Tuesday, May 21, 2013

BARAZANI:...JARIBU USHINDWE

...Natumaini mu wazima wa afya njema kabisa, n akwa wale ambao hali si njema basi Inshallah! Mwenyezi Mungu atawapa ahueni na mkono wa faraja.

leo katika kona yetu ya barazani nimekuja na kitu hiki ambacho nahisi ndio kikwazo kwetu wengi wetu kufikia malengo, matakwa ama mahitaji yetu!




Mathalani, unahitaji sana msaada wa mtu lakini namna ya kumuanza inakuwa ngumu. Kwa kuhalalisha kushindwa kwako unaanza visingizo ooh yule anadharau...yule yuko hivi ama vile lakini ukweli unabaki ndani ya moyo wako kuwa hujawahi kujaribu kumtafuta akakufanyia dharau....

Mara ngapi, nafasi ngapi zimetupita na kisha tunagundua kuwa laiti tu tungefanya hiki ama kile safasi zile zingekuwa zimetupigisha hatua kubwa maishani mwetu?

Watu tunachukulia kushindwa kama laana, matusi, mkosi au aibu kubwa sana maishani mwetu. Tunasahau uwa kama maisha yanapanda na kushuka basi kusimama na kunyanyuka ni sehemu ya maisha. Tazama mtoto anavyoanza kusimama dede mpaka kupiga hatua yake ya kwanza. Unadhani endapo mtoto huyu ataogopa kuanguka kila mara atawezaje kujifunza kupiga hatua na hatimaye kutembea na kukimbia?

JARIBU USHINDWE!... haamanishi uingie kujaribu ujua kuwa utashindwa la hasha! Jaribu ukiwa na imani zote kuwa mafanikio ni halali yako na kama itatokea ukashindwa basi ipo sababu njema zaidi. Simama na jaribu tena na tena inaweza isiwe kujaribu juu ya kitu kile kile lakini usibaki chini kusononeka kuwa umeanguka na waa usibaki chini kuhesabu umeanguka mara ngapi... itakuvunja moyo, itakunyong'onyeza na itakufanya ukate tamaa haraka kabla ya kujaribu tena na tena.

Hebu leo hii ukiwa peke yako jaribu kuorodhosha mambo kadhaa uliyowahi kuyakatia tamaa na aidha kutoyajaribu kabisa au kuyaacha baada ya kunguka mara moja. Yawezekana ni wazo la biashara uliloona ni kubwa kuliko uwezo wako lakini hukuwahi hata kulifanyia utafiti....yawezekana ni kijana mwenzio unayempenda lakini unashindwa kumwambia kwa kuhofia atakwambia hapana au atakudharau

...yawezekana na biashara uliyoanzisha na ikafa mara moja na ukadhani hutaweza tena kufanya biashara nyingine yoyote ile....yawezekana ni hili au lile! hebu weka hofu na woga pembeni jaribu sasa!

jaribu kwa moyo mmoja ukitarajia mafanikio zaidi na kinyume chake ukingoja kupambana na vikwazo aina zote. Usikae chini na kudhani mafanikio, mambo mazuri yameandikwa kwa ajili ya watu fulani tu...hata wewe unaweza kuyafikia au kuyapata... UKIAMINI KUWA UNAWEZA NA UKAJARIBU KUTENDA KWA HAKIKA UTAPATA UTAKALO!

....NENDA KAJARIBU LEO ULICHOSHINDWA JANA SI AJABU KIKAKULETEA FURAHA KESHO....

No comments:

Post a Comment



Snowfall Widget for Blogger


Snowfall Widget for Blogger