakuonekana kushtuka mpaka pale Fiona alipoufunga mlango.

Dennis kkunja uso, mishipa ya kichwa ikamsimama, wivu ulimtambalia kupitiliza hata kabla ya kuujua ukweli halisi. Daniella alichelewa sana kurudi na alijitetea kuwa alikuwa kazini mpaka muda ule. Akakunja ngumi na kujaribu kujituliza lakini haikuwezekana.

Akanyanyuka kwa hasira na kuchukua ufunguo wa gari uliokuwa mezani, akakwanyua koti lililokuwa limewekwa nyuma ya kiti na na kulivaa huku akiuufuata mlango akatoka.
Alikuwa anamfuata Daniella ofisini kwake, ilimchukua nusu saa tu kuingia ofisini kwa Daniell ambaye alikuwa na kikao na watu wawili wengine waliokuwa wameketi kwenye viti mbele ya meza yake ya kazi.

Dennis akaingia na kusimama akimtazama Daniella kwa hasira. Kwa kutambua shari aliyoingia nayo, Daniella akawaomba radhi wale watu wawili na kuwaomba wawapishe.

‘Now what?!’ Daniella akauliza baada ya kufunga mlango wa ofisi
‘Ulikuwa wapi jaman usiku?’ Dennis akauliza akisikilizia jibu kwa umakini
‘Hapa ofisini kwani vipi?’ Daniella akajibu akijaribu kujiamini na jibu lake huku akijua wazi alikuwa anadanganya. Asingeweza kusema ukweli kwa vile Francois alimuomba asimwambie Dennis kuhusu uwepo wake pale.

‘Daniella!... nakuuliza kwa mara ya mwisho jana usiku ulikuwa wapi?... na nani?... tafadhali hii stori ya nilikuwa kazi iweke kando kwanza’ Dennis akaongea akimfuata mkewe ambaye alihisi kuna kitu hakikuwa kawaida

‘…ulikuwa na mzungu’ akatamka Dennis na kumsogelea zaidi mkewe ambaye alishusha pumzi kwa kujua amekamatwa
‘I’m sorry’ akatamka kwa sauti ya chini
‘Hiki sio kitu nilichoomba kuambiwa… nataka kujua ulikuwa na nani… usijaribu kunidanganya Ella… nilitarajia ungekuwa mtu wa mwisho kuanza kusaliti ndoa Ella’ Dennis aliongea kwa hasira mishipa ya shingo ikimkakamaa. wivu ulifikia nyuzi sentigredi mia! Mtenda akitendewa ujihisi anaonewa.

‘… Nilikuwa na Francois’ Daniella akajibu upesi sana akichelela kuzidi kumpandisha mumewe hasira kwa hisia za usaliti. Jibu lake likaishusha hasira ya Dennis kama mtungi uliojaa maji kisha kupasuka ghafla.

Mshangao ukamtembelea, akamtazama mkewe aliyekuwa anajitoa karibu yake na kurudi kusimama karibu na kitri chake.
‘Francois?!... what the hell is he doing in here?... nilidhani tulishamaliza kesi yake na kumrudisha?’ Dennis alionekana kutoamini
‘I’m sorry Den… amerejea na yupo kule porini…doing the same thing’ kwa unyonge Daniella akajibu akikwepa kwepa macho ya Dennis
‘Sitaki kuhatarisha tena taaluma yangu… kumuepusha na kesi au kifungo… nilikaribia kuchafua image ya kampuni yangu sababu yake… baada ya kujua yupo hapa kwanini hukuniambia?... mnaficha nini?’ Dennis alizidi kuwa mkali

‘hakutaka nikuambie… nilitaka kumuondoa bila kukusumbua’ Daniella akajitetea
‘you have one week!...one week!...i mean seven days!!... kumrejesha Francois anapostahili kuwa…vinginevyo nitachukua hatua mimi mwenyewe’ Dennis akatoa onyo, akatoa amri, akageuka na kuondoka akimuacha Daniella amechoka mwili na roho.
88888888888888888888

Jioni hii ufukweni mwa bahari Sindi na Francois pamoja na mbwa wanapilika pilika muda huu. Mzee yule alikuwa anamfundisha Sindi kuendesha gari. Alijaribu kwa kdti alivyoweza kumuelewesha Sindi namna ya kuwasha gari, gia za kukanyaga na mambo mengine mengi. Sindi alionekana kuwa mwepesi kuelewa na kujaribu achilia mbali kuifurahia ile hali.
Baada ya kujifunza kuendesha na kujaribu mara kadhaa. waliliacha gari kando na kwenda kuketi sehemu iliyo karibu na maji. Sindi aliketi pale akiyatazama maji na kutabasamu wakati Francois akimfuata pamoja na yule mbwa huku akiwa na madafu mawili.

