Thursday, May 9, 2013

SINDI....NA LAURA PETTIE (13)

13


SEHEMU YA 13
….Ilimchukua nusu saa nzima kwa Jenifa kuhisi ukimya uliokuwepo haukuwa wa kawaida. akaliweka gazeti kando na kumtazama mama yake kule kitandani. Kwanza alihisi kama ganzi ikimtembelea mwili mzima kwa mtindo wa shoti, moyo wake ukadunda mara mbili ya kawaida alipoutazama uso wa mama yake.

‘Mungu wangu jamani…’ akapiga yowe akinyanyuka haraka na kukimbilia alipolala mama yake. Alionekana kama mtu aliyetulia huku macho yakiwa wazi. Jenifa akamtikisa mama yake lakini mkono wa kushoto wa mama yake uliposerereka na kudondoka pembeni ya kitandani.



Jenifa alishtuka mno, akajaribu kuunyanyua na kuuachia hewani akitegemea pengine mama yake angeliamka lakini, mkono ule uliserereka tena na kurudi chini kama jiwe lililotupwa hewani. Jenifa akarudi nyuma taratibu, mikono ikiwa kifuani. Taharuki ikiwa imemvaa na hali ya kuchanganyikiwa ikiwa imemtawala.

‘No…Nooo…Nooo’ alirudi nyuma akipiga kelele za kuikataa ile hali, mwili sasa ukimtetemeka kiasi cha meno yake kuonekana yakigongana. Ni muda mfupi tu alikuwa akiongea na mama yake na hali yake ikionekana kuanza kutulia baada ya daktari mwingine kuzungumza naye usiku uliopita kwa muda mrefu sana.

Ni nini hiki kimetokea sasa?....swali lilimpitia akilini wakati akigota ukutani, na machozi kushika nafasi machoni mwake.
‘Mama…Mama’ Jenifa aliita kwa sauti, aliita akiitazama maiti ya mama yake pengine akitegemea angeligeuka na kumtazama. alitamani iwe ndoto na kwa wakati ule akili yake ilisimaam kufanya kazi sawasawa kiasi cha kujikuta akishindwa kumuita daktari na akishindwa pia kuidhibiti taharuki iliyomkumba.

Baada ya sekunde kadhaa alizosimama pale akiweweseka, Jenifa alikurupuka na kutoka wodini mle akikimbilia mapokezi. Koridoni mule akikaribia kuangusha watu wengine kwa kiwewe alichokuwa nacho. Nesi aliyempkea pale mapokezi alimtafuta daktari na wote wakakimbilia wodini alikokuwa Sophia. Ikathibitishwa kuwa ameshafariki!

Jenifa Agapela alipoipokea ile taarifa kwanza aliduwaa kama mtu aliyepotewa na kufikiri kisha taratibu akalegea, akifumba macho na udondoka kama mzigo. Alizirai!

Sophia akawa ameondoka maishani mwa watotot wake, akiwaachia simanzi ya kutosha. Jerry na Jenifa wakamzika mama yao makaburi ya kinondoni. Wakashuhudia baba yao akijitokeza na msiba ukifanyika nyumbani kwake. Akapokea rambirambi kubwa kubwa kana kwamba yeye ndiye aliyemuuguza mkewe.

Kristus Agapela akamzika mkewe kwa mazishi ya gharama, akilia na kuomboleza huku ndugu na jamaa pamoja na watoto wake waliokuwa wakijua namna alivyomtelekeza Sophia wakisikitika na kuumia zaidi. Kutokana na nafasi ya Kristus Agapela kama balozi mstaafu, mazishi ya mkewe Sophia yalihudhuriwa na viongozi mbalimbali maarufu na msiba ule uliripotiwa na vyombo mbali mbali vya habari.
888888888888888888888888

