33
mke wa Mzee Okello, mama wa Pamella alikata simu na
kusimama akiwa kama mtu aliyetaka kupayuka kitu kwa sauti ya juu na asiweze.
Mdomo ulikuwa aukiwayawaya huku macho yakipepesuka na kutembea huku na kule.
Mchecheto!
Akalazimika kujiweka sawa pamoja na mchecheto ule ili binti
yake aliyekuwa anaingia pale dukani asigundue hali aliyokuwa nayo.
‘Vipi?’ akamuuliza Pamella aliyefikia kuketi kwenye kiti
kilichokuwa karibu na pale alipokuwa amesimama mama yake.
‘Ni kama naota..’ Pamella akajibu akishusha pumzi ndefu kiasi
‘Kwanini?’ mama yake akamsogelea zaidi na Pamella akatikisa
kichwa kulia na kushoto kuashiria kutojielewa yeye mwenyewe sembuse kumweleza
mtu mwingine na akaelewa.
Mama akakunja sura kidogo na kumkazia macho binti yake,
akiyaweka yak wake kando na kuyabeba ya mwanawe.
‘Pam!...what’s wrong?’
akamsogelea zaidi na kutaka kujua lakini Pamella akainua mikono juu kama
mateka na kufumba macho kwa sekunde kadhaa, alipoyafumbua akahitimisha!
‘Tuachane na haya mama… twende tukajaribu hizo nguo’
akanyanyuka na kuanza kukifuata chumba cha kujaribishia nguo, akimuacha mama
yake amesimama pale pale akimtazama binti yake kwa namna ya kutom muelewa.
8888888888888888888
Jerry Agapela alikuwa yu kitandani akisoma gazeti alilomtuma
Sindi akanunue asubuhi hiyo. Lile gazeti lilikuwa mkononi kama ushahidi tu kila
mara alimtazama Sindi aliyekuwa anaandaa meza kwa ajili ya kustaftahi muda huo
wa saa tano.
Alimtazama kwa sekunde chache kisha akarudisha akili yake
gazetini. Akafunua ukurasa mmoja baada ya mwingine, hakuelewa lolote sembuse
kulisoma tu. Akaliweka pembeni na kuteremsha miguu chini akiitazmaa meza ndogo
iliyokuwa na chakula mbele yake.
Sindi akangia na beseni dogo lililokuwa na jagi ndani yake.
Akaja nalo mpaka pembeni ya Jerry na kummiminia maji wakati akinawa. Jerry alinawa
akimtazama Sindi usoni na kutaka kutaka kutabasamu, lakini alishindwa.
‘Niko kwa Jamila hapo’ Sindi akamsemesha wakati akigeuka na
lile beseni akijiandaa kuufuata mlango
‘Kha! kwa hiyo chai nakunywa mwenyewe?’ Jerry akauliza kwa
mshangao
‘Ukinywa mwenyewe hushibi?’ Sindi naye akamuuliza
‘yaani uandae chai mke wangu kisha unisusie hapa niinywe
mwenyewe…umeiweka limbwata?’ Jerry akatania akivuta kikombe. alitania tu,
alifanya masikhara na asijue utani wake ulingeleta balaa gani.
Sindi akafinya uso na kumtazama Jerry kwa jicho kali sana la
pembeni.
‘umesemaje?’ akamuuliza kwa shari sasa na Jerry akainua uso
na kushangaa ile shari ilikotokea
‘Sindi!’ Jerry akamshangaa, hakuona mantiki ya ile shari
‘Nakuuliza umesemaje?’ Sindi akageuka sasa na kumtazama Jerry
moja kwa moja, akimung’unya mikono yake. Kitumbua kilichokuwa mkononi mwa Jerry
kikashindwa kusogea mdomoni wala kurudi kwenye sahani. Jerry akatikisa kichwa asimuelewe mwenzake
aliyepaza sauti kuuliza kana kwamba alikuwa akigombana na mtu aliye upande wa
pili wa barabara.