Sindi akalipokea dafu na kulinywa kwa kusikilizia huku Francois akimtazama na kucheka.
Sindi akajinyooshea mkono na kutamka neno sindi!... Mzungu hakumuelewa haraka. Sindi akamnyooshea mbwa kidole na kulitamka jina la mbwa kama ambavyo humsikia yule mzungu akimuita kisha akajinyooshea yeye na kutamka jina lake. Msingi akaelewa sasa na kumtaka arudie jina lake
‘Si-ndi!’ Sindi akalitamka jina lake kwa hatua na mzungu akamfuatisha
‘syindye’ akajaribu kulitamka na namna alivyolitamka kulimfanya Sindi acheke sana
Wakati Sindi akicheka kule porini Adella alikuwa akigomba kwa nguvu na hasira nyingi baada ya aliowatuma kurejea na taarifa za kutokumpata Nadina kabisa. Hakuamini! alikaribia kuishia nguvu kwa hamaniko alilokuwa nalo.

‘Camera zote zichekiwe na niletewe ripoti ya siku nzima ya tukio… natoa saa 24 tena huyu mwana haramu awe hai au mfu niletewe hapa… Joka nakupa kazi ya kumfuatia Meddy… I hope unamjua’ Adella akamtazama huyo joka ambaye aliitikia kuwa anamjua
‘..atakapo kanyaga hapa hakikisha unaye kila anapokwenda nina wasiwasi anajua Nadina alipo…’ akazungumza kwa sauti ya chini yenye hasira kali ndani yake huku akitapatapa.

Alikuwa hajalala wala kula vya kutosha sababu ya kutoroka kwa Nadina. hakuwa mtu wa kushindwa hasa kushindwa katika namna ya kushtukiza kama ile. Alitaka kupambana na Meddy na kumletea maumivu ya kutosha Meddy kama ambayo moyo ulifurahia kuona mateso kwa wengine. Lakini hili tukio la Nadina kutoweka ghafla lilimchanganya mno na hakuwa tayari kukubali kuwa ameshindwa!

Wale watu waliokuwa wakipewa maagizo walipoondoka, Adella aliirusha glasi aliyokuwa nayo mkononi na kuibamiza ukutani kwa hasira. akabaki akihema kwa nguvu, jasho likimtoka japo kiyoyozi kilikuwa kikifanya kazi yake ipasavyo.
88888888888888888888888888

Siku zilikatika kwa kasi, ikawa asubuhi,ikawa jioni siku zikatimia na hatimaye siku iliyokuwa ikiongelewa sana mtaani ikawadia. harusi ya mtoto wa Mzee Agapella, balozi mstaafu na mtoto wa Mzee Okello, mfanyabishara mkubwa bongo walikuwa wanaoana. Kulikuwa na pilika pilika nyingi sana  na mbwembwe za kutosha huku habari ya sendoff ya kifahari aliyofanyiwa Pamella Okello ikiwa ndio imepamba moto.

Wengi walitaka kuona kama ukubwa wa sherehe ya ndoa ungeifunika sherehe ya sendoff ya msichana. magazeti ya udaku yalikuwa na kazi ya kunasa mambo mbalimbali ili kujitafutia upekee wa habari.
Asubuhi hii angavu kabisa iliyobarikiwa mawingu meupe machache yaliyosafiri taratibu ilianzia kwa Agapella. kulikuwa na pilika nyingi sana pale kwake. Watumishi walifanya usafi, walibeba zawadi na kupokea wageni. Wakati yeye Agapella akiwa amejitenga ghorofani akizungumza na simu.

‘Mimi sioni cha ajabu wewe kuwa hapa… nataka watu wakuone… kwanini unaogopa?... Iloma anakuomba… sina nia ya kuwa na wewe na kukuacha…hapana… hatujaachana ndio ila tumetengana na sina mpango wa kumrudia… Iloma… please!.. naelewa…’ Agapella aliendelea kuongea na simu yake mpaka pale aliposikia hatua zikipigwa nyuma yake nay eye kugeuka.

