Saturday, June 8, 2013

SINDI....NA LAURA PETTIE (20)

20

Jua la asubuhi lilishachomoza, pilika pilika za hapa na pale zilishaanza na kuifanya siku kuwa vurumai za kutosha. Ilikuwa Ijumaa na kama ilivyo ada watu wengi walikuwa wakijiandaa kupumzika siku inayofuata.

Sindi Nalela aliamka asubuhii akiwa mnyonge mno. Alikuwa amekumbuka kwao bambali na hayo alikuwa amemkumbuka Nyanza mno. Kuna kitu kama majuto kilikuwa kikimpitia kila sekunde ya asubuhi hii.


Akili yake ilianza kuwaza mbali na kujijazia lawama za kukurupuka kuondoka kwao pasipo kujua akimbiliapo alikuwa anaenda kufanya nini la maana.
Muda ulishakatika pasipo yeye kuwa na kibarua wala kazi yoyote ya maana ya kumuingizia kipato. Hakupenda ile hali ya kuachiwa pesa za matumizi na Jerry kila alipoondoka.

Kwake yeye alihitaji kujishughulisha ili kupata pato lake binafsi na kumpunguzia Jerry mzigo wa kumlea na akikumbuka zile pesa alizomlipia deni kwa Mzee Dunia. Alijua Jerry alikuwa akihangaika kuzilipa, laiti tu angeujua ukweli!

Baada ya usafi wa hapa na pale, alitulia chumbani kwake muda huo wa saa nne asubuhi akisikiliza redio huku akichambua dagaa zake kwenye ungo na kuwatia katika bakuli dogo kando yake. Mara tu kibao cha Matonya cha Vaileth kilianza kupigwa redioni na Sindi akajikuta akimsaidia Matonya kuimba na hapo hapo akimkumbuka zaidi Nyanza.

Hamu ya kumuona, hamu ya kumsikia, hamu ya kumgusa na ile hamu ya kutaka kuwa naye karibu vikampalia moyoni na roho ikamuuma mno. Jerry alikuwa akichelewa kuitimiza ahadi yake ya kumleta Nyanza kama walivyokubaliana, akajiapiza kuliulizia hili suala usiku wa siku hiyo Jerry atakaporejea.

Wakati akikazana kuchambua dagaa zake huku akiburudika, Sindi akasikia mtu akimuita dirishani, akaitika tu na kusikiliza, alishaitambua ile sauti ya muitaji
‘Umejifungia ndani mwenyewe’ yule mtu kule nje akamchokoza
‘nimeingia muda huu…vipi umeleta maji?’ Sindi akauliza na yule muuza maji ambaye ndiye aliyemuita Sindi kule nje akajibu alikuwa amepita tu kuchukua hela kwa mpangaji wa jirani.

‘basi jioni niletee madumu mawili…. kisima cha nyuma hapo kimechafuka kweli maji hayafai kupikia sasa’ Sindi akaagiza maji na yule muuza maji akamkubalia na kumuaga huku wakitaniana kisukuma na kucheka. Kile kibao redioni ndio kilikuwa kinaishia ishia na Sindi akanyanyuka na kutua ungo wake kwenye kijimeza kidogo mbele yake na kuikaza khanga yake. Akatoka nje kuangalia jiko lake la mkaa lililokuwa likichemsha Maji ya kunywa. akawakuta kina mama kadhaa pale kwenye kordo aliotaniana nao kidogo na kisha kurejea ndani.

Hakurudi kuketi pale kitandani, alilifuata kabati la nguo na kulifungua, akakung’uta mikono yake aliyohisi bado imeharufu ya dagaa, akaing’uta na kuinusa. Huku akitabasamu akatoa mkoba mdogo aliorudi nao mpaka kitandani na kuufungua. Akatoa hela, kibunda cha noti na kuzihesabu. tabasamu lingine likatanda usoni pake, mtaji alioutaka alishautimiza, akazifunga na kuzirudisha zile pesa mahali pake kula kabatini.

