Thursday, June 13, 2013

SINDI....NA LAURA PETTIE (21)

21
Sindi Nalela alitulia vile alivyojikunyata kwa sekunde kadhaa akibana pumzi na kukisubiria kipigo pasipo kukipata, utulivu ule ndio uliomfanya aisikie ile harufu ya pombe ambayo Jerry aliitoa kupitia pumzi na jasho lake.

Taratibu akainyanyua kichwa na kumtazama Jerry usoni, akianza kuondoa mikono yake kichwani na kubaki ameduwaa baada ya kugundua Jerry mwenyewe hakuwa hata akimtazama. Alikuwa ameinamisha kichwa chini akionekana kuwayawaya na kusumbulia kihisia.


‘Jerry…’ akaita kiuoga akimtumbulia macho ya wasiwasi kana kwamba Jerry angelimrushia ngumi ya ghafla. Jerry hakuitika wala hakumjibu chochote zaidi ya kugeuka kizoba na kutembea hatua chache zilizomfikisha katika lile sofa na kujitupa hapo kama kiroba.

Akakilaza kichwa chake kwenye ukingo wa juu wa sofa uso ukielekea juu, akifumba na macho yake na kuupitisha mkono wake  wa kulia juu ya paji lake na kuutuliza hapo. Sindi akazidi kumshangaa si kwa kuisikia harufu ya pombe bali pia kwa ule unyonge wa ghafla uliomvaa baada ya kutaka kuchapana ngumi na muuza maji.

Kwa tahadhari akatembea kwa kunyata na kwenye kusimama karibu na mlango aasijue ni nini afanye wa wakati ule. Moyo ulikuwa ukimuenda mbio, haya si maisha aliyoyataka na wala hakuwahi kuyaishi achilia mbali vipigo toka kwa baba yake, hakuwahi kuishi na mwanaume mwingine ndani ya nyumba moja kiasi cha kuwaelewa wanaume. Hii kwake ilikuwa aina mpya ya maisha.

Wakati akiwa ameipakata mikono yake kifuani, sala zisizoeleweka zikisonga mawazoni, Sindi akashtuka kumuona Jerry akijiinua huku akishusha pumzi na kusimama. Akahisi ugomvi ulitaka kuzuka upya. Akajisogeza nyuma akiugusa mlango kwa mgongo wake na akimtazama Jerry kwa tahadhari.

Jerry hakumfuata wala hakumtazama, alifngua vifungo vya shati lake na kulivua kisha akalitupia sofani. Akafungua zipu ya suruali yake na kuanza kuiteremsha ile suruali. Tendo lile lilimfanya Sindi akodoe macho kwa bidii na hapo hapo akiachama mdomo na kuukunja uso wake kwa mshangao. Haikuwa tabia ya Jerry!

Akamshuhudia akiivua suruali yote na kuiacha pale pale sakafuni kisha akatembea akiwa na nguo ya ndani kulifuata sanduku lake la nguo. Sindi akameza mate kwa bidii mkono wa kulia ukikitafuta kitasa cha mlango pasipo kuutazama mlango wenyewe na macho yakigoma kuhamia uko mlangoni. Alikuwa akimtazama Jerry na asimmalize! Pombe si uji wa ulezi!

Jerry alipogeuka kivivu na kumtazama Sindi pale mlangoni, Sindi aligeuza kichwa chake haraka na kuugeukia mlango, akaufungua na kutoka nje, almanusura agongane na watu wawili waliokuwa wamesimama mlangoni pake. Jamila na mpangaji mwingine wa kike nao wakashtuka. Umbeya uliowafanya wategeshe masikio mlangoni ukawayeyuka na kuwafanya wachanganye miguu kila mtu na njia yake na kumuacha Sindi naye akiwatazama kwa mshangao.

