Saturday, January 5, 2013

MAMBO 10 NINAYOKUOMBA UJARIBU 2013!!!


Habari zenu wadau....

Mwaka ndio umeanza hivi, wiki ya kwanza kwanza, kama hujatoa sadaka ya shukrani nenda ndugu yangu upendeleo aliokupa Mungu kuuona mwaka mwingine si mdogo. Ni zaidi ya mibaraka elfu moja. Uhai kitu kingine jamani.

Sasa  mdau hebu ngoja tuzungumze kitu.... katika maisha nimegundua kuna vitu huwa tunajiwekea mipaka wenyewe pasipo kushurutishwa wala kutishwa. Tunajinyanyapaa, tunajitenga tunajohofisha, tunajishusha mno kabla ya kutendewa haya yote na mtu yoyote na mwisho wa siku tunawalaumu wengine kwa mambo tuliyoyajenga wenyewe.....

Umenielewa?....bado?...hebu rudia tena kusoma hapo juu basi....tulioelewana twende kazi....
Umewahi kujiuliza kwanini unaweza kukwepa kuingia mahali kwa vile unahisi huna hadhi ya kuingia mle ndani?....hujakatazwa na mtu....wewe tu na hofu zako unajiwekea mipaka...
'aah pale kuna wenyewe bwana' hao wenyewe na wewe mna tofauti gani?....kuna mwenye mkataba na Mungu? au kuna mwenye kufa na kufufuka? jibu ni hakuna wako sawa tu na wewe, ukiacha mbali kupishana kimatabaka hususani kwenye kumiliki pesa na vitu vya mpito tu!

Sasa hebu tuangalia mambo ambayo binafsi nahisi unaweza kujaribu kuyafanya na pengine yakaongeza kujiamini kwako, yakakufanya ukajifunza zaidi, ama ukajikuta ukipata njia ya kutokea kimaisha bila kutarajia.


1. JARIBU ENEO/ HUDUMA MPYA ......



.......Umekuwa ukizipita hoteli mbalimbali kwa kigezo tu kuwa huna hadhi ya kuingia pale, ama kwa kigezo tu gharama zao ni kubwa sana. Hebu weka choyo ya nafsi kando na uingie uagize japo maji tu ya 1,500 utulie na glasi yako uburudike na kuyasoma mazingira...sio kila siku kwenye vigrosari na vibanda vya chini ya mti hahahahaaaaa.....nenda sehemu mpya ujifunze hata kufungua milango ya kisasa!!....



nenda kafanye massage ya 15,000 tu uexperience the difference. nenda kaoshe miguu na kusafishwa nyayo hata mara moja kwa miezi kwa shilingi 10,000 tu ile hali ya kuhudumiwa, kurelax inaupa mwili positive energy. Acha ubahili wa mwaka mzima jamani kha!!!

......Ingia maduka ya nguo makubwa ya kisasa, fanya window shopping!!....hakuna tangazo pale kuwa ukiingia na kutoka bila kununua vitu utashtakiwa..... Itaongeza hata upeo wako kidogo kwenye masuala ya mitindo, uvaaji, bei na unaweza pata kilicho bora kwa bei unayoiweza tofauti na unavyofikiria.... osha macho, osha macho jamani.... Ingia saluni za kisasa osha hata nywele tu huku ukicheki bei na mazingira,  cheki huduma mbalimbali zinazotolewa! unaweza kushangaa ni bei unazoweza kuafford sema hofu yako tu kisa Saluni uko ghorofani kweye vioo haahahahaaaa


2. KUTANA NA MTU MPYA..... 

.......umewahi sana kutumani kukutana na mtu mwenye ujuzi fulani ambao unahisi una faida sana kwako. Weka kando hofu na jaribu kuwasiliana naye. hata usipoonana naye ama asipokujibu angalau utakuwa umepata ujasiri wa kuzungumza na yule mtu..... inaweza kuwa bahati yako na ukajikuta ukitimiza ndoto zako kwa njia hii, ukijingea kujiamini zaidi... it is funny!! jaribu leo ukiamini yule ni binadamu tu kama wewe.....JARIBU USHINDWE! usikubali mtu akukatishe tamaa kirahisi


3. JARIBU CHAKULA KIPYA.....

......unasikia tu kuna hiki na kile sea cliff, samaki samaki, Serena sijui wapi uko....hebu jitutumue siku moja moja nawe upate kitu kipya. Ujaribu ladha mpya! chakula hakimbagui mlaji  ni wewe mlaji ndio hujipi nafasi ya kukijaribu....hii pia apply hata nyumbani kwako.

Usikariri chai mkate asubuhi mwaka mzima....chai vitumbua wiki nzima.....wali wa mafuta na chumvi kila siku khe! tia karoti, soma vitabu vya mapishi.... nenda sokoni au supermarket nunua viungo mbalimbali na ujue matumizi yake.....sio uwapishe hizo sehemu wazungu tu na akina mama lishe kila siku!!


