ANNIE NG'INGO...
Annie |
Nimeamua tu siku moja moja kuwa na mgeni humu
ndani…nimuulize machache, tuongee hiki na kile. Wahenga walisema mgeni baraka
nami ndio nazikaribisha baraka hizo ndani ya blog hii…. Naanza na Annie huyu dada nimependa tu na hulka yake, hana makuu na mtu hana chokochoko na watu...hajui kujivuna wala kupanda seuze ile kujiskia juu wakati aliyejuu ni Maulana peke yake. Nilimuuliza machache naye bila hiyana akanijibu
LAURA: Je una
Nickname yoyote mbali na jina lako?
ANNIE: Hapana sina
LAURA: Heheheee you need one darling! may be nikupe nickname moja Kamamaa*wink*
LAURA:Uko
katika mahusiano?…kama ndio unayaelezeaje mahusiano
yako, kama hapana kwanini hauko katika mahusiano?
ANNIE: Hapana siko kwenye mahusiano yoyote,sababu nimeamua kutulia
kwa muda ili niishi maisha ya peke yangu
LAURA: Time will tell dear, you might need somebody to lean on someday....wish you luck!
LAURA: Unapenda
burudani gani?
ANNIE: Kusikiliza mziki wenye mashairi mazuri, kucheki movie
kubadilishana mawazo na marafiki
LAURA: ...Oooh hujasema unapenda kusoma riwaya... and you seem to be a cooool lady
LAURA: Ukiambiwa
uchague watu watatu popote duniani wa kupata nao dinner usiku mmoja katika
hoteli ya nyota tano. Utawachagua akina nani na kwanini?
ANNIE: Ni mama yangu....mwanangu na mdogo wangu kwa kuwa
ni watu peeke ninao wapenda sana
LAURA: HAHAHAHAAAA! umenisahau na mimi *wink*
LAURA: Je
unafuatilia siasa za nchi hii, kama ndio unadhani
zinakidhi matakwa ya demokrasia?....kama hapana
kwanini hufuatilii?
ANNIE: Sio mfuatiliaji wa ndani sana
ila ni juu juu tu....hapana haikidhi matakwa ya demokrasia
LAURA: I see!
LAURA: Wewe
ni mpenzi wa chama gani cha siasa?
ANNIE: Ningekuwa nafanya biashara ndogondogo
LAURA: Usiniambie ungekuwa unamiliki genge saa hizi....Nice!
LAURA: Nani
kimbilio lako unapikuwa katika wakati mgumu?
ANNIE: Ni familia yangu asa mama yangu
LAURA: Unatamani
kufika wapi ambako hujawahi kwenda?
ANNIE: Canada
LAURA: Aaaww!....mbali kote huko nilidhani ungesema Mabwepande *wink*
LAURA: Unapenda
rangi gani?
ANNIE: Yellow
LAURA: Umewahi
kusoma hadithi za Laura Pettie?...kama ndio
ulivutiwa na ipi hasa
ANNIE: Nimewahi navutiwa sana na utunguji wake maana ni story
zinazokuwa katika jamii yetu
LAURA:...I'm humbled! thanks!
LAURA: Unapenda
chakula gani?
ANNIE: Wali,ugali maharage
LAURA:....Really???....heheheee usiniambie hupendi Burger? *wink*
LAURA:Ni
vitu gani huvipendi kabisa katika maisha yako
ANNIE: Huwa sipendi unafiki....pili kufuatiliwa maisha yangu
LAURA: UZUSHI.COM:
kipi huwa kinakuvutia kwa jinsia nyingine mara ya kwanza unapokutana
naye…urefu, rangi, umbo au nini?
ANNIE: urefu na umbo
LAURA: Hahahahaaaa Annie stop being choosy!
LAURA: UPEKUPEKU.COM:
Ungepewa nafasi ya kujibadili haiba yako ni kitu gani cha kwanza
ungekibadili?
ANNIE: kwa hapa nilipo ningebaki hivi hivi
THANKS ANNIE FOR A LITTLE CHITCHAT.....STAY BLESSED DEAR!
asante sana Laura kwa nafasi iliyo nipa mie penda wewe jamani
ReplyDeleteMajaribio
ReplyDelete