Sindi akatoka mule chumbani na kwenda nje, akasimama uani pale akiwaza na kuwazua lakini pia akishindwa kuelewa aliyopaswa kuelewa. Akaifuata ndoo moja na pastiki pale nje na kuikalia. Akili yake ilikuwa na mvurugiko wa kutosha!.

Akakaa pale kwa dakika kadhaa mpaka aliposikia mlio wa viatu kordoni ukija kule alipokuwa. Akatulia na kuutazama mlango ulioishika kordo kwa shauku. Jerry akatokezea pale uani akiwa na taulo kiunoni.

‘Niwekee maji nioge’ akafanya kumuamrisha na yeye akarejea chumbani
Sindi akashusha pumzi, ni kama vile alitembelewa na kiwewe. Kwa dakika zote alizokuwa amejizungusha pale uani na hata kujiketisha katika ndoo akili yake haikumfanya awaone wapangaji wenzake wengine waliokuwa na shughuli zao hapo uani. Nao kama mazumbukuku waliacha kila kitu na kumkodolea macho Sindi wasimuelewe.
Baada ya nusu saa Sindi alikuwa chumbani kwake akipakua chakula na kukiweka kwenye meza ya kulia chakula wakati Jerry akioga. Alipomaliza akakifunika na wakati akinyoosha shuka kitandani na kumuwekea Jerry mashuka yake kwenye sofa, Jerry akaingia akitokea bafuni na kama ilivyo ada Sindi alitaka kumpisha ili avae. Hii ilikuwa desturi yao.

Alipompita Jerry ili atoke nje Jerry alimuwahi kwa kuushika mkono wake kwa nguvu na kumrudisha alipotoka. Sindi akakodoa tena macho lakini hali ile ya kukodoa haikudumu aliyakwepesha macho yake yalipogongana na ya Jerry.
‘Sijisikii kula’ Jerry akatamka kwa sauti ya chini akimtazama Sindi usoni akiwa bado amemshikilia Sindi vile vile.

Sindi akaukwatua mkono wake kidogo kujitoa mkononi mwa Jerry na kuitikia kwa kichwa asihoji sabau za kushindwa kula kama ambavyo angehoji siku zote. Akatoka kwa kasi na kufika kuhema kule nje asijielewe kilichompa kiwewe namna ile.  alitumia nusu saa nyingine nzima akiwa nje mpaka alipotaka kwenda maliwatoni kuoga ndipo aliporejea ndani na kumkuta Jerry amehsjikunyata kwenye sofa, akiwa amejifunika gubigubi.

Sindi akaenda kuoga, aliporudi akasukuma pazia lililotenganisha sofa na kitanda na kuvaa khanga nyingine, akijipaka na mafuta na kisha kupanda kitandani kuutafuta usingizi. Ilikuwa mapema mno kwa siku  hiyo. Kule kwenye sofa Jerr naye alikuwa kimya akiwa melala chali akiwaza yake. Ukimya uliokuwepo uliwapa nafasi ya kila mtu kuwaza lake.

Wakati Sindi akigeukia ukutani na kujikunyata ndani ya shuka, alishusha pumzi ndefu na kufumba macho lakini hali ile haikudumu aliyafumbua na kugeuka tena upande mwingine akilitazama pazia lililomtenganisha na Jerry. Wakati akigeuka Jerry naye alijigeuza na kulala kiubavu akilitazama pazia lililomtenganisha na Sindi. Ikawa kama watu waliokuwa wakitazamana pasipo kuonana.

Sindi akalala chali na kisha akageukia ukutani tena akatulia hivyo kwa muda usingizi ukianza kumchukua taratibu. Masaa machache baadaye. Usiku ulikuwa mzito, Ukimya ulikuwa umetawala eneo zima la nyumba. Jerry alimka taratibu na kulitupilia mbali shuka lake. Akatembea taratibu kulifuata pazia lile lililomtenganisha na Sindi na kulitanua mwishoni  lilikoishia. Akasimama kimya pazia mkononi, macho kitandani.

