Thursday, January 15, 2015

UREMBO NA LAURA....USAFI WA MWILI WA MWANAMKE....




Kama ilivyokuwa mwaka jana kila alhamisi tuna makala ya urembo hapa… na kabla ya yote hebu tumshukuru Mungu kwa wema wake kwanza kwa kutuumba wanawake na kisha akatuweka hai mpaka sasa halafu akatupa nafasi ya kusoma hata hii makala unayoisoma.

Nakuita mwanamke!...nakuita binti…nakuita hapa tuelezane machache kuhusu usafi wetu kwa ujumla. Wanasema usafi ni hulka ya mtu ni kweli lakini ukiamua kuwa msafi hushindwi…na kwanini ushindwe! Nitagusia mambo 15 ambayo kuhusu usafi wa miili yetu maana urembo na usafi ni kama kobe na jumba lake haviachani!

Hebu tuanze…

1. USAFI WA NYWELE

Utatia aibu kama utasukia weaving lako wiki mbili hadi nne na usiwe umepitisha maji kichwani… haijalishi uko wapi ila kukaa na nywele wiki nne pasi kuosha ni UCHAFU bibi!!... toa nywele bandia hizo…au fumua mzigo wa yebo yebo huo uoshe kichwa kama huwezi kuosha zikiwa kichwani…watu wanaweza wasikwambie ukweli ila pembeni ukapewa cheo cha yule dada mchafu maana huwa zinanuuuuka acha!!



2. USAFI WA KUCHA

Hii trend ya watu kufuga kucha pasipo kujua namna ya kuzitunza ni shida tupu. Kama unajijua huwezi kutunza kucha zako usifuge kufuata mkumbo. kucha zinahitaji usafi jamani… halafu unakuta mtu kafuga kucha ndeeefu halafu mbayaaa…hivi uone au ndio makusudi tu!...

mmmh mmmh fuga fupi basi kidogo kama huwezi kutunza…. Au katilia mbali zote tujue moja…. Kumbuka mikono inashika vingi, inagusa sehemu zetu zile, mikono inaingia jikoni, mikono inasalimia watu!!...zisafishe, zing’arishe kwa rangi mpaka mtu anasikia raha kukusalimia!...na za miguuni usisahau maana uko ndiko majanga matupu…ukucha haufai kuvalia sendozi wala ndala…why?

3. USAFI WA MAKWAPA

Umevaa nguo ya kukata mikono…kwapa lina nywele… hapo maksi zinapungua…. Za nini mwali?... unataka kuweka relaxer au kusukia weaving?... vinyweleo kwapani huchangia kuleta kikwapa na zaidi hulowesha hata nguo uliyovaa... Nasty!… achilia mbali kukupunguzia sifa ya usafi…nyoa kwapa lako bwana we!... lisugue na baking soda au limao ling’ae…  huwezi jua ukute usafi wa kwapa lako ndio uliomvutia mtu wako au utamvutia mtu wako…kalaghabao!

4. USAFI WA KINYWA

Hapa kuna kutokujua namna ya kuswaki vizuri au ugonjwa… hebu kunja mkono kama unataka kufumba mdomo kisha achia pumzi ya mdomo hapo mkononi…unasikia harufu gani?.... au jilambe kidogo nyuma ya kiganja kisha sekunde tano nusa ulipojilamba…unasikia  harufu gani?.... hiyo ndio harufu wanayoisikia watu kinywani mwako….  

Swaki ulimi vizuri, kunywa maji mengi kinywa kisikauke, tafuta zile chew gum flani za kurefresh kinywa…it is a must have kwenye pochi yako …. Unajua tena! Sasa unakosaje kitu kama hicho kwenye pochi . mwisho kabisa angalau jitahidi kuswaki kabla ya kulala…swaki tu halafu asubuhi utagundua tofauti ya ukilala bila kuswaki na ukiswaki  kabla ya kulala!

