Friday, March 20, 2015

UREMBO NA LAURA:...JINSI YA KUCHORA SIMPLE EYELINER!!

Make up by Laura! 
and the eyeliner too heheheee!


Nimejaribu nilivyoweza.....

Mpo wadau?!

Natumaini mu wazima na mambo yanakwenda vizuri na palipo na mushkeli baaasi Mungu aingilie kati!

Haya leo tuna kitu kinaitwa  Eyeliner…  kusema ukweli miaka miwili nyuma au niseme mwaka mmoja nyuma  ungeniuliza masuala ya eyeliner ningekukodolea macho tu kama si kugoogle ama kutafuta dictionary!... mambo ya kujipamba yalikuwa mbali sana na mimi yaani mbali mnoooo! Urembo pekee ulikuwa kushonea weaving na kutinda nyusi baaasi…make up  sijui mazagazaga gani nilikuwa naona vitu viguuuumu sana…


 Lakini sasa  hivi karibuni tu katika kutafuta hobby mpya nikajikuta nakuwa interested  na masuala ya urembo wa makeup  kwa ujumla… si kwa kutaka kuwa mpambaji basi tu nimejitafutia hobby mpya na ninaifurahia kila ninapopata nafasi na kuifanyia majaribio!


It feels good mnooo unapojaribu kitu kipya na ukaona matokeo…yawe mazuri kidogo au mazuri sana…cha muhimu umejaribu, maisha mafupi kuishi kwa mazoea na kukariri routines!
Sometimes jitazame na ujitafute muonekano mpya…  

YOU ONLY LIVE ONCE DEAR!!!

Eyeliner ni hako kamchoro kwenye macho
ni aina fulani ya urembo inayofanya hata uso wako uonekane tofauti
Kuna dizaini tofauti tofauti za uchoraji macho.

Yaani zipo nyiiingi mno!
Mimi kwa vile si mpambaji na ni mwanafunzi nikachagua simple style tu

Ili kuchora eyeline  unahitaji Eyeliner gel au  eyeliner pencil au eyeliner marker pen


hizi hapa ni aina mbili Eyeliner Marker pen na Eyeliner Pencil

Ninayotumia mimi ni hii hapa!!



hii ndio Eyeliner Gel


Eyeliner gel ninayotumia ndio hiyo hapo!
kuna black na brown
Sio lazima uwe nazo mbili ni uamuzi tu...lakini nasuggest eyeliner marker pen
kwangu mimi ndio rahisi zaidi na nzuri zaidi

UNACHORAJEEE/

Unaona hizo alama za dots kipicha cha juu
Basi fuatiza hivyo hivyo ukiwa umefumba jicho.
Ni rahisi mno usianze kuguna hapo...kama nakuona vile hahahahaaaaa

ukishachora hivyo jazia jazia kidogo basi umemaliza
yaani hata dakika kumi haziishi


BEFORE NA AFTER HIYO HAPO!!

Unafanya meka up yako hiyo eyeliner malizia mwisho maana inachukua muda kidogo tu

NATUMAINI UMEPATA KITU HAPA!
Wikendi ndio hiyo hebu kachore eyeliner bwana kesho harusi ndio vileee
full kutokelezea na smokey eyes na nini na nini!!

CHEI CHEI!!







1 comment:

  1. Hi laura.Nimependa sana mafundisho yako naomba tuwasiliane kwa email elitebeautypoint@gmail.com au namba 0754860403. Kutujuza zaidi na mafunzo

    ReplyDelete



Snowfall Widget for Blogger


Snowfall Widget for Blogger