Mwezi mmoja tangu Sophia azikwe. Fiona aliwaita Jerry na Jenifa nyumbani kwao. alikuwa na mazungumzo nao. Alipowaweka mbele yake aliongea mengi yaliyomfanya Jerry amtazame kwa chuki hasa. Lakini alipogusia suala la wao kurejea nyumbani kwao kwa masharti, Jerry alimbwatukia
‘huwezi kuwa mama yangu….na huwezi kuchukua nafasi ya mama yangu’ alimkaripia Fiona ambaye kama kawaida yake aliachia lile tabasamu lake zuri lenye ufedhuli ndani yake.
‘…na kama huwezi kuniheshimu kama mama yako...it is okay, it means upo tayari kukata mizizi yote inakuunganisha wewe na sisi’ Fiona alimtishia na Jerry akacheka kwa ghadhabu
‘una mizizi gani na mimi?....kauli hii aitoe baba yangu sio wewe…sikutambui’ Jerry alijibu kwa hasira na Fiona akiendela kutabasamu kana kwamba hakuna lolote baya alilooongea Jerry.

Fiona akashusha pumzi na kumgeukia Jenifa, huku akiliendeleza lile tabasamu
‘and you dear?....sidhani kama unataka kuendelea kuzurura mitaani kama mbuzi asiye na mwenyewe….it is time urudi nyumbani na upate huduma zote kama mtoto wa Agapela…. ready to come back?’ Fiona akamuuliza Fiona ambaye alimtazama kwa huruma, alimtazama katika namna ya kuhitaji mno kurudi nyumbani lakini si kwa masharti kama yake aliyokuwa anampa.

Jenifa alishindwa kutoa jibu la moja kwa moja na Fiona aliiona hali ile ya kusita.
‘Uhitaji kujibu now dear….take your time Jeni’ akamwambia kwa upole, akiahamisha uso wenye tabasamu na kumtazama Jerry, akikata lle tabasamu ghafla.
‘Think twice!...’ akampa ushauri uliomfanya Jerry anyanyuke na kumtaka Jenifa waondoke
‘Uhitaji kumburuza Jenifa kwa kila kitu….atachagua what is the best for her…goodluck’ Fiona alijibu kwa mbwembwe akimtazama Jerry usoni.

Wakatoka mule ndani na kuingia mitaani. Kwa wiki nzima walijadiliana lile sharti la Fiona pasipo muafaka. Mwisho wa yote, Jerry alimuweka Jenifa chini na kumwambia uamuzi wake.
‘I’m not gonna bow before her…never!....over my dead body Jeni!.... unajua alichomfanyia mama…right?...how can you live na shetani kama yule na bado ukamheshimu kama mama yako….mama hataweza kupumzika kwa amani uko aliko….ni sawa na kumsaliti mama Jeni….bora ushauri wangu wa kuhamia kwa Pamela’ Jerry aliongea kwa msisitizo ambao haukumwimgia Jenifa hata kidogo. Jenifa alisimama na kutembea hatua chache kisha akamgeukia kaka yake

‘Nitamtumikia kafiri nilipwe ujira wangu…. I have a long way to go….nataka kurudi chuo, nataka kusoma Jerry…ntaka kuishi maisha yasiyo na stress ili nitulie na kusoma… kama kodi tu inakupiga chenga kiasi cha kumtegemea Pamela hiyo karo utaiweza?.... okay! tukaishi na Pamela…..unataka kuniambia Pamela atanisomesha?...it is my future we are talking about….sio inshu ya wapi nitakaa, kula na kulala’ Jenifa naye alijitetea.

‘Siamini umeamua kusurrender Jeni….’ Jerry alisikitika
‘sina uchaguzi mwingine…. naumia sana kumpoteza mama….naumia zaidi kuwa nataka kumlamba miguu mtu aliyesababisha mama apate hali ile iliyomtoa uhai….lakini nifanyeje?....ameshika mpini sisis tumeshika makali…. huu ndio wakati wa kumuweka karibu adui yako upate unachotaka…it is not a time kufight against her….we will lose Jerry….hatutafika popote’ Jenifa aliongea kimsisitizo akirejea kuketi mbele ya kaka yake katika kumshawishi ajiunge naye upande wake.