5. USAFI WA MATAKO

Ona ulivyoguna!.... hapa akitokea mtu akasema kila mtu atembee matako wazi tutaona mambo makuu hahahahaaaa…tako lina vipele utasema umevaa ganda la fenesi nyuma…why?.... hebu chukua  mafuta ya nazi upake hapo nyuma kila usiku kila asubuhi anhaaaa!.... sio bebi anapeleka mkono nyuma anashtuka na kuuliza umevaa nini? Kumbe ndio ngozi imeharibika!.... ukiona si muhimu sawaaa!

6. USAFI WA USO

Kama ni product za bei cheee nimeshakuwekea humu rudi post za nyuma… kama ni njia za kusafisha uso nimekuwekea…. Sasa unaanzaje kuwa na uso mchafu mchafu mpenzi?.... wewe ni mwanamke bwana!...kupendezesha uso ndio jadi yako…. Wala huitaji kupendeza sababu ya mtu…. Pendeza tu uongeze kujiamini…. Uso msafi ukiongezea na vipodozi…hivi hutojisikia raha hata kusimama mbele za watu!

7. USAFI WA MASIKIO

Huwa namtoa maksi kabisaa mdada ambaye ukikaa naye karibu unakuta sikio lina nta hilo balaa…yuuuck!...au nyuma ya sikio na kwenye kona kona za sikio kuna weusi flani hivi unaoonyesha sikio halisafishwi na hapo ukute ana mkoba wa elfu 70… nguo ya laki!...na usafi mdogo wa sikio umemshinda!...mwaka huu usiwe wewe mwenye sifa hizi…safisha sikio lako hata mara moja kwa wiki…na safisha sikio lako kila ukioga khaaa!

8. USAFI WA KITOVU!

Heheheheee hapa naweza kukamata wengi…. Ukute kitovu kina magamba hicho!.... wanasema ni sehemu sensitive sana kuchokonolewa chokonolewa sijui  ni kweli au myth tu …lakini ndio hata mara moja kwa mwezi chukua kitambaa chovya kwenye maji ya uvugu uvugu safisha kitovu chako taratiiiiiiibu!

9. USAFI WA MIGUU

Unamkuta mdada ana dhahabu mbili tatu hapa na pale… kajisugua mwili katakata…. Ila mguu ana zagamba!... ana gaga hilo limemganda!... ana sugu za vidole balaaa....mmh mmh huu ni uchafu  na uzembe bwana!.... unaanzaje kupata mazagamba mjini hapa kama si uvivu wa kusafisha miguu…. 

Sio lazima ukaanike miguu uoshwe na watu saluni….hata kwako unasafisha miguu yako na inang’aa tu…unahitaji beseni, maji ya uvuguvugu… shower gel… brashi na ubao wa kusugulia gaga unaopatikana maduka ya urembo wa elfu moja mia tano tu! Namna ya kusafisha nitakuletea juma lijalo

10. USAFI WA UKE

Basi kipengele hiki ndio watu huzodoana mpaka basi….unasikia usitie vidole ukiswafi…wengine tia vidole bwana mbona mama zetu sijui bibi zetu walitia vidole…. Vyovyote unavyoamini sawaaa!
Hapa ni kwa mtazamamo wangu na maoni yangu mimi binafsi…

Kuosha uke wala sio kazi kubwa sana…. ni vile uupende tu uke wako na usiuone kero…. Ondoa nywele zile kule chini… ziondoe mara kwa mara ndugu yangu usingoje ziwe msitu huooo unasubiri kuufanyia kwa mfano hata ukae na limsitu!!....mechi ya ghafla pyaaa mtu anakukuta na forest lako kama mchoma mkaa hahahahahaaaaaaa hebu mie!

