13
….Ilimchukua nusu saa nzima kwa Jenifa kuhisi ukimya
uliokuwepo haukuwa wa kawaida. akaliweka gazeti kando na kumtazama mama yake
kule kitandani. Kwanza alihisi kama
ganzi ikimtembelea mwili mzima kwa mtindo wa shoti, moyo wake ukadunda mara
mbili ya kawaida alipoutazama uso wa mama yake.
‘Mungu wangu jamani…’ akapiga yowe akinyanyuka haraka na
kukimbilia alipolala mama yake. Alionekana kama mtu aliyetulia huku macho yakiwa
wazi. Jenifa akamtikisa mama yake lakini mkono wa kushoto wa mama yake uliposerereka
na kudondoka pembeni ya kitandani.
Jenifa alishtuka mno, akajaribu kuunyanyua na kuuachia hewani
akitegemea pengine mama yake angeliamka lakini, mkono ule uliserereka tena na
kurudi chini kama jiwe lililotupwa hewani. Jenifa
akarudi nyuma taratibu, mikono ikiwa kifuani. Taharuki ikiwa imemvaa na hali ya
kuchanganyikiwa ikiwa imemtawala.
‘No…Nooo…Nooo’ alirudi nyuma akipiga kelele za kuikataa ile
hali, mwili sasa ukimtetemeka kiasi cha meno yake kuonekana yakigongana. Ni
muda mfupi tu alikuwa akiongea na mama yake na hali yake ikionekana kuanza
kutulia baada ya daktari mwingine kuzungumza naye usiku uliopita kwa muda mrefu
sana .
Ni nini hiki kimetokea sasa?....swali lilimpitia akilini
wakati akigota ukutani, na machozi kushika nafasi machoni mwake.
‘Mama…Mama’ Jenifa aliita kwa sauti, aliita akiitazama maiti
ya mama yake pengine akitegemea angeligeuka na kumtazama. alitamani iwe ndoto
na kwa wakati ule akili yake ilisimaam kufanya kazi sawasawa kiasi cha kujikuta
akishindwa kumuita daktari na akishindwa pia kuidhibiti taharuki iliyomkumba.
Baada ya sekunde kadhaa alizosimama pale akiweweseka, Jenifa
alikurupuka na kutoka wodini mle akikimbilia mapokezi. Koridoni mule akikaribia
kuangusha watu wengine kwa kiwewe alichokuwa nacho. Nesi aliyempkea pale
mapokezi alimtafuta daktari na wote wakakimbilia wodini alikokuwa Sophia.
Ikathibitishwa kuwa ameshafariki!
Jenifa Agapela alipoipokea ile taarifa kwanza aliduwaa kama
mtu aliyepotewa na kufikiri kisha taratibu akalegea, akifumba macho na udondoka
kama mzigo. Alizirai!
Sophia akawa ameondoka maishani mwa watotot wake, akiwaachia
simanzi ya kutosha. Jerry na Jenifa wakamzika mama yao
makaburi ya kinondoni. Wakashuhudia baba yao
akijitokeza na msiba ukifanyika nyumbani kwake. Akapokea rambirambi kubwa kubwa
kana kwamba yeye ndiye aliyemuuguza mkewe.
Kristus Agapela akamzika mkewe kwa mazishi ya gharama, akilia
na kuomboleza huku ndugu na jamaa pamoja na watoto wake waliokuwa wakijua namna
alivyomtelekeza Sophia wakisikitika na kuumia zaidi. Kutokana na nafasi ya
Kristus Agapela kama balozi mstaafu, mazishi ya mkewe Sophia yalihudhuriwa na
viongozi mbalimbali maarufu na msiba ule uliripotiwa na vyombo mbali mbali vya
habari.
