Thursday, January 16, 2014

USALITI...TALAKA...MAUAJI... NDANI YA MAISHA YA BETTY NA DANIEL BRODERICK



Walipouawa Daniel na Linda Broderick

.....Pengine waliamka asubuhi hii wakiwa na mipango mingi ya kutimiza.. au labda walizungumza mengi na kupanga hili na lile lakini kwa siku hiyo ya  Novemba 5, 1989 Daniel T. Broderick (44) na mkewe  wa miezi nane tu Linda Kolkena Brodreck (28) hawakujua kuwa asubuhi ya siku hiyo ingekuwa ni siku ya mwisho ya uhai wao.

TUANZIE MWANZO KWANZA… PAUKWAAA… PAKAWAAA!
 MUUAJI Elisabeth Anne Bisceglia... 
'Betty' Broderick Mtalaka wa Daniel

Mnamo November 7, 1947 Elisabeth Anne Bisceglia alizaliwa kwenye familia ya Frank Bisceglia na mkewe Marita, akiwa mtoto wa tatu kati ya watoto sita wa familia hiyo. Elisabeth au Betty kama anavyojulikana zaidi alikuwa binti wa kawaida, asiye na purukushani za kwenda na wakati na mwenye ndoto za kuwa mke wa mtu na mama wa nyumbani mwenye kuijali familia yake. Alikuwa ametoka katika familia yenye kipato kizuri tu.


Mwaka 1965 akiwa chuoni, Betty alikutana na Daniel T. Broderick, kijana mtanashati, aliyeonekana kuwa na msimamo, ari ya mafanikio na sifa zote alizohitaji kuwa nazo mwanaume aliyeota kuolewa naye. Na April 12, 1969 miaka minne tangu wakutane. Daniel na Betty walifunga ndoa takatifu katika kanisa la Immaculate uko Eastchester. Alipotoka ‘Honeymoon’ Betty alikuwa na ujaizito wa kwanza wa mtoto wao Kim Broderick na baadaye alimzalia mumewe watoto wengine wanne wakiume wawili ambao ni Daniel na Rhett na wa kike mmoja aitwaye Lee huku mwingine wa mwisho akifariki siku mbili tu baada ya kuzaliwa.

Betty na Daniel siku ya Harusi yao... April 12, 1969
'...aiyaa iyaa kuolewa utarudi nyumbani kutembea...'

Maisha ya wanandoa hawa hayakuwa mazuri sana, Betty alilazimika kufanya vibarua hapa na pale… huyu dada alifanya mpaka kazi ya uyaya kwa majirani zake ili kukidhi mahistaji ya familia wakati huo mumewe alikuwa akimalizia digrii yake ya utabibu katika chuo cha Cornell na hata baada ya kuzaliwa kwa mtoto wake Kim, Daniel aliamua kurudi shule kusomea digrii ya sheria ili kutimiza ndoto yake ya kuwa na ujuzi katika masuala ya kitabibu na sheria pia. Inasemekana Betty alikuwa na mchango mkubwa wa kifedha katika kufanikisha digrii ya sheria ya mumewe aliyoipata chuo kikuu cha Havard… Dada alipenda huyu khaaa!

Aliishi maisha ya kujibana sana… maisha ya kimasikini ili tu aweze kuchangia karo ya mumewe chuoni, amudu kuwahudumia watoto na kuwafurahisha kwa burudani mbalimbali walihitaji, Betty hakununua hata lipstick tu akihofia kuharibu bajeti ya pesa alizopata kwa kufanya vibarua huku na kule. Hakutaka mumewe asumbuke kwa stress ya aina yoyote ile akiwa chuoni hivyo alipambana mwenyewe kutunza familia huku akiamini uvumilivu wake na mchango wake ungeleta matunda mema kwa familia yake mara baada ya Daniell kuhitimu.
Daniel, Betty pamoja na watoto wao
kabla mambo hayajaenda mrama!

WAHENGA WALISEMAAAA…!!

‘Pata pesa tujue tabia yako’…. Mara baada ya kumaliza digrii ya sheria Daniel hakukawia kupata kazi uko San Diego ambako maisha yalianza kubadilika sasa… wakanunua nyumba ya ghorofa moja na vitu vingi muhimu…. hata baada ya mumewe kupata kazi Betty aliendelea kufanya vibarua ili kumpa support mumewe na kujenga maisha yao. Alikuwa mwanamke mtulivu, mcha Mungu mwenye ndoto za kuishi maisha mazuri sana na familia yake.

 
Daniel T. Broderick... Mtalaka wa Betty na mume wa Linda...

