Wednesday, July 17, 2013

SINDI....NA LAURA PETTIE (27)

27

Wakati alipopiga mihayo kwa mara ya pili, Meddy alionyesa hali zote za kutaka kulala. Alikuwa ameishikilia ile simu yake ya mkononi kama pambo Fulani huku akiitikia kwa kichwa kile alichokuwa anakisikia toka upande wa pili.


Akaachia mwayo mwingine na kupiga piga kinywa chake kwa mkono wa kushoto kupunguza makali ya mwayo ule. Alikuwa amechoka na simu ndio vile hakuweza kuikata!
‘Pamella….Pam!’ akaita kwa kituo kama namna ya kumkatisha Pamella simuni
‘….Relax… tulia kwanza…kulia hakusaidii wala kumlaani Jerry hakutabadili hali uliyonayo…sawaa….ndio maana nakwambia utilize kichwa kwanza…. najuaa…najua Pam…sio kwamba nachukulia easy….najua unaumia sana….’ Meddy akabiashana na Pamella na sasa akionyesha hali ya kuyachoka yale mazungumzo.

‘Are we gonna stay awake kwa ajili ya Jerry?.... kama amekukatia simu it means hataki kuongea na wewe…leave him alone kwanza…unavyozidi kumpigia ndio atakavyozidi kukuignore Pamella…. sio kwamba nakuumiza, mi nakwambia ukweli mchungu ambao utakusaidia….we tulia lala kesho nitawekana naye sawa…. trust me nitazungumza naye sawa?....sawa Pam?’ akauliza akitega sikio vema kusikilizia jibu la Pamella naye akakubali kutulia, Meddy akapata ahueni sasa na wakati huo huo akihisi Kengele ikilia.

Akaharakia kuagana na Pamella aliyemkatishia usingizi wake kwa simu yake ya malalamiko kuhusu Jerry kutopokea simu na kisha kumkatia na kuzima simu bila kujua simu yenyewe ilikuwa imepasuliwa mbali na Sindi.

Akaikata ile simu na kuiweka kitandani mkono wa kushoto ukilala na kunyooka kuifikia meza ndogo iliyokuwa na taa ya mezani ambayo ndio iliyoweka mwanga hafifu chumbani mule kwa wakati ule. Akaigeuza saa ndogo ya mezani na kusoma muda. Saa saba kasoro!

Akaguna na kulitupilia shuka mbali, akijiuliza maswali ambayo haya kuwa na majibu kwa wakati ule. Akalifuata vazi maalumu la kulalia mfano wa gauni na kulitupia mwilini, akitoa mule ndani huku akilfunga mikanda yake kwa mbele na kuufuata mlango wa sebuleni.
 Akawasha taa ya sebuleni na kutizama tena saa ya ukutani iliyompa jibu lile lile kuwa ilikuwa saa saba kasoro vichapo kadhaa. Akaguna na kuukaribia mlango.
‘Nani?’ akauliza na kutega sikio
‘Mimi Meddy…fungua basi’ Jerry akajibu kwa sauti ya juu kidogo
‘Wewe nani…’ Meddy akauliza kwa sauti kali akitega tena sikio
‘Jerry bwana…fungua basi aargh’ Jerry akajibu kwa ukali na Meddy akajikuta akiutazama mlango kwa mshangao kana kwamba ule mlango ndio uliomjibu.

akakorokochoa kitasa na kuufungua mlango wa mbao. Akatanguliza jicho moja na kumuona Jerry akiwa amejiinamia hapo mlangoni. Akapata nguvu ya kuufungua hata ule mlango wa chuma. Jerry akaingia ndani sasa akimuacha Meddy hoi kabosa kwa vile alivyokuwa amevaa.

Almanusura acheke kwanza! akaufunga mlango na kumgeukia Jerry akiwa bado na uso uliojaa mshangao uliopambwa na hali ya kutaka kucheka.
‘vipi?’ akamuuliza Jerry aliyekuwa ameketi sofani na kujiinamia
‘ni Pamela?’ Meddy akauliza tena na Jerry akatikisa kichwa kulia na kushoto kukataa kuwa si pamella. Meddy akakunja uso na kumkaribia Jerry zaidi.

‘ kumetokea nini sasa? na hizo nguo vipi tena?’ Meddy akahoji akimshangaa vile  alivyokuwa amevaa Jerry. Alikuwa akionekana mtu tofauti kabisa kwa lile shati kubwa la mtumba na suruali iliyopauka, chini akiwa na viatu vilivyochoka kwelikweli. Hakuwa Jerry anayemjua!

