Nyumba ya Darlie na Darin Routier
Yalikofanyika mauaji
June 6 mwaka 1996, polisi wa mji wa Rowlett ukoTexas
walipokea simu ya dharura toka nyumbani kwa familia ya Routier. Katika simu
hiyo Mwanamama Darlie Routier alikuwa akipiga kelele za hamaki na kudai yeye na
wanawe wawili wa kiume walikuwa wamevamiwa na kuchomwa visu na mvamizi na
kwamba watoto wake walikuwa wana hali mbaya ya kukaribia kukata roho.
Kelele zile za hamaki zilimuamsha mumewe aitwaye Darin
Routier ambaye alikuwa amelala ghorofani na mtoto mdoo aitwaye Drake, kwani ndio ilikuwa saa 2:30 usiku. Darin alikurupuka na kukimbilia sebuleni
ambako masaa machache kabla ya kwenda kulala alikuwa pamoja na mkewe na wanawe
wawili wa kiume wakitazama TV. Darin alipoingia pale sebuleni alishuhudia damu
ikiwa imetapakaa kwenye miili ya watoto wake wawili na mkewe.
Akiwa ametaharuki na pasipo hata kumuuliza mkewe aliyeonekana
kuchanganyikiwa kwa tukio lile, Darin alimuinamia mtoto wake Devon
(6) aliyekuwa hapumui na kujaribu kumpatia huduma ya kwanza kwa kuigandamiza
mikono yake kifuani pa mtoto wake na kukikanda kanda kile kifua ili kumrejeshea
uwezo wa kupumua, haikusaidia!
Darin alijaribu kumziba pua kwa viganja vyake kisha kupulizia
pumzi midomoni mwa Devon ambaye alikuwa bado hapumui
lakini damu nyingi ilimrukia Darin usoni
na wakati huo huo Damon (5) mtoto mwingine wa Darin akiwa na jeraha lililochimbika
kifuani alitapatapa kuitafuta pumzi.
Devon na Damon Routier
Enzi za uhai wao
Muda mfupi baadaye eneo la nyumba yao
lilijaa magari ya watoa huduma ya kwanza, waliofika na polisi. Wale watoa
huduma ya kwanza walikuwa wakihangaika kuokoa maisha ya watoto hawa huku polisi
wakijaribu kumtafuta huyo mvamizi ambaye kwa mujibu wa Darlie Routier alisema
alikuwa amekimbilia eneo la wanaloegesha gari lao (huku tunaita gereji lol) lililokuwa sehemu ya nyumba yao .
Askari polisi David
Waddell and sajenti Matthew Walling walikiona kisu kilichokuwa na damu juu ya
kabati fupi eneo la jikoni, pochi ndogo ya mkononi ya Darlie pamoja na kidani
aghali. Vitu vyote hivi vilikuwa karibu na kile kisu.
kulikuwa na mpasuko kwenye kioo cha dirisha la gereji pamoja na
matone ya damu sakafuni.
Watoa huduma ya kwanza hawakuweza kuwaokoa watoto wale,
majeraha waliyokuwa nayo yalikuwa makubwa mno. Kisu kilichotumika kuwachoma
kilizama ndani zaidi na kuchimba vifua vya watoto hawa kiasi cha kuchana mpaka
mapafu yao .
Walikufa vifo vya
maumivu makali sana . Majeraha ya
Darlie ambaye ni mama yao mzazi
hayakuwa makubwa kiasi cha kuhatarisha afya yake, yalionekana kuwa majeraha ya
kawaida sana wakati Darlie
alipokuwa akitoa maelezo ya tukio lile la kuogofya.
Majeraha ya Darlie
Darlie Routie akiwa amesimama ndani ya gauni
la kulalia lililokuwa limetota damu aliwaambia polisi kuwa anachokumbuka ni
kule kuvamiwa kwake na watoto wake basi. Alisema mvamizi aliingia ndani akiwa
amelala kwenye kochi na wanawe
wakiwa wamelala sakafuni huku luninga ikiendela kuwaka, alizinduka na kupiga
kelele huku kujaribu kupambana naye. Darlie alisema mvamizi yule alimjeruhi na
kukimbilia eneo la ‘gereji’ na hapo ndipo alipogundua watoto wake wawili
walikuwa walikuwa ndani ya dimbwi la damu
Akadai hakusikia kitu chochote wakati watoto
wake walipokuwa wakiuawa kwa kuchanwa na kisu kifuani. Alimuelezea mvamizi huyo
kama mtu mwenye urefu wa kadiri, aliyevalia T shirt na suruali vilivyokuwa na rangi nyeusi pamoja
na kofia aina ya Cap.