Daniel hakukawia kujulikana kwa kazi yake kule alikoajiriwa naye hakuchelewa kutambua thamani aliyokuwa nayo hivyo akafungua kmapuni yake binafsi mnamo mwaka 1978 na mambo yakaanza kuwa mazuri zaidi. Betty alidhani sasa angetulia na kupumzika ili afaidi matunda ya nguvu zake na uvumilivu wake kwa mumewe wa ndoa ya miaka 11 sasa,…mambo yakawa sivyo ndivyo!


LINDA KOLKENA AKAINGIA SASA….

Linda Kolkena siku ya harusi yake na Daniel....

Huyu alikuwa ni binti mdogo tu aliyekuwa receptionist wa rafiki wa Daniel, kabla ya hapo alikuwa mhudumu kwenye ndege na akafukuzwa kwa utovu wa nidhamu wa kunywa pombe kazini na ku ‘flirt’ mmoja wa wasafiri katika ndege. Baada ya kutimuliwa uko ndio akajiweka kwa rafiki wa Daniel kama mtu wa mapokezi…

 Mwaka 1983 hiyo akiwa na miaka 21 tu… Daniel akamuona mtoto mbichiiii… Daniel akachombeza na akakubaliwa…unaambiwa hakuwa na digrii ya medical wala law… wala digrii yoyote ile lakini baada ya kuanza kutoka na Daniel… Linda akapewa cheo cha Legal assistant pale kwenye kampuni ya Daniel… Daaamn! such a descendant of Dalila Lol!!


Penzi kikohozi kukizuia huwezi!... Betty maskini ya Mungu akagundua ukweli… pambana huku na kule…pigania ndoa yake kwa nguvu zooote… yaani ile heka heka ya kuchoma mpaka nguo za mumewe ili aone ni jinsi gani anaumia…waaapi… akatumia njia zote za kike akilia na kununa… akabembeleza na kunasihi waaapi… mume alikuwa anakataa katakata la mwisho akaomba radhi na akajitahidi kujiweka mbali na Linda Kolkena ambaye alitoka uko mikono mitupu akakuta jumba hilooo… akapewa gari la gharama… akapewa ofisi nzuri mno na mshahara juu… kisa ni mistress!! daaah!

 

kipind flani siku ya birthday ya Daniel akitimiza miaka 39… Betty akajibeba na surprise zake mpaka ofisini kwa Daniel..kwani alimkuta?.... au hata huyo Linda alimkuta?... dada wa watu akarudi kulia vya kutosha nyumbani kwake. kipindi hicho wakahama kwenye lile jumba lao na kuhamia nyumba ya kupanga ili kupisha ukarabati wa lile jumba.


TALAKA!!

Linda na Daniel... walipoanza kujiachia kwa nafasi...
unakonda kwa mawazo wenzio waaaaala! meno 42 nje!

Feb, 1984 Daniel aka ‘file’ talaka bwana!... sababu kubwa ni kuwa na uhusiano na Linda Kolkena. Hata msamaha hakuomba, wala hakujishughulisha na Betty kabisa sanasana alipigania haki ya kubaki na watoto na akaipata hivyo alipofungua jalada la talaka akawakomba watoto akarudi nao kwenye lile jumba na kumuacha Betty peke yake kule nyumba ya kupanga na kule kwenye jumba akawa anaishi na wanawe hao wanne na Linda Kolkena! kudadadadeeeki! stress juu ya msongo chini ya hasira!

visa na migongano vikaanza sasa, Betty alikwenda kuwanaona wanawe, alipofika akakuta Linda alimuandalia pie Daniel… kwa vile hawakuwepo basi akaichukua ile pai akaipaka paka kitandani na kwenye nguo akishia zake. Daniel aliporudi akamuwekea kizuizi cha kufika pae kwake.

Betty sasa kaanziasha vita ya kwenye simu… anapiga simu anaacha ujumbe wa maneno akimtukana Linda. Angeacha ujumbe mara nyingi alivyoweza mpaka pale Daniel alipomshtaki na ikawa akiacha ujumbe wowote wenye matusi… kila tusi linachajiwa $100 Lol!..wenzetu hawana mchezo… na wakati huo Daniel akaamuriwa kumpa pesa za matumizi kwani alikuwa hajamtaliki Betty…. baada ya mambo kadhaa ya kisheria akatakiwa kumpa $16,000 pesa iliyoonekana nyingi lakini ukweli ilikuwa dhulumati kubwa kwa Betty kwani Daniel alishirikiana na kaka yake kuficha sehemu kubwa ya mali zake na kwa mwezi pato lake lilikuwa $300,000… jamaaani!!

