Sunday, November 17, 2013

PERUZI YA ENZI.... MUZIKI ASILI YAKE WAPI BY REMMY ONGALA NA LYRICS ZAKE.




NI MOJA KATI YA NYIMBO ZA REMMY ONGALA NINAZOZIPENDA SANA....


Muziki asili yake wapi eeeeee,Muziki ni wa nani eeeeeeeeeeeee,
Muziki hakuna mwenyewe,Muziki ni mwito,
Muziki ni fundisho,Muzi maombolezo kilio
Usinione nikiimba,ukadhani ninayo furaha,kumbe ninayo huzuni moyoni.


Muziki alivyo na nguvu ulimwenguni kote,
Hata makanisani wanaimba kwaya kwa kumuomba Mungu,kumuabudu Mungu,kwa kumsifu Mungu,
Hata kukiwa sherehe za serikali,mbele ya Mwenyekiti kuhutubia,ni Muziki unaanza kuwakusanya watu;
Kumbuka Paulo na Sila waliimba gerezani Mungu amewasikia,
Kumbuka Mussa aliimba Muziki wa aina yake,kuwakomboa wana wa Israel waliopo utumwani katika nchi ya Misri..

Kukiwa na sherehe utaimba nyimbo za furaha,kukiwa na tabu utaimba nyimbo za masikitiko;
Ukifa leo utapelekwa kaburini na nyimbo za maombolezo;
Ni mzuiki pekee ulio na nguvu,utawakusanya wabaya na wazurimsiku ya mwisho Mungu akitoa hukumu.

Muziki sio uhuni,kama muziki ni uhuni kwa nini unanunua kaseti;
Kama muziki ni uhuni kwa nini unaomba nyimbo redioni;
Kama muziki ni uhuni kwa nini kwa nini unanunua rekodi;
Kama muziki ni uhuni kwa nini unacheza muziki weeee;
Kama muziki ni uhuni kwa nini unafanya top ten show...

Kumbuka siku ya mwisho ikifika,kutakuwa mlio mmoja wa parapanda utawakusanya wateule wote,
walioteuliwa katika pembe nne za dunia siku ya mwisho mungu akitoa hukumu,hukumu,hukumu.
Hata kwa Mungu malaika wanaimba oooooooooooooooooooo

Muziki asili yake wapi eeeeee,Muziki ni wa nani eeeeeeeeeeeee,
Muziki hakuna mwenyewe,Muziki ni mwito,
Muziki ni fundisho,Muzi maombolezo kilio
Usinione nikiimba,ukadhani ninayo furaha,kumbe ninayo huzuni moyoni.


ENJOY!!!

3 comments:



Snowfall Widget for Blogger


Snowfall Widget for Blogger