Monday, May 27, 2013

SINDI....NA LAURA PETTIE (18)

18


Jerry Agapela alilipapasa shavu lake la kushoto kwa mkono wake wa upande huo huku akimtazama Pamela kwa mshangao.

Alitaka kumuuliza Pamela sababu ya kibao kile lakini kwa haaki aliyokuwa nayo hakuweza hata kufumbua mdomo wake na kuhoji. Alimtazama tu kana kwamba kule kumtazama kungelimfanya Pamela ajieleze. Alikosea!


Pamela naye alimtazama kwa ghadhabu pasipo kueleza sababu ya adhabu ile aliyompatia. Walitazamana kama majogoo yaliyojiandaa kupigana, kila mmoja akipitiwa na yake kichwani. Meddy Hakim akatembea kwa haraka na kuja kusimama katikati yao, naye mshangao ukimtembelea.

‘Pamela kuna nini?’ Meddy akaona auvunje ukimya haraka kabla Jerry hajachukua hatua yoyote ya kuihoji ile adhabu kimatendo. Mwanaume kuchapwa kibao na mwanamke kwa staili ile ilikuwa zaidi ya dharau!

‘Napoteza muda wangu kufuatilia suala lake, najiingiza kwenye gharama za ajabu ajabu kukodi watu wachunguze suala lake…and you know what!...anazurura mitaani kana kwamba yaliyomfika shinyanga yalikifika kivuli chake… kama unadhani hujali kilichokutokea kwanini usiseme tukaacha kuhangaika kwa ajili yako’ Pamela aliongea mfululizo kwa hasira akiwatazama Meddy na Jerry kwa awamu. ghadhabu ya Pamela ilisomeka wazi usoni.

‘Ukiwa na maana gani?’ Jerry naye sasa alihoji akiliachia shavu lake
‘Ulikuwa mchikichini mchana wa leo na umeonekana posta pia…. unatafuta nini?....’ Pamela alihoji tena akimakzia macho Jery
‘Sidhani kama kila ninalofanya unapaswa kujua’ Jerry alijibu akianza kupiga hatua kuelekea kule alikokuwa ameketi na Meddy mwanzoni kabla ya Pamela kufika pale.

‘What!.... kwamba sipaswi kujua yanayokuhusu?.... okay!’ Pamela akalivuta lile neno okay kwa maumivu ya ndani kwa ndani. Alikuwa amejitoa mno kumsaidia Jerry
‘No!...Pamela sikiliza kwanza…’ Meddy akataka kuingilia kati
‘Enough!.... nimenawa….najiondoa katika hili suala na chochote kiakachokutokea usinihusishe….i can how stupid i am….kuacha shughuli zangu kukufuata vijijini just kuhakikisha uko salama….’ Pamela aliongea taratibu lakini kwa sauti ilionyesha kuvunjika moyo

Akageuka na kuanza kuondoka eneo lile huku Meddy akishindwa kumfuata na akishindwa kumkaripia Jerry kwa dharau aliyoionyesha. Pamela alipotoka na kufunga mlango wa geti. Meddy alichapua hatua za harakaharaka na kumfuata Jery pale alipokuwa ameketi akiinywa juisi yke taratibu kana kwamba hakuna lililokuwa limetokea.

‘Jerry!’ akamuita kwa mshangao. Jerry alinyanyua kichwa na kumtazama Meddy aliyekuwa amesimama mbele yake mikono kiunoni.

‘hiki nini sasa?’ Meddy akauliza akivuta kiti na kuketi mbele ya Jerry ambaye usoni alionekana kuwa na utulivu mkubwa hali moyoni akiwa na hamaniko la kutosha.
‘Hastahili kuniwasha kibao….Mwanamke hawezi kuniwasha kibao mimi just because ananisaidia’  Jerry alitoa dukuduku lake.

‘Tatizo sio kibao tatizo ni kwanini amekuwasha kibao…. unajua ni kiasi gani Pamela anahangaika kwa ajili yako…. na una sababu gani za kuzurura kwa nafasi kama hivi wakati unajua unatafutwa na humjui anayekutafuta…. come on Jerry!’ Meddy alizungumza kwa hisia akimuunga mkono Pamela.