Ushaweka uwanja msafiiii… na njia nzuri ya kunyoa ili usitoke vipele…ni nyoa kufuata nywele zako zinavyoota… shaver yako ielekee kule ninakolalia mpaka uwanja uwe msafiii kisha weka sabuni au shaver gel nyoa against sasa pole pole juu juu bila kugandamiza shaver  utabaki softiiiii

Au…tumia veet! Ni nzuri mnoooo na hukuacha msafiii
Au…nenda kafanye wax saluni…kuna saluni maeneo ya kijitonyama…nasikia ni kama elfu 20 na kitu hv… ukiwax unakaa muda mrefu kidogo kabla hazijaota… fanya hivyo kama huna aibu mwenzangu... na wax huwa inauma kidogo…usijaribu kuwax home kama huna utaalamu utaunguza ikulu hahahahaaa

Na unaposhave shave mpaka nyuma huku kwenye mstari wa ikweta…shave tu ubakia msafi sehemu yote!...kumbuka kupaka mafuta ya nazi au mchaichai ukishashave...hupati vipele... ama tumia maji ya liwa...chovya pamba pitisha pitisha maeneo uliyonyoa...ukitoka vipele labda ulitumia wembe butu au used heheheheee

Sasa ushanyoa…tutumbukize vidole au lah!.... binafsi NO VIDOLE kila mara!... this is my rule!...kwanini?... kwasababu sihitaji kuusafisha uke kwa kutumbikiza vidole ambavyo sijui ni visafi kiasi gani… uke hujisafisha wenyewe after all …. Hivyo mara nyingi unaihitaji kuosha mashavu ya uke kwa maji mengi na sabuni basi. 

Sasa inakuja situation unahitaji kutumbukiza kidole ili ujihisi umetakata….  Hapa sasa unaosha mkono wako vizuri kabisaaa…. Ndio unatumbukiza kidole chako na hakikisha huna kucha ndefu aisee… kama hutumbukizi kidole na unanuka my dear wewe mgonjwa!! Nenda hospitali!

Mwanamke ukivua nguo ya ndani na ukasikia harufu flani isiyo ya kawaida, au harufu kali ni kwamba wewe una matatizo unahitaji tiba…ute unaotoka huku chini huwa hauna harufu mbaya au harufu kali…huwa una harufu ya kawaida ya uke…harufu nyingine yoyote inakupa taarifa kuwa uke wako hauko sawa mwenzangu…. Usisingizie ni kwa vile huweki vidole!!...No! kuna watu hatuweki vidole ovyo na wala hatuna harufu!...wahi hospitali ukapate tiba!

… kingine jifunze kujiosha kwa maji baada ya kutumia tishu kufuta uchafu… kisha tumia tishu kukausha maji maji… usitumie tishu tu halafu basi labda mazingira yakubane sana kama vile maji yaliyopo yana viluilui… au hakuna maji kabisa…vinginevyo jioshe kwa maji my dear utakate ukaushe!

Vaa chupi za cotton hasa kipindi hiki cha joto…. Tafuta siku uziloweke na uzifue na kuandika sehemu yenye jua… wapo wanaopiga pasi pia…ni wewe tu!

Pads zibadilishwe kila inapojaa, sio pad moja siku nzima na limejaa tota tota...unapishana na mtu anakugezia singo nyuma kujiuliza umebeba nini chenye harufu... usilazimishe paketi moja ya pad itoshee siku zako...hebu jijali bwana!

Kuna mengi ila ngoja niishie hapa!!

NIKUTAKIE SIKU NJEMA RAFIKI….

Kama una la kuongeza karibu utupe maoni yako!! kama lipo lolote umejifunza karibu tena

ALHAMIS NJEMA!


2 comments:

  1. Kama kuna jambo ungependa tuliongelee kwenye kipengele hiki basi jisikie huru kuwasilina nasi

    LAURA

    ReplyDelete
  2. Safi Dada. Nimepata neno walao na mimi nikarihubiri kwa mataifa yote! Shukran.

    ReplyDelete



Snowfall Widget for Blogger


Snowfall Widget for Blogger