Darlie na Darin walipelekwa hospitali huku
nyuma Polisi wa Rowlett , Texas
waliifunga nyumba na kuanza uchunguzi.
Darlie, Devon, Damon na Darin kabla ya sakata
hapa alikosekana Drake....
UCHUNGUZI WAANZA….
Ndani ya siku kumi na moja tangu mauaji yae yafanyike. Polisi
wa Rowlett walimuweka chini ya ulinzi Darlie Routier kama
mtuhumiwa namba moja, pia wakimfungulia mashtaka ya mauaji ya watoto wake.
- Afisa
aliyezifanyia uchunguzi maiti zile Janice Townsend-Parchman alisema majeraha ya
watoto wale yalikuwa makali na yaliyochimba kuelekea ndani zaidi kulinganisha
na majeraha ya Darlie ambayo kuna uwezekano yalikuwa ya kujikwangua mwenyewe.
-
Mtoa huduma ya kwanza Larry Byford
alidai kuwa Darlie hakupata kuulizia hata hali ya watoto wake wakati walipokuwa
katika ‘Ambulance’. Alitiliwa mashaka hapa na ni kama
alishahitimisha kuwa wamekufa! ile hali ya kutoamini haikuwepo.
-
Tom Bevel, Mtaalamu wa damu
alisema, damu iliyokuwa katika gauni la kulalia la Darlie ilikuwa ya watoto
wake na kwamba ilikuwa kama iliyopuliziwa.
alifafanua kuwa ilionekaana kama iliyopuliziwa sababu ya
mruko wa damu ya watoto wake pale alipokuwa akiwashindilia kisu kwa nguvu
nyingi
-
Nesi katika hospitali
aliyohudumiwa Darlie alisema kuwa, Darlie hakuonekana kuwa mzazi mwenye kuguswa
na vifo vya watoto wake zaidi ya kujieleza kila mara kuwa alipomfuatilia yule
mvamizi (kulingana na madai yake) alikiona kisu na kakishika hivyo kuacha alama
za mikono yake katika kisu katika kisu
- Kitu
kingine kilichomtia hatiani Darlie ni damu iliyokutwa chini ya mashine ya kusafishia carpet (vacuum
cleaner) pamoja na kwenye mashine yenyewe ambayo inaonekana iliweka pale baada
ya tukio.
-
Charlie Linch, mtaalamu wa kutambua alama alisema haikuwa rahisi kwa mvamizi
huo kuondoka bila kuacha ahta mtone la damu, hii ni kutokana na kutoonekana kwa
damu yoyote nje ya nyumba ya Routier
Mpelelezi wa FBI Al Brantley, alitoa ushahidi
wake kwa kusema sehemu ya kioo kilichokatwa ilikuwa ni sehemu ambayo muuaji
angeweza kukiondoa pasipo haya kukivunja kioo. Pia, aliongeza kuwa kidani
aghali cha Darlie hakikuwa kimeguswa hivyo kuondoa dhana kwamba aliyewavamia
alikuwa ni mwizi. Kuna wakati Darlie alidai mvamizi yule alitaka kumbaka, na
kwa dai hili mpelelezi Brantley alidai kama nia ilikuwa ni kumbaka basi muuaji
angewatumia watoto wa Darlie kama mateka na si kuwaua ili kutimiza azma yake. Mwisho alidai kuwa
unyama waliofanyia watoto wale kwa maoni yake binafsi ni kuwa ni tendo
lililofanywa na mti aliyekuwa na hasira za hali ya juu dhidi yao
na sio mtu baki ambaye hakuwafahamu wale watoto.
- Darlie
aliposimama mbele ya jopo la wanasheria, aliulizwa kwanini alikuwa akitoa maelezo
tofauti tofauti kwa polisi, walimuhojii kuhusu mbwa wake ambaye hubwekea watu
asiowajua, kwamba ilikuwaje mbwa huyo hakubweka wakati mvamizi/ muuaji
alipowavamia na kuingia ndani. Walimuuliza kuhusu eneo la jiko lake
lililoonekana kufanyiwa usafi lakini
bado likakutwa na matone ya damu katika sehemu zilizojificha. Katika maswali
haya yote, Darlie Routier alikuwa akijibu kuwa hakumbuki ama hajui!
jopo la majaji lilimtia hatiani Darlie
Routier na kuhukumiwa kifo!
upande wa pili uliopingana na hukumu ya kesi ya Darlie ulidai ushahidi wa kimazingira
na nadharia ndio ulitumika zaidi kumtia hatiani Darlie. upande huu ulidai
hukumu haikuwa ya haki kwani kuna sehemu za ushahidi hazikujadiliwa na jopo la
waamuzi.