Sindi akainama, akakichukua kile kikombe cha chain a
kuimimina chao kwenye lile beseni la kunawia ambalo bado lilikuwa mikononi
mwake. Akainyanyua sahani ya vutumbua na kuvimimina kwenye lile beseni la
kunawia llilokuwa na maji machafu pia. Akainuka na kumtazama Jerry.
‘Nenda kanywe chai uko usikokuwa na wasiwasi wa kuwekewa
limbwata’ Akageuka na kuanza kuuelekea mlango. Jerry bado alikuwa haamini kama
lile tukio lilikuwa limetokea mbele yake. Hata kile kitumbua kilichokuwa
mkononi mwake alikiona kama kipande cha jiwe. Akakiweka juu ya meza na kumkazia
macho Sindi. Naye Jazba zikionekana kumvaa!
‘We’ Sindi..’ akamuita kwa sauti yenye hasira ndani yake.
Sindi hakugeuka aliufungua mlango na kutoka nje. Akaubamiza kwa nguvu na
kumfanya Jerry afinye macho na kukaribia kuaziba masikio yake. Kama mazaha tu
chai ndio ilishapotea mbele yake na vitumbua alivyokuwa anavingijea ndio
vilishayeyuka.
Alijiinamia na kukuna kichwa, hakumuelewa na ile dhana kwamba
huyu mwanamke alikuwa na mimba inayompelekesha ilimrudia tena kwa kasi
akiunganisha na tukio la kukuta kile kifaa cha kupimia mimba. Akanyanyuka na
kuufuata mlango, akatoka kwenye kordo na kukuta akina mama kadhaa wakiwa na
majiko yao wakijishughulisha na mapishi ya hiki na kile.
Hakusemezana na mtu akapiga hatua mbili tu na kuufikia mlango
wa Jamilla. Akagonga mara mbili na mlango ukafunguliwa na Jamilla ambaye
hakupata hata nafasi ya kuuliza kulikoni. Alishtukia tu mlango alioushikilia
ukitanuliwa kwa nguvu na Jerry akaingia mle ndani mwake na kumkuta Sindi
ameketi kitandani.
Hakusemeshana naye zaidi ya kumvaa na kumshika mkono akimvuta
kumuondoa mule chumbani. Sindi akagoma akifoka na kumshambulia Jerry amuachie.
Jamilla akataka kuingilia kati kumnusuru shoga yake lakini Jerry akamuwahi.
‘….Hayakuhusu’ Jibu fupi tu lilimtosha kumfanya Jamilla
akasimame kando akiwashangaa. Yale makelele yalifanya wanawake waliokuwa
kordoni nao wasogee eneo la tukio.
‘Jamani amefanya nini unamvuta hivyo….we Jerry hebu muachie
kwanza…. hebu muachie basi khaaa!’ Kila mtu alisema lake lakini Jerry hakujibu
kitu alikazana kumuondoa Sindi mule kwa Jamilla na akaweza. alipomuingiza Sindi
chumbani kwake akafunga mlango kwa ufunguo na kuuchomoa. Majirani wakanasa
mlangoni!
Sindi alikuwa na anahema na hasira alizokuwa nazo
zilimuongezea machozi usoni. wote wawili walikuwa na jazba kubwa sana.
‘Nirudishe kwetu…siwezi maisha haya’ Sindi alisema kwa jazba
na Jerry akacheka kwa dharau
‘Kwenu?...wapi?’ akamuuliza Sindi kwa hasira akimkaribia na
Sindi akairudi nyuma
‘kwani tulipokuokota tulikuokota wapi?’ Sindi naye
akapandisha
‘Sindi nitakuumiza…nitakuumiza unajua…’ Jerry sasa alitamba
akiume akimtanulia Sindi kifua na Sindi akaona hali inazidi kuchafuka. Kule
mlangoni sauti mchanganyiko zilisikika zikimtaka Jerry afungue mlango la sivyo
wangeubomoa.