Akarudi kuchambua dagaa zake na safari hii wimbo wa kisukuma ukimtoka mdomoni mwenyewe akikumbuka kilimo cha jembe la mkono kijijini kwao.
8888888888888888888

Jerry alijipindua kitandani wakati mlio wa simu ya mezani ulipokazana kulia na kumtoa usingizini. Alijigeuza akipiga mihayo na kuunyoosha mkono wake wa kulia kuufikia mkonga wa simu na kuukwanyua, akiuvutia sikioni sambamba na mwayo mwingine huku mkono wa kushoto ukiteleza toka pajini mpaka kidevuni.

‘Yes…mruhusu’ akazungumza kichovu akiurudisha mkonga wa simu sehemu yake na kunyoosha mikono yake juu katika namna ya kuunyoosha mgongo wake pia. Akashusha miguu yak echini baada ya kutupilia blanketi lake kando na kusimama, akirudia tena kujinyoosha na akijitazama kwenye kioo kirefu kilichokuwa mbele yake.

Akaelekea maliwatoni, dakika mbili tatu akatoka na mswaki mdomoni akisukutua na akiufuata mlango baada ya kusikia kengele ya chumbani ikilia. Pamela Okello akaingia mara tu mlango ulipofunguliwa

‘Unahitaji kuzungumza na Patrick!’ pasipo salamu akasem kilichomleta na Jerry akaukunja uso wake akiacha kusukutua na kumkodolea macho Pamela. akauachia mswaki na kutrupa mikono yake hewani kama ishara ya kuuliza kwanini akionyesha pia kutomuelewa.

‘Hebu kamalize hiyo kazi kwanza…’ Pamela akamuonyesha bafu, akianza kukereka na kuzungumza na mtu anayepiga mswaki. Wakati Jerry akielekea bafuni, Pamela akaketi kwenye sofa zuri la kisasa la hoteli lililokuwa chumbani hapo. Akatulia tu akionekana kuzama katika fikra nyingi na kugutuka pale Jerry aliporejea pale chumbani akiwa amefunga taulo kiunoni na dalili zote kuwa alikuwa ameoga pia.

Jerry akaketi kitandani na kumtazama Pamela, akaachi mguno mwenye maana ya kuitikia kwa kutaka kusikia zaidi toka kwa Pamela.
‘Unahitaji kuzungumza na Patrick’ Pamela akarudia kauli yake kwa msisitizo
‘Why?...’ kama mtu ambaye bado alikuwa hajaelewa kauli ya Pamela akauliza hali akiupeleka moko wake wa kushoto juu ya ile meza iliyokuwa na simu na kuchukua lotion ya Valesine kwa wanaume na kuimimina kiganjani.

‘Hivi ni nani alitekwa na kuripotiwa kupotea huku wengine wakisema amekufa?... akili yako bado haijazinduka kujua Patrick amekuona na kila unalopanga sasa liko hatarini kutokamilika?’ Pamela akajieleza kwa haraka akionyesha dalili zote za kuogopa

Jerry akaganda kama sanamu kwa sekunde kadhaa, akili yake akifanya kazi kupitiliza kiasi cha kumuacha akifinya macho kwa mshangao. Ni dhahiri hakuwa amewaza yote hayo. Kwake yeye maisha ayaliashaanza kusonga mbele akihitimisha kuwa baba yake ndiye aliyetaka kumuua na alikuwa akijipanga kumkabili baba yake moja kwa moja ili kumfikishia ujumbe kuwa ameshajua mipango yake na baada ya hapo angeripoti polisi.

Mawazo yake yalipingana nay a Pamela mbaye alikuwa akihisi si Mzee Agapela anayehusika. Kupingana kwao huko ndiko kulikomfanya Pamela makini kufuatilia nyendo za Jerry ilhali mtu mwenyewe akiwa hana hata chembe ya umakini katika nyendo zake.