Jerry akakataa akakataa katakata
‘Nitafia mitaani Jeni…. kumtegemea Pamela ni tusi tosha kwangu lakini kumsujudia Fiona ni zaidi ya tusi katika maisha yangu…. nakutakia mema Jenifa kama unadhani ni bora kurejea nyumbani kumtumikia Fiona…then well ni uamuzi wako ila kwangu I wont back off….Never’ Jerry alitoa msimamo wake na kunyanyuka, akiondoka na kuelekea nje.

Jenifa akamtazama mpaka aliporudishia mlango. Akabaki mwenyewe pale sebuleni.
Akalia peke yake kwa muda, akiitazama picha ya mama yake iliyokuwa kwenye meza ndogo hapo sebuleni.

Wiki chache zilizofuata, Jenifa alrudi nyumbani kwao, akikubali masharti ya Fiona. Akapokelewa na maisha yakaanza. Maisha ya unyeyekevu na utiifu kwa Fiona kwa mwezi mmoja tu yalitosha kumhakikishia angeingia chuo mwkaa unaofuata, alinunuliwa gari na kupewa kila alilohitaji. Fiona alimuweka Jenifa karibu yake zaidi kumkoga Kristus kuwa alikuwa mwanamke bora kwake na kwamba alikuwa anawapenda watotot wake.
Mapenzi ya upofu yalimuonyesha Kristus kuwa hakukosea kumchagua Fiona kuwa mkewe. akampenda maradufu!

Maisha ya Jerry na Pamela katika nyumba moja hayakuwa na  amani hata kidogo. Jerry alilazimika kuvumilia kumuona Pamela akitolewa outing na wanaume aliokuwa nao katika uhusiano ilhali yeye Jerry alikuwa anampenda Pamela.

Aliumia sana kumkosa Pamela na matarajio yake kuwa endapo wangeishi pamoja basi uhusiano wao ungekuwa imara yalififia na kutoweka. Alijikuta katika jakamoyo kubwa la kuvumilia asivyostahili kuvumilia huku Pamela akionekana kutojali hisia zake kabisa.

Pamela aliung’ang’ania urafiki aliodhani ndio hasa ulipaswa kuwepo kati yao na si mapenzi ya wapendanao kama Jerry alivyotaka. Pamoja na misaada ya hapa na pale, Pamela Okello alizidi kushikilia msimamo wake hata baada ya kukutana kimwili na Jerry mata mbili zote bado Pamela alimuwekea Jerry vikwazo.

Uvumilivu ulipofikia kikomo Jerry aliondoka nyumbani kwa Pamela na kwenda kuishi na rafiki yake Meddy akihisi pengine kule kumtegemea sana Pamela andiko kulikomfanya Pamela amkatae. Maisha hayakuwa rahisi hata kidogo changanya na mapenzi yake kwa Pamela Jerry alikuwa katika wakati mgumu zaidi.

Miezi michache baada ya kuondoka kwa Pamela, Jerry alifanya jaribio la kusikitisha, alitaka kujiua! tukio lile lilimfikia Mzee Kristus Agapela na mara moja katika maisha yake alijikuta akijiuliza ni nini alikuwa anafanya! Kwa mara ya kwanza katika maisha yake hakumsikiliza Fiona alipomtaka asimtembelee hospitali alikokuwa amelazwa akiondolewa sumu mwilini.

Kwa mara ya kwanza katika maisha yake alimkumbuka marehemu Sophia, mara tu alipomuona Jerry akiwa mahututi hospitali na siku hiyo ndio aliyolia machozi mbele ya kijana wake akiiona taswira ya Sophia!

Alipotoka Hospitali, Mzee Agapela alibadilia umiliki wa kampuni yake ya mafuta ya Agape Oil na kuandika jina la Jerry. Akamkabidhi mwanaye awe mmiliki na mkurugenzi na hapo ndipo vita ya Fiona kwa Jerry ilipoanzia!.