Alikuwa Fiona!
Agapella akaagana na Iloma aliyekuwa aanaongea naye simuni akichelea kumsikilizisha kelele za Fiona. Alimjua.
‘Unafanya nini hapa na nani amekupa ruhusa ya kuingia hapa?’ Agapella akauliza akimtazmaa Fiona kwa hasira
‘… sijatalikiwa na bado mimi ni mke wako halali… na hii ni harusi ya mwanangu wa kufikia…nina haki zote za kuwa hapa’ akajibu Fiona kifedhuli
‘unadhani Jerry anakuhitaji hapa au angependa kukuona hapa?’ Agapella akauliza
‘Sijali nani anataka kuniona au hataki kuniona… ili mradi nina haki ya kuwa hapa na nitakuwa hapa’ Fiona akajibu akitabasamu
‘…usiongozane na mimi, hili sio ombi ni amri’ Agapella akazungumza akianza kuondoka eneo lile

‘Sidhani kama unataka kuleta hali ya viulizo kwa watu kwa kutuona mbalimbali… nilidhani untaka harusi ya mtoto wako iwe ya kipekee bila maswali ya ovyo kuibuka…’ Fiona akatabasamu tena wakati Agapella akiumeza ule ukweli kwa uchungu. Akatulia sekunde tatu na kumgeukia Fiona
‘Okay!... baada ya harusi, ningependa kuona unabeba kila kilicho cha kwako na kurudi ulikotoka… nafasi yako imeshajazwa na mtu mwingine’ Agapella akamshushia nondo kali sana ya utosi. Fiona akaweweseka kwelikweli.
‘Kristus!...’ bado  alikuwa haamini
‘utakuwa kando yangu siku ya leo… lakini hutatambulishwa popote kama mke wangu au mama wa Jerry… malipo ya show utakayoonyesha leo utaipata katika mgao kupitia talaka nah ii itategemea utaigiza vizuri kiasi gani’ Agapella akaonyesha upande wa pili wa roho yake.

Fiona akahisi kizunguzungu wakati akimtazama Agapella anavyoishia. maneno aliyotamkia hakuyategemea kabisa, alizoea kumjibu agapella anavyojua na mwanaume huyu alikaa kimya. imekuwaje? alijiuliza moto ukiwaka kifuani pake. nafasi yake kuchukuliwa na mtu? hili lilikaribia kumzimisha. Akaushika moyo wake kana kwamba ulikuwa uantaka kuchomoka.

Pamella alikuwa chumbani kwake… akiwa ndani ya vazi la kulalia. Mama yake akisoma gazeti kwa sauti, Santina akimuweka rolazi kichwani na Annie akisikiliza zile habari za gazeti. habari ilikuwa inahusu Sendoff ya Pamella. Wakacheka kwa furaha wakizitazama picha za gazetini na kujadili watu maarufu waliohudhuria. Pamella alikuwa na furaha mno. Ilikuwa siku yake ya kipekee na alikuwa anaolewa na mwanaume aliye rafiki yake na kipenzi chake.

Kwa Meddy kulikuwa na utulivu kidogo, alikuwa akijiandaa kumfuata Jerry ili wajiandae pamoja lakini alitaka sana Nadina aambatane naye.
‘hapana… mmh mmh’ Nadina alikataa kwa kutikisa kichwa kulia na kushoto wakati Meddy akimbembeleza watoke wote.
‘Kwanini?’ Meddy akamuuliza akimtazama kwa upendo
‘sina cha kuvaa..simjui mtu uko… ni sherehe ya watu wenye pesa… sistahili hata kuwa nje ya ukumbi achilia mbali kuingia ndani’ Nadina akakataa na Meddy akasikitika

‘Muonekano wako wa nje nitaushughulikia mimi… nataka ujiamini Nadina…nataka ujione ni mtu sawa na wengine…pesa ni nini ikutofautishe na binadamu mwenzio’ Meddy akatetea uamuzi wake
‘Ulikonitoa nilikuwa bidhaa… ulikuwa unaninunua kwa pesa… hukuiona hiyo tofauti?’ Nadina akamuuliza akijisikia vibaya kiasi cha uso wake kupwaya
‘Tulikubaliana hatutazungumzia tena suala la ulikotoka… unavunja makubaliano Nadi..’ meddy akambembeleza na nadina hakuonekana hata kufikiria kukubali

‘hapana!’ akakataa na kuinuka toka pale sofani na kuanza kuelekea jikoni. Meddy akamuita na Nadina akageuka na kumtazama Meddy
‘Hivi unanipenda Nadina?’ akamuuliza na Nadina akatabasamu
‘Sijui…’ akajibu kwa upole tu na kuelekea jikoni akimuacha Meddy akajisikia vibaya kwa jibu lile.