‘Niumize….kwani umeshaniumiza mara ngapi….mara ngapi…niumize
sasa’ Sindi alijibu kwa sauti ya unyonge akilia kwa kwikwi na hapo hapo akirudi
nyuma na kuufikia ukuta. Jerry alishamkaribia naye akiwa amefura
‘mimi ni nani kwako Sindi?’ Jerry akauliza akihema
‘Sikujui’ Sindi akajibu kwa kiburi lakini sauti yake
ilikisaliti kiburi na kutoka kwa unyonge, hofu ya kupigwa ilishamvaa!
‘hunijui?...unaishije na mtu ambaye humjui…nakuuliza wewe
unaishije na mtu usiyemjua?.... ulitekwa kuletwa hapa?.....si ulikuja kwa
hiyari yako yako’ Jerry alikuwa anaongea kwa hasira kwelikweli
‘Ulinidhanganya….ungeniambia dhamira yako wazi nisingekuwa
hapa hapa mimi….Yuko wapi Nyanza aliyejidai ungemfuata yuko wa…’ Sindi
alikatisha sentensi yake na kupiga ukunga
‘Uwiii mamaaa’ Akainamisha kichwa na kukiziba kwa mikono yake
mara tu alipoona Jerry amenyanyua mkono. Mkono ule ulibaki hewani ukitetemeka
na Jerry akijaribu kuzuia jazba zake zisitende kilichotaka kutendeka.
Akaushusha mkono wake na taratibu akaketi kitandani na
kujiinamia. akihisi maumivu yaliyochanganyikana na hasira. Akainua uso na
kumtazama Sindi aliyekuwa anatetemeka na kumtazama Jerry kwa woga.
‘Sindi…’ akamuita akihemea mdomo
‘Sindi…’ akaita tena na tena na kufumba macho kama mtu anayesikilizia
maumivu ya ndani kwa ndani.
‘una mimba!’ akatamka alichotaka kutamka. Lile tamko sit u
lilimfanya Sindi aachame mdomo na kutoa macho hata kule mlangoni wale
waliobanana kusikilizia na kuwaomba wasiumizane walinyamaza ghafl na kutazamana
kama watu waliosikia tarehe zao za kufa!
‘Kasemaje?....nini?....mimba ina nini?’ wale walikosa kusikia
vema wakautoa ukimya mlangoni kule na kuulizana mradi tafrani.
Jerry alinyanyuka na kukifuata kile kifaa mlangoni. Zile
hatua za kuufuata mlango ziliwafanya wapangaji watawanyike mbali na mlango na
kusimama kusikilizia, wakingoja mlango ufunguliwe. Hola!
Akakitoa kile kifaa toka kwenye mfuko wa shati na kuja nacho
mbele ya Sindi.
‘ulinunua hiki cha kazi gani?’ Jerry akauliza akiwa
amemsogelea Sindi pua kwa mdomo. Sindi akatazama pembeni uso ukiwa chini. Jerry
akatumia mkono wake kukishika kidevu cha Sindi na kukitumia kuugeuza uso wa
sindi urejee mbele ya macho yake.
Macho yaliyometameta kwa machozi yalimtazama kwa huruma.
alikuwa binti mdogo tu, hakuwa na uzoefu wowote wa kuishi na mwanaume, ilikuwa
mimba ya kwanza, mkanganyiko wa hisia ulimpelekesha mno, pengine alifanya vitu
na asielewe kwanini alivifanya!
Jerry akamtoa Sindi pale ukutani na kumleta kitandani.
Akamketisha nay eye kuketi kando yake. Sindi alikuwa kimya, kama mtu aliyevamiwa
na hamaniko lisilo rasmi.
‘unataka kupima?’ Jerry akamuuliza kwa upendo akimsugua sugua
mgongoni na Sindi akaitikia kwa kichwa. malengelenge ya machozi yakiteremka
mashavuni mwake. Jerry akamfuta machozi na kunyanyuka.
Akapekua huku na kule na kurejea na kifaa alichodhani
kingesaidia kukamilisha kazi yao. Wakaupata mkojo na kukitumbukiza kile kifaa.
