Saturday, March 7, 2015

HAPPY WOMEN'S DAY



HAPPY WOMEN’S DAY 2015!!
KWAKO…

1. Wewe mwanamke uliyejikubali ulivyo! hii iende kwa wanawake wote weusi tiii kama mimi Waliosema no to mkorogo just to impress somebody! Maana kujichubua sasa ni janga la kitaifa…..Wanawake wenye figa nene za afya sio kupitiliza; pamoja na kudhihakiwa na unene wetu mradi tuna afya njema TUMEJIKUBALI!!

2. Wewe mwanamke unayejithamini! Hii iende kwa wanawake wote waliokataa  unyanyasaji wa aina yoyote toka popote kwasababu zozote!... Mwanaume ni kiumbe kama wewe, anazaliwa na kufa kama wewe, anapenda na kuchoka kama wewe. Ukipendwa pendeka ukichokwa nyanyuka tokaaa!! huko ndiko KUJITHAMINI!! Kung’ang’ania mtu it is so 90’s women! learn to move on shaaa! Uvumilivu wa manyanyaso hauna tuzo dada si peponi si motoni!!

3. Wewe mwanamke unayejituma kutafuta kipato chako!... Hii iende kwa wanawake wote ambao hawamuabudu mwanaume kwa shilingi yake! Hawadhalilishi utu wao kwa pesa! Wanapigana hata kwa kuuza maji ya viroba ili kujisitiri! ….kuhudumiwa ni haki yako….narudia ni haki yako mwaya kama uhudumiwi weka viulizo, mkato, alama ya kushangaa na mwisho fanya magazijuto hicho ni kimeo kubali kataa!!.... ila isikufanye ubweteke kukinga mkono kila siku, kila saa, kila wiki…wanaume wenyewe hawa wa siku hizi hawatabiriki awe mume wa ndoa au mpenzi wanafanana kama ugali wa jana tofauti yao majina! JITUME!!

4. Wewe mwanamke unayejitambua!... matusi si lugha yako, chuki za chini chini si sifa yako, wivu wa kijinga si hulka yako na unyonge si silika yako. Chukua dole gumba! Ama sivyo unahitaji mabadiliko haraka sana. Mwanamke anayejitambua hatukani anatoa facts, hachukii anakupa za uso, ana wivu wa maendeleo sio kwa kuumiza roho  na si mnyonge abadani!!

5. Mwisho kwa Wanawake wote wanaotambua wajibu wao….Mbele za Mungu, kwa waume, kwa wapenzi, kwa mchumba, kwa mchepuko (kwani uongo?) kwa watoto, kwa majirani na kwa  jamii na jamii yenyewe hususani kupendana, kuinuana na kuheshimiana na wanawake wenzao!!...ukiona mwanamke anachekelea madhila ya mwanamke mwenzake ujue HAJITAMBUI na HATAMBUI WAJIBU WAKE!!... kama una wifi humpendi, sijui ma mkwe  sijui nani huwapendi ndugu hii inakuhusu pia!

HAPPY WOMEN’S DAY WANAWAKE WENZANGU!!

BILA SISI DUNIA INGEBOA KUSEMA UKWELI…

No comments:

Post a Comment



Snowfall Widget for Blogger


Snowfall Widget for Blogger