Shetani na malaika wakimuweka mtu kati. Nguvu ya mwili ikimsukuma kumfuata Sindi pale kitandani na hapo hapo kichwa kikimuonya kutokukisogolea kitanda kwa namna yoyote ile. Wakati akiwaza haya Sindi akageuka kihasara hasara na kusababisha ile khanga aliyokuwa ameifunga kifuani iteleze kidogo na kuacha sehemu kubwa ya mapaja nje hali titi lake moja bivu lililoshiba likichomoza na kubaki tupu.

Jerry akameza mate na kuhisi nguvu ya mwili ilielekea kuishinda ile ya kichwani. Akamfuata Sindi kitandani na kulala ubavuni pake akimtazama usoni vile alivyokuwa amelala chali. Akafumba macho na kuifuta midomo wa sindi kisha taratibu akaiunganisha na kulivumbua busu la upande mmoja.

Sindi Nalela akashtuka, wakati akitaka kupiga ukunga wa hofu, Jerry alimuwahi na kumziba mdomo, akimpa nafasi ya kuituliza akili yake na kujua nini kilikuwa kinaendelea. Dakika mbili tu zilimtosha Sindi kujua nani alikuwa pale.

‘Hapana…’ akahamaki akiikusanya khanga yake na kukistiri kifua chake
‘Please… sitakulazimisha but Sindi…busu tu… leo tu’ Jerry akabembeleza kwa sauti ya chini akimkaribia Sindi zaidi
‘Sitaki..’ Sindi akajirudisha nyuma lakini akagotea ukutani na Jerry akawa ameshamfikia
‘….Sindi’ akaita kwa suati ya kubembeleza na mikono yake ikikifuata kiuno cha Sindi na kukigusa kwa kupapasa. Sindi akajinyonga kidogo na kutaka kunyanyuka kabisa ili atoke pale kitandani. Jerry akamuwahi na kumrudisha kitandani

‘Usiniguse usikii’ Sindi akafoka kwa sauti kubwa kidogo kiasi cha kumfanya jerry ashushe pumzi na kujua kazi iliyokuwa mbele yake haikuwa ndogo.
‘Sikubikiri sawa?’ akawa mkweli
‘Usiniguse pia’ Sindi akajibu kwa hasira akihema

Jerry akachoka! akaketi kitandani na kumtazama Sindi katika namna Fulani ya kuhitaji huruma. Klikuwa na baridi mno, na baridi ile ndio ilimuhamasisha Jerry kumfuata Sindi pale kitandani na sasa kwa mbali manyunyu yalilivamia bati na mvua ikaanza kunyesha kwa maringo na kuacha ulele Fulani juu ya bati.

Sindi akageukia ukutani na kuamua kuusaka usingizi, akijifunika gubigubi na Jerry akibaki anamtazama asijue la kufanya. Alitulia vile kwa dakika kadhaa na alipotanua shuka na kugeuka kumtazama Jerry almkuta amekaa vile vile akimtazama yeye.

Sindi akageuka mzima mzima na kuketi kitandani sambamba na Jerry
‘busu na so mengine’ akasema uso wake ukionyesha kutopendezwa hata na lile alilolikubalia.  Wakasogeleana kama watoto waliotaka kujaribu kitu hatari na kushikamana. Hali ile ikakolea!

Sindi akaserereka taratibu na kulalia mgongo hali Jerry akiwa juu yake na akiitumia fursa ile kumfanya Sindi asijutie kutoa ruhusa ya kitu kile. Walidumu vile kwa dakika kadhaa Sindi Nalela akielea katika bahari ya huba na mihemo isiyokwisha, akiihisi raha mbayo hakuwahi kuhisi ipo dunia hii pamoja na kuwahi kuwa na mpenzi.