Darlie Routier
pamoja jitihada zote za familia yake kumuokoa
Anangoja hukumu ya kifo muda wowote kwa miaka 17 sasa!!
Mwanasheria aliyeendesha kesi ya Darlie alikuwa na mgongano
wa kimaslahi kwa vile alionana na Darin Routier (mumewe Darlie) na familia yake
na kuwataka kutofanya utetezi wa aina yoyote ambao ungemuweka Darin matatani.
Mwanasheria huyu alituhumiwa kuzuia kumalizika kwa ushahidi wa kisayansi
(Forensic Evidence) wenye nia ya kumtetea Darlie.
kulikuwa na alama za vidole vyenye damu kwenye sehemu ya meza
pale sebuleni, alama hizi za vidole hazikufanana na za Darlie, Darin, watoto
wala mtu yoyote wakiwemo polisi waliofika nyumbani kwa Routier kwa ajili ya uchunguzi.
Mkanganyiko huu ulikinzana na ushahidi ulioonyesha kuwa hakukuwa na alama za
vidole hata nje ya nyumba ya Routier.
UTETEZI WA DARLIE ULITAKA KUJUA
YAFUATAYO…..
-
Zile alama za vidole vyenye damu
mezani sebuleni, ni za nani?
-
Kulikuwa na alama hizo zilionekana
kwenye mlango wa ‘gereji’ ni za nani?
-
Suruali ya Jeans ya Darin ilikuwa
na damu, damu ile ni ya nani?
-
Kulikuwa na damu kwenye moja ya
mashati ya Darlie, ilifikaje kwenye shati na ni ya nani?’
-
unywele unaosemekana ni wa sehemu
za siri ulikuwa sebuleni wa Routier, unywele ule ni wa nani?
-
Darin Routier aliwahi kukiri
kujaribu utapeli wa bima ambao alipanga ufanyike kwa kisingizo cha kuibiwa
nyumbani. Alikiri kuwa alikuwa kati hatua za awali za kufanya hivyo na wizi huo
bandia ungetokea wakati ambapo kusingekuwa na mtu ndani. kukiri huku kwa Darin
hakukufikishwa mbele ya jopo la majaji
-
Video ya ‘birthday’ inayolenga kuzidi kumtia
hatia Darlie ilionyesha Darlie akicheza kwenye kaburi la mtoto wake pamoja na wanafamilia wengine
lakini video hii haikuonyesha mwanzo wa tukio ambapon alilia kwa uchungu juu ya
kaburi pamoja na mumewe Darin, kwanini kipengele hicho cha video hakikuonyeshwa
kwa jopo la majaji?
-
Baadhi ya majirani walidai kuona
gari jeusi mbele ya nyumba ya Routier wiki moja kabla ya mauaji. Jirani
mwingine alidai kuona gari hilo
hilo likiondoka eneo la tukio usiku
huo wa mauaji. Je taarifa hizi zilifanyiwa kazi?
-
kuna tuhuma kuwa polisi
hawakulinda ushahidi waliotoka nao nyumbani kwa Routier hivyonkuna uwezokano wa
kuharibiwa na kuzidi kumdidimiza Darlie. Tuhuma hizi hazikuthibitishwa.
- Zaidi
inadaiwa katika taarifa za awali, zinasema
kioo kilichovunjwa kilionekana kuvunjiwa kwa ndani lakini baadaye
ilionekana kilivunjwa toka nje. Watoa huduma ya kwanza walipowasili walidai
kumkuta Darin nje ya nyumba lakini ukweli ni kuwa Darin alikuwa ndani akiokoa
watoto wake.
Mwanaume aliyeonekana nje alikuwa ni nani?
na je ni kweli alionekana? Daktari
aliyemtibu Darlie alisema jeraha la Darlie shingoni alikuingia ndani
sababu lilizuiwa na mkufu aliokuwa amevaa. mkufu huo ndio ulioharibika na hivyo
kuzuia kisu kuzama ndani. Je jopo la majaji haliokuona jambo hili kama
jambo lenye uzito katika kesi hii. Mtu angewezaje kujidhuru namna ile.
Uchunguzi - wa kisayansi unaohusisha damu
haukufikia tamati wala kufikishwa mahakamani. Je ni kwanini na kwa maslahi ya
nani?
-
baadhi ya waandishi walijitokeza
kuwa upande wa Darlie lakini walikuwa wakizuiwa kuonana na Darlie.