‘And after the whole thing….unatarajia Pat atanisikiliza?’ Jerry akauliza kwa sauti ya mashaka lakini yenye kebehi kiasi Fulani. Pamela akazungusha macho yake makubwa ya mviringo katika namna ya kuchoshwa na ubishi wa Jerry

‘Pamoja na hili….you guys should meet mtatue kilichotokea….For God’s sake I need my man back….your stupid kiss wont cost my relationship with Patrick…fanya unachojua…’ Pamela akaja juu kidogo akinekana kutojali tena kuhusu suala la Jerry.

‘Kuwa straight Pam….inshu hapa si kuwa Pat ameniona…it is all about your man si ndio?’ wivu ulimtembelea
‘Sio kosa langu…. I didn’t invite you in…sikukuita na wala sikutarajia ungekuja….’ Pamela anaye alikuja juu zaidi na kumfanya Jerry ahisi Pamela hakuwa pale kwa ajili yake kama alivyoanza

‘Okay! I get it…. unahofu kuwa Patrick atakuacha si ndio?’ akauliza tena kizembe
‘kwani unadhani baada lile tukio Patrick atakuja miguuni pangu kuniangukia?.... Ni mwanaume wa kipekee kwangu siwezi kumkosa sababu yako…niko tayari igharimu urafiki wetu lakini sio kuvunja mahusiano yangu na Patrick’ Pamela akauliza akiwa na ghadhabu usoni
‘What?’ Jerry akauliza kwa kubweka, akisimama, macho yakimtoka na dalili zote za wivu zikionekana usoni pake ‘…umesema?’ akauliza akimkaribia Pamela ambaye naye alisimama akimkodolea macho Jerry

‘You heard!’ akajibu kijeuri na Jerry akafumba macho akiumeza ukweli mchungu kuwa Pamela alimthamini Patrick kuliko yeye. Ukweli uliopita kwenye mishipa yake ya damu na kuingia moyoni.

‘Do we have any future?’ akajikuta akiropoka hili swali ambalo lilimfanya Pamela abweue kwanza, kisha kicheko kidogo kikamtoka, kisha akaunga cheko refu ambalohalikuleta maana yoyote kwa Jerry.

‘Baada ya miaka yote hii Jerry…..why don’t you get it man?...Damn! I’m in love with Patrick…PATRICK NOT YOU Pamela alijibu kwa ghahabu, akipandisha sauti wakati akiyataja jina la Patrick mbele ya Jerry ambaye almanusura taulo limdondoke.

Pamela Okello alikuwa na hasira, alimka na hasira hizo tangu alikotoka, alikuwa katika msongo wa mawazo baada ya kuzungumza na Patrick ambaye alimwambia hamtaki tena sababu ya Jerry. Alipoifikiria sababu ya kugombana kwake na Patrick, Pamela alipata jasira zaidi kuwa Jerry ndiye chanzo kwa sababu za kipuuzi.

Jerry Agapela akajikuta akimkaribia Pamela zaidi kama zoba huku akiwa amemtolea macho, akajikuta tu akimkamata Pamela mikononi mwake na kumvutia kifuani pake wakati huo huo akiukimbizia mdomo wake midomoni mwa Pamela ambaye hakulikubali tukio lile kirahisi, alipambana!

Jerry alimzidi nguvu kiasi cha kupelekeshana naye mpaka kitandani ambako alimbwaga Pamela kama mzigo, alipotaka kumpandia hapo kitandani Pamela aliachia kofi kali lililotua shavuni mwa Jerry barabara na akajikuta akisimama huku akihema na kuligusa shavu lake kwa viganja vyake.

Wote walikuwa wanahema kwa jazba, na ni wakati huo akili ya Jerry ilirudi mahala pake na akajikuta akifumba macho kwa sekunde kadhaa pengine akikisikilizia ile kibao au alikuwa akitafakari nini alitaka kufanya muda mfupi uliopita.

