Thursday, May 16, 2013

INAKUWAJE?.... JAMANI SOOOO SAAAD....DARLIE, MAMA ANAYENGOJA HUKUMU YA KIFO KWA MAUAJI YA WANAWE....


Nyumba ya Darlie na Darin Routier
Yalikofanyika mauaji
June 6 mwaka 1996, polisi wa mji wa Rowlett ukoTexas walipokea simu ya dharura toka nyumbani kwa familia ya Routier. Katika simu hiyo Mwanamama Darlie Routier alikuwa akipiga kelele za hamaki na kudai yeye na wanawe wawili wa kiume walikuwa wamevamiwa na kuchomwa visu na mvamizi na kwamba watoto wake walikuwa wana hali mbaya ya kukaribia kukata roho.



Kelele zile za hamaki zilimuamsha mumewe aitwaye Darin Routier ambaye alikuwa amelala ghorofani na mtoto mdoo aitwaye Drake,  kwani ndio ilikuwa saa 2:30 usiku. Darin alikurupuka na kukimbilia sebuleni ambako masaa machache kabla ya kwenda kulala alikuwa pamoja na mkewe na wanawe wawili wa kiume wakitazama TV. Darin alipoingia pale sebuleni alishuhudia damu ikiwa imetapakaa kwenye miili ya watoto wake wawili na mkewe.

Akiwa ametaharuki na pasipo hata kumuuliza mkewe aliyeonekana kuchanganyikiwa kwa tukio lile, Darin alimuinamia mtoto wake Devon (6) aliyekuwa hapumui na kujaribu kumpatia huduma ya kwanza kwa kuigandamiza mikono yake kifuani pa mtoto wake na kukikanda kanda kile kifua ili kumrejeshea uwezo wa kupumua, haikusaidia!

Darin alijaribu kumziba pua kwa viganja vyake kisha kupulizia pumzi midomoni mwa Devon ambaye alikuwa bado hapumui lakini damu nyingi  ilimrukia Darin usoni na wakati huo huo Damon (5) mtoto mwingine wa Darin akiwa na jeraha lililochimbika kifuani alitapatapa kuitafuta pumzi.

Devon na Damon Routier
Enzi za uhai wao

Muda mfupi baadaye eneo la nyumba yao lilijaa magari ya watoa huduma ya kwanza, waliofika na polisi. Wale watoa huduma ya kwanza walikuwa wakihangaika kuokoa maisha ya watoto hawa huku polisi wakijaribu kumtafuta huyo mvamizi ambaye kwa mujibu wa Darlie Routier alisema alikuwa amekimbilia eneo la wanaloegesha gari lao (huku tunaita gereji lol)  lililokuwa sehemu ya nyumba yao.

Askari polisi  David Waddell and sajenti Matthew Walling walikiona kisu kilichokuwa na damu juu ya kabati fupi eneo la jikoni, pochi ndogo ya mkononi ya Darlie pamoja na kidani aghali. Vitu vyote hivi vilikuwa karibu na kile kisu.
kulikuwa na mpasuko kwenye kioo cha dirisha la gereji pamoja na matone ya damu sakafuni.

Watoa huduma ya kwanza hawakuweza kuwaokoa watoto wale, majeraha waliyokuwa nayo yalikuwa makubwa mno. Kisu kilichotumika kuwachoma kilizama ndani zaidi na kuchimba vifua vya watoto hawa kiasi cha kuchana mpaka mapafu yao
Walikufa vifo vya maumivu makali sana. Majeraha ya Darlie ambaye ni mama yao mzazi hayakuwa makubwa kiasi cha kuhatarisha afya yake, yalionekana kuwa majeraha ya kawaida sana wakati Darlie alipokuwa akitoa maelezo ya tukio lile la kuogofya.

Majeraha ya Darlie

Darlie Routie akiwa amesimama ndani ya gauni la kulalia lililokuwa limetota damu aliwaambia polisi kuwa anachokumbuka ni kule kuvamiwa kwake na watoto wake basi. Alisema mvamizi aliingia ndani akiwa amelala kwenye kochi na wanawe wakiwa wamelala sakafuni huku luninga ikiendela kuwaka, alizinduka na kupiga kelele huku kujaribu kupambana naye. Darlie alisema mvamizi yule alimjeruhi na kukimbilia eneo la ‘gereji’ na hapo ndipo alipogundua watoto wake wawili walikuwa walikuwa ndani ya dimbwi la damu

Akadai hakusikia kitu chochote wakati watoto wake walipokuwa wakiuawa kwa kuchanwa na kisu kifuani. Alimuelezea mvamizi huyo kama mtu mwenye urefu wa kadiri, aliyevalia T shirt  na suruali vilivyokuwa na rangi nyeusi pamoja na kofia aina ya Cap.

