Monday, August 5, 2013

SINDI....NA LAURA PETTIE (33)

33


mke wa Mzee Okello, mama wa Pamella alikata simu na kusimama akiwa kama mtu aliyetaka kupayuka kitu kwa sauti ya juu na asiweze. Mdomo ulikuwa aukiwayawaya huku macho yakipepesuka na kutembea huku na kule. Mchecheto!

Akalazimika kujiweka sawa pamoja na mchecheto ule ili binti yake aliyekuwa anaingia pale dukani asigundue hali aliyokuwa nayo.


‘Vipi?’ akamuuliza Pamella aliyefikia kuketi kwenye kiti kilichokuwa karibu na pale alipokuwa amesimama mama yake.
‘Ni kama naota..’ Pamella akajibu akishusha pumzi ndefu kiasi
‘Kwanini?’ mama yake akamsogelea zaidi na Pamella akatikisa kichwa kulia na kushoto kuashiria kutojielewa yeye mwenyewe sembuse kumweleza mtu mwingine na akaelewa.

Mama akakunja sura kidogo na kumkazia macho binti yake, akiyaweka yak wake kando na kuyabeba ya mwanawe.
‘Pam!...what’s wrong?’  akamsogelea zaidi na kutaka kujua lakini Pamella akainua mikono juu kama mateka na kufumba macho kwa sekunde kadhaa, alipoyafumbua akahitimisha!
‘Tuachane na haya mama… twende tukajaribu hizo nguo’ akanyanyuka na kuanza kukifuata chumba cha kujaribishia nguo, akimuacha mama yake amesimama pale pale akimtazama binti yake kwa namna ya kutom muelewa.
8888888888888888888
Jerry Agapela alikuwa yu kitandani akisoma gazeti alilomtuma Sindi akanunue asubuhi hiyo. Lile gazeti lilikuwa mkononi kama ushahidi tu kila mara alimtazama Sindi aliyekuwa anaandaa meza kwa ajili ya kustaftahi muda huo wa saa tano.

Alimtazama kwa sekunde chache kisha akarudisha akili yake gazetini. Akafunua ukurasa mmoja baada ya mwingine, hakuelewa lolote sembuse kulisoma tu. Akaliweka pembeni na kuteremsha miguu chini akiitazmaa meza ndogo iliyokuwa na chakula mbele yake.

Sindi akangia na beseni dogo lililokuwa na jagi ndani yake. Akaja nalo mpaka pembeni ya Jerry na kummiminia maji wakati akinawa. Jerry alinawa akimtazama Sindi usoni na kutaka kutaka kutabasamu, lakini alishindwa.
‘Niko kwa Jamila hapo’ Sindi akamsemesha wakati akigeuka na lile beseni akijiandaa kuufuata mlango

‘Kha! kwa hiyo chai nakunywa mwenyewe?’ Jerry akauliza kwa mshangao
‘Ukinywa mwenyewe hushibi?’ Sindi naye akamuuliza
‘yaani uandae chai mke wangu kisha unisusie hapa niinywe mwenyewe…umeiweka limbwata?’ Jerry akatania akivuta kikombe. alitania tu, alifanya masikhara na asijue utani wake ulingeleta balaa gani.

Sindi akafinya uso na kumtazama Jerry kwa jicho kali sana la pembeni.
‘umesemaje?’ akamuuliza kwa shari sasa na Jerry akainua uso na kushangaa ile shari ilikotokea
‘Sindi!’ Jerry akamshangaa, hakuona mantiki ya ile shari
‘Nakuuliza umesemaje?’ Sindi akageuka sasa na kumtazama Jerry moja kwa moja, akimung’unya mikono yake. Kitumbua kilichokuwa mkononi mwa Jerry kikashindwa kusogea mdomoni wala kurudi kwenye sahani.  Jerry akatikisa kichwa asimuelewe mwenzake aliyepaza sauti kuuliza kana kwamba alikuwa akigombana na mtu aliye upande wa pili wa barabara.