‘kuna mambo ni yangu binafsi Meddy…. hawezi kujua kila kitu na hawezi kunicontrol nisiende hapa au pale… yeye ni nani?’ Jerry bado aliusimamia ubishi wake
‘Mambo binafsi?..... amekukodia mtu wa kukufuatilia kujua kama unafuatiliwa…. amehangaika kukufuata mpaka shinyanga ulikokuwa huna hata tumaini la wapi pa kuanzia nab ado unafanya vitu vya kijinga jinga kama hivi….. ulitakiwa utulie ndani uletewe taarifa…. ufanye uchunguzi wa kina ujue who was behind your kidnapping…’ Meddy aliongea kwa hasira sasa na Jerry alitazama pembeni kana kwamba yale aliyokuwa anayaongea Maddy hayakumhusu.

‘Kama unataka kumuaminisha Sindi kuwa wewe ni hohehahe…..tumia njia nyingine sio hii ya kuzurura ovyo…. and too bad unataka kuiteka akili ya Sindi kwa wakati usio sahihi na sababu zisizo sahihi… Pamela was right to slap you’ Meddy akamalizia na kunyanyuka toka pale alipokuwa ameketi, akageuka na kuishia zake.

Jerry akabaki peke yake, akishusha pumzi ndefu na kutikisa kichwa chake katika namna ya kujihurumia na hapo hapo akishindwa kujielewa. Robo tatu ya maneno ya Meddy yalikuwa kweli, kweli tupu! Alikuwa amejisahau!
8888888888888888888888888
Mzee Agapela alipata nafuu na kuondolewa hospitali, Dakatari wa familia akimtaka atulie nyumbani kwanza na aachane na kazi kwa muda ili kujipa mapumziko. Mchana huu akiwa kwake, aliteremsha ngazi taratibu akiwa na mkongojo wake uliomsaidia kutembea kutokana na kudhoofika kwa hali yake.

Aliifiia sakafu ya sebule na kutembea kwa shida kidogo kukifuta akiti chake kilichokuwa umbali mfupi toka pale zilipo ngazi za kuelekea ghorofani. Jenifa alitoka jikoni na kumfuata baba yake sebuleni akiwa na sinia lenye juisi. akaongoja baba yake aketi kisha akamsogezea stuli na kuliweka lile sinia la juisi juu ya ile stuli.

‘Mama yako yuko wapi?’ Mzee Agapela akmuuliza binti yake
‘Nadhania ametoka sijamuona kabisa…’ Jenifa akajibu na baba yake akatikisa kichwa kwa huzuni
‘…baba!....kuna tatizo?’ Jenifa akamuuliza baba yake akiketi sofa lililokuwa pembeni ya kile kiti alichokuwa ameketi baba yake
‘mmh mmh’ Mzee akaguna mara mbili, akiusisitizia mguno wake kwa kutikisa kichwa mara mbili lakini uso wake ukiwa kwenye tafakari nzito

Akainua uso wake uliokuwa unatazama chini wakati akiguna na kumtazmaa binti yake.
‘unamuonaje mama yako?’ akamuuliza Jenifa ambaye alibetua mabega yake na kutanua midomo yake akitafuta cha kujibu na akaishia kuuliza swali
‘Kivipi baba?’
‘Tabia zake, mienendo yake…’ Mzee akafafanua akitanua viganja hewani
‘She is great…so lovely....’ Jenifa akatoa mtazamo wake bila wasiwasi

Mzee Agapela akaupokea ule mtazamo kwa kutikisa kichwa juu na chini, asiweke wazi kama aliuafiki ama alikuwa akiuitikia tu.
‘Nisaidie kusimama’ Akamrai binti yake ambaye kwanza alimshangaa kwa vile alikuwa hajaigusa ile juisi na pili, alikuwa amketi pale kwa takribani dakika tano tu. Jenifa akanyanyuka na kumsaidia baba yake kuinuka. Mzee Agapela akaanza kutembea kwa taabu kurudi kwenye zile ngazi. Alikuwa anaelekea tena chumbani!