Darlie na Darin walipelekwa hospitali huku nyuma Polisi wa Rowlett, Texas waliifunga nyumba na kuanza uchunguzi.


Darlie, Devon, Damon na Darin kabla ya sakata
hapa alikosekana Drake....

UCHUNGUZI WAANZA….



Ndani ya siku kumi na moja tangu mauaji yae yafanyike. Polisi wa Rowlett walimuweka chini ya ulinzi Darlie Routier kama mtuhumiwa namba moja, pia wakimfungulia mashtaka ya mauaji ya watoto wake.
-           Afisa aliyezifanyia uchunguzi maiti zile Janice Townsend-Parchman alisema majeraha ya watoto wale yalikuwa makali na yaliyochimba kuelekea ndani zaidi kulinganisha na majeraha ya Darlie ambayo kuna uwezekano yalikuwa ya kujikwangua mwenyewe.

-                     Mtoa huduma ya kwanza Larry Byford alidai kuwa Darlie hakupata kuulizia hata hali ya watoto wake wakati walipokuwa katika ‘Ambulance’. Alitiliwa mashaka hapa na ni kama alishahitimisha kuwa wamekufa! ile hali ya kutoamini haikuwepo.

-                     Tom Bevel, Mtaalamu wa damu alisema, damu iliyokuwa katika gauni la kulalia la Darlie ilikuwa ya watoto wake na kwamba ilikuwa kama iliyopuliziwa. alifafanua kuwa ilionekaana kama iliyopuliziwa sababu ya mruko wa damu ya watoto wake pale alipokuwa akiwashindilia kisu kwa nguvu nyingi

-                     Nesi katika hospitali aliyohudumiwa Darlie alisema kuwa, Darlie hakuonekana kuwa mzazi mwenye kuguswa na vifo vya watoto wake zaidi ya kujieleza kila mara kuwa alipomfuatilia yule mvamizi (kulingana na madai yake) alikiona kisu na kakishika hivyo kuacha alama za mikono yake katika kisu  katika kisu

-           Kitu kingine kilichomtia hatiani Darlie ni damu iliyokutwa  chini ya mashine ya kusafishia carpet (vacuum cleaner) pamoja na kwenye mashine yenyewe ambayo inaonekana iliweka pale baada ya tukio.

-           Charlie Linch, mtaalamu wa kutambua alama alisema haikuwa rahisi kwa mvamizi huo kuondoka bila kuacha ahta mtone la damu, hii ni kutokana na kutoonekana kwa damu yoyote nje ya nyumba ya Routier

             Mpelelezi wa FBI Al Brantley, alitoa ushahidi wake kwa kusema sehemu ya kioo kilichokatwa ilikuwa ni sehemu ambayo muuaji angeweza kukiondoa pasipo haya kukivunja kioo. Pia, aliongeza kuwa kidani aghali cha Darlie hakikuwa kimeguswa hivyo kuondoa dhana kwamba aliyewavamia alikuwa ni mwizi. Kuna wakati Darlie alidai mvamizi yule alitaka kumbaka, na kwa dai hili mpelelezi Brantley alidai kama nia ilikuwa ni kumbaka basi muuaji angewatumia watoto wa Darlie kama mateka na si kuwaua  ili kutimiza azma yake. Mwisho alidai kuwa unyama waliofanyia watoto wale kwa maoni yake binafsi ni kuwa ni tendo lililofanywa na mti aliyekuwa na hasira za hali ya juu dhidi yao na sio mtu baki ambaye hakuwafahamu wale watoto.
-           Darlie aliposimama mbele ya jopo la wanasheria, aliulizwa kwanini alikuwa akitoa maelezo tofauti tofauti kwa polisi, walimuhojii kuhusu mbwa wake ambaye hubwekea watu asiowajua, kwamba ilikuwaje mbwa huyo hakubweka wakati mvamizi/ muuaji alipowavamia na kuingia ndani. Walimuuliza kuhusu eneo la jiko lake lililoonekana kufanyiwa usafi lakini bado likakutwa na matone ya damu katika sehemu zilizojificha. Katika maswali haya yote, Darlie Routier alikuwa akijibu kuwa hakumbuki ama hajui!
jopo la majaji lilimtia hatiani Darlie Routier na kuhukumiwa kifo!
 Watoto wake wakazikwa kwenye jeneza moja ndani ya kaburi moja, wakiwa wameshikana mikono. Soooo Sad!

LAKINIII.....
upande wa pili uliopingana na hukumu ya  kesi ya Darlie ulidai ushahidi wa kimazingira na nadharia ndio ulitumika zaidi kumtia hatiani Darlie. upande huu ulidai hukumu haikuwa ya haki kwani kuna sehemu za ushahidi hazikujadiliwa na jopo la waamuzi.