Jerry aliyekuwa nacho mkononi. alihisi kutetemeka mstari wa kwanza
ulipojichora, almanusura aangushe kile kikpo alichokuwa ameshika. Mstari wa
pili ukajichora na jibu likapatikana. Kiumbe kilishaumbwa! mchezo walioucheza
ulitoa matokeo chanya! Mioyo yao ilidunda kwa kasi walipotazamana!
Sindi alijiinamia na Jerry ndio alihisi mwili ukipigwa na
ganzi ghafla! pamoja na yote aliyoambiwa na Meddy hakuyatarajia maneno ya Meddy
yawe kweli. Kila mmoja aligeukia upande wake akiwaza lake
888888888888888888888888888
Kule kwa Agapela, Sehemu kubwa ya nje ilishafungwa maturubai
meupe machache yaliyokuwa na meza
zilizoanza kufungwa urembo na viti kuvishwa vitambaa kuongeza nakshi. Fiona
alikuwa amesimama akiiwatazama wapambaji lakini pia akionekana kukosa raha.
Mumewe alimfuata mpaka pale alipokuwa amesimama
‘I thought umeshaenda shopping’ alimsemesha Fiona ambaye
aligeuza kichwa akitabasamu na kumtazama mumewe
‘Kristus….winning your heart will do me good kuliko shopping’
akamjibu kwa tabasamu na kugeuka, taratibu akipiga hatua na kumuacha mumewe
anamtazama pasipo kumuelewa kabisa.
‘Winning my heart?...’ akajiuliza kwa sauti nab ado hakuelewa
Fiona alimaanisha nini. Akamtazama Fiona aliyekuwa ameshawafikia wapambaji na
kupitia kazi zao. alimtazama mpaka pale Fiona alipogeuza uso na kumtazama.
Wakatazamana!... Fiona hakutabasamu nah ii iliashiria kitu kizito nyuma ya
kauli yake lakini ndio mzee hakuielewa kwa wakati ule.
Akageuka na kuondoka. Wakati akizikaribia ngazi za kuelekea
ndani kwake akasikia kelele na akajikuta anageuka.
‘Aawww! See who is here…Clariiii…Jenifa alimkimbilia rafiki
yake aliyekuwa nadio ameingia getini na kumkumbatia kwa furaha. Marafiki hawa
walikumbatiana kidogo wadondoshane na Mzee Agapela akajikuta akitabasamu tu na
kuendelea na safari yake ya kuelekea ndani.
‘Mungu wangu!....una tabia mbaya Clarita hukuniambia unakuja
jamani…why?’ Jenifa alimzonga rafiki yake wakati wakielekea kuketi katika moja
ya viti vilivyokuwa vinangoja kufanyiwa kazi.
‘Nilitaka nikusurprise….Jerry yuko wapi?’ Clarita Gabson
akauliza akiangaza angaza
‘Hebu msahau huyo mtu kwanza…. we have a lot to talk…yaani
siamini yeyiii…. twende ndani kwanza…’ Jenifa akasimama akitaka kuhama toka
pale walipokuwa wameketi
‘Talk show room!’ Clarita akatania akikumbushia walivyopenda
kukiita chumba cha Jenifa cha kulala sababu ya kukigeuza sehemu ya kupigia soga
zao
Jenifa na Clarita wakacheka na kunyanyuka, wakaondoka eneo
lile kuelekea ndani.
8888888888888888888888888888
Taa zilizokuwa zikiwaka kila kona zililipejndezesha eneo la
tukio kwa kiwango kikubwa mno. Magari ya kifahari yaliyokuwa yamekaribia kuziba
njia yalitapakaa kila kona. geti la nyumba ya Mzee Agapela lilikuwa wazi, ingia
tokay a hapa na pale iliendelea kila muda ulipozidi kukatika. Palikuwa
pamechangamshwa zaidi na muziki wa taratibu uliokuwa unasikika vizuri hewani.
nje ya nyumba watu walikuwa wamesimama wakipata vinywaji na
kubadilishana mawazo huku wengine wakiwa wameketi kwenye viti. mlango wa
kuingilia ndani ulikuwa wazi pia ukiruhusu watu kuingia katika sebule pana ya
kisasa ambako ndiko hasa alikokuwa Mzee Agapela.
muda huu wa saa moja watu ndio walikuwa wakiingia na wenza
wao. Kule juu vyumbani kulikuwa na mengi yanaendelea. chumba cha Fiona na
mumewe, Fiona alikuwa amesimama dirishani akiwa amevalia gauni lake la kulalia.