Ilianza ndoa kwenye bustani nzuri ufukweni mwa bahari, mandhari ya jua likizama ilipendezesha eneo zima la kufungia ndoa. mapambo ya kuvutia na watu wachache waliokuwa nadhifu. Jerry Agapella akamuoa Pamella Okello kwa kiapo kitakatifu. Wakitabasamu na kuifurahia siku yao. Meddy msimamizi wake akiwa na uso mtulivu usio na chembe ya kushangilia alijua kwanini. pembeni ya Pamella alikuwa binamu wa Pamella kama msimamizi wake.

Sherehe ya kukata na shoka sasa ikafuatia kwenye ukumbi wa hoteli hiyo ya kifahari. Kulikuwa namuziki wa kuvutia. rangi ya harusi ikiwa Rangi ya maziwa na samawati. Watu waliofahamiana walikutana na kusalimiana kwa furaha kubwa.

Meddy akamuomba radhi Jerry kuwa anamfuata mtu nje. wakati huo baadhi ya watu wakiwa wamesimama na wengine kukaa sherehe zikiendelea. Meddy akatoka na aliporejea alikuwa ameongozana na msichana mrembo aliyekuwa aliyeonekana kujawa na soni kutokana na kule kugeuka kwa watu kumtazama msichana huyo. Alikuwa Nadina.

Fiona aliyekuwa meza moja Agapella alitoa macho na kuachia mdomo wakati akimtazama Nadina alivyopiga hatua na kutembea kwa madaha huku akiwa amemshikilia mkono Meddy..
‘Nadina!!!’ alishangaa, alishangaa akilitamka jina la Nadina kwa sauti kidogo. Ilikuwa kama kuona mzuka. Alikodoa macho kwa bidii zote.

Kati ya watu waliogeuka kuwatazama Meddy na Nadina ni Santina ambaye sasa alikuwa karibu na Pamella wakiongea na baadhi ya watu. Santina ndiye aliyemgusa Pamella na kumuonyesha aliko Meddy. moyo ukimpasuka vibaya mno kumuona Meddy na msichana mwingine, tena akiwa ameshikwa vile.

‘Nadinaaa!!’ Pamella naye alishangaa akiliita jina la Nadina
‘unamjua?’ Santina akamuuliza kwa kiherehere
‘Oh my God!...’ Pamella akazidi kuhamanika akiwa mdomo wazi akimtazama Nadina kwa mshangao wa wazi kabisa. hakuamini!

Hawakuwa peke yao waliokodoa macho na kushangaa kumuona Nadina pale, Dennis Mazimbwe alikuwa mmoja kati ya watu waliovua miwani na kumtazama vizuri binti wa watu
‘Nadina…’ akatamka kwa sauti ya chini wakati akivua miwani na kumtazama Nadina anavyozidi kusogea.
‘unamfahamu?’ mkewe akamuuliza akishangaa
‘This is impossible…Nadina!’ Dennis alishangaa waziwazi akimfuatisha Nadina kule alikokuwa akielekea. ni Jerry pekee alitabasamu kumuona rafiki yake na binti yule, sasa alianza kuamini kuwa Meddy alikuwa amempenda kwa dhati msichana yule.

ITAENDELEA….

NIPE MAONI YAKO MSOMAJI

4 comments:

  1. Maisha yangu Maajabu yanashangaza ushuhuda, Jinsi nimepata kisanduku chenye nguvu sana ambacho sasa ni pesa yangu mara mbili kutoka mia hadi elfu ya pesa ndani ya masaa 24, na pia jinsi nimerudisha mpenzi wangu wa zamani, sababu kuu niliwasiliana na Dk Lomi kwa msaada mimi kumrudisha mpenzi wangu wa zamani, basi ananisaidia ni nguvu kubwa ya kumrudisha mpenzi wangu wa zamani, na ananipenda na ananithamini sasa, basi mimi na Dr Lomi tukawa marafiki, baada ya mazungumzo kadhaa namuuliza ikiwa kuna njia anaweza kuniganga ili nipate pesa, hapo ndipo aliponiambia juu ya sanduku hili la uchawi, akaniambia kuna aina na saizi tofauti ya sanduku, aliniambia aina zote za sanduku, ningeweza kumudu ndogo tu ya sanduku, baada ya maombi muhimu anayofanya kwenye sanduku, ananipeleka kupitia huduma ya kujifungua, aliniambia niweke pesa ndani, niliweka ndani ya sanduku 100 euro baada ya masaa 24 nikagundua ilikuwa elfu 10 euro ndani, na nimekuwa nikitumia sanduku kwa miezi 7 sasa, mimi na mchumba wangu tunaishi maisha bora, ikiwa unahitaji b ack mpenzi wako au pesa spell wasiliana na Dr Lomi kwa barua pepe: lomiultimatetemple@gmail.com au WhatsApp namba +2349034287285 unaweza pia kumwandikia kupitia Jina la Mtumiaji la Snapchat: drlomi20 atakusaidia nje, asante kwa kusoma,