Darlie Routier
pamoja jitihada zote za familia yake kumuokoa
Anangoja hukumu ya kifo muda wowote kwa miaka 17 sasa!!

Mwanasheria aliyeendesha kesi ya Darlie alikuwa  na mgongano wa kimaslahi kwa vile alionana na Darin Routier (mumewe Darlie) na familia yake na kuwataka kutofanya utetezi wa aina yoyote ambao ungemuweka Darin matatani. Mwanasheria huyu alituhumiwa kuzuia kumalizika kwa ushahidi wa kisayansi (Forensic Evidence) wenye nia ya kumtetea Darlie.
kulikuwa na alama za vidole vyenye damu kwenye sehemu ya meza pale sebuleni, alama hizi za vidole hazikufanana na za Darlie, Darin, watoto wala mtu yoyote wakiwemo polisi waliofika nyumbani kwa Routier kwa ajili ya uchunguzi. Mkanganyiko huu ulikinzana na ushahidi ulioonyesha kuwa hakukuwa na alama za vidole hata nje ya nyumba ya Routier.
  UTETEZI WA DARLIE ULITAKA KUJUA YAFUATAYO…..
-                     Zile alama za vidole vyenye damu mezani sebuleni, ni za nani?

-                     Kulikuwa na alama hizo zilionekana kwenye mlango wa ‘gereji’ ni za nani?

-                     Suruali ya Jeans ya Darin ilikuwa na damu, damu ile ni ya nani?

-                     Kulikuwa na damu kwenye moja ya mashati ya Darlie, ilifikaje kwenye shati na ni ya nani?’

-                     unywele unaosemekana ni wa sehemu za siri ulikuwa sebuleni wa Routier, unywele ule ni wa nani?

-                     Darin Routier aliwahi kukiri kujaribu utapeli wa bima ambao alipanga ufanyike kwa kisingizo cha kuibiwa nyumbani. Alikiri kuwa alikuwa kati hatua za awali za kufanya hivyo na wizi huo bandia ungetokea wakati ambapo kusingekuwa na mtu ndani. kukiri huku kwa Darin hakukufikishwa mbele ya jopo la majaji

-                      Video ya ‘birthday’ inayolenga kuzidi kumtia hatia Darlie ilionyesha Darlie akicheza kwenye kaburi la  mtoto wake pamoja na wanafamilia wengine lakini video hii haikuonyesha mwanzo wa tukio ambapon alilia kwa uchungu juu ya kaburi pamoja na mumewe Darin, kwanini kipengele hicho cha video hakikuonyeshwa kwa jopo la majaji?

-                     Baadhi ya majirani walidai kuona gari jeusi mbele ya nyumba ya Routier wiki moja kabla ya mauaji. Jirani mwingine alidai kuona gari hilo hilo likiondoka eneo la tukio usiku huo wa mauaji. Je taarifa hizi zilifanyiwa kazi?

-                     kuna tuhuma kuwa polisi hawakulinda ushahidi waliotoka nao nyumbani kwa Routier hivyonkuna uwezokano wa kuharibiwa na kuzidi kumdidimiza Darlie. Tuhuma hizi hazikuthibitishwa.

-           Zaidi inadaiwa katika taarifa za awali, zinasema  kioo kilichovunjwa kilionekana kuvunjiwa kwa ndani lakini baadaye ilionekana kilivunjwa toka nje. Watoa huduma ya kwanza walipowasili walidai kumkuta Darin nje ya nyumba lakini ukweli ni kuwa Darin alikuwa ndani akiokoa watoto wake.

Mwanaume aliyeonekana nje alikuwa ni nani? na je ni kweli alionekana? Daktari  aliyemtibu Darlie alisema jeraha la Darlie shingoni alikuingia ndani sababu lilizuiwa na mkufu aliokuwa amevaa. mkufu huo ndio ulioharibika na hivyo kuzuia kisu kuzama ndani. Je jopo la majaji haliokuona jambo hili kama jambo lenye uzito katika kesi hii. Mtu angewezaje kujidhuru namna ile. Uchunguzi -  wa kisayansi unaohusisha damu haukufikia tamati wala kufikishwa mahakamani. Je ni kwanini na kwa maslahi ya nani?

-                           baadhi ya waandishi walijitokeza kuwa upande wa Darlie lakini walikuwa wakizuiwa kuonana na Darlie.