888888888888888888888888
Mwezi mmoja tangu Sophia azikwe. Fiona aliwaita Jerry na
Jenifa nyumbani kwao. alikuwa na mazungumzo nao. Alipowaweka mbele yake
aliongea mengi yaliyomfanya Jerry amtazame kwa chuki hasa. Lakini alipogusia
suala la wao kurejea nyumbani kwao kwa masharti, Jerry alimbwatukia
‘huwezi kuwa mama yangu….na huwezi kuchukua nafasi ya mama
yangu’ alimkaripia Fiona ambaye kama kawaida yake
aliachia lile tabasamu lake zuri
lenye ufedhuli ndani yake.
‘…na kama huwezi kuniheshimu kama
mama yako...it is okay, it means upo tayari kukata mizizi yote inakuunganisha
wewe na sisi’ Fiona alimtishia na Jerry akacheka kwa ghadhabu
‘una mizizi gani na mimi?....kauli hii aitoe baba yangu sio
wewe…sikutambui’ Jerry alijibu kwa hasira na Fiona akiendela kutabasamu kana
kwamba hakuna lolote baya alilooongea Jerry.
Fiona akashusha pumzi na kumgeukia Jenifa, huku akiliendeleza
lile tabasamu
‘and you dear?....sidhani kama unataka
kuendelea kuzurura mitaani kama mbuzi asiye na
mwenyewe….it is time urudi nyumbani na upate huduma zote kama
mtoto wa Agapela…. ready to come back?’ Fiona akamuuliza Fiona ambaye
alimtazama kwa huruma, alimtazama katika namna ya kuhitaji mno kurudi nyumbani
lakini si kwa masharti kama yake aliyokuwa anampa.
Jenifa alishindwa kutoa jibu la moja kwa moja na Fiona
aliiona hali ile ya kusita.
‘Uhitaji kujibu now dear….take your time Jeni’ akamwambia kwa
upole, akiahamisha uso wenye tabasamu na kumtazama Jerry, akikata lle tabasamu
ghafla.
‘Think twice!...’ akampa ushauri uliomfanya Jerry anyanyuke
na kumtaka Jenifa waondoke
‘Uhitaji kumburuza Jenifa kwa kila kitu….atachagua what is
the best for her…goodluck’ Fiona alijibu kwa mbwembwe akimtazama Jerry usoni.
Wakatoka mule ndani na kuingia mitaani. Kwa wiki nzima
walijadiliana lile sharti la Fiona pasipo muafaka. Mwisho wa yote, Jerry
alimuweka Jenifa chini na kumwambia uamuzi wake.
‘I’m not gonna bow before her…never!....over my dead body
Jeni!.... unajua alichomfanyia mama…right?...how can you live na shetani kama
yule na bado ukamheshimu kama mama yako….mama hataweza kupumzika kwa amani uko
aliko….ni sawa na kumsaliti mama Jeni….bora ushauri wangu wa kuhamia kwa
Pamela’ Jerry aliongea kwa msisitizo ambao haukumwimgia Jenifa hata kidogo.
Jenifa alisimama na kutembea hatua chache kisha akamgeukia kaka yake
‘Nitamtumikia kafiri nilipwe ujira wangu…. I have a long way
to go….nataka kurudi chuo, nataka kusoma Jerry…ntaka kuishi maisha yasiyo na
stress ili nitulie na kusoma… kama kodi tu inakupiga
chenga kiasi cha kumtegemea Pamela hiyo karo utaiweza?.... okay! tukaishi na
Pamela…..unataka kuniambia Pamela atanisomesha?...it is my future we are
talking about….sio inshu ya wapi nitakaa, kula na kulala’ Jenifa naye
alijitetea.
‘Siamini umeamua kusurrender Jeni….’ Jerry alisikitika
‘sina uchaguzi mwingine…. naumia sana
kumpoteza mama….naumia zaidi kuwa nataka kumlamba miguu mtu aliyesababisha mama
apate hali ile iliyomtoa uhai….lakini nifanyeje?....ameshika mpini sisis
tumeshika makali…. huu ndio wakati wa kumuweka karibu adui yako upate
unachotaka…it is not a time kufight against her….we will lose Jerry….hatutafika
popote’ Jenifa aliongea kimsisitizo akirejea kuketi mbele ya kaka yake katika
kumshawishi ajiunge naye upande wake.
