Saturday, January 5, 2013

PERUZI YA ENZI....SOLEMBA BY JUWATA JAZZ BAND




Naupenda huu wimbo sana.... sauti ya mwanamuziki mwenye ulemavu wa macho  Zengakala ni burudani ya aina yake. kuna stori nyingi kuhusu huyu jamaa....ila tisa kumi Mungu alimjaaliwa kipaji cha aina yake.

hapa chini mashairi ya huu wimbo...kama kuna vijimakosa mtaniwia radhi wadau

Ulinipa ahadi tukutane kwenu.........Nikitumaini nimewahi
Nilichopata kwako ni matusi oo, oo na dharau tele
Ungenieleza ukweli solemba......Kuliko kunidanganya oo
Najuta kuitimiza ahadi oo ambayo si ya kweli.

 KORASI SASA....
Nilikupenda kimapenzi Solemba ee...... ila dharau uliweka mbele solemba.

ZENGAKALA SASA.....
Nilichomwa na jua toka asubuhi....... mpaka saa nane Solemba sababu ya kukungoja wewe
Kumbe ulikua ndani ukichungulia dirishani
Nimeshituka Solemba , Nimeshituka Solemba

 KORASI....

ZENGAKALA ANARUDI.....
Sikutaki tenaaa...... sina haja nawe......nimeshapata mwingine atakaye nipenda kwa roho moja, Tafuta bwana mwingine utakae mbabaisha kama mimi Huna huruma Solemba.......Aloi I love you baby

KORASI INARUDIWA HAPA



ENJOY!!



No comments:

Post a Comment



Snowfall Widget for Blogger


Snowfall Widget for Blogger