4
Sehemu ya nne
Njia nzima Sindi na Jerry walibishana hiki na kile,
wakaelezana haya na yale. Kwa muda mfupi tu waliozungumza njiani Jerry
aligundua Sindi Nalela alikuwa na upeo mkubwa tofauti na elimu yake ya shule ya
msingi aliyokuwa nayo.
Pasipo kujua Nyanza alikuwa akiwafuatilia nyuma, walisimama
na kubishana, wakisontana kwa vidole na mara kadhaa Jerry akikwepa vibao vya
Sindi pale alipomtania na kumcheka. Nyanza aliyaona yote haya na aliyafuatilia
kwa umakini mkubwa mpaka pale alipohisi asingeweza kuwafuatilia tena baada ya
Sindi na Jerry kuagana na kila mmoja kushika njia yake.
Uso wa Nyanza uliojaa
makunyanzi ya wivu uliochanganyikana na kutokuuelewa ule karibu kati ya Sindi
na Jerry.
Kwa hatua za kinyonge alitembea kurudi kule alikotokea, akiwa
na hali ya kutaka kujiuliza maswali kwa sauti na hapo hapo akighairi na
kujaribu kuimezea hali ile. Aliumia!
Sindi Nalela aliingia katika uwanja wa nyumba yao
na kusimama kwanza akichungulia upenuni mwa nyumba yao
ambako mama yake alikuwa akitwanga mpunga kwenye kinu kikubwa. Akaamua kuingia
ndani kwanza kupeleka vifaa vyake vya kufundishia na kisha akatoka akiwa
amejifunga upande wa khanga kiunoni na kubadili viatu.
Alizunguka kule alikokuwa mama yake na kumsalimia, akibonyea mpaka chini kama
ilivyo desturi. Mama yake hakujibu, alimtupia jicho kali sana
kisha akaendelea kutwanga mpunga wake. Uso wake tu ulitosha kumfanya Sindi ajue
kuna kitu kilikuwa kimemkera mama yake.
‘kuna nini mama?’
aliuliza kwa upole
‘Sina roho ya chuma wala sura ya bati kuweza kustahimili
unayoyafanya Sindi…’ mama aliacha kutwanga na kuongea kwa jazba
‘ nimefanya nini mama!?….’ swali lenye ladha ya mshangao
lilimtoka Sindi na hapo hapo akimsogelea mama yake na kumtazama kwa udadisi.
Ni kama vile Mama Sindi alitaka kumtesa binti yake kwa
maswali ya kichwa. Hakulijibu swali lake, akaamua kuinua mche wa kutwangia na
kuendelea kutwanga. Sindi akatulia kwanza akimtazama mama yake pasipo kujua ni
nini hasa kilikuwa kimemkwanza. Taratibu akapiga hatua na kuanza kuondoka pale
karibu na mama yake. Hatua zile zilimfamfanya Mama Sindi asimamishe shughuli
yake na kumtazama Sindi kwa jicho kali, jicho lililoshiria mkusanyiko wa hasira
moyoni mwake.
‘Unayoyafanya uko yote analetwa hapa…we jitie umajinuni wakati
mahari imeshapokelewa’ akamnanga Sindi ambaye alimsikiliza mama yake kwa
unyonge
‘Sasa mama nimeuliza nililokosea…hutaki kuniambia…unanisemea
mafumbo tu… haya basi litakalonikuta ni langu..nitalibeba mwenyewe’ akajikuta
akimjibu mama yake kwa jazba na kuondoka kwa kazi kuelekea ndani.
Sindi alikimbilia chumbani, akasimama katikati ya chumba
akihema kwa hasira zilizomvaa ghafla lakini pia kwa wasiwasi usio rasmi
ukimtembelea. Akaamua kuvua ile blauzi aliyokuwa amevaa na kuipandisha kifuani
khanga aliyokuwa ameifunga kiunoni.
Wakati akiikaza ile khanga mama yake aliingia na kusimama karibu na kizingiti
cha mlango.
‘Ndio amekupa jeuri ya kuja kunijibu unavyojua?’ mama hakuwa
na mzaha
‘Mama jamani…. kwanini usiseme tatizo ni nini?’ Sindi
aliongea kwa sauti ya kukereka akitupa mabega juu chini na kumtazama mama yake
kwa kituo.
‘ wanakuona uko ukizunguka na yule mwanaume….’ mama akasema
dukuduku lake
‘yupi?’ Sindi akadakia haraka sana ,
vinyweleo vikimsimama
‘Mi namjua?.....yule mlimuokota porini uko sijui wapi…. watu
wanakuona naye mawio kwa machweo….tukueleweje?’ akamshikia kiuno binti yake na
uso sasa ukimkunjuka kiasi baada ya kusema dukuduku lake.