 WALIKOTOKA DARLIE NA DARIN......
Darlie na Darin Routier walikuwa wapenzi tangu Darlie akiwa high school, mwaka 1988 walifunga ndoa mara baada ya Darlie kumaliza shule. Mwaka 1989 walibarikiwa mtoto wao wa kwanza Devon Rush Routier na mwaka 1991 walipata mtoto wao mwingine Damon Christian Routier, kisha baadaye walibarikiwa tena kupata mtoto wa mwisho Drake ambaye wakati wa mauaji alikuwa amelala na baba yake.

Kwa kadiri familia yao iliyokuwa ikiongezeka, ndivyo pia biashara ya Darin iliyohusiana na Computer ilivyozidi kushamiri. Familia ikahamia sehemu nzuri ijulikanayo kama Dalrock Heights Addition in Rowlett, Texas. maisha yao yalikuwa mazuri mno kiasi cha kuweza kuzungukwa na vitu vyenye thamani kubwa kama nyumba kubwa, samani, nguo na vidani vyaa gharama, vacation mbalimbali huku pia wakimiliki gari jipya aina ya jaguar pamoja na boti ya kifahari.

Miaka michache baada ya kuishi maisha ya kifahari, biashara ya Darin ilianza kwenda kombo na matatizo ya kifedha kuanza kuwakabili. Uvumi ukaanza kuenena kuwa wanandoa hawa walikuwa katika matatizo ikiwemo suala wa kuwa na wapenzi nje ya ndoa yao. Kwamba Darlie alikuwa akiuchukia muonekano wake na hakuwa na ustahimilivu na watoto. Pamoja na uvumi wote huo 1995, Darlie na Darin walipata mtoto wao wa tatu aitwaye Drake. Baada ya uzazi huu Darlie alipata msongo utokanao na uzazi (postpartum depression).
Darlie akaanza kuhangaika kupunguza unene alioupata kipindi cha ujauzito, kuhangaika uko kukapelekea aanze kutumia vidonge vya diet abavyo havikumsaidia zaidi ya kumletea mkanganyiko wa hisia. aliwahi kumweleza Darin kuhusu kutaka kujiua. May 3, 1996 Darin alimfuma mkewe akilia hukua akiandika katika Diary yake... alichokiandika kipo kwenye kumbukumbu
"Devon, Damon and Drake, I hope you will forgive me for what I am about to do. My life has been such a hard fight for a long time, and I just can't find the strength to keep fighting anymore. I love you three more than anything else in this world and I want all three of you to be healthy and happy and I don't want you to see a miserable person every time you look at me..."
Darin akaamua kuketi chini na kuzungumzia matatizo yao na yajayo. mambo yakaonekana kuanza kutulia bila kujua janga lililokuwa linawanyemelea mwezi mmoja baadaye.
Darlie na wanawe watatu.....

KWA SASA HALI IKOJE….
Darlie bado yupo jela, akisubiri hukumu yake ya kifo mara baada ya rufaa zake kushindwa. Anasema anaumia sana kuona jamii inamhukumu kwa kitu ambacho hakufanya
Amekuwa mtu mzima sasa...Almost 43 yrs old!
Baada ya kusimama na mkewe pamoja akimtetea kama mkewe, Mwaka 2011 baada ya miaka 15 tangu mkewe aingie matatani Darin alimtaliki mkewe rasmi. Ingawa amemtaliki mkewe Darin amesema hategemei kuoa tena maishani mwake wala hataacha kumpigania mkewe anayeamini kuwa hana hatia.

Darin Routier hivi sasa

Drake Router ambaye kwa kiasi kikubwa amelelewa na wazazi wa mama yake ni kijana mkubwa sana sasa hivi. Drake alikuwa mdogo mno wakati mauaji yakitendeka na salama yake ilikuwa ni kulala na baba yake kule ghorofani. Darlie alizuiwa kumkaribia Drake kwa miaka kadhaa. ingawa aliruhusiwa baadaye kumtembelea mama yake, Drake amefanya hivyo mara chache sana na hili lina muumiza mo mama yake.

Drake Routier sasa hivi
huyu ndiye aliyenusurika akiwa amelala na baba yake


JE NI KWELI HUYU MAMA ALIWAUA WANAWE KIKATILI VILE?..... KAMA HAPANA NI NANI SASA NA KWANINI KUWE NA VIJIUSHAHIDI VYENYE KUMBANA DARLIE?.....AU DARIN PIA ANAHUSIKA?.... NI SIRI GANI IMEFICHIKA HAPA?....

Aliingia jela akiwa na miaka 26 tu….mpaka leo amegonga miaka 40 Darlie anasota kwenye kichumba kidogo akilala na kuamka huku akiwazia kifo cha sumu kinachongoja saini moja na kuhitimika!

MWISHO!

SOURCE: MITANDAO MBALIMBALI
TAFSIRI:  LAURA PETTIE




No comments:

Post a Comment



Snowfall Widget for Blogger


Snowfall Widget for Blogger