Sindi akainama, akakichukua kile kikombe cha chain a kuimimina chao kwenye lile beseni la kunawia ambalo bado lilikuwa mikononi mwake. Akainyanyua sahani ya vutumbua na kuvimimina kwenye lile beseni la kunawia llilokuwa na maji machafu pia. Akainuka na kumtazama Jerry.

‘Nenda kanywe chai uko usikokuwa na wasiwasi wa kuwekewa limbwata’ Akageuka na kuanza kuuelekea mlango. Jerry bado alikuwa haamini kama lile tukio lilikuwa limetokea mbele yake. Hata kile kitumbua kilichokuwa mkononi mwake alikiona kama kipande cha jiwe. Akakiweka juu ya meza na kumkazia macho Sindi. Naye Jazba zikionekana kumvaa!

‘We’ Sindi..’ akamuita kwa sauti yenye hasira ndani yake. Sindi hakugeuka aliufungua mlango na kutoka nje. Akaubamiza kwa nguvu na kumfanya Jerry afinye macho na kukaribia kuaziba masikio yake. Kama mazaha tu chai ndio ilishapotea mbele yake na vitumbua alivyokuwa anavingijea ndio vilishayeyuka.

Alijiinamia na kukuna kichwa, hakumuelewa na ile dhana kwamba huyu mwanamke alikuwa na mimba inayompelekesha ilimrudia tena kwa kasi akiunganisha na tukio la kukuta kile kifaa cha kupimia mimba. Akanyanyuka na kuufuata mlango, akatoka kwenye kordo na kukuta akina mama kadhaa wakiwa na majiko yao wakijishughulisha na mapishi ya hiki na kile.

Hakusemezana na mtu akapiga hatua mbili tu na kuufikia mlango wa Jamilla. Akagonga mara mbili na mlango ukafunguliwa na Jamilla ambaye hakupata hata nafasi ya kuuliza kulikoni. Alishtukia tu mlango alioushikilia ukitanuliwa kwa nguvu na Jerry akaingia mle ndani mwake na kumkuta Sindi ameketi kitandani.

Hakusemeshana naye zaidi ya kumvaa na kumshika mkono akimvuta kumuondoa mule chumbani. Sindi akagoma akifoka na kumshambulia Jerry amuachie. Jamilla akataka kuingilia kati kumnusuru shoga yake lakini Jerry akamuwahi.
‘….Hayakuhusu’ Jibu fupi tu lilimtosha kumfanya Jamilla akasimame kando akiwashangaa. Yale makelele yalifanya wanawake waliokuwa kordoni nao wasogee eneo la tukio.
‘Jamani amefanya nini unamvuta hivyo….we Jerry hebu muachie kwanza…. hebu muachie basi khaaa!’ Kila mtu alisema lake lakini Jerry hakujibu kitu alikazana kumuondoa Sindi mule kwa Jamilla na akaweza. alipomuingiza Sindi chumbani kwake akafunga mlango kwa ufunguo na kuuchomoa. Majirani wakanasa mlangoni!

Sindi alikuwa na anahema na hasira alizokuwa nazo zilimuongezea machozi usoni. wote wawili walikuwa na jazba kubwa sana.
‘Nirudishe kwetu…siwezi maisha haya’ Sindi alisema kwa jazba na Jerry akacheka kwa dharau
‘Kwenu?...wapi?’ akamuuliza Sindi kwa hasira akimkaribia na Sindi akairudi nyuma
‘kwani tulipokuokota tulikuokota wapi?’ Sindi naye akapandisha
‘Sindi nitakuumiza…nitakuumiza unajua…’ Jerry sasa alitamba akiume akimtanulia Sindi kifua na Sindi akaona hali inazidi kuchafuka. Kule mlangoni sauti mchanganyiko zilisikika zikimtaka Jerry afungue mlango la sivyo wangeubomoa.

