Monday, December 3, 2012

MGENI WANGU.....ANNIE

ANNIE NG'INGO...

Annie
Nimeamua tu siku moja moja kuwa na mgeni humu ndani…nimuulize machache, tuongee hiki na kile. Wahenga walisema mgeni baraka nami ndio nazikaribisha baraka hizo ndani ya blog hii…. Naanza na Annie huyu dada nimependa tu na hulka yake, hana makuu na mtu hana chokochoko na watu...hajui kujivuna wala kupanda seuze ile kujiskia juu wakati aliyejuu ni Maulana peke yake. Nilimuuliza machache naye bila hiyana akanijibu
LAURA: Je una Nickname yoyote mbali na jina lako?
ANNIE:  Hapana sina
LAURA: Heheheee you need one darling! may be nikupe  nickname moja  Kamamaa*wink*

LAURA:Uko katika mahusiano?…kama ndio unayaelezeaje mahusiano yako, kama hapana kwanini hauko katika mahusiano?
ANNIE: Hapana siko kwenye mahusiano yoyote,sababu nimeamua kutulia kwa muda ili niishi maisha ya peke yangu
LAURA: Time will tell dear, you might need somebody to lean on someday....wish you luck!


LAURA: Unapenda burudani gani?
ANNIE: Kusikiliza mziki wenye mashairi mazuri, kucheki movie kubadilishana mawazo na marafiki
LAURA: ...Oooh hujasema unapenda  kusoma riwaya... and you seem to be a cooool lady

LAURA: Ukiambiwa uchague watu watatu popote duniani wa kupata nao dinner usiku mmoja katika hoteli ya nyota tano. Utawachagua akina nani na kwanini?
ANNIE: Ni mama yangu....mwanangu na mdogo wangu kwa kuwa ni watu peeke ninao wapenda sana
LAURA:  HAHAHAHAAAA! umenisahau na mimi *wink*

LAURA: Je unafuatilia siasa za nchi hii, kama ndio unadhani zinakidhi matakwa ya demokrasia?....kama hapana kwanini hufuatilii?
ANNIE:  Sio mfuatiliaji wa ndani sana ila ni juu juu tu....hapana haikidhi matakwa ya demokrasia
LAURA: I see!

LAURA: Wewe ni mpenzi wa chama gani cha siasa?
ANNIE: Chadema
LAURA: Heheeee M4C!! for life

LAURA: Kama si kuwepo hapo ulipo unadhani ni kazi gani ungekuwa unafanya sasa?
ANNIE: Ningekuwa nafanya biashara ndogondogo
LAURA: Usiniambie ungekuwa unamiliki genge saa hizi....Nice!

LAURA: Nani kimbilio lako unapikuwa katika wakati mgumu?
ANNIE: Ni familia yangu asa mama yangu

LAURA: Unatamani kufika wapi ambako hujawahi kwenda?
ANNIE: Canada
LAURA: Aaaww!....mbali kote huko nilidhani ungesema Mabwepande *wink*

LAURA: Unapenda rangi gani?
ANNIE: Yellow

LAURA: Umewahi kusoma hadithi za Laura Pettie?...kama ndio ulivutiwa na ipi hasa
ANNIE: Nimewahi navutiwa sana na utunguji wake maana ni story zinazokuwa katika jamii yetu
LAURA:...I'm humbled! thanks!

LAURA: Unapenda chakula gani?
ANNIE: Wali,ugali maharage
LAURA:....Really???....heheheee usiniambie hupendi Burger? *wink*

LAURA:Ni vitu gani huvipendi kabisa katika maisha yako
ANNIE:  Huwa sipendi unafiki....pili kufuatiliwa maisha yangu
   
LAURA: UZUSHI.COM: kipi huwa kinakuvutia kwa jinsia nyingine mara ya kwanza unapokutana naye…urefu, rangi, umbo au nini?
ANNIEurefu na umbo
LAURA: Hahahahaaaa Annie stop being choosy!

LAURA: UPEKUPEKU.COM: Ungepewa nafasi ya kujibadili haiba yako ni kitu gani cha kwanza ungekibadili?
ANNIE: kwa hapa nilipo ningebaki hivi hivi

THANKS ANNIE FOR A LITTLE CHITCHAT.....STAY BLESSED DEAR!














2 comments:

  1. asante sana Laura kwa nafasi iliyo nipa mie penda wewe jamani

    ReplyDelete



Snowfall Widget for Blogger


Snowfall Widget for Blogger