4. JARIBU UTALII WA NDANI.....

..... hata kwa mwaka mara moja au mbili. tembeleo vivutio vya utalii, nenda makumbusho ya Taifa, nenda mikumi, nenda zanzibar, nenda bagamoyo na kadhalika! iwe peke yako au na wenzako. Itakupa maarifa mapya, itakupa nafasi ya kupumzisha akili, itakupa nafasi ya kujisikia furaha kwa kujaribu kitu kipya

.....Usisingizie gharama, dunduliza! tunza tunza! haba na haba hujaza kibaba! Starehe si kila siku kukutana na marafiki kwenye vigrosari na kutandika maji....




5. JISOMEE....

.......Nikianza na biblia na Quraan. kimojawapo kulingana na imani yako lazima uwe nacho na ujue kiko wapi na kila siku hata usipokisoma ukione na kukigusa. Imani tu kuwa kwa kukigusa umejisogeza karibu na Mungu na sia ajabu ukajikuta ukisema naye kimya kimya....kisha jijengee tabia ya kujisomea vitabu vya hadithi ana maarifa mengine.

....All in all unahitaji kujisomea hii njia moja wapo ya kupunguza stress za maisha! kupata muda binafsi wa kukaa kimya na kuishughulisha akili yako katika utulivu.... Acha kuwa nyuma nyuma kama koti......kuongeze hii point hebu miliki diary...ama daftari tu ujue kwa siku unafanya nini?



6. UKIMBIZE WAKATI..... 

.......Sizungumzii ukimbizane nao kwa njia ya fashion na kadhalika japo pia si vibaya. nazungumzia kuiweka akili yako katika mtindo wa kujua ni nini kinaendelea nchini mwako, kitaifa na kimataifa. Soma magazeti, pitia mitandao ya kijamii upate habari mbalimbali kabla ya kuzama katika udaku wa hapa na pale. unahitaji kuwa na listi ya magazeti hata kama ni moja, kuna mitandao unayotembelea kwa ajili ya kupata habari na mingine ya kupata maarifa.

mf. binafsi nina access ya kupata magazeti kama si yote basi la Nipashe au mwananchi lazima lipite mikononi.....ninapitia mitandao ya kijamii kama michuzi, jamii forums, yahoo, BBC nk kupata mwanga wa masuala ya kijamii, kitaifa na kimataifa...kisha nina blog za burudani sasa ambazo hunipa taarifa za udaku, fashion, mapishi na mahusiano hapa na pale....kwa njia hii akili hushughulishwa katika kila nyanja.....hata wewe unaweza! sio ukiulizwa kitu kuhusiana na siasa huelewi chochote!.....

 ZAIDI YA YOTE KUWA MTU WA KUJALI MUDA!!!!! NARUDIA WA KUJALIA MUDA...wabongo tunajijua kituc ha saa nne kinaanza saa sita.....usiukubali ujinga huu mwaka huu....



7.  MABADILIKO - MAKAZI.....

......Badili mpangilio wa fenicha, badili aina ya mapazia, badili doormat, panda maua, weka sehemu katika usafi wa hali ya juu...badili uelekea wa kabati au kitanda. weka extra things bafuni kama freshner, soap dish za kisasa, sabuni za kuogoa za maji, dettol nk. weka kapeti jipya au taa mpya za kisasa. Just fanya mabadiliko hata kidogo tu. kisaikolojia hukupa motisha mpya, hukufanya ujisikie mpya.

Mf. hukuwa na mazoea na kuweka picha za ukutani, hebu tafuta picha nzuri iwe yako, mtoto wako, picha za maua au za kidini. iweke kwenye fremu nzuri na uitundike mahali ambapo utaiona kila siku, jaribu kuweka vitu katika mpangilio mzuri wa kuvutia, si vibaya ukiingia mtandaoni na kutafuta namna ya upambaji chumba kidogo. wengine wanaweza wewe unashindwa nini?.....na mapambo ya kichina yaliyojaa mitaani. hebu make changes!!



8. MABADILIKO - NAFSI/ MUONEKANO BINAFSI...... 

.......wewe na maweaving, wewe na mawigi wewe na kipara, wewe na kipilipili, wewe na yeboyebo, bora hata wanaume hawana choices nyingi, wanawake mpaka mtu anajua akifumua hizi atasuka hizi.....eeeeh jamani jifanyie hata mabadiliko kidogo....ujisikie mpya kuanzia nje! badili mswaki hahahhaaa.....kama ulizoea sendozi sana hebu jaribu na kiatu cha kufunika, kama ulizoea mapochi makubwa hebu tafuta saizi ya kati....badili wallet.....jifunze kuvaa saa ya mkononi..... acha kutafuna kucha....just try something new!!!