Alianyonga nyonga pale kitandani akitamani Jerry amtafune mzima mzima. Katikati ya raha ile Jerry akanyanyuka na kumuachia Sindi.
‘Nini…’ Sindi akauliza akihema
‘Tutafika mbali… Asante kwa busu’ akajibu na kuanza kujiburuza kuufuata ukingo wa kitanda ili ateremke. Sindi akaikusanya khanga yake kifuani akihema, mwili ukimhitaji Jerry kupitiliza na kwa wakati ule Sindi alikuwa tayari hata kumuachia Jerry afanye lolote atakalo ila ndio hivyo Jerry mwenyewe alishasimama kando ya kitanda na kumtakia usiku mwema. Binti wa watu hakulala!

Jerry alipotoka na kulivuka pazia, alitabasamu. tabasamu la ushindi. alijua alichofanya kilikuwa na matekeo gani kwa Sindi. Akajirusha sofani na kujituliza, akiutafuta usingizi na kujaribu kuutuliza mwili wake urudie hali yake. Alimuweza Sindi Nalela!
8888888888888888888

Nyanza aliamka katikati ya usiku ule na kuanza kusali, alisali mno akikemea mambo mengi na akimlilia Mungu mengi pia. Alikuwa amemuota Sindi akivuta ngambo ya bahari huku akimpungia mkono wa kwaheri licha ya yeye Nyanza kumlilia mno. Nyanza alisali jasho likimtoka.

Alipomaliza akaketi kitandani na kuitoa picha ya Sindi  chini ya mto na kuitazama sana, alitulia nayo mikononi akimkumbuka kwa mengi mno. Alivyokuwa akicheka, alivyokuwa akigombana naye na hata alipokuja pale kitandani kwake kwa mara ya kwanza kumruhusu amvue nguo.

Sindi Nalela alikuwa msichana wake wa kwanza kumfuata na kumtaka uhusiano, alikuwa msichana wake wa kwanza kuwa naye katika mahusiano na kilichotokea kwake kilikuwa ni pigo zito. Akaiweka picha kando na kuanza tena kusali.
888888888888888

Asubuhi ya saa tano iliyopambwa na mawingu mazito, madimbwi ya maji na manyunyu yaliyokuja na kutoweka ilianza kwa utulivu. Ilishatimia wiki moja tangu Pamela Okello na Jerry Agapela wagombane. Pamella alikuwa ofisini kwake lakini akili yake ilikosa umakini kabisa. Ilikuwa siku yake ya kuzaliwa, na mpaka dakika hiyo Jerry alikuwa hajamtakia kila la heri wala kumwambi lolote achilia mbali kuletewa maua kama ilivyokuwa kawaida ya Jerry.

Aliisubiri simu ya Jerry kana kwamba ndiye aliyehusika na siku yake hii lakini hakukuwa na dalili zozote za Jerry hata kuachia beep. Akajikuta akiinyanyua simu na kumpigia Jerry ili japo amkumbushe siku ile muhimu kwake lakini simu iliita bila kupokelewa.

Wakati akihangaika na Jerry, Patrick alimpigia na kumfahamisha kungekuwa na sherehe yake ya kuzaliwa katika hoteli ya moja ya kifahari mjini. Pamella alitikia kwa unyonge na kukata simu kisha taratibu akanyanyuka na kuukwanyua mkoba wake akatoka ofisini kwake na kuingia garini. Akimfuata Jerry New Afrika. Hasira zilishaisha na sasa alimuhitaji rafiki yake.

Kabla ya kuondoa gari akamtumia Jerry ujumbe kujua aliko, akatulia na kusubiri majibu na akalipata
‘With my babe at home, nikusaidie nini?’ lile jibu lilimfanya Pamella ahisi kuna nyundo ilikuwa imemuangukia kichwani ghafla….

.....ENHEEE???? IKAWAJE???.... TUKUTANE HAPAHAPA

1 comment:



Snowfall Widget for Blogger


Snowfall Widget for Blogger