Thursday, January 10, 2013

KOREAN DRAMA..... SONG II GOOK a.k.a JUMONG!!


Nazipenda sana tamthiliya za kikorea ambazo nyingi zimeonyeshwa na kituo cha ITV....enzi za Anologia.... nimeshaziona nyingi sana na nimejikuta niwa na my favorite Korean drama hadi favorite korean actors na kwa leo nimzungumdie kwa ufupi tu huyu jamaa wenyewe tunamuita jumong....ila kwao uko wanamtambua kama  SONG II GOOK
Song II Gook .......a.k.a Jumong
Aaaww he is Damn haaawt!

Ni muigizaji mashuhuri toka korea ya kusini. Akiwa ameigiza tamthilia kadhaa za kihistoria kama Jumong ambayo imempatia umaarufu mkubwa nchini, Emperor of the Sea na nyingine nyingi. 



Song II Gook na mkewe Jung Seung Yeon
Lucky woman...... ukitaka kuomba talaka niambie nikurithi hahahahaaaa *wink*

Song II Gook ana umri wa miaka 41, na alizaliwa Oktoba 1, 1971 nchini korea ya kusini. Mnamo tarehe 15 machi,  2008, Song II Gook alifunga ndoa ya siri na Jung Seung Yeon ambaye kitaaluma ni judge. Wawili hawa wamejaaliwa kupata watoto mapacha watatu wa kiume mwaka jana machi 16. kinachofurahisha ni majina waliyopewa watoto hao wa kiume wa kwanza ni Dae Han (ikimaanisha Korea) , 
Min Kook (ikimaanisha republic) and Man Se (ikimaanisha Viva) hivyo muunganiko wa majina yao huleta neno Hurrah Korea!. hahahahaaa kuna watu wazalendo usipime!! waaaapi Hurray Tanzania jamani!




Kijana kazini sasa......sura hii ikiachia mshale kama 'hukufaring' basi lazima 'uzimiering'
napenda userious wake katika kazi yaani unashindwa kutofautisha na kitu halisi
sio movie zetu hizi mtu ngumi tu anatafuta pa kudondokea asijekuvunja stuli ya watu... watu wanaparazana parazana eti ngumi/......ingeni kazini kikwelikweli mnachapana mpaka mtazamaji anatamani kuamulia....




Song II Gook ni mhitimu wa vyuo vikuu Cheongju University na Chung-Ang University akiwa na shahada inayohusiana na masuala ya sanaa ambayo aliianza rasmi mwkaa 1988 mpaka sasa. Sanaa mbayo imempatia umaarufu ulimwenguni na kumtunuku tuzo kadhaa kwa kazi zake zenye ubora wa hali ya juu. We kumbukia tu kazi ya Jumong!!.....uwiiii i didnt know Korean guys are so hawwwwt till i sawSong II Gook.. halafu kuna mwingine alicheza kitu Winter sonata.....pale mimi baaaasi!!


Hawa ndio watoto wake....Mapacha watatu!!
Katika interview moja alidai ilifika kipindi walitamani kumtoa mmoja maana mimba ilikuwa na kilo 6!!.... ilibidi avumilie sana kero za ujauzito huku mkewe akikubali yote mpaka dakika ya mwisho.


Kuna wakati pia ilivuma kuwa jamaa alimuona huyu judge ambaye ni binti wa kibopa uko Korea kuwa alimuoa kwa sababu ya pesa, wengine sababu ya umri tu kwa vile mahusiano yao hayakuwahi kuanikwa kwenye vyombo vya habari

Jumong akakanusha kabisaaa....akasema alidate jamani heheheeee sio kila kitu mjue .... kumbe ya sirini matamu ukiyaficha watu wanazusha yao sasa....oooh watanzania wana MAJUNGU mmeona MASUFURIA ya wakorea??

Muwe na jioni njema wadau!!






1 comment:



Snowfall Widget for Blogger


Snowfall Widget for Blogger