Vita ile ikasogeaaa… 
Aprili 22, 1989 siku kumi tu baada ya kile ambacho kingekuwa ni sherehe ya miaka 20 ya ndoa yao… Daniel na Linda wakaoana wakimuacha Betty hoooi! Ilikuwa miezi mitatu tangu atalikiwe na kulipwa $30,000 tu. Lile jumba la ghorofa moja lilikuwa limeuzwa bila ruhusa ya Betty kupatikana na sasa walikuwa kwenye nyumba nyingine nzuri zaidi

Daniel na Linda Siku ya harusi....
Kuachwa ni shughuli pevu jamani.....

Maskini sheria aliyodhani ingemlinda na kukosekana kwa uaminifu wa mumewe wala haikujishughulisha kumhukumu kabisa. Mbaya zaidi watoto wake wakionekana kuwa upande wa Linda na baba yao ispokuwa mtoto wake wa mwisho ambaye baadaye alihama toka kwao na kwenda kuishi na mama yake. Waliobaki walikuwa wakimwambia mama yao aendelee na maisha mengine na sio kupambana na Linda bila kujali mamumivu aliyokuwa anayasikia kwa usaliti aliofanyiwa na Daniel

 

MAUAJI….!!

Kitanda kikiwa kimeloana damu ya Linda

Nov. 5. 1989… Asubuhi ya siku ya mauaji Betty aliketi mezani kwake akiwa na barua mbili mbele yake. Moja ilikuwa toka kwa mwanasheria wa mumewe iliyokuwa inamueleza kuwa kutokana na kutokuwa na akili njema ya kuweza kulea watoto, hivyo haki ya kuishi na watoto kwa mara ya pili ilikuwa imekwenda kwa mumewe… na barua nyingine ilikuwa ya deni la pesa alizotakiwa kulipa kwa matusi aliyotuma kwa Daniel na Linda…. ‘I can’t take it anymore’ akaandika chini kwenye barua aliyoiacha juu ya meza.

 

Betty akachukua bastola yake na kuiweka kwenye pochi, akaendesha gari mpaka mbele ya nyumba mpya ya Daniel, akajaribu kupitia mlango wa mbele na akakuta umefungwa, akazunguka nyuma na kukuta mlango uko wazi. Akaingia na kupandisha ngazi kuelekea chumbani ambako aliwakuta Daniel na Linda wakiwa kitandani.


Linda alipomuona Betty alipiga yowe akimtaka Daniel apige simu kuita Police… ukelele ule ndio uliompa kiwewe Betty (kama ambavyo anadai mwenyewe) akajikuta akichomoa bastola yake na kumlenga Bang! Bang!Linda kichwani akaachia risasi mbili za kichwa.. Daniel akajiviringisha kuwahi simu iliyokuwa kando ya kitanda lakini kabla hajaifikia Betty akaachia risasi iliyomkosa Daniel kwanza kisha akaachia nyingine ya kifua na ikampeleka chini Daniel.

 Na kuhakikisha hakuna simu inayopigwa, Betty akang’oa waya simu na kuutupilia mbali.

Muda mchache baada ya mauaji, Betty alimpigia simu binti yake Lee na kumweleza kuhusu mauaji aliyofanya. Akajisalimisha polisi mwenyewe na mnamo Nov. 1991 kesi yake ilianza kusikilizwa mahakamani.

 
Mwaka 1991... 
Betty akiwa mahakamani kwenye muendelezo wa kesi yake

Betty Broderick alihukumiwa kwenda jela miaka 32!!... na mpaka dakika hii yupo jela akijaribu mara kadhaa kuomba kutoka kwa Parole lakini ombi lake limekuwa likitupiliwa mbali. Kati ya watoto wake wanne ni Lee tu ndio humtembelea mama yake na kuzungumza naye, wengine wote wamemtenga na hata kuomba asitolewe kwa Parole!

 
Makaburi wana Daniel na Linda Broderick.

kuna movie na kitabu kuhusu hii story.... 
Inasikitisha sana ila 

WALIMWENGU NDIVYO TULIVYO….!

SOURCE: MITANDAO
MWANDISHI/ MFASIRI: LAURA PETTIE






















1 comment:

  1. natamani niione movie yake pia dogo.du!Mungu atusaidie wanawake jamani mtu kuvumilia kooote unaambulia kula mbovu kabisa.mambo hayo yapo mwenzangu sio story tu.magie -shy.

    ReplyDelete



Snowfall Widget for Blogger


Snowfall Widget for Blogger