Jerry akakataa akakataa katakata
‘Nitafia mitaani Jeni…. kumtegemea Pamela ni tusi tosha
kwangu lakini kumsujudia Fiona ni zaidi ya tusi katika maisha yangu…. nakutakia
mema Jenifa kama unadhani ni bora kurejea nyumbani
kumtumikia Fiona…then well ni uamuzi wako ila kwangu I wont back off….Never’
Jerry alitoa msimamo wake na kunyanyuka, akiondoka na kuelekea nje.
Jenifa akamtazama mpaka aliporudishia mlango. Akabaki
mwenyewe pale sebuleni.
Akalia peke yake kwa muda, akiitazama picha ya mama yake
iliyokuwa kwenye meza ndogo hapo sebuleni.
Wiki chache zilizofuata, Jenifa alrudi nyumbani kwao,
akikubali masharti ya Fiona. Akapokelewa na maisha yakaanza. Maisha ya
unyeyekevu na utiifu kwa Fiona kwa mwezi mmoja tu yalitosha kumhakikishia
angeingia chuo mwkaa unaofuata, alinunuliwa gari na kupewa kila alilohitaji.
Fiona alimuweka Jenifa karibu yake zaidi kumkoga Kristus kuwa alikuwa mwanamke
bora kwake na kwamba alikuwa anawapenda watotot wake.
Mapenzi ya upofu yalimuonyesha Kristus kuwa hakukosea
kumchagua Fiona kuwa mkewe. akampenda maradufu!
Maisha ya Jerry na Pamela katika nyumba moja hayakuwa na amani hata kidogo. Jerry alilazimika
kuvumilia kumuona Pamela akitolewa outing na wanaume aliokuwa nao katika
uhusiano ilhali yeye Jerry alikuwa anampenda Pamela.
Aliumia sana
kumkosa Pamela na matarajio yake kuwa endapo wangeishi pamoja basi uhusiano wao
ungekuwa imara yalififia na kutoweka. Alijikuta katika jakamoyo kubwa la
kuvumilia asivyostahili kuvumilia huku Pamela akionekana kutojali hisia zake
kabisa.
Pamela aliung’ang’ania urafiki aliodhani ndio hasa ulipaswa
kuwepo kati yao na si mapenzi ya
wapendanao kama Jerry alivyotaka. Pamoja na misaada ya
hapa na pale, Pamela Okello alizidi kushikilia msimamo wake hata baada ya
kukutana kimwili na Jerry mata mbili zote bado Pamela alimuwekea Jerry vikwazo.
Uvumilivu ulipofikia kikomo Jerry aliondoka nyumbani kwa
Pamela na kwenda kuishi na rafiki yake Meddy akihisi pengine kule kumtegemea sana
Pamela andiko kulikomfanya Pamela amkatae. Maisha hayakuwa rahisi hata kidogo
changanya na mapenzi yake kwa Pamela Jerry alikuwa katika wakati mgumu zaidi.
Miezi michache baada ya kuondoka kwa Pamela, Jerry alifanya
jaribio la kusikitisha, alitaka kujiua! tukio lile lilimfikia Mzee Kristus
Agapela na mara moja katika maisha yake alijikuta akijiuliza ni nini alikuwa
anafanya! Kwa mara ya kwanza katika maisha yake hakumsikiliza Fiona alipomtaka
asimtembelee hospitali alikokuwa amelazwa akiondolewa sumu mwilini.
Kwa mara ya kwanza katika maisha yake alimkumbuka marehemu
Sophia, mara tu alipomuona Jerry akiwa mahututi hospitali na siku hiyo ndio
aliyolia machozi mbele ya kijana wake akiiona taswira ya Sophia!
Alipotoka Hospitali, Mzee Agapela alibadilia umiliki wa
kampuni yake ya mafuta ya Agape Oil na kuandika jina la Jerry. Akamkabidhi
mwanaye awe mmiliki na mkurugenzi na hapo ndipo vita ya Fiona kwa Jerry
ilipoanzia!.