Maisha yalibadilika ghafla, Jerry alibadilika pia, toka kijana wa mtaani akisotea maisha mpaka kuwa Mkurugenzi wa kampuni ya mafuta. Akamiliki nyumba yake, magari yake, vitega uchumi vyake na zaidi matumaini ya kumpata Pamela Okello yalizidi kukua.

Alikosea! Pamela alizidi kumuweka karibu kama rafiki na sio mpenzi! Kuimarika kwa Jerry hakukumfurahisha Fiona hata kidogo. Alichunguza hili na lile na siku moja alimhoji Dennis Mazimbwe wakili wa Agapela kuhusu aliyeandikwa katika usia na

Dennis akamjibu kuwa Jerry ndiye mrithi mkubwa. Alipewa jibu lile pasipo ushahidi lakini alimuamini Dennis na alipochanganya akili yake na ukweli kuwa Agape Oil ilikuwa chini ya umiliki wa Jerry, Fiona alihisi tonge lake likimegwa na hatimaye kupokonywa! Aliamua kulipigania!

Ukweli ulikuwa usia wa Kristus Agapela ulimtaja Fiona kama mrithi wa  robo tatu ya mali zake zote. Ukweli huo ambao laiti tu Fiona angeliujua basi angelitulia na kuishi maisha yake kwa amani ndio ulikuwa ukimuangamiza Fiona akitaka kupambana kuikamata mali ya Kristus, mume aliyekwanyua toka na rafiki yake kipenzi marehemu Sophia!

Uhusiano kati ya baba na wanawe ulizidi kushamiri na kumtisha zaidi Fiona. Akawaamua kuwafarakanisha, na ufedhuli wake ulimfanya amtafute mtu amfanyie kile alichotaka. Pesa mwanaharamu! Akampatia Jenifa gari jipya la kisasa alilopewa na mumewe na kisha akampa kazi!
Kazi ya kuandika ujumbe mfupi katika simu ya Jerry kwenda kwenye simu ya Fiona kuonyesha anamtaka kimapenzi. Akampa kila kitu cha kuandika na Jenifa akamsaliti kaka yake na kufanya alivyoambiwa.

Kasheshe iliyoibuka hapo ilikuja kutulizwa na viongozi kadhaa wa kanisa. Mzee Agapela alikaribia kumuua kijana wake kwa ghadhabu na Fiona akichochea kwa kukaa kimya bila kuongea lolote akidai hataki kugimbanisha familia ila ushahidi wa simu ndio uongee!

Jerry alijitetea sana lakini ushahidi wa simu ulimfanya ajikute akimuomba masamaha baba yake kwa kosa ambalo hakufanya. Kitendawili cha nani aliyemfanyia umafia huo kilibaki kichwani mwake bila jibu!

Iliwachukua zaidi ya miezi sita kwa baba na kijana wake kukaa meza moja na kupata chakula kama familia na ndio wakati wakijaribu kurejesha mahusiano yao katika mstari. Jerry akatoweka! akapotea! Baba akihisi ametekwa kwa ajili wa watekaji kudai fidia na hilo halikutokea. Alikuwa amekosea adui yake alikuwa mkewe!

Fiona alikuwa amemamua kummaliza Jerry baaada ya kuona mbinu yake ya kuwafarakanisha imeshindwa. na wakati ule alikuwa akisheherekea kifo cha Jerry! Alikuwa amekosea, Jerry alikuwa bado mzima wa afya!

Jerry alikuwa akihisi baba yake alikuwa abado hajamsamehe kwa kosa ambalo hakulifanya na hakuwahi kufikiria kulifanya na ndio alitaka kumuadhibu kwa kumuua. Alikuwa amekosea, adui yake alikuwa mama yake wa kambo!


.....SASA UMEJUA NI NINI KINAENDELEA KWENYE FAMILIA YA BALOZI MSTAAFU .....

No comments:

Post a Comment



Snowfall Widget for Blogger


Snowfall Widget for Blogger