Monday, May 12, 2014

KOREAN DRAMA.... LEE MIN HO a.k.a CITY HUNTER!!



Lee Min Ho 

 Nilikosa tu kazi ya kufanya nikajikuta natamani kuangalia chochote cha kunichangamsha…. Katika harakati za kutafuta kiburudisho nikaletewa CD ya series ya kikorea…. Mimi ni mpenzi mkubwa wa series za kikorea .… kuanzia zile za kihistoria mpaka za kisasa, weka mapenzi na maisha au visasi na vita kwa wakorea hunibandui kwenye kiti!


Safari hii nikakumbana na hii series ya CITY HUNTER!... Wakati naanza kuiangalia kidogo nighairi na kuiweka kando lakini saa moja mbele nikajikuta nang’ang’ania kuiangalia masaa. Sio tu kwa utamu wa hadithi na maudhui yake bali pia kwa waigizaji mahiri walioshiriki hususani muigizaji mkuu LEE MIN HO!!
Aisee!... ni miaka mingi sijakaa kwenye Tv nikatazama kitu kwa usongo na kuvutiwa na muigizaji wa kiume kiasi cha kuhisi nawehuka…ila kwa Lee Min Ho heheheeee I had to rewind and rewind some parts of the series  and guess what….i couldn’t get it enough LOLEST!!
Mkorea Lee Min Ho
Ni ndani ya miezi miwili tangu niitazame Ciy Hunter…. Na tayari nimeshatazama series zake zingine tatu…
kuna hiyo City Hunter …. Hii ni ya kipelelezi, visasi na karate za kutosha, mtoto anaibiwa toka kwa mama yake, aliyemuiba ni rafiki wa marehemu baba wa mtoto. Anamkuza porini uko kama mwanaye kisha amatuma mjini kulipa kisasi… yanayoendelea hapo hadi mtoto kuja kugundua kisasi anacholipisha ni kwa maslahi ya baba mlezi tu… ngoma imeranduka vibaya mno! Piga nikupige zimeshatembea vya kutosha!
Kuna hii Personal taste…. Hii bwana Jamaa mtu wa michoro ya ramani, baada ya mzee wake kudhulumiwa mali akaamua kufungua kampuni yake akihangaikia tenda hapa na pale ili afikie malengo… katika kutafuta namna ya kushinda tenda ambayo anaishindania na kijana mwenzake ambaye baba yake ndiye aliyewadhulumu akina Lee min ho… 
SOMA ZAIDI....


anajikuta akilazimika kuingia katika kashfa ya ushoga ili kutimiza malengo…. Kuna vichekesho humo ndani vya kufa mtu… mikasa ya kutosha… na hasa siri inapofichuka kuwa sio shoga huku binti aliyemkaribisha kuishi naye alijiachia akijua anaishi na mtu asiye rijali… hahahahahaaaa! Hii si ya kusimuliwa uione mwenyewe ushikilie mbavu!



Kisha kuna Boys over flowers:… hii ya kitambo kidogo na ndio iliyomtoa Lee Min Ho. Ni nzuri sana… anacheza kama mwanafunzi mtoto wa tajiri na kundi lake la watu wanne wote watoto wa matajiri… full kunyanyasa watu shuleni hapo…. Bwana we! Akatokea binti wa dobi mmoja ambaye baada ya kumuokoa mwanafunzi hapo shuleni naye akapata nafasi ya kusoma…. Kwanza zilianza kashda za kufa mtu… mateso mateso… shida shida…binti hakubali kunyanyasika kabisaaa ila mwisho wa siku Lee min ho na kundi lake wakajikuta mikononi mwa binti huyo chakaramu… full mapenzi full kujali… yaani haichoshi kutazama!!

FUNGA KAZI SASA…. Kuna kitu THE HEIRS… hii naiita dhoruba! Imetoka mwaka jana tu… hii sijui nisimulie nini sasa maana hapa anaenda kwa jina la Kim Tan!... mwanafunzi wa level ya Diploma hivi… mtoto wa pili wa tajiri mmoja mkubwa sana… tunaanzia marekani tunahamia korea…kuna stori nzuri ya mapenzi kati ya mtoto wa tajiri na mtoto wa mtumishi a.k.a housegirl… wakati huo huo Kim Tan ni mchumba wa binti wa mama tajiri… weeewe! Kuna ngumi mbili tatu… kuna machozi… kuna unyanyasaji…. Kuna mahaba… kuna biashara…yaani haichoshi
Ndani ya The Heirs.... Kim Tan na Young Do wakiamuliwa
Ngumi zilitembea hapa mpaka raha hahahahaaa

LEE MIN HO NI NANI?
Akiwa mtoto mdogo

Alizaliwa June 22, 1987 uko seoul, korea ya kusini…Ni muigizaji na Model wa matangazo… akiwa mtoto wa pili na wa mwisho katika familia yake. Lee Min Ho hakuwahi kuwa ndoto za kuwa muigizaji kabisa!... katika maisha yake ya utoto Lee Min Ho alitamani sana kuwa mcheza soka na hata katika kukua kwake alijishughulisha sana na Soka. Ndoto yake hii ya kuwa mwanasoka ilizimika ghafla alipokuwa high school baada ya kupata ajali mbaya iliyotaifisha ndoto yake ya kucheza soka.