    Kwaheri Gerd Ulrich

    ReplyDelete
  2. Sikuamini kuwa ningeweza kuungana tena na mpenzi wangu wa zamani, nilipatwa na kiwewe nikiwa nimesimama peke yangu bila mwili kusimama na mimi na kuwa nami, lakini nilipata bahati sana siku moja nilikutana na mchawi huyu wa hodari Dk. ASUBUHI, baada ya kumueleza hali yangu alifanya kila liwezekanalo kumuona mpenzi wangu anarudi kwangu, kweli baada ya kunifanyia uchawi mpenzi wangu wa zamani alirudi kwangu chini ya masaa 48, mpenzi wangu wa zamani alirudi akiniomba kuwa hatawahi. niache tena, miezi 3 baadaye tulioana na kuoana, ikiwa pia una hali sawa. Ana nguvu nyingi katika mambo yake;
    *penda uchawi
    * kama unataka ex wako nyuma
    * Acha talaka
    *kuvunja mawazo
    * huponya viharusi na magonjwa yote
    * uchawi wa ulinzi
    *Ugumba na matatizo ya ujauzito
    Wasiliana na Dk DAWN kwa barua pepe yake: dawnacuna314@gmail.com
    Whatsapp: +2349046229159

    ReplyDelete
  3. Sikuamini kuwa ningeweza kuungana tena na mpenzi wangu wa zamani, nilipatwa na kiwewe cha kusimama peke yangu bila mwili wa kusimama na kuwa nami, lakini nilipata bahati sana siku moja nilikutana na Dk DAWN, baada ya kumwambia. kuhusu hali yangu alifanya kila liwezekanalo kumuona mpenzi wangu anarudi kwangu, kiukweli baada ya kunifanyia uchawi mpenzi wangu wa zamani alirudi kwangu chini ya masaa 48, mpenzi wangu wa zamani alirudi huku akiniomba kuwa hatoniacha kamwe. tena. Miezi 3 baadaye tulioana na kuoana, ikiwa una hali sawa. Ana nguvu nyingi katika mambo yake;
    * upendo
    inaelezea * inaelezea kivutio
    * kama unataka ex wako nyuma
    *acha talaka
    *kuvunja mawazo
    * huponya viharusi na magonjwa yote
    * uchawi wa kinga
    *Ugumba na matatizo ya ujauzito
    * bahati nasibu
    * bahati nzuri
    Wasiliana na Dk Ediomo kwenye barua pepe yake: dawnacuna314@gmail.com
    Whatsapp:+2349046229159

    ReplyDelete
  4. Kwa zaidi ya miaka 13 ya ndoa sikuweza kuzaa, naendelea kuharibika hata nikipata mimba, madaktari wote hawakuweza kunisaidia, hadi dada yangu akanielekeza kwa Dr DAWN, ambaye alinisaidia nikapata ujauzito na sasa hivi kuwa na mtoto mzuri wa kike,
    Anasaidia pia marafiki zangu wengi niliowaelekeza, Dr DAWN ni baraka kwa kila mtu anayewasiliana naye,
    *Kama unataka kupata mimba.
    *Ukitaka kuacha kuharibika kwa mimba.
    *Ukitaka kumrudisha mpenzi wako.
    *Kama unataka mume/mkeo arudishwe.
    *Kama unataka kurejesha mali yako iliyoibiwa au Pesa.
    *Ukitaka kutibu aina yoyote ya ugonjwa,
    Wasiliana naye kwa WhatsApp: +2349046229159

    ReplyDelete



Snowfall Widget for Blogger


Snowfall Widget for Blogger