Jerry akashusha pumzi na kuinua uso juu akipatia Meddy jibu
‘Ni Sindi…’
‘amegundua ukweli?’ Meddy sasa akakimbilia kuketi kando ya Jerry na mshawasha wa kujua mengi zaidi ukimpanda, ule usingizi aliokuwa nao ukikimbilia kusikojulikana.

‘Pamella amemvuruga sana…’ Jerry akalalamika  akionekana wazi kuelemewa na hali ya huzuni na kuchanganyikiwa
‘Aisee…mi siwaelewi si wewe wala Pamella…. muda huu nimetoka kuzungumza na Pamella kuhusu wewe na sasa nakusikia wewe ukilaumu kuhusu Pamella….hey guys mna matatizo gani ?’ Meddy alishindwa kuwaelewa

Jerry akasimama ghafla na kushika kiuno, akianza kutembea hatua chache mbele na kisha kurudi pale alipokuwa amesimama. Akashusha pumzi

‘ Nisimzungumzie Pamella… lets talk about sindi…. kuna vitu sivielewi…’ akalalamika
‘Kuhusu nani sasa Pam au Sindi?’ Meddy alikuwa bado hajaelewa
‘Nimesema tumuweke Pamella kando kwanza…it is about Sindi…. dah! hivi sasa kitu kidogo yanazuka makubwa….yaani ana hasira za haraka haraka mno…may be sikuwa namfahamu vizuri but kwa hii tabia ya kutonisikiliza na kuharakia kuzua ugomvi sijui kama tutawezana’ Jerry akatoa dukuduku lake

‘Mmmh!.... haya mengine sasa khe!...’ Meddy akahisi uzito wa tatizo
‘Imagine kapasulia mbali simu niliyomnunulia na ile yangu…. hiyo ni leo…juzi juzi ile tulitibuana kitu kidogo akarusha sahani ya wali niliyokuwa nakula na wala hakuniomba radhi…. ni nini sasa hiki?’ Jerry akauliza akirudia kuketi chini

‘Mmmh…kwa kweli hapo kazi ipo mshikaji….kama ndio tabia zake hizo… think twice Jerry’  Meddy akatoa ushauri wake mwenyewe hakiwa hauamini kama utafaa au lah.
‘…Nimechoka,  naenda kulala tutazungumza kesho’ Jerry akasimama na kuelekea chumba cha wageni akimuacha mwenyeji wake ameketi pale sofani akitabasamu na asijue alikuwa akitabasamia nini.
888888888888888888888888

Asubuhi hii Nyaza alishaamka na kujiandaa. Alikuwa ameketi kitandani akisugua sugua mikono yake kama ishara ya kuwa na mshawasha na mwanzo wa siku yake. alitulia kidogo na kuchungulia nje kisha kuketi sawa tena. Alipousikia mlango ukigongwa akaamka haraka na kwenda kuufungua.
‘Ooh Sakala…’ Nyanza alimlaki binamu yake kwa furaha na kukumbatiana. Binamu yake akingia ndani na wote wakasimama wakizungumza kilugha kwa furaha kubwa.
‘Vipi upo tayari?’ Sakala akamuuliza
‘nipo tayari…’ Nyanza akaitikia akimuonyesha mizigo yake
‘Sasa…’ Sakala akasita kwanza na kuwaza kwa sekunde
‘Nitakupeleka Buguruni ninakoishi kisha mimi nitaelkea mchikichini kuchukua mzigo niupeleke Mwenge kazini….kisha ndio nije nyumbani hivyo utakuwa mwenyewe kwa muda mrefu’ akajieleza.

‘usitie shaka… tutaenda wote huko kwenye mzigo nami niuone mji hapa na pale’ Nyanza akasema kwa furaha na Sakala akaonyesha kulifurahia jibu la Nyanza kwa vile hata yeye alitaka iwe hivyo lakini alihofia uchovu aliokuwa nao ndugu yake huyu ambaye mara ya mwisho kuonana naye na kumpatia mawasiliano yake ilikuwa miaka mine iliyopita.

‘Sawa basi…twende zetu’ Sakala akamsaidia Nyanza baadhi ya vitu na kutoka nja ya chumba
‘Ngoja nimuage jamaa f’lani aliyenisaidia simu jana’ Nyanza akaonyesha uungwana wake na kugonga chumba cha pili huku Sakala akitangulia mapokezi. Punde wote walikuwa nje wakikifuata kituo cha daladala.