Sindi akashusha pumzi kama mtu
aliyeshtukizwa na taarifa ile, macho ya wasiwasi yalimcheza lakini moyoni alijua
haikuwa vile watu walivyofikiria
‘kwa hiyo nisiongozane na watu?’ akauliza kwa unyonge
‘alipokuwa hayupo uliongozana na nani?.... watu hapa wanamjua
Nyanza na hivi tunangoja kumfuta huyo Nyanza…..umeanza kunyooshewa kidole juu
ya mtu asiyehusika kwa ndewe wala sikio…. mahari kipande imeshaliwa usitake
tuozwe wote humu kwa mtu mmoja….’ Mama alimpasulia ukweli na akitoka pasipo
kumpa nafasi ya kujitetea.
Sindi akaketi kitandani kwa kujipweteka. Alifumba macho
taratibu na kuyasikilizia maneno ya mama yake. Yalimuuma kuliko kidonda
kilichotoneshwa. Ile kauli tu ya kumfuta Nyanza ilimuumiza sana .
Mpaka dakika ile alikuwa hajamwambia Nyanza chochote kuhusu yeye kutolewa mahar
na Mzee Dunia. Alikaa vile akiwa
amefumba macho kwa sekunde kadhaa kabla ya kushusha pumzi ndefu zilizomfanya
akinyanyue na kukishusha kifua chache chenye matiti mateketeke yaliyokuwa
yamesitiriwa na ile khanga kifuani.
Alifumbua macho na kuytatembeza mule chumbani kana kwamba
alikuwa akitafuta kitu ambacho kingempa faraja muda ule. Hakuona! Akayatuliza
macho yake kwenye kikapu cha nguo kilichokuwa umbali mfupi toka pale,
akikitazama pasipo kukitambua akilini. Alikuwa na mtihani mkubwa mbele yake,
mtihani ambao hakutaka kujipa hata nusu ya sekunde kuufikiria hali akijua
kutokuufikiria kusingesaidia.
888888888888888888
Baada ya chakula cha usiku Sindi aliingia kulala pamoja na
wadogo zake. Wakati wao wakitandika kitanda na kuweka sawa mazingira ya kulala.
Sindi alikuwa akinyoosha nguo kwa pasi ya mkaa huku akimulikwa na mshumaa
uliokuwa unawaka juu ya kigoda kilichokuwa mbele yake.
Walikuwa wakiongea na kucheka, wakikumbushana matukio ya
kufurahisha ya siku hiyo. Vicheko vyao vilitulia ghafla walipohisi dirisha lao
la mbao likitikisika. Wakasikilizia kidogo na kwa mara nyingtine dirisha
lilitikisika tena na wote wakatazamana, ni kama vile
waliijua ile ishara ilimaanisha nini. Sindi akanyanyuka haraka na kukimbilia
dirishani na wakati huo huo wadogo zake wakimfuata na kumsaidia kuchungulia.
Nyanza aliyekuwa chini ya mti alipunga mkono na wasichana hawa wakaomuona. huku
wakicheka kichinichini walimsaidia Sindi kutoka nje kupitia pale dirishani
kisha wakafunga dirisha na kurejea haraka ndani, wakikimbilia kitandani na
kuunganisha mito . Walifanya haraka
haraka kwa kuifunika ile mito
mithili ya mtu aliyelala.
Kule nje Sindi alitembea kwa kunyata mpaka alipomfikia Nyanza
aliyekuwa amesimama kwenye giza
kidogo. Sindi akataka kumkumbatia Nyanza lakini mikono yake ilipanguliwa kwa
kasi na kumfanya Sindi amtazame Nyanza kwa mshangao
‘nini tena?’ Sindi aliuliza akizidi kumsogelea Nyanza
‘ameanza kuwa wa maana sana
kuliko mimi?’ Nyanza aliongea kwa ghadhabu
‘Nani?’ Sindi akauliza akitupa mikono yake yote miwili hewani
‘Jerry!’ kwa sauti ya kiume iliyojaa wivu, Nyanza alilitamka
jina la Jerry na kumfanya Sindi ashushe pumzi tena. Jioni ile alikuwa
amegombana mama yake kuhusiana na Jerry na sasa Nyanza alikuwa amemkasirikia
sababu ya Jerry. Kichwani mwake hakuona sababu ya watu hawa wawili kumhofia
Jerry ambaye kwake alikuwa kama mwanakijiji mwingine yoyote
yule, achilia mbali ugeni wake kijijini.
