Thursday, August 27, 2015

UREMBO NA LAURA:.... PRE - POO USHUHUDA WANGU BINAFSI!!


Pre - Poo inasimama badala ya Pre-shampoo
Hii kitu unafanya kabla ya kuosha nywele zako.

Sitaki kuongea maneno matupu ila nataka nikupe mfano mwenyewe kwa kutumia picha.
Ni treatment inayofaa zaidi watu wenye nywele za asili ila hata wenye dawa wanaweza fanya.

inakupa nywele safiiii... hakuna cha mba wala harara kichwani.... inazuia kukatika kwa nywele yaani ile ukichana mpaka unaogopa kutazama chanuo hahahaaa

Inakuza na kujaza Nywele!

 cheki hii picha hapa chini



hiyo ya kwanza ni nywele zilikatika vibaya mno yaani hata kufunga kifagio ilikuwa shida
Huku mbele ziliisha mnooooo sana sana sana

Nikaamua kuanza kufanya Pre Poo kila wiki. Kwanza zikaacha kukatika ovyo yaani nilishangaa nachana nywele ule mzigo niliozoea kwenye chanuo haupo ni vile zinapukutika kidoooogo sana

Pili Nywele zikajaa mpaka raha.... na mba uliokuwa kero ukatoweka ghafla.

NAMNA YA KUFANYA PRE POO!

Ni rahisi sana
1. Tafuta mafuta unayotaka kufanyia pree poo...yako aina nyingi sana
Mimi nilichukua Mafuta ya nazi na mafuta ya olive tena haya nilinunua maduka ya asili

2. changanya mafuta yako kisha gawanya nywele na upake kwenye ngozi kichwa kizima

3. Paka kwenye nywele pia yaani nywele ziloe mafuta kiasi kisha fanya kama unamassage ngozi ya kichwa kwa dakika kadhaa

4. Funga nywele zako na mfuko wa nailoni, vaa ile cap ya kuogea... ikibidi fungia na khanga juu

5. acha kwa nusu saa hadi saa nzima ukiweza lala nayo

Mwisho ukitoa osha na shampoo yako  vizuri.

Wengi wetu pia tunakosea katika uchaguzi wa shampoo. ukitumia shampoo isiyoendana na nywele zako lazima zikatike pia.

Ukifanya hivi kwa mwezi kila wiki au wiki mbili utaona tofauti kubwa katika nywele zako

Zipo pia Pre poo za aina tofauti tofauti
Kama ndizi iliyoiva, parachichi, Pree poo ya Yogurt na asali ambayo huwa naifanya mara chache ila nzuri saaaaana pia.

Wewe ambaye nywele zinakatika sana hebu jaribu hii kitu!
Mwanamke nywele mwenzangu sio kila siku bandia kichwani siku nyingine baki ulivyo tuone unavyojiamini hahahahaaa


No comments:

Post a Comment



Snowfall Widget for Blogger


Snowfall Widget for Blogger