Maisha yalibadilika ghafla, Jerry alibadilika pia, toka
kijana wa mtaani akisotea maisha mpaka kuwa Mkurugenzi wa kampuni ya mafuta.
Akamiliki nyumba yake, magari yake, vitega uchumi vyake na zaidi matumaini ya
kumpata Pamela Okello yalizidi kukua.
Alikosea! Pamela alizidi kumuweka karibu kama
rafiki na sio mpenzi! Kuimarika kwa Jerry hakukumfurahisha Fiona hata kidogo.
Alichunguza hili na lile na siku moja alimhoji Dennis Mazimbwe wakili wa
Agapela kuhusu aliyeandikwa katika usia na
Dennis akamjibu kuwa Jerry ndiye mrithi mkubwa. Alipewa jibu
lile pasipo ushahidi lakini alimuamini Dennis na alipochanganya akili yake na
ukweli kuwa Agape Oil ilikuwa chini ya umiliki wa Jerry, Fiona alihisi tonge lake
likimegwa na hatimaye kupokonywa!
Aliamua kulipigania!
Ukweli ulikuwa usia wa Kristus Agapela ulimtaja Fiona kama
mrithi wa robo tatu ya mali
zake zote. Ukweli huo ambao laiti tu Fiona angeliujua basi angelitulia na
kuishi maisha yake kwa amani ndio ulikuwa ukimuangamiza Fiona akitaka kupambana
kuikamata mali
ya Kristus, mume aliyekwanyua toka na rafiki yake kipenzi marehemu Sophia!
Uhusiano kati ya baba na wanawe ulizidi kushamiri na kumtisha
zaidi Fiona. Akawaamua kuwafarakanisha, na ufedhuli wake ulimfanya amtafute mtu
amfanyie kile alichotaka. Pesa mwanaharamu! Akampatia Jenifa gari jipya la
kisasa alilopewa na mumewe na kisha akampa kazi!
Kazi ya kuandika ujumbe mfupi katika simu ya Jerry kwenda
kwenye simu ya Fiona kuonyesha anamtaka kimapenzi. Akampa kila kitu cha
kuandika na Jenifa akamsaliti kaka yake na kufanya alivyoambiwa.
Kasheshe iliyoibuka hapo ilikuja kutulizwa na viongozi kadhaa
wa kanisa. Mzee Agapela alikaribia kumuua kijana wake kwa ghadhabu na Fiona
akichochea kwa kukaa kimya bila kuongea lolote akidai hataki kugimbanisha
familia ila ushahidi wa simu ndio uongee!
Jerry alijitetea sana
lakini ushahidi wa simu ulimfanya ajikute akimuomba masamaha baba yake kwa kosa
ambalo hakufanya. Kitendawili cha nani aliyemfanyia umafia huo kilibaki
kichwani mwake bila jibu!
Iliwachukua zaidi ya miezi sita kwa baba na kijana wake kukaa
meza moja na kupata chakula kama familia na ndio wakati
wakijaribu kurejesha mahusiano yao
katika mstari. Jerry akatoweka! akapotea! Baba akihisi ametekwa kwa ajili wa
watekaji kudai fidia na hilo halikutokea.
Alikuwa amekosea adui yake alikuwa mkewe!
Fiona alikuwa amemamua kummaliza Jerry baaada ya kuona mbinu
yake ya kuwafarakanisha imeshindwa. na wakati ule alikuwa akisheherekea kifo
cha Jerry! Alikuwa amekosea, Jerry alikuwa bado mzima wa afya!
Jerry alikuwa akihisi baba yake alikuwa abado hajamsamehe kwa
kosa ambalo hakulifanya na hakuwahi kufikiria kulifanya na ndio alitaka
kumuadhibu kwa kumuua. Alikuwa amekosea, adui yake alikuwa mama yake wa kambo!
.....SASA UMEJUA NI NINI KINAENDELEA KWENYE FAMILIA YA BALOZI MSTAAFU .....
No comments:
Post a Comment