‘Amekuwaje?’ Sindi aliuliza kwa ukali kidogo na kuzidi
kumpandishia Nyanza hisia za wivu
‘ina maana hujui unachofanya au umeamua kunidharau?’ Nyanza
alizidi kuja juu
‘Nimefanya nini?.... kuongoza naye ndio kumezua ugomvi au ni
nini?’ Sindi sasa alionyesha kukereka zaidi
‘ona unavyonijibu kwa jeuri….kwa vile mimi maskini eeh…. kwa
vile sina kazi ya maana Sindi….’ Nyanza alikuwa akilalamika na Sindi alimkatiza
‘Nyanza kama utarudia tena hizi kauli zako za mimi maskini
sijui sina kazi….nakuapia tutatengana vibaya zaidi unavyowaza…. kwani hao wenye
kazi siwaoni au unadhani hao wenye pesa siwaoni…..unadhani kwanini mpaka dakika
hii nimetoroka kwetu kuja hapa?.... na kama mwito huu ni wa shari…usiku mwema’
Sindi aliongea kwa jazba akitaka kugeuka na kuondoka. Nyanza alimdaka na
kumzuia asiondoke
‘nimekuona naye jioni ya leo…naumia Sindi mwanaume mwingine
anapokusogelea vile’ Nyanza sasa sauti ilikuwa ya kulalamika
‘Wivu nyanza!....huu wivu ulionao ndio unafanya tunagombana
kila siku….Jerry hajanitongoza na ni mtu mwenye heshima zake na sidhani kama
anawazia unavyowaza wewe’ Sindi alijitetea
‘Mimi ni mwanaume mpenzi wangu…. najua inavyokuwa na
nakuhakikishia Sindi…Jerry atatutenganisha usipokuwa makini’ Nyanza alizidi
kushusha malalamiko mikono yake
ukimvutia Sindi kwake
‘Una uhakika gani?.... ananichukulia kama
dada yake na si zaidi ya hapo…. hebu tuachane na hayo kwanza….’ Sindi
aliyakatisha mabishano yao na
kujisogeza kwa Nyanza zaidi kiasi cha kuwa sambamba pua kwa pua
‘Nimevumilia mwaka sasa…. niahidi nitakubikiri mimi Sindi’
Nyanza alisema kwa sauti yenye mihemo ya mahaba wakati akizipapasa chuchu za
Sindi kwa matamanio ya hali ya juu
‘Mimi ni wako jamani…’ Sindi alijibu akijaribu kuutoa mkono
wa Nyanza uliotaka kuzama ndani ya blauzi yake nyepesi aliyokuwa amevaa
Wakapapasana, wakichezeana na Sindi alipogundua Nyanza
alikuwa katika hali mbaya, alicheka akiitazama suruali yake iliyokuwa
imetutumka eneo la mbele. Akajitoa mikononi mwa Nyanza na kumrushia busu akianza
kurudi mbio kule dirishani. Nyanza aligugumia maumivu ya msisimko alioupata. Alikuwa akiingoja kwa
hamu siku ambayo angeliupokea usichana na wa Sindi. Aliiota siku hii,
aliitamani mno na sasa alitaka ifike kwa namna yoyote ile akihofia kuzidiwa
kete na huyu mgeni asiyejua alikotokea.
Wakati Sindi na Nyanza wakimjadili Jerry Agapela, yeye
alikuwa kitandani katika moja ya vyumba nyumbani kwa mwenyekiti. Chumbani
alimokuwemo, kulikuwa na kijana wa mwenyekiti aliyekuwa anagundisha viatu
vyake. Umeme uliokuwa katika nyumba ya mwenyekiti ulimsaidia Jerry kusoma
kitabu alichokuwa nacho mkononi lakini mara kadhaa akikitua na kuzungumza na
yule mtoto wa mwenyekiti aitwaye Chidi.
‘nani Sindi?....hahahahaaaa yule kwanza kumpata inahitaji
nguvu ya ziada’ Chidi alizungumza akicheka wakati wakimjadili Sindi
‘Kwanini?’ Jerry aliuliza kwa pozi kidogo akiwa amelala
chali, mkono mmoja ukiwa kisogoni na mwingine ukiwa na kitabu kilichokuwa
kimelala kifuanim pake
‘She is smart aisee…. kuna jamaa anaitwa Nyanza ndio kashika
makali pale….ila nasikia anasotea mwaka mzima hajala mzigo’ Chidi alisema
akijiandaa kucheka
‘What! mwaka?…kwanini’ Jerry aliuliza kishabiki akijiinua
kidogo na kulala kiubavu
‘Ohooo!.... Sindi hajaguswa yule…. anapangua mitego so
kitoto’ Chidi alijibu na kumfanya Jerry alitoe macho kwa mshangao
‘Kwamba ni bado bikra au?’ alikuwa bado hajaamini
‘ndio maana yake’ Chidi akajibu akinyanyuka na kwenda
kuviweka viatu vyake sehemu yenye upepo wakati huo Jerry akiwa anaonekana
kutoamini alichosikia.
Akaliita jina la Sindi mara kadhaa na kumfanya chidi acheke
na kutikisa kichwa…..
MAMBO YALIANZA HIVI..... USIKOSE KUJUA KILICHOJIRI
No comments:
Post a Comment