Kichwani mwa Mzee huyu kulionekana kujaa maswali mengi mno, mawazo ya kila aina na majuto ambayo sasa yaliacha kujificha na kuamua kuchomoza taratibu. Jenifa akamtazama baba yake alivyokuwa akipanda ngazi kwa shida pasipo kumuelewa. Wakati akimtazama baba yake, alisikia mngurumo wa gari nje. Mngurumo ule hata Mzee agapela aliusikia na akasita kidogo na kugeuka kumtazama Jenifa

‘Ni nani?’ akamuuliza bintiye ambaye aliamua kulifuata dirisha kuchungulia nje
‘ni Mama’ Jenifa alijibu kwa furaha na kuufuata mlango. akatoka nje na kumlaki Fiona aliyekuwa anashuka garini.

‘Nina booonge la zawadi mwanangu…Mwambie dada wa kazi atuletee kitu tuburudike huku bustanini’ Fiona aliagiza hukua akifungua mlango wa kiti cha nyuma cha gari lake na kutoa mifuko kadhaa iliyoonyesha alikuwa ametoka kufanya shopping ya maana.

Jenifa akafungua mlango na kupaza sauti akitoa maagizo kwa huyo dada wa kazi. kisha akaufunga na kumfuata Fiona pale kwenye gari, akamsaidia kubeba mifuko kadhaa na Fiona kubaki na michache. Wakaelekea bustanini kwa pamoja wakiongea na kucheka.
‘Basi nikwambie mama…’ Jenifa akamfanya Fiona akate kicheko na kumtazama kwa umakini kabla hawajaketi

‘Nini?’ akamhimiza aseme
‘Baba alikuwa anakuulizia asubuhi’ Jenifa akaanza maelezo na Fiona akakunja ndita na kulaza shingo upande kidogo, akaguna!
‘…ni kama ana mashaka na wewe hivi….’ Jenifa akazidi kumkoroga Fiona ambaye nguvu ya kubeba ile mifuko na kule kusimama ikamuishia. akaitua mifuko juu ya meza ya duara na kuketi haraka, akionekana kupaparika na lile swali

‘Nadhani anahisi labda una mtu uko nje….maana aliuliza mienendo yake sijui tabia….nikakusifiaje sasa’ Jenifa akauma na kupuliza bila kujua maana halisi ya baba yake kumuuliza vile. Fiona akashusha pumzi hata yeye alijua Jenifa hakumuelewa baba yake. uso wenye tabsamu ukatoweka na uso uliojaa mashaka ukamvaa na akajikuta amajilazimisha kutabasamu pasipo hiari.
‘Baba yako bwana!....’ alijilazimisha kuonyesha alikuwa pamoja na Jenifa katika ule mtazamo lakini moyoni hali haikuwa hivyo. alikumbwa na hofu na maswali yaliyomiminika kichwani mwake bila majibu. Amejua nia yake?...amegundua mipango yake?....au…au…au… Alipanga maswali kichwani pasipo hitimisho. Aliogopa!

Wakati wawili hawa wakiongelea hili, Mzee Agapela alikuwa ghorofani, dirishani, akiwa watazama wanawake hawa wawili kwa jicho lisilotoa tafsiri rasmi ya nini alikuwa anawaza juu yao.
888888888888888888888888

Siku mbili mbele baada ya ugomvi wake na Jerry, Pamela aliingia kwake usiku akitokea kazini. Aliifungua mlango wa sebuleni kwake na kuingia ahuku akitembea kivivu, Aliwasha taa. Akavua skuna yake ndefu na kuitupia kando kisha akavua skuna nyingine na kuirushia pembeni. Akautua mkoba wake na kibegi kidogo cha laptop kwenye sofa.

Akaifuata redio ya kuiwasha, akiongeza sauti ya muziki wa ala ya muziki waForever in love wa Kenny G, ala inayotumika kipindi cha chombeza time cha redio one, ala ile iliyokuwa inatoka katika CD aliyoweka ikasikika taratibu. Alijishika shingoni na kujaribu kujinyooosha  akiitanua mikono yake hewani na kuubinua mgongo wake katika namna ya kuunyoosha. Akapindisha pindisha shingo yake huku akitembea peku kuifuata meza yenye kinywaji. Akajimiminia whisky na kuipiga funda moja kisha akaitua bilauri juu ya ile ile meza. Akaelekea chumbani kwake.