‘Niumize….kwani umeshaniumiza mara ngapi….mara ngapi…niumize sasa’ Sindi alijibu kwa sauti ya unyonge akilia kwa kwikwi na hapo hapo akirudi nyuma na kuufikia ukuta. Jerry alishamkaribia naye akiwa amefura
‘mimi ni nani kwako Sindi?’ Jerry akauliza akihema
‘Sikujui’ Sindi akajibu kwa kiburi lakini sauti yake ilikisaliti kiburi na kutoka kwa unyonge, hofu ya kupigwa ilishamvaa!

‘hunijui?...unaishije na mtu ambaye humjui…nakuuliza wewe unaishije na mtu usiyemjua?.... ulitekwa kuletwa hapa?.....si ulikuja kwa hiyari yako yako’ Jerry alikuwa anaongea kwa hasira kwelikweli
‘Ulinidhanganya….ungeniambia dhamira yako wazi nisingekuwa hapa hapa mimi….Yuko wapi Nyanza aliyejidai ungemfuata yuko wa…’ Sindi alikatisha sentensi yake na kupiga ukunga
‘Uwiii mamaaa’ Akainamisha kichwa na kukiziba kwa mikono yake mara tu alipoona Jerry amenyanyua mkono. Mkono ule ulibaki hewani ukitetemeka na Jerry akijaribu kuzuia jazba zake zisitende kilichotaka kutendeka.

Akaushusha mkono wake na taratibu akaketi kitandani na kujiinamia. akihisi maumivu yaliyochanganyikana na hasira. Akainua uso na kumtazama Sindi aliyekuwa anatetemeka na kumtazama Jerry kwa woga.
‘Sindi…’ akamuita akihemea mdomo
‘Sindi…’ akaita tena na tena na kufumba macho kama mtu anayesikilizia maumivu ya ndani kwa ndani.

‘una mimba!’ akatamka alichotaka kutamka. Lile tamko sit u lilimfanya Sindi aachame mdomo na kutoa macho hata kule mlangoni wale waliobanana kusikilizia na kuwaomba wasiumizane walinyamaza ghafl na kutazamana kama watu waliosikia tarehe zao za kufa!
‘Kasemaje?....nini?....mimba ina nini?’ wale walikosa kusikia vema wakautoa ukimya mlangoni kule na kuulizana mradi tafrani.

Jerry alinyanyuka na kukifuata kile kifaa mlangoni. Zile hatua za kuufuata mlango ziliwafanya wapangaji watawanyike mbali na mlango na kusimama kusikilizia, wakingoja mlango ufunguliwe. Hola!

Akakitoa kile kifaa toka kwenye mfuko wa shati na kuja nacho mbele ya Sindi.
‘ulinunua hiki cha kazi gani?’ Jerry akauliza akiwa amemsogelea Sindi pua kwa mdomo. Sindi akatazama pembeni uso ukiwa chini. Jerry akatumia mkono wake kukishika kidevu cha Sindi na kukitumia kuugeuza uso wa sindi urejee mbele ya macho yake.

Macho yaliyometameta kwa machozi yalimtazama kwa huruma. alikuwa binti mdogo tu, hakuwa na uzoefu wowote wa kuishi na mwanaume, ilikuwa mimba ya kwanza, mkanganyiko wa hisia ulimpelekesha mno, pengine alifanya vitu na asielewe kwanini alivifanya!

Jerry akamtoa Sindi pale ukutani na kumleta kitandani. Akamketisha nay eye kuketi kando yake. Sindi alikuwa kimya, kama mtu aliyevamiwa na hamaniko lisilo rasmi.
‘unataka kupima?’ Jerry akamuuliza kwa upendo akimsugua sugua mgongoni na Sindi akaitikia kwa kichwa. malengelenge ya machozi yakiteremka mashavuni mwake. Jerry akamfuta machozi na kunyanyuka.

