6
SEHEMU YA SITA
Nyanzambe alitembea kwa mwendo wa kasi akionekana mwenye
jazba mno. Sindi alikuwa nyuma akimkimbilia, akajitahidi kumharakia na
kumfikia, huku uso ukiwa umesawajika, jasho likimtoka na machozi yakimlenga,
Sindi alisimama mbele ya Nyanza akiomba huruma yake
‘Sio hivyo unavyofikiria Nyanza…’ alitaka kujitetea
‘Kumbe ni vipi?....bila soni Sindi unashikwa shikwa na
mwanaume mwingine zaidi yangu?...kweli?’ Nyanza aliongea akitetemeka kwa jazba
‘Sikumruhusu aniguse’ Sindi akajitetea tena
‘Unadhani sikuona kila kitu?....unadhani nilimvamia tu bila
sababu?.... naona sikufai mama….mimi maskini tu nitakupa nini?….nitakupeleka
wapi mimi? kuwa huru tu’ Nyanza aliongea kwa uchungu akijitazama na kumtazama
Sindi ambaye alikuwa akitikisa kichwa muda wote kuashiria kutokukubaliana na
kauli za Nyanza. Ile sentensi ya kuwa
huru tu ilimfanya Sindi ahamanike. Akamzuia Nyanza kumpita na kumshikilia kama
mtoto anayemzuia mama yake kuondoka na kumuacha
‘Una maana gani?’ akamuuliza kwa huzuni
‘Nimekuacha huru….yoyote utakayemtaka mchukue tu….
nimeshapigana vya kutosha sababu yako’ Nyanza alijibu akikwatua mkono na
kuondoka tena kwa kasi. Sindi hakumfuata nyuma wala hakutazama kule alikokuwa
anaelekea Nyanza. Alitulia akitazama sehemu moja pasipo kupepesa hata macho kwa
sekunde kadhaa. Kwa unyonge akashika njia ya kumrejesha kwao akiwa na jitimai
ya kumtosha.
888888888888888888888
Mzee Agapela alikuwa ofisini kwake, mbele ya laptop yake
alikuwa akiendelea kuchapa kile alichokuwa akikichapa katika laptop yake lakini
ghafla aliachana na ile kazi na kuhamishia macho yake katika picha ndogo ya
mezani iliyokuwa kando ya laptop.
Picha yake na kijana wake Jerry Agapela. Alitulia kwa sekunde
kadhaa akiitazama tu ile picha mpaka
pale alipoamua kuvua miwani yake na kutumia vidole vya kiganja chake cha mkono
wa kushoto kuzia machozi yaliyokuwa njiani kumtembelelea. Aliyabinya macho yake
kwa sekunde kadhaa akijizuia kulia nap engine akizisikilizia zile hisi a za
uchungu zilizomjia moyoni. Alikumkumbuka mtoto wake na kupotea kwake
kulimkumbusha marehemu mke wake Sophia, mama mzazi wa Jerry Kristus Agapela,
mkewe wa kwanza.
Mzee Agapela alishusha pumzi na kutoka pale kitini,
akalifuata dirisha na kusimama hapo kitambo akitazama nje, lakini pia akili
yake ikizunguka kupita maelezo. Moyo wake ulijaa wasiwasi, mashaka na sononeko
kubwa juu ya kijana wake. Alikuwa wapi?... alikuwa hai?.... alikuwa na hali
gani?....nini kilimpata?.....na kwanini?.....na kwa vipi?.... Maswali
yaliyokosa majibu yalikimbia mchakamchaka kichwani mwake na kumuongezea sononi.
Alizama mawazoni akitazama kule nje, mawazo yaliyomchota
yalimfanya asisikie hata kule kufunguliwa mlango wa ofisi yake wakati mkewe
Fiona alipoingia mule ofisini. Kwa hatua za taratibu Fiona alimfuata mumewe na
kusimama nyuma yake akimtazama namna alivyokuwa ametopea mawazoni. akamgusa
began a kumshtua.