Ni kama alikuwa amesusia sherehe ya mumewe. alisimama dirishani na kutazama nje
huku akiwa na glasi yake ya mvinyo, akionekana kuzama mbali kimawazo mpaka pale
Mzee Agapela alipoingia.
‘You are not doing this to me Fiona!...kwanini?’ Mzee Agapela
alimuuliza mkewe akimfuata pale alipokuwa amesimama
‘Nazungumza na wewe’ mzee aliongea tena na Fiona hakutikisika
hata kidole sembuse kugeuza kichwa ama kujibu alichoulizwa.
Mzee wa watu akasogea tena na kusimama pembeni kabisa ya
mkewe
‘Fiona?...nini tatizo?’ akamuuliza mkewe kwa upole na Fiona
akahamisha macho yake toka kule mbele na kumtazama Kristus!
‘hakuna kitu!’ akajibu kwa ufupi na kukirudisha kichwa kule
mbele
‘sasa kwanini unanifanyia hivi katika siku muhimu kwangu….
kila mtu anakuulizia uko chini….unanipa wakati mgumu sana kwanini Fie’ mzee
akalalamika na Fiona akaguna kwa kejeli na kujinywea funda la mvinyo wake
pasipo kuhangaika na Agapela.
‘kama una tatizo ama chochote kile….nakuomba tumalize hii
sherehe salama kisha tukae chini uniambie…kwa wakati huu nakuomba Fiona… iondoe
hii aibu unayotaka kuileta kwangu’ Mzee akabembeleza akimgusa mkewe bega
‘Ondoa mkono wako’ akamkemea mumewe pasipo kumtazama
Mzee Agapela akashusha pumzi na kuamua kutoka mule chumbani
akimuacha Fiona palepale alipokuwa amesimama.
Chumbani kwa Jenifa, Clarita alikuwa amesimama akitembea huku
na kule kama mtu mwenye mchecheto na akiitazama saa yake ya mkononi. Alienda
mpaka mlangoni na kurudi mpaka kona moja ya chumba alienda tena na kurudi
akfanya safari zenye idadi inayochanganya kuhesabu. Ghafla tu akasimama na
kuutazama mlango ukifunguliwa na Jenifa akaingia akiwa ameongozana na Jerry.
‘Surprise!’ Jenifa akammwambia kaka yake akimuonyesha Clarita
Watu hawa wawili wakaganda kama masanamu kwa sekunde mbili
tatu kabla ya Jenifa kuwaondolea bumbuwazi lililowatembelea.
‘you guys can talk now….am out!’ akajitoa taratibu na
kuufunga mlango akiwaacha hawa wawili wamesimama tu wakitazamana.
‘za siku?’ Jerry akavunja ukimya na Clarita akatabasamu
‘njema…how have you been?’ Clarita akauliza akijaribu kuzuia
tabasamu lake na asiweze. mapenzi yake kwa Jerry yalikuwa na uzito ule ule
‘poa’ jerry akajibu naye akijilazimisha kutabasamu.
ukimya ukapita kati yao kila mmoja asijue aseme nini kwa
mwenzake
‘umependeza sana’ Clarita akavunja ukimya na Jerry
akatabasamu zaidi
‘Na wewe pia’ akajibu sasa akili yake ikitafuta cha kuzugia
na asipate
‘Jerry…’ Clarita akaita kwa upole na Jerry akaongeza tu
ukubwa wa macho yake kuashiria alikuwa anasikiliza
‘hujanimiss hataa?’ Clarita akauliza na Jerry akajikuta
akikata lile tabasamu na kumuwekea Clarita uso wa mkavu!