Akapekua huku na kule na kurejea na kifaa alichodhani kingesaidia kukamilisha kazi yao. Wakaupata mkojo na kukitumbukiza kile kifaa. Jerry aliyekuwa nacho mkononi. alihisi kutetemeka mstari wa kwanza ulipojichora, almanusura aangushe kile kikpo alichokuwa ameshika. Mstari wa pili ukajichora na jibu likapatikana. Kiumbe kilishaumbwa! mchezo walioucheza ulitoa matokeo chanya! Mioyo yao ilidunda kwa kasi walipotazamana!

Sindi alijiinamia na Jerry ndio alihisi mwili ukipigwa na ganzi ghafla! pamoja na yote aliyoambiwa na Meddy hakuyatarajia maneno ya Meddy yawe kweli. Kila mmoja aligeukia upande wake akiwaza lake
888888888888888888888888888

Kule kwa Agapela, Sehemu kubwa ya nje ilishafungwa maturubai meupe  machache yaliyokuwa na meza zilizoanza kufungwa urembo na viti kuvishwa vitambaa kuongeza nakshi. Fiona alikuwa amesimama akiiwatazama wapambaji lakini pia akionekana kukosa raha. Mumewe alimfuata mpaka pale alipokuwa amesimama
‘I thought umeshaenda shopping’ alimsemesha Fiona ambaye aligeuza kichwa akitabasamu na kumtazama mumewe
‘Kristus….winning your heart will do me good kuliko shopping’ akamjibu kwa tabasamu na kugeuka, taratibu akipiga hatua na kumuacha mumewe anamtazama pasipo kumuelewa kabisa.

‘Winning my heart?...’ akajiuliza kwa sauti nab ado hakuelewa Fiona alimaanisha nini. Akamtazama Fiona aliyekuwa ameshawafikia wapambaji na kupitia kazi zao. alimtazama mpaka pale Fiona alipogeuza uso na kumtazama. Wakatazamana!... Fiona hakutabasamu nah ii iliashiria kitu kizito nyuma ya kauli yake lakini ndio mzee hakuielewa kwa wakati ule.

Akageuka na kuondoka. Wakati akizikaribia ngazi za kuelekea ndani kwake akasikia kelele na akajikuta anageuka.
‘Aawww! See who is here…Clariiii…Jenifa alimkimbilia rafiki yake aliyekuwa nadio ameingia getini na kumkumbatia kwa furaha. Marafiki hawa walikumbatiana kidogo wadondoshane na Mzee Agapela akajikuta akitabasamu tu na kuendelea na safari yake ya kuelekea ndani.

‘Mungu wangu!....una tabia mbaya Clarita hukuniambia unakuja jamani…why?’ Jenifa alimzonga rafiki yake wakati wakielekea kuketi katika moja ya viti vilivyokuwa vinangoja kufanyiwa kazi.

‘Nilitaka nikusurprise….Jerry yuko wapi?’ Clarita Gabson akauliza akiangaza angaza
‘Hebu msahau huyo mtu kwanza…. we have a lot to talk…yaani siamini yeyiii…. twende ndani kwanza…’ Jenifa akasimama akitaka kuhama toka pale walipokuwa wameketi
‘Talk show room!’ Clarita akatania akikumbushia walivyopenda kukiita chumba cha Jenifa cha kulala sababu ya kukigeuza sehemu ya kupigia soga zao

Jenifa na Clarita wakacheka na kunyanyuka, wakaondoka eneo lile kuelekea ndani.
8888888888888888888888888888

Taa zilizokuwa zikiwaka kila kona zililipejndezesha eneo la tukio kwa kiwango kikubwa mno. Magari ya kifahari yaliyokuwa yamekaribia kuziba njia yalitapakaa kila kona. geti la nyumba ya Mzee Agapela lilikuwa wazi, ingia tokay a hapa na pale iliendelea kila muda ulipozidi kukatika. Palikuwa pamechangamshwa zaidi na muziki wa taratibu uliokuwa unasikika vizuri hewani.

nje ya nyumba watu walikuwa wamesimama wakipata vinywaji na kubadilishana mawazo huku wengine wakiwa wameketi kwenye viti. mlango wa kuingilia ndani ulikuwa wazi pia ukiruhusu watu kuingia katika sebule pana ya kisasa ambako ndiko hasa alikokuwa Mzee Agapela.