Kuhusu nafsi, ahapo ni wewe na habits zako. unazijua habits zinazokuhinder usifikie malengo, hebu taratibu ziohorodheshe ba uzifanyie kazi. kama ni matumizi mabaya ya pesa hebu nunua kibubu uwe unatumbukiza noti ya pesa kila siku, kama ni vimada na vidumu hebu viweke kando kwanza kwa miezi uone kama hutaishi.....kama ni mahusiano yasiyoeleweka hebu yatafutie ufumbuzi na ikishidikana yaweke kando mapemaaaa

.....Furaha na amani ya nafsi ni kitu cha maana sana japo wengi tunakipuuzia na kuviuza hivi vitu kwa wengine kwa kisingizo cha kupenda!!....wakifa tunazikwa nao??....tunalia na tunasahau.....nawe sasa lia usahau...life goes on! fanya yale yanayokupa faida, yanayoupa moyo wako furaha na zaidi ayankufanya ujisikie kubarikiwa na Mungu na sio ayanayokufanya umlilie Mungu kana kwamba amekulaani.


9. MKARIBIE MUNGU KWA SALA NA SADAKA.....

......hili suala watu huwa tunalichukulia kimzaha sana....Mungu anakumbukwa wakati mambo yanapoenda mrama....kuna watu katika maongezi yao ya kinafsi mpaka ya watu wengine neno Mungu ni taboo. kuna watu kusali ni adhabu kubwa sana, kuna watu hata kama wako wenyewe kumkaribia Mungu ni mpaka akumbane kitu ambacho kitamkumbusha Mungu yupo....kwanini??

Jipe hofu ya Mungu kidogo, itakuepusha na mabalaa ya ajabu ajabu, aitakufanya robo tatu ya maisha yako uwe na amani kidogo. si kwamba unapaswa kuishi kama mlokole....la hasha....ila ukiwa kama binadamu mwenye imani kwa Mungu kuwa yupo na ndiye aliyekuumba na ndiye mwenye mamlaka ya kukuchukua kwa wakatia anaotaka.....unapaswa kukumbuka kumshukuru, kuzungumza naye nyakati mbalimbali hata mara tatu kwa siku.....

Naamini si lazima usali mpaka usikike mtaa wa saba....jamani hata kazini ukiwa na shughuli zako....bado unaweza kutulia tu ukazungumza na Mungu kimya kimya....

Sadaka yako iwe kanisani ama msikitini, ama iwe msaada kwa wahitaji ifanye iwe siri yako mwenyewe, ifanye iwe sadaka ya kweli isiyo na nia ya kuuonyesha ulimwengu kuwa umemsaidia nani na nini. Na endapo ni mkusanyiko wa msaada wenye kuhitaji kumbukumbu kama picha, epusha majivuno na majigambo...

maana kuna watu akitoka kituo cha yatima utasikia tumeulisha umati, wamekunywa na kusaza....eeeh ndugu yangu Mungu akianika anayokusaidia wewe utapita mtaani gani kwa amani.... sikio na asikie!



10. JENGA MAHUSIANO MEMA..... 

Samehe kabisa, na sahau....kuna watu ukitibuana nao aisee...ni mwaka hata mwaka mpaka ajirudi akusamehe! maisha mafupi haya manuno nuno ya nini?....ukimsamehe mwenzio haraka tu kuna tatizo gani, hata kama hutakuwa na ukaribu naye lakini moyo wako ubaki safi juu yake na salamu za hapa na pale mnapokutana zitoke. fanya yako na mie nifanye yangu....mambo ya kuchunguza wenzio, ukiwaombea mabaya, ukiwafanyia majungu hayajengi ndugu yangu....Duniani tunapita tu.....

......akibarikiwa yako yakakudodea huna haja ya kumchukia ndio kwanza unajirudisha nyuma kwenye foeni ya mibaraka.....chuki hazijengi tafuta kuwa na amani na watu wote......wapo vichanchuda vyenye kukutafuta vita....lakini jua kuvikwepa na kuiingia vitani hakikisha umesambaratisha kisha ondoka kwa amani yako..... mpende adui yako!! awe ndugu yako, jirani ama mpita njia!

katika mahusiano ya kimapenzi...hii mada nyingine ila kikubwa....uvumilivu cuhukue nafsi ila tu kuwe na kikomo si uvumilie gunia la misumari huku una kipara....tutakuzika kabla ya siku zako.....asotaka kupendwa mwache aende zake.... Asojua kupendwa mvue pendo atambae zake.....asojua tahamani yako, geuka piga kwata za hatua ndefundefu.....utampata wa kukupigia saluti mbele ya safari.....usiishi kwa uchungu, ukivumilia yasovumilika, uslie kila siku hayo machozi mpelekee Mungu akuzidishie uhai na mibaraka badala ya kulilia jitu lisilojua tahamni yako....poooh! huu sio mwka awa kulia lia....MOVE ON jamani khe!!!!


Imendaliwa na Laura Pettie.
........NI HAYO TU KATIKA KUUANZA MWAKA...SINA LA ZIADA......










1 comment:

  1. Asante dada yaani umenigusa sana. u mwandishi mzuri kwa kweli. nimeipenda hii

    ReplyDelete



Snowfall Widget for Blogger


Snowfall Widget for Blogger