‘no!’ akajibu akimtazama Clarita usoni.
Ule uso wa tabasamu ukaanza kutetereka na Jerry akaona dalili
za kuingizwa kwenye kazi ya kubembelezana na mtu
‘Nimefurahi kukuona Clarita….’ Jerry akaongea akiunga na
ishara ya kutupia dole gumba nyuma kuonyeshea kuwa alitaka kutoka, na hakungoja
ruhusa akatoka na kumuacha Clarita ameduwaa. Alipotoka tu na Jenifa akaingia na
kumkuta rafiki yake amejiinamia
‘Amekwambiaje?’ jenifa akauliza kwa wasiwasi lakini hakupata
jibu. Clarita alikuwa amepoteza nuru ya uchangamfu aliokuwa nao tangu asubuhi.
Saa moja baadaye kule chini sebuleni, Mzee Agapela alikuwa
akibadilishana mawazo na mwanasheria wake Dennis Mazimbwe, wakiwa na vinywaji
vyao mkononi. mlangoni Familia ya Okello ilikuwa inaingia, ikisalimiana na watu
mbalimbali na wakati huo Jenifa na Clarita na baadhi ya mabinti wa wageni
wengine walikuwa wamesimama kwenye kona moja wakiongea na kuteta hili na lile.
‘The devil herself!’ Jenifa akatamka alipomuona Pamella
Okello akiwa na wazazi wake wakiingia. wenzake wakageuka na kumtazama Pamella
ambaye wala hakuwa na habari kuwa kulikuwa na watu waliokuwa wanamtazama kwa
chuki.
‘Nikimuangalia sioni cha kunizidi…sioni cha kunitoa knock out
kwa Jerry… that girl is a witch’ Clarita alizungumza na kumtazama Pamella kwa
chuki. Wasichana wengine wakacheka tu na kuzidi kumkodolea macho Pamella
alipokuwa akijongea kumfuata Mzee Agapella akiwa na wazazi wake.
‘My Princess!’ Mzee Agapela akamlaki Pamella kwa furaha
‘happy birthday baba Jerry’ Pamella akamtakia heri ya siku ya
kuzaliwa huku akiwaacha wengine wakicheka kwa vile alivyomuita
‘Asante mwanangu…’ Mzee Jerry akaitikia na Pamella akamtazama
Dennis Mazimbwe na kumsalimia kwa bashasha, moyoni akijua kwanini alimsalimia
vile. alikuwa shemeji yake kwa Patrick!
Dennis akajikaza kuipokea ile salamu kwa uchangamfu moyoni akijua yule ni binti
yake, damu yake!
Rebecca alijaribu kuzuga kutabasamu akikwepesha macho yake
yasikutane nay a Dennis kabisa. Mzee Okello akaunga salamu kwa Dennis,
akiongezea utani kwa kuchomeka maneno ya kimahakama kumtania Dennis. Kila mmoja alicheka isipokuwa
Rebecca!
Wakati maongezi yakipamba moto, Meddy alifika na kumfuata
Agapella akamnong’oneza kitu kisha akawasabahi aliowakuta. Mzee Agapella
akawataka radhi na kusogea kando na Meddy. Kuondoka kwa Mzee Agapella akukawapa
Mzee Okello na Dennis nafasi za kuongea zaidi wakati Mkewe na Pamella
wakijumuika na wanawake wengine wakiokuwa hapo karibu!
Meddy alipomalizana na Mzee Jerry akatoka na kulifuata kundi
la akina Jenifa
‘Hey warembo…nani amemuona Jerry?’ akauliza
‘Chumbani juu’ Jenifa akajibu na Meddy akaachana nao na
kuzifuata ngazi na kwenye ngazi hizo akapisha na Fiona aliyekuwa anaziteremsha
kwa madaha na kwa kujiamini kuwa alikuwa amependeza hasa. Mzee Agapella
akatabasamu wakati akimtazama mkewe.