Nyabnza Mugilagila ndio  alikuwa ameingia mjini rasmi. Kicwani mwake kulijaa mengi mno lakini kikubwa kikiwa kumuona tena Sindi Nalela. tangu alipotoka kijijini mpaka dakika ile alishapisha na watu wegi mno wake kwa waume. alishapishana na warembo wa kila aina lakini hakuna aliyemfikia Sindi Nalela mbele ya macho yake.
88888888888888888

Saa tano asubuhi pilika pilika zikiwa zimepamba moto. Jerry alikuwa na Meddy mezani wakipata staftahi. Jerry akionekana kutopea mawazoni. Meddy akainuka na kuelekea jikoni kisha akarudi na juisi kwenye glasi, akaiweka mbele ya Jerry.
‘I wish ningekuwa najisikia hata kunywa hata maji’ akajitetea akiisukumia mbali ile juisi
‘Tell her the truth…it will set you free Jerry…’ Meddy akamuwekea wazi
‘How?...nianzeje asi-panic?.... maana now kila aninalofanya ni nalaumiwa umenibikiri umeniharibia maisha…my man did this my man did that…laiti ningejua it was gonna turn my life to hell hata kumgusa nisingemgusa’ Jerry alijilaumua na kumfanya Meddy acheke kwa sauti kubwa.

‘…Be a man!...face her like you faced her ulipombikiri…. and it is gonna be that way mpaka ajue mahusiano si bikira….lile ni geti tu la kuingilia kwenye ulimwengu wa mapenzi…. she is gonna learn it polepole…. ‘ Meddy alisema akicheka na akishindwa kumhurumia Jerry

‘…pamoja na yote I lover her…’ Jerry akakiri akijilazimisha kutabasamu
‘Kuliko Pam Okello?’ Meddy akamchokoza na Jerry akajikuta akicheka na kutishia kumpiga ngumi Meddy aliyenyanyuka akiendelea kucheka na kwenda kuongeza sauti ya wimbo wa bebe winans wa I wanna be the only one, akaucheza kidogo na kutikisa kichwa kuashiria alikuwa anaukubali mno

‘Unanikumbusha yule demu wako wa kimasai…dah! yaani ilikuwa ukiingia ukitoka ni I wanna be the only one …the only one…waaapi hahahaaaa’ Jerry akacheka akimkumbusha Meddy inshu za zamani na Meddy akacheka zaidi

‘Yule aisee…. yaani mtu angeiambia angekuja kunisaliti vile ningemkata mapanga…. sitaki kukumbuka but yeeeah the girl was was hoot…I miss her na nikiisikia huu wimbo namkumbuka mno…nitamtafuta tu na atarudi tu….’ Meddy akajibu akirejea mezani na mazungumzo yakichangamka na kubadilika.
88888888888888888888888

Jioni ya siku hii, Sindi Nalela alikuwa gengeni, baada ya manunuzi ya vitu alikatisha barabara ba kurejea kwake. Akawakuta kina mama uani wamekusanyana wakichambua chambua nguo za mitumba.
‘we mama Jerry njoo uchague huku angalau mzee akija akuone mpyaaa’  Jamila alimtania na Sindi wakati akiingia pale uani na Sakala akiwa ameketi kwenye kiti akimtazama Sindi. Alikuwa peke yake kwa wakati ule akiwa amemuacha Nyanza kule mwenge nay eye kuletea wateja wake nguo huku Sinza.

Sindi hakujibu wala hakuzisogelea hata zile nguo, aliingia chumbani kwake moja kwa moja
‘Huyu dada mzuri jamani khaaa!....anaitwa nani?’ Sakala akauliza ikiwa ni mara yake ya kwanza kumuona Sindi pale licha ya kuja mara kwa mara
‘We jina lake la nini?...’ Jamila akamzodoa
‘Yaani mimi nikose mukme kabisa ilasi kuolewa na dereva taksi, muuza genge, fundi cherehani au muuza mitumba…. ona sasa!’ Mwanamke mmoja aliyekuwa akijaribisha sketi kwa juu alitania na kufanya wengine wacheke

‘Wee taratibu mke wa Hashimu asikusikie….mumewe fundi cherehani mwenge kule…’ Jamila akasema akicheka na wengine wakiongezea matani kwa Sakala
‘Kwani mke wa mtu huyu….ila muiteni basi atoke nimuone vizuri….jamani ni mzuri mno dah…muite basi’ Sakala akakazania

‘Nikimuita utanipa sketi hii bure?’ jamila akauliza kimattani
‘Hata ukitaka robota hili lote nitakupa… muite basi jamani’ akabembeleza
Jamiala akacheka na wakati akijiandaa kupaza sauti na kumuita Sindi, Jerry akafungua mlango wa geti la kuingilia pale uani na kuwasabahi wale kina mama na Sakala. Akaingia ndani

‘Mumewe ndio huyo’ Jamila akasema chinichini na kuzua matani mengine na vicheko pale uani


……… TWENDE KAZI…PANAPO MAJAALIWA….

No comments:

Post a Comment



Snowfall Widget for Blogger


Snowfall Widget for Blogger