muda huu wa saa moja watu ndio walikuwa wakiingia na wenza wao. Kule juu vyumbani kulikuwa na mengi yanaendelea. chumba cha Fiona na mumewe, Fiona alikuwa amesimama dirishani akiwa amevalia gauni lake la kulalia. Ni kama alikuwa amesusia sherehe ya mumewe. alisimama dirishani na kutazama nje huku akiwa na glasi yake ya mvinyo, akionekana kuzama mbali kimawazo mpaka pale Mzee Agapela alipoingia.

‘You are not doing this to me Fiona!...kwanini?’ Mzee Agapela alimuuliza mkewe akimfuata pale alipokuwa amesimama
‘Nazungumza na wewe’ mzee aliongea tena na Fiona hakutikisika hata kidole sembuse kugeuza kichwa ama kujibu alichoulizwa.

Mzee wa watu akasogea tena na kusimama pembeni kabisa ya mkewe
‘Fiona?...nini tatizo?’ akamuuliza mkewe kwa upole na Fiona akahamisha macho yake toka kule mbele na kumtazama Kristus!

‘hakuna kitu!’ akajibu kwa ufupi na kukirudisha kichwa kule mbele
‘sasa kwanini unanifanyia hivi katika siku muhimu kwangu…. kila mtu anakuulizia uko chini….unanipa wakati mgumu sana kwanini Fie’ mzee akalalamika na Fiona akaguna kwa kejeli na kujinywea funda la mvinyo wake pasipo kuhangaika na Agapela.

‘kama una tatizo ama chochote kile….nakuomba tumalize hii sherehe salama kisha tukae chini uniambie…kwa wakati huu nakuomba Fiona… iondoe hii aibu unayotaka kuileta kwangu’ Mzee akabembeleza akimgusa mkewe bega
‘Ondoa mkono wako’ akamkemea mumewe pasipo kumtazama

Mzee Agapela akashusha pumzi na kuamua kutoka mule chumbani akimuacha Fiona palepale alipokuwa amesimama.

Chumbani kwa Jenifa, Clarita alikuwa amesimama akitembea huku na kule kama mtu mwenye mchecheto na akiitazama saa yake ya mkononi. Alienda mpaka mlangoni na kurudi mpaka kona moja ya chumba alienda tena na kurudi akfanya safari zenye idadi inayochanganya kuhesabu. Ghafla tu akasimama na kuutazama mlango ukifunguliwa na Jenifa akaingia akiwa ameongozana na Jerry.

‘Surprise!’ Jenifa akammwambia kaka yake akimuonyesha Clarita
Watu hawa wawili wakaganda kama masanamu kwa sekunde mbili tatu kabla ya Jenifa kuwaondolea bumbuwazi lililowatembelea.
‘you guys can talk now….am out!’ akajitoa taratibu na kuufunga mlango akiwaacha hawa wawili wamesimama tu wakitazamana.

‘za siku?’ Jerry akavunja ukimya na Clarita akatabasamu
‘njema…how have you been?’ Clarita akauliza akijaribu kuzuia tabasamu lake na asiweze. mapenzi yake kwa Jerry yalikuwa na uzito ule ule
‘poa’ jerry akajibu naye akijilazimisha kutabasamu.
ukimya ukapita kati yao kila mmoja asijue aseme nini kwa mwenzake

‘umependeza sana’ Clarita akavunja ukimya na Jerry akatabasamu zaidi
‘Na wewe pia’ akajibu sasa akili yake ikitafuta cha kuzugia na asipate
‘Jerry…’ Clarita akaita kwa upole na Jerry akaongeza tu ukubwa wa macho yake kuashiria alikuwa anasikiliza
‘hujanimiss hataa?’ Clarita akauliza na Jerry akajikuta akikata lile tabasamu na kumuwekea Clarita uso wa mkavu!
‘no!’ akajibu akimtazama Clarita usoni.