Chumbani, alikokuwemo Jerry ndio chumba alichokulia akiwa
mtoto. alikuwa ameketi chini na chupa ya mvinyo katikati yake. Aliikunja miguu
yake na kuyafanya magoti yake egemeo la mikono yake. alikuwa na zaidi ya
msongo. Meddy alipofungua mlango na kuingia ndani alimshangaa Jerry.
‘Hey man!....vipi?’ akamuuliza akimfuata kwa kasi pale chini
‘Jerry…’ Meddy aliita akiitoa ile chupa ya mvinyo mbele ya
Jerry na kuiweka juu ya meza kisha akaketi kitandani na kumtazama rafiki yake
ambaye sasa alinyoosha mguu moja sakafuni na kuegemeza kichwa ukutani
akimtazama Meddy.
‘She is pregnant!’ akaongea kama mtu aliyekata tama
‘Whaat!.....Sindi?’ Meddy akauliza akimtazama Jerry ambaye
aliilegeza tai yake ya kipepeo na kuiondoa kabisa. Akalijibu swali la Meddy kwa
kichwa
‘Congrats man! huh!’ Meddy akajibu akitabasamu na hapo hapo akionyesha kutoamini
‘Nifanyeje?...’ Jerry akauliza akifumba macho na kutulia
‘Dah!....’ Meddy akakosa jibu wakabaki kutazamana tu.
88888888888888888888
Sherehe ilishachangamka na watu kupata chakula, katika eneo
la maegesho. Watu wawili walikuwa wamesimama wakizungumza. Mazungumzo yao
hayakuonyesha kuwa ya amani sababu ya lugha ya mwili iliyoonekana.
‘It is a taboo Dennis….huonyeshi kujali lakini mimi
najali….she is my daughter’ Rebecca aliongea kwa Jazba mbele ya Dennis
‘Nani amekwambia sijali?....lakini unapanic kiasi kwamba ni
rahisi kuhisiwa visivyo…. tumeitunza siri hii kwa miaka sasa…nini kinakupa
mchecheto kiasi cha kukosa amani?’ Dennis alionekana kukerwa na wasiwasi wa
Rebecca mke wa Okello.
‘kama si mdogo wako kuwa na binti yangu….nisingehangaika hata
kuzungumza na wewe… muondoe Patrick maishani mwa binti yangu haraka
iwezekanavyo…’ Rebecca alikuja juu
‘talk to Pamella…sawa?...talk to her akwambie ukweli….ukute
anakutania’ Dennis alizidi kubisha
‘Atanie kwa kumtaja mdogo wako?....kivipi?....na kipi
kinakuaminisha kuwa Patrick hatoki na Pamella?’ Rebecca aliuliza kwa hasira
sasa. hofu aliyokuwa nayo ilionekana kutomgusa mwenzake
‘Kwa sababu Patrick ana binti mwingine….na ameshamleta kwangu
juzi baada ya binti huyo kutoka masomoni. na yuko hapa!...nashangaa
unapokazania kuumba kitu kisichokuwepo’ Dennis alitetea kujiamini kwake
‘Yupo hapa?....who is she?’ Rebecca akauliza kwa udadisi
‘Clarita Gabson…Jenifa’s bestfriend’ Dennis akajibu
akitarajia kuona utulivu usoni mwa Mwanamke huyu!
Rebecca akamtazama Dennis kwa kituo
‘Clarita!.... so ndio mchumba wa Patrick sasa?’ Rebecca
akauliza akiwa bado haamini
‘Una hofu ya bure Rebecca…hofu ya kujitakia…. relax… siri
yetu iko salama na ukitulia itabaki salama milele…okay!’ Dennis akaongea akiwa
amemshika Rebecca mabega. Taratibu mwanamke huyu akakilaza kichwa chake kifuani
pa Dennis na Dennis akampokea na kumhifadhi.
majanga premier!!!! iam speechless uwiiii.....
ReplyDeleteduh ingine line i like the story wish uiandike kila siku congrats
ReplyDelete