Aliingia bafuni, akaoga, akarejea chumbani na kufanya maandalizi ya kulala. Akiwa ndani ya gauni lake lenye matirio ya kung’aa akarudi sebuleni na kuwasha luninga, akiifuata ile whisky yake na kuketi sofani. Ni kama vile kulikuwa na sinema ambayo aliishia kati na sasa aliiamua kuimalizia. akiwa ametulia na kuiweka akili yae kwenye ile sinema. Simu yake ikaita toka kwenye mkoba uliokuwa umetelekekwa kwenye lile kochi.

Akaitoa simu na kukitazama kioo cha simu. Alikuwa Jerry. Akasita kuipokea kwanza. Akaitupa kando na simu ikaita mpaka ikakatika. Lakini ghafla simu ile ikaanza tena kuita na akaichukua na kuipokea

‘Nifungulie mlango Pam’ akaisikia sauti ya Jerry. Akiwa bado na simu sikioni akanyanyuka na kwenda kufungua mlango. Akagongana uso kwa uso na Jerry ambaye naye simu ilikuwa bado iko sikioni. Wakatazamana tu!

‘What do you want?’ Pamela akauliza akitoka pale mlangoni na kurudi kuketi, akiwa ameshakata ile simu na kuitupia simu yenyewe kwenye sofa karibu na pochi yake.
Jerry aliingia na kufunga mlango, kisha akamfuata Pamela pale sofani, akisogeza makorokoro yaliyokuwa kando ya Pamela juu ya lile sofa.

‘Pam…’ akamuita kwa upole akimtazama usoni na akishusha uso wake na kuyatazama mapaja laini ya Pamela yaliyositiriwa nusu na lile gauni la kulalia.
‘I’m sorry’ akatamka kwa sauti ya kunong’ona na Pamela akakunja uso na kumgeukia Jerry

‘Toka nje!’ akamuamrisha na kurudisha uso wake luningani
‘Pamela…please’ akajaribu kumgusa lakini Pamela alipangua ile mikono na kuimung’unya midomo yake, akijaribu kukazia uso wake kwenye luninga.
Jerry akatulia na kuinamisha kichwa chini kama mtu anayetafakari

‘Pamela…’ akainua uso na kumuita tena kwa sauti ya chini lakini iliyomfikia vema Pamela ambaye wala hakugeuka
‘I love you…’ akalitamka neno hili kimahaba akimsogelea zaidi Pamela kiasi cha pumzi zilitoka puni mwake kugonga eneo la sikio la kulia la Pamela.

Pamela akakisogeza kichwa chake mbali kidogo na Jerry ambaye sasa aliinua mikono yake na kuupapasa mkono wa Pamela akianzia begani na kuteremsha kuelekea kwenye kiwiko, Pamela akageuka mzima mzima
‘What do you want from me Jerry?....’ akauliza kwa ghadhabu ‘…si ulisema sihusiki kwenye maisha yako?’ akaendelea kufoka ‘….sasa now una…..’ hakumalizia sentensi ile kwani Jerry alimdaka na kukiwahi kinywa chake. akaiunganisha midomo yao. Pamela akapinga kwa sekunde tu na kulegea. Akajikuta anatoa ushirikiano na wakati wakifanya hili. Mlango wa sebuleni kwa Pamela ukafunguliwa, na mwanaume mmoja jamali aliyeingia akitabasamu, akaduwaa na kupigwa na butwaa.

....NINI KITATOKEA?..MWANAUME HUYU NI NANI....JE MZEE AGAPELA AMEGUNDUA HILA YA FIONA?
/

1 comment:

  1. Hey there I am so delighted I found your site,
    I really found you by accident, while I was searching on Askjeeve for something
    else, Regardless I am here now and would just like to say thanks for a incredible post and a all round interesting blog (I also love the theme/design), I don’t have time
    to go through it all at the minute but I have saved it and also added in your
    RSS feeds, so when I have time I will be back to read much more,
    Please do keep up the excellent b.

    Feel free to surf to my site ... Psn Code generator

    ReplyDelete



Snowfall Widget for Blogger


Snowfall Widget for Blogger