NAPKIN
Wengi wetu nadhani tunajua ni
kitu gani. Kwa maelezo ya juu juu ni karatasi au kitambaa kinachokaa mezani kwa
ajili ya kufutia pembe za mdomo na
vidole wakati wa kula au baada ya kumaliza kula.
Kinaweza kuwa kitambaa cha
material yoyote ile ila cotton
inapendeza zaidi kwa kuwa ni rahisi kuikunja kwa staili mbalimbali za kupendeza
kuliko kitambaa laini.
Kitambaa hiki unaweza ukakikuta
mezani hotelini, nyumbani kwa mtu au kwenye sherehe. Hata wewe unaweza kuandaa msosi wako mzuri
nyumbani na kualika wageni wako kisha
ukakitumia kuongeza umaridadi mezani pako. Si unakumbuka charger plates!!
Kuwa Classic ndio habari ya mjini
my dear!.... mumeo kaalika watu wa kazini kwake, hebu fanya kitu cha kuwafanya
wakitoka hapo waone mwenzao ana mtu anayependa vitu vizuri. Simple table
setting ya uhakika!! Hakuna kuomba omba tishu heheheeee!
Zipo staili mbali mbali za namna
ya kuiweka napkin mezani. Kuna wengine hufunga kama kipepeo, kuna wengine
huikunja pembe tatu na kuiweka juu ya sahani yaani staili za kuifunga ni nyingi
sana, ni wewe tu na uamuzi wako.
NAPKIN HUKAA WAPI?
Kama ni mlo wa kawaida na si ule
rasmi wa shughuli maalumu Napkin inakaa popote kulingana na nafasi kwenye meza
yako. Ila kwenye shughuli kubwa utaikuta napkin mezani juu ya sahani.
UMEIKUTA NAPKIN KWENYE MTOKO WAKO…UFANYEJE?
Umealikwa mahali mwenzangu, sehemu yenye mchanganyiko wa watu. Nadhani hutotaka kuonekana mshamba saaana au kushindwa kujua ustaarabu wa matumizi ya Napkins au sio? Hahahahaaaa!!
1. Ukifika mezani usikimbilie
kuchukua napkin haraka haraka…ngoja watu wawili watatu wakae…na kama mko wawili
ngoja mwenzio naye akae!
2. Chukua napkin yako iweke
mapajani. Napkin inakaa mapajani kamwe usiweke napkin shingoni. That is not a
bib jamani. Bib ni kile kidude tunafungiaga watoto shingoni wakati wa kula, kwa
Kiswahili sijui kinaitwaje. Bibs are for babies not adults!! Labda kama
unafanya comedy.
3. Ukishaiweka mapajani anza
kupata mlo wako kama kawaida. Unapofuta midomo ikunje upate ncha hivi na kufuta
kando ya midomo yako. Usitumie napkins kufuta lips za midomo yako. Hahahahahaa na
utafutaje mdomo mzima mwenzangu kwani unakulaje kwa mfano?
4. Labda katikati ya mlo umelazimika
kunyanyuka na kwenda maliwatoni, nje kupokea simu au vyovyote lakini ndio
umelazimika kutoka mezani. USIWEKE NAPKIN MEZANI!!....iweke kwenye siti yako,
pale ulipokuwa umekaa. Usiondoke nayo wala usiitundike kwenye mkono wa kiti
yakhe! Kuiweka mezani kunamaanisha umemaliza kula na hurejei mezani!
5. ukirudi irudishe mapajani
mwako na uendelee na mlo wako! Utakapomaliza kula usiweke napkin juu ya sahani
uliyotumia. Iweke pembeni ya sahani kistaarabu. Mwenyeji wako atajua umemaliza
kula hata kama kwenye sahani yako kuna chakula. Kutoa napkin mapajani na
kuiweka mezani kunamaanisha umeshiba au umemaliza kula.
NINI USIFANYE KWA KUTUMIA NAPKIN
1. Usiitumie kama handkerchief! Labda
kupengea kamasi ama kufutia jasho
2. Usifutie midomo yote kama
unanawa vile
3. Usiikunjekunje kama mpira au
fundo
4. Usiitemee chakula kama kipande
cha nyama kigumu hivi… vitu kama hivi huwekwa kwenye charger plate
5. Mwisho ndio kama hivyo
ukiondoka katikati ya mlo usiiweke mezani na ukimaliza kula usiiache kwenye
kiti… utaratibu nimekupa hapo juu.
Haya kazi kwenu waungwana! Usiwe kama
jiwe kutotaka kusogea wala kujifunza…. Maisha ndio haya haya mwenzangu…. Na mambo
ya kujifunza ndio haya haya…usiwe mgumuuuuu khaaaa!! Ukang’ang’ana na mambo ya
kizamaaani LOL
Natumaini umejifunza kitu eeh!!
No comments:
Post a Comment