‘Pamela?....hivi mimi sio mwanaume kwako?’ akamuuliza akiwa bado alisugua shavu lake na Pamela akijivuta na kuteremsha miguu kitandani
‘Sijui…. ninachojua sikupendi na sina hisia zozote kwako’ Akajibu Pamela akiinama na kuangaza kutafuta kiatu chake kimoja kilichokuwa kimemvuka miguuni.

‘Pamela!’ Jerry akaita asiamini alichosikia
‘Usinivuruge….huna haki ya kunigusa kila unapotaka… na umeenda mbali unaforce sex…Jerry! wewe ni wa kunilazimisha kitu kama hiki?....nilipokuvulia nguo mara mbili ulinilazimisha?....huna shukrani punda wewe’ Pamela alimfokea na akikiona kiatu chake karibu na mlango

‘Akajinyanyua na kukifuata na baada ya kukivaa aliikwanyua pochi yake iliyokuwa kwenye sofa na kujiweka sawa mwilini. Kisha kama mtu aliyekuwa najiandaa kuteremsha bomu, akaimung’unya midomo yake kwa ghadhabu na kumpasulia Jerry ukweli.

‘….Grow up Jerry! tafuta a girl of your class, anzisha uhusiano unipunguzie hizi karaha zako….otherwise hata huu urafiki utakufa….’ akampasulia Jerry ukweli na kugeuka kuelekea mlango na kabla hajaufungua akageuka tena na kurusha kombora lingine lenye skadi za kutosha

‘Nimezoea kunyoosha kila unapoharibu….this time too nitamrejesha Patrick kwa akili zangu…stay away from me anapokuwa around otherwise you need to behave yourself boy!’ akaufungua mlango na kutoka.

Jerry akaketi kitandani, akihisi mikuki kadhaa ikishindiliwa kifuani pake. Kauli za Pamela Okello zilirejea akilini mwake kama marudio ya vipande vya filamu na kumfanya ajibwage kitandani na kulalia mgongo. Hali aliyokuwa anaisikia wakati ule ilimfanya mishipa ya damu itutumke mikononi mwake hali taya zake zikisigishana. Alikuwa na zaidi ya hamaniko wacha niseme weweseko!
88888888888888888888888

Nyanzambe Mugilagila alikuwa Kanisani, tangu mama yake afariki dini ilikuwa imemkamata kwelikweli. Baada ya shughuli zake alishinda kanisani akisali na kujifunza neno la Mungu. Taratibu alianza kupachikwa jina la utani la mtumishi wa bwana.

Uchangamfu wake ulitoweka, alikuwa kimya mwenye kuonekana kuwa na mawazo mengi mno huku akiwa akejiachia rafu kupitiliza. Mtu yoyote aliyepata kumuona alijua kijana wa watu alikuwa katika hali ngumu kihisia.
Baada ya kusali na kusoma neno la Mungu, Nyanza alitoka kanisani na kutembea taratibu kurejea nyumbani na biblia yake mkononi. Njiani alijikwaa mara kadhaa wakati akitembea huku akili yake ikionekana kuwa mbali. Alipita mbele ya chumba alichopenda kukitumia Sindi kufundishia watoto wadogo. Alijipa dakika nzima kuzimama pale na kupatazama kana kwamba Sindi angelitokea mule ndani ya kile chumba na kuzungumza naye.

Aliitazama ile sehemu na taswira ya Sindi akifundisha na zile sauti za watoto zikifuatiza sauti ya Sindi wakati akifundisha ilimpitia akilini na kumuongezea unyonge. Akatembea kama taratibu zaidi akiliacha lile eneo na kushika njia kuelekea kwake.