Ule uso wa tabasamu ukaanza kutetereka na Jerry akaona dalili za kuingizwa kwenye kazi ya kubembelezana na mtu
‘Nimefurahi kukuona Clarita….’ Jerry akaongea akiunga na ishara ya kutupia dole gumba nyuma kuonyeshea kuwa alitaka kutoka, na hakungoja ruhusa akatoka na kumuacha Clarita ameduwaa. Alipotoka tu na Jenifa akaingia na kumkuta rafiki yake amejiinamia

‘Amekwambiaje?’ jenifa akauliza kwa wasiwasi lakini hakupata jibu. Clarita alikuwa amepoteza nuru ya uchangamfu aliokuwa nao tangu asubuhi.

Saa moja baadaye kule chini sebuleni, Mzee Agapela alikuwa akibadilishana mawazo na mwanasheria wake Dennis Mazimbwe, wakiwa na vinywaji vyao mkononi. mlangoni Familia ya Okello ilikuwa inaingia, ikisalimiana na watu mbalimbali na wakati huo Jenifa na Clarita na baadhi ya mabinti wa wageni wengine walikuwa wamesimama kwenye kona moja wakiongea na kuteta hili na lile.

‘The devil herself!’ Jenifa akatamka alipomuona Pamella Okello akiwa na wazazi wake wakiingia. wenzake wakageuka na kumtazama Pamella ambaye wala hakuwa na habari kuwa kulikuwa na watu waliokuwa wanamtazama kwa chuki.
‘Nikimuangalia sioni cha kunizidi…sioni cha kunitoa knock out kwa Jerry… that girl is a witch’ Clarita alizungumza na kumtazama Pamella kwa chuki. Wasichana wengine wakacheka tu na kuzidi kumkodolea macho Pamella alipokuwa akijongea kumfuata Mzee Agapella akiwa na wazazi wake.

‘My Princess!’ Mzee Agapela akamlaki Pamella kwa furaha
‘happy birthday baba Jerry’ Pamella akamtakia heri ya siku ya kuzaliwa huku akiwaacha wengine wakicheka kwa vile alivyomuita
‘Asante mwanangu…’ Mzee Jerry akaitikia na Pamella akamtazama Dennis Mazimbwe na kumsalimia kwa bashasha, moyoni akijua kwanini alimsalimia vile.  alikuwa shemeji yake kwa Patrick! Dennis akajikaza kuipokea ile salamu kwa uchangamfu moyoni akijua yule ni binti yake, damu yake!

Rebecca alijaribu kuzuga kutabasamu akikwepesha macho yake yasikutane nay a Dennis kabisa. Mzee Okello akaunga salamu kwa Dennis, akiongezea utani kwa kuchomeka maneno ya kimahakama kumtania  Dennis. Kila mmoja alicheka isipokuwa Rebecca!

Wakati maongezi yakipamba moto, Meddy alifika na kumfuata Agapella akamnong’oneza kitu kisha akawasabahi aliowakuta. Mzee Agapella akawataka radhi na kusogea kando na Meddy. Kuondoka kwa Mzee Agapella akukawapa Mzee Okello na Dennis nafasi za kuongea zaidi wakati Mkewe na Pamella wakijumuika na wanawake wengine wakiokuwa hapo karibu!

Meddy alipomalizana na Mzee Jerry akatoka na kulifuata kundi la akina Jenifa
‘Hey warembo…nani amemuona Jerry?’ akauliza
‘Chumbani juu’ Jenifa akajibu na Meddy akaachana nao na kuzifuata ngazi na kwenye ngazi hizo akapisha na Fiona aliyekuwa anaziteremsha kwa madaha na kwa kujiamini kuwa alikuwa amependeza hasa. Mzee Agapella akatabasamu wakati akimtazama mkewe.