‘unawaza sana
mume wangu….’ Fiona alimsemesha Mzee Agapela akimpapasa mgongoni
‘Jerry!....inaniumiza kuliko ninavyoweza
kuelezea….inanivuruga sana nadhani
it is time niajiri mpelelezi binafsi’ Agapela alijibu akitoka pale dirishani na
kuifuata meza iliyokuwa na kahawa. Akajimiminia kidogo na kupiga funda kadhaa
wakati Fiona akiwa anamatazama kama mtu aliyetaka kusema
jambo lilimponyoka ghafla.
‘Mpelelezi binafsi?..... Come on Darling!.....huliamini jeshi
la polisi….Kwanini usi…usi… au….’ alitafura maneno ya kujazia sentensi yake na
akakosa
‘Inaelekea wiki ya tatu…siwezi kutulia na kufanya kazi pasipo
kujua kijana wangu yu wapi….. no!...nguvu ya ziada inahitajika….siwezi kukaa
idle huku sioni la maana linaloendelea….’ Agapela alizungumza akizunguka na
kurejea kuketi kochini
‘huo ni uamuzi wako…..and what about the will?’ Fiona
akauliza kwa amcho makavu, sura yake ikionyesha wazi kutopendezwa na uamuzi wa
mumewe.
‘Sidhani kama huu ni wakati wa kuzungumzia will Fiona!....’
Agapela alikuja juu kidogo
‘ni mrithi wa robo tatu ya mali
zako…. hivi huoni kuna haja ya kuchange kitu hapo….’ Fiona alisisitiza
akimfuata Agapela pale alipokuwa ameketi
‘Sijaona bado….sijapata uhakika kuwa mwanangu hayuko hai….na
zaidi ya yote sijaipa akili yangu nafasi ya kufikiria will….my son is alive and
healthy…sijali umeguswa na jambo hili au lah…bado huna haki ya kuulizia
chochote kuhusu will…right!?’ alizungumza kwa sauti kali kidogo kiasi cha
kumfanya Fiona ajishtukie na kugundua alikuwa amevuka mipaka ya kuhoji
alichokuwa akikipigia mahesabu.
‘….. nimeuliza kwa nia njema darling…. nimekuwa nawe kwa kila
hali kwa hatua zote… ina maana hujawahi kuniamini kuwa naumizwa na hili tukio….
kweli?....okay!’ Fiona alitoka kwa mwendo wa kasi kidogo akiufuata mlango.
Agapela akataka kumuita lakini akaona isingefaa kitu, hakutaka kulumbana na
wala hakuwa na nguvu ya kubembeleza mtu kwa wakati ule. Akamuacha atoke na
kuubamiza mlango. Akashusha pumzi na kujiinamia tena.
Miaka miwili ya ndoa yake na Fiona, imekuwa miaka ya malumbano
na matatizo mengi kuliko alivyotazamia. Mara kadhaa alijikuta akimkumbuka
marehemu mkewe Sophia na kutamani hata kuurudisha wakati nyuma na kuzugumza
naye machache. Alimkumbuka sana
mwaamke huyu sit u kwa uvumilivu wake kwake bali pia kwa uzuri wake wa shani.
Aliumizwa na mengi aliyomfanyia Sophia wakati alipokuwa hai,
aliumizwa na namna alivyomtendea Sophia sababu tu ya uwepo wa Fiona pembeni ya
ndoa yao . Alimzika kwa machozi ya uongo na kuoa tena
mwezi mmoja tu tangu afiwe. Lakini leo hii alikuwa anamlilia Sophia kwa machozi
ya kweli, machozi ya majuto na toba. Kwa kumuoa Fiona aliyeitikisa ndoa yake
alikuwa ametema jiwe na kubugia kaa la moto.
Kule nje ya mlango Fiona alisimama akiwaza, ile hali ya
kutoitwa hata kubembelezwa haikumfurahisha. Alisimama pale mlangoni akiguna
guna mara kadhaa na kuamua kumchungulia mumewe kupitia tundu la mlango.