ILIKUWAJE AKAWA MUIGIZAJI?
Akiwa na miaka 18

Anasema mara kadhaa watu wanaomzunguka walimwambia alikuwa na mvuto mkubwa na angependeza kuwa muigizaji… haikuwa rahisi kushawishika lakini mara kadhaa hata watu wageni kwake walimpatia kadi za mawasiliano ili atakapoamua kuwa muigizaji awatafute… taratibu akaanza kuhudhuria majaribio na akajikuta akishiriki kama muigizaji msaidizi.
Alipoigiza Boys over flowers kama mhusika mkuu… mafanikio yalifunguka katika namna ya kipekee, alipata umaarufu nchini Korea, china, na maeneo mengi barani Asia huku akipenya mipaka mpaka sehemu kadhaa  America.

Wapo waliomvunja moyo kuwa asingefika mbali kwani kazi iliyomtoa alibahatisha. Lee Min Ho hakukata tamaa… alizidisha juhudi katika kazi zake na kushiriki kazi zingine kikamilifu zikiwemo tamthiliya na filamu huku akifaya tour nchi mbalimbali kwa ajili ya kuonana na mashabiki wake.

KIPENZI CHA WANAWAKE…

Mama yake anasema Lee Min Ho alikuwa mtoto wa kipekee tangu akiwa mdogo… mara nyingi alikujulikana na kutambulika haraka katikati ya kundi la watoto wenzake sio tu kwa urefu alio nao bali pia kwa sura nzuri na mvuto alio nao. Lilikuwa jambo la kawaida wasichana kupigana au kugombania kuwa naye karibu.
Hali hiyo imekuwa hivyo mpaka leo hii… hahahahaaa  I confess I’m in love with Lee… OMG! The guy is haaawt!...kwa mara ya kwanza I find a Korean guy sooooo attractive!... Mungu wangu umkute analalamika sasa uwiiiii utarewind mpaka ukome…. Those sexy jaws…those lips…them eyes… that long nose…. the height…. How smart he is…. Daaamn! Lee Min can I cook dinner for you hahahahahahaaaa!!
Na kwa taarifa yako katika kila list ya hottest guys in Korea… Lee Min Hoo yupo ndani ya kumi bora kama si tano bora!
Mamia ya mashabiki wake hufunga safari kwenda kumuona Lee Min Ho kila anapokuwa location, wengine hukata tiketi maalumu za kungojea sehemu anazofanyia tour. Tunaobaki hukodolea tv kwa bidii na kuongeza rate za tamthiliya zake zote zinazorushwa hewani.

MAISHA BINAFSI….


Lee hajaoa ingawa amekwisha husishwa na waigizaji wenzake wa kike, akiwemo mmoja aliyecheza naye City Hunter. Ulikuwa uvumi lakini hatimaye walikiri kuwa katika uhusiano kabla ya kuachana na kuweka bayana kuwa wote walishindwa kuwa pamoja muda mrefu kutokana na kubanwa na shughuli zao za uigizaji. Baada ya taarifa za kuachana Lee Min Ho amebaki kuwa single huku akificha maisha yake binafsi mbele ya jamii inayomfuatilia kwa kila kitu.

ANAJIONAJE?

Lee min Ho anajiona wa kawaida  japo anakiri kujua yu mzuri na mwenye mvuto lakini hilo halimfanyi asiseme mapungufu yake mengine kwa kuweka bayana mwanamke anayetaka kuwa naye ajue kuwa Lee ni binadamu wa kawaida…. Lee anasema anapenda sana kulala, anaweza kulala muda mrefu sana bila kuchoka… ana mazoea na kuzungumza usingizini… haya ni moja ya mapungufu yake …. Lolest! Man kwangu mimi hata uimbe no sweat hahahahaa!

ELIMU
Lee min Ho ni mhitimu wa chuo kikuu nchini korea, akiwa na digrii ya Film & Arts toka chuo kikuu cha Konkuk. Amejifunza kupigana taekwondo tangu akiwa high school na alipochukua kazi ya City Hunter ilimpasa kujifua barabara ili kuweza kuimudu kzi yake ambayo kwa hakika ameipatia kwelikweli. Kazi zake zimemletea tuzo nyingi sana  na sasa ni mmoja kati ya waigizaji mahiri  na wanaopendwa mno ndani nje ya Korea ya kusini.

Waaapi Bongo movie... ngumi za kuchapana makofi tuuupa kule nendeni mkajifunze kupigana bwanaaa... tunasikia kishindo cha ngumi duuuuushi huku tunaona ngumi imeparaza  shavu...Lol!!


HUYO NDIO LEE MIN HO!!...tafuta tu series zake uone makeke yake!!!

2 comments:

  1. Hi laura, Umenifikisha napenda sana tamthilia za wakorea i have watched a couple of them, iliyonifungua macho ni ile ya brilliant legacy/shining inheritance. Unalink yoyote inayoweza fanya mtu aangalie online? if Yes pliiiiiiiz nisaidie au hata link ya kudownload hizi za wakorea, utakua umenisaidia pakubwa sana. Asante.

    ReplyDelete
  2. Like to watch movie li min hoo

    ReplyDelete



Snowfall Widget for Blogger


Snowfall Widget for Blogger