Anayekuja pasina hodi, huondoka pasina kuaga
Wahenga hao, waliliona hili wakaona watuachie usia. Hii ni Methali ya kiswahili yenye nia ya kukukumbusha kuwa unapoparamia kitu si ajabu kikakuparama mwenyewe!
Mathalani umekuta watu wanaongea, katikati ya maongezi, usijue yameanzia watu na kuelekea wapi... unaingilia kati maongezi ya watu pasipo hata hodi upewe muhtasari! aibu sehemu ka ahii itakuhusu! na sijui kama utakumbuka hata kuaga!
Hivyo, ndugu yangu popote pale hodi lazima, ichukulie hii hodi kama kukijua kitu kabla ya kukiingia, itakuepusha na mengi mno na kikubwa ni aibu ya kuondoka bila kuaga!
Wasalaam!
No comments:
Post a Comment