Alma na Maria walikuwa walikuwa na ndoo za maji kichwani wakati walipomuona Nyanza akiwa amesimama pale akikitazama kile chumba.
‘Kwanini tusimwambie?’ Alma akajionea hatia kuendelea kuficha
‘Mmmh…mambo yameshatulia sasa ukayazue tena’ Maria akajitetea
‘Nyanza anaisha jamani…hivi huoni anavyodhoofika?’ Alma akasimama kabisa na ndoo yake kichwani

‘…Jihurumie kwanza….unakumbuka alivyofuatwa na Mzee Dunia….Kipondo kama kile nanai anakitaka shost?.... halafu ndio tutafungwa hata jela maana tulikuwa wapi kusema yote hayo?’ Maria akauliza akiona uzito wa ndoo unamuelemea, akaitua!
‘Si tunamwambia Nyanza peke yake?’ Alma akaona atoe wazo
‘Kayaanze tu mwaya…mimi usinitaje kabisa….yaani ukiwa unaelezea elezea kama vile mimi niko ulaya uko nakula raha hata siwajui nyie akina nani’ akasema akijitwika ndoo yake tena kuchapua hatua zake kubwa kubwa. Alma akacheka na kumfuata nyuma

Wakati wakimjadili Sindikule kujijini, yeye mjadiliwa alikuwa na pilikapilika zake ndani mwake. Akatoka nje na kwenda kuangalia kama muuza maji amefika. hakumuona, akarejea ndani na kuendelea na mambo yake. Giza lilipoaza kuingia akaonysha kupata wasiwasi. Akatoka na kumgongea Jamila chumbani kwake.
‘Vipi?’ sauti ya Jamila ikaitikia ndani uko na asitoke
‘Muuza maji ameshapita?’  akauliza akitega sikio mlangoni
‘Mmmh sijamsikia leo…. mbeep kama anakuja atakupigia tu’ Jamila akampa wazo ambalo Sindi aliliafiki na kurudi chumbani kwake. Wakati akitafuta simu yake huku na kule akasikia mlango ukigongwa. Akaachana simu na kwenda kufungua

‘Nikajua huji….sijui ningepikia nini leo’ akamsemesha muuzamaji huku akicheka na kumtanulia mlango zaidi huyo muuza maji akayamimine kwenye chombo alichomuonyesha. Muuza maji akafanya kazi yake. Alipomaliza akamgeukia Sindi

‘Nisaidie maji ya kunywa dada’angu’Muuza maji akarai na Sindi akakitafuta kikombe na kuifuata ndoo ya maji iliyokuwa imebebeshwa juu ya kiti cha mbao na kuwekwa kikombe juu. Wakati akimimina, mlango wa chumba ukafunguliwa na Jerry akaingia.

Akakunja uso akimtazama muuza maji katika namna isiyotabirika. Sindi akageuka na kikombe chake na kutaka kumkabidhi muuza maji na hapo hapo akipiga goti ili salamu kwa Jerri ifuate. Hakutimiza vyote kwani Jerry alikiputa kile kikombe kwa ghadhabu na maji kumwagikia kulehuku kikombe kikimponyoka Sindi na kuangukia mbali.

‘Huyu nani?’ Jerry akauliza kwa jazba akimtazama muuza maji ambaye macho yakikaribia kuzidi upana wa macho yake kwa hofu.
‘Kaka Jerry huyu…’ Sindi akataka kujieleza
‘Nani kaka yako?’ Jerry akamuwahi kwa hasira huku akihema

Sindi akaduwaa, Jerry azua zogo kubwa kati yake na muuza maji kiasi cha wapangaji wawili watatu kuja kuamulia lile zogo na kumnusuru Muuza maji. Watu walipotoka Jerry akamgekia Sindi aliyekuwa amesimama mbali kidogo na yeye akiwa  ameweka mikono kichwani kama mateka, akihema na kutaka kuanza kujieleza upya na asiweze.


Jerry alipopiga hatua maoja kumfuata, Sindi alijikunyata na kuinamisha kichwa chini. Yowe la woga likitoka ‘Uwiiii’ alihisi harufu ya kipigo kitakatifu. Jazba za Jerry haikuwa za kawaida!

...... NDIO IKAWAJE SASA...RUDI HAPA HAPA TUSIMULIANE....

No comments:

Post a Comment



Snowfall Widget for Blogger


Snowfall Widget for Blogger