Chumbani, alikokuwemo Jerry ndio chumba alichokulia akiwa mtoto. alikuwa ameketi chini na chupa ya mvinyo katikati yake. Aliikunja miguu yake na kuyafanya magoti yake egemeo la mikono yake. alikuwa na zaidi ya msongo. Meddy alipofungua mlango na kuingia ndani alimshangaa Jerry.
‘Hey man!....vipi?’ akamuuliza akimfuata kwa kasi pale chini
‘Jerry…’ Meddy aliita akiitoa ile chupa ya mvinyo mbele ya Jerry na kuiweka juu ya meza kisha akaketi kitandani na kumtazama rafiki yake ambaye sasa alinyoosha mguu moja sakafuni na kuegemeza kichwa ukutani akimtazama Meddy.

‘She is pregnant!’ akaongea kama mtu aliyekata tama
‘Whaat!.....Sindi?’ Meddy akauliza akimtazama Jerry ambaye aliilegeza tai yake ya kipepeo na kuiondoa kabisa. Akalijibu swali la Meddy kwa kichwa
‘Congrats man! huh!’ Meddy akajibu akitabasamu  na hapo hapo akionyesha kutoamini
‘Nifanyeje?...’ Jerry akauliza akifumba macho na kutulia
‘Dah!....’ Meddy akakosa jibu wakabaki kutazamana tu.
88888888888888888888

Sherehe ilishachangamka na watu kupata chakula, katika eneo la maegesho. Watu wawili walikuwa wamesimama wakizungumza. Mazungumzo yao hayakuonyesha kuwa ya amani sababu ya lugha ya mwili iliyoonekana.
‘It is a taboo Dennis….huonyeshi kujali lakini mimi najali….she is my daughter’ Rebecca aliongea kwa Jazba mbele ya Dennis
‘Nani amekwambia sijali?....lakini unapanic kiasi kwamba ni rahisi kuhisiwa visivyo…. tumeitunza siri hii kwa miaka sasa…nini kinakupa mchecheto kiasi cha kukosa amani?’ Dennis alionekana kukerwa na wasiwasi wa Rebecca mke wa Okello.

‘kama si mdogo wako kuwa na binti yangu….nisingehangaika hata kuzungumza na wewe… muondoe Patrick maishani mwa binti yangu haraka iwezekanavyo…’ Rebecca alikuja juu
‘talk to Pamella…sawa?...talk to her akwambie ukweli….ukute anakutania’ Dennis alizidi kubisha
‘Atanie kwa kumtaja mdogo wako?....kivipi?....na kipi kinakuaminisha kuwa Patrick hatoki na Pamella?’ Rebecca aliuliza kwa hasira sasa. hofu aliyokuwa nayo ilionekana kutomgusa mwenzake

‘Kwa sababu Patrick ana binti mwingine….na ameshamleta kwangu juzi baada ya binti huyo kutoka masomoni. na yuko hapa!...nashangaa unapokazania kuumba kitu kisichokuwepo’ Dennis alitetea kujiamini kwake
‘Yupo hapa?....who is she?’ Rebecca akauliza kwa udadisi
‘Clarita Gabson…Jenifa’s bestfriend’ Dennis akajibu akitarajia kuona utulivu usoni mwa Mwanamke huyu!

Rebecca akamtazama Dennis kwa kituo
‘Clarita!.... so ndio mchumba wa Patrick sasa?’ Rebecca akauliza akiwa bado haamini
‘Una hofu ya bure Rebecca…hofu ya kujitakia…. relax… siri yetu iko salama na ukitulia itabaki salama milele…okay!’ Dennis akaongea akiwa amemshika Rebecca mabega. Taratibu mwanamke huyu akakilaza kichwa chake kifuani pa Dennis na Dennis akampokea na kumhifadhi.

…………MKOROGANO……….

2 comments:

  1. majanga premier!!!! iam speechless uwiiii.....

    ReplyDelete
  2. duh ingine line i like the story wish uiandike kila siku congrats

    ReplyDelete



Snowfall Widget for Blogger


Snowfall Widget for Blogger