Alimuona vizuri namna alivyokuwa ameketi na kukipakata kichwa chake kwa mikono
yake.
Fiona akasimama na kushusha pumzi, akipepesa macho huku na na
kuuma kidole chake cha shahada cha mkono wa kushoto, ni kama
vile alitembelewa na mchecheto. Haraka akatoka eneo lile na kutokomea. Mali
za Agapela zilikuwa zinampeleka asikotarajia na Mzee agapela hakujua nyoka
aliyekuwa amemuuma alikuwa anamfuga mwenyewe.
88888888888888888
Siku mbili baada ya ugomvi wa ngumi kati ya Jerry na
Nyanzambe. Jerry alikuwa akizungumza na Mama Alma ,
nesi aliyekuwa akimhudumia na kumtazamia kidonda chake.
‘Hali yako haijawa njema bwana mdogo….sitarajii ujitoneshe
kiasi hiki na uone ni jambo dogo’ Mama Alma alimgombeza Jerry wakati akifunga
vifaa vyake baada ya kumsafisha kidonda
‘Ilikuwa bahati mbaya mama…’ Jerry alisema akijitutumua
kutabasamu katikati ya maumivu aliyokuwa anayasikia
‘Na isijirudie tena…umenielewa?’ Mama Alma alimuuliza uso
ukiwa na ile huruma ya kimama. Jerry akaitikia kwa kichwa na akuagana na mama Alma
ambaye alitoka na kuishia akimuacha Jerry pale alipokuwa akiuma meno na
kujilaza chali.
Akili yake ilikuw ana mengi kwa wakati ule. Alitabasamu
alipofikiria sababu za yeye kutoneshwa vile. Mwanamke!
Hakuwa mtu wa kupigana sababu ya mwanamke na mpaka dakika ile
hakukuwa na mwanamke mbaye angesimama na kudai Jerry alikuwa mali
yake. Wakati akiwaza hili jina la mtu likapita katika akili yake Pamela Okello!
Mwanamke mrembo, msomi mwenye maisha yake, rafiki yake wa muda mrefu sana
na mwanamke ambaye alikuwa akimpigia misele siku nyingi, akimbembeleza awe
wake, akimshawishi na kujitahidi kumvutia kwake bila mafanikio.
Pamela Okello alikuwa amegoma kuwa mpenzi wake, alikuwa
amegoma kuvunja urafiki wao sababu ya mapenzi, alimkatalia Jerry katakata
akiutetea urafiki wao. Alikuwa akimngoja Pamela maishani mwake lakini ghafla
hisia zake zilianza kutekwa na Sindi Nalela ambaye ni kama
alimvamia na kuuchukua moyo wake jumla jumla. Jerry alicheka kivivu akikumbuka
tukio la yeye kutandikwa ngumi.
Tabasamu lile likafifia taratibu alipoirudisha akili yake
katika kile alichokuwa akikiwaza usiku na mchana. Moyo wake uliumia na
akajikuta akifumba macho na kuyasikilizia maumivu yale sambamba na hasira
zilizomtembelea kila alipofikiria kitu hiki
‘baada ya kumuua mama ameona na mimi animalize….i hate you….i
hate you’ alitamka kwa ghadhabu kali alimfikiria baba yake. Alizisikia vema
kauli za wale waliomteka na kumburuza kama gunia.
Aliwasikia vema wakati wakipokea maelezo ya namna ya kumuua na aliisikia vema
mmoja wa wale watu waliomteka akimuarisha mwenzake ampigie simu Agapela.
Moyo ulitikisika kwa ghadhabu…. Aliuma meno na kudumba tena
macho safari hii akiyasikilizia maumivu ya moyo na maumivu ya kidonda chake.
.....ILIKUWAJE?..... NA ITAKUWAJE...FUATANA NAMI
No comments:
Post a Comment