Sunday, June 29, 2014

10 MINUTES WITH GOD...MFALME WA AMANI LYRICS NA SOLOMONI MUKUBWA!!




Mfalme wa Amani ni moja kati ya nyimbo za Solomon Mukubwa zinazonibariki sana
Ni wimbo unaogusa hisia za ndani na maisha ya kila siku ya binadamu
Usikilize...utafakari.... utagundua Pamoja na majaribu yote ya dunia bado tunalo kimbilio ambalo ndilo Mfalme wa Amani....
Unapomaliza kuusikiliza wimbo kwa dakika mbili mwambie Mungu shida yako, mpe Mungu shukrani zako!!

Daudi kasema,nilikuwa kijana sasa ni mzee (x2) 

Sijawahi kuona mwenye ameachwa mimi 
Wala watoto wake kuombaomba mikate barabarani 
Mungu ni mwaminifu, kwa ahadi zake wanadamu 
Mungu ni mwaminifu, kwa ahadi zake si kama wanadamu 
Akiongea Yesu ameongea, 
Akikuahidia kitu, Baba ameahidi na ujasiri 
Atatenda kwa wakati wake 
Ninamwita Bwana wa amani 
Ninamwita mfalme wa amani 

Ndio maana mimi ninaimba kwa sababu ya amani yake 
Ni uwezo gani, uwezo gani unaominga Baba 

Uwezo gani, uwezo gani, uwezo gani 

Refrain:

Mfalme wa amani, mfalme wa amani uinuliwe 
Wewe ni mwema, wewe ni mwema Bwana wangu 

(Refrain)
Usilie, usilie, usiliwe wewe

Usilie Bwana anakujua ndugu yangu 
Amesikia kilio chako wewe mama 
Unalia nini kwa wanadamu, mama yangu 

Wanadamu hawatakusaidia na kitu 

Wanadamu hawatakuwezesha kwa kitu chochote 
Tunaye mmoja anayepanguza machozi ya watu wake

Ni yule mfalme wa amani 




Ni yule aliyesema yote imekwisha 
Mama unayoyapitia ni yeye anayeyaona 

anajua shida yako mama yangu 

Anajua magumu yako baba yangu 
Ukiwa na shida usiende kwa waganga wa dunia 
Ukiwa na magumu usiende kwa wafumu wa dunia 
Muite mfalme wa amani, yeye anajibu maombi (x2)  
Ni uwezo gani, uwezo gani unaominga Baba 
Uwezo gani, uwezo gani, uwezo gani 

(Refrain)
Mfalme wa amani, uinuliwe Bwana wangu 

yale unayotenda inashangaza dunia nzima 
Wanaokosa amani ndani ya nyumba zao wape amani 

Wanaokosa amani ndani ya kazi zao wape amani 

Ni wewe Bwana wa amani ya kudumu 

Ni wewe Bwana wa amani ya Afrika 

Amerika wanalia amani 
Tunawe Bwana mfalme wa amani )(x2)
Hakuna kitu kile kinachokushinda Bwana 
Yeye Mfalme wa Amani 

  

No comments:

Post a Comment



Snowfall Widget for Blogger


Snowfall Widget for Blogger