Darlie na Darin Routier
walikuwa wapenzi tangu Darlie akiwa high school, mwaka 1988 walifunga ndoa mara
baada ya Darlie kumaliza shule. Mwaka 1989 walibarikiwa mtoto wao wa kwanza
Devon Rush Routier na mwaka 1991 walipata mtoto wao mwingine Damon Christian
Routier, kisha baadaye walibarikiwa tena kupata mtoto wa mwisho Drake ambaye
wakati wa mauaji alikuwa amelala na baba yake.
Kwa kadiri familia yao iliyokuwa ikiongezeka, ndivyo pia biashara ya Darin
iliyohusiana na Computer ilivyozidi kushamiri. Familia ikahamia sehemu nzuri
ijulikanayo kama Dalrock Heights Addition in Rowlett , Texas . maisha yao yalikuwa mazuri mno kiasi cha kuweza kuzungukwa na
vitu vyenye thamani kubwa kama nyumba kubwa, samani, nguo na vidani vyaa gharama, vacation
mbalimbali huku pia wakimiliki gari jipya aina ya jaguar pamoja na boti ya
kifahari.
Miaka michache baada ya kuishi maisha ya kifahari, biashara
ya Darin ilianza kwenda kombo na matatizo ya kifedha kuanza kuwakabili. Uvumi
ukaanza kuenena kuwa wanandoa hawa walikuwa katika matatizo ikiwemo suala wa
kuwa na wapenzi nje ya ndoa yao .
Kwamba Darlie alikuwa akiuchukia muonekano wake na hakuwa na ustahimilivu na
watoto. Pamoja na uvumi wote huo 1995, Darlie na Darin walipata mtoto wao wa
tatu aitwaye Drake. Baada ya uzazi huu Darlie alipata msongo utokanao na uzazi
(postpartum depression).
Darlie akaanza kuhangaika kupunguza unene alioupata kipindi
cha ujauzito, kuhangaika uko kukapelekea aanze kutumia vidonge vya diet abavyo
havikumsaidia zaidi ya kumletea mkanganyiko wa hisia. aliwahi kumweleza Darin
kuhusu kutaka kujiua. May 3, 1996 Darin alimfuma mkewe akilia hukua akiandika katika Diary yake... alichokiandika kipo kwenye kumbukumbu
"Devon, Damon and Drake, I hope you will forgive me for what I am about to do. My life has been such a hard fight for a long time, and I just can't find the strength to keep fighting anymore. I love you three more than anything else in this world and I want all three of you to be healthy and happy and I don't want you to see a miserable person every time you look at me..."
Darin akaamua kuketi chini na kuzungumzia matatizo yao
na yajayo. mambo yakaonekana kuanza kutulia bila kujua janga lililokuwa
linawanyemelea mwezi mmoja baadaye.
Darlie na wanawe watatu.....
KWA SASA HALI IKOJE….
Darlie bado yupo jela, akisubiri hukumu yake ya kifo mara baada ya rufaa zake kushindwa. Anasema anaumia
Amekuwa mtu mzima sasa...Almost 43 yrs old!
Baada ya kusimama na mkewe pamoja akimtetea kama mkewe, Mwaka 2011 baada ya miaka 15 tangu mkewe aingie matatani Darin alimtaliki mkewe rasmi. Ingawa amemtaliki mkewe Darin amesema hategemei kuoa tena maishani mwake wala hataacha kumpigania mkewe anayeamini kuwa hana hatia.
Darin Routier hivi sasa
Drake Router ambaye kwa kiasi kikubwa amelelewa na wazazi wa mama
yake ni kijana mkubwa sana sasa
hivi. Drake alikuwa mdogo mno wakati mauaji yakitendeka na salama yake ilikuwa
ni kulala na baba yake kule ghorofani. Darlie alizuiwa kumkaribia Drake kwa
miaka kadhaa. ingawa aliruhusiwa baadaye kumtembelea mama yake, Drake amefanya
hivyo mara chache sana na hili lina
muumiza mo mama yake.
Drake Routier sasa hivi
huyu ndiye aliyenusurika akiwa amelala na baba yake
JE NI KWELI HUYU MAMA ALIWAUA WANAWE KIKATILI VILE?..... KAMA
HAPANA NI NANI SASA NA KWANINI KUWE NA VIJIUSHAHIDI VYENYE KUMBANA DARLIE?.....AU DARIN PIA ANAHUSIKA?.... NI SIRI GANI IMEFICHIKA HAPA?....
Aliingia jela akiwa na miaka 26 tu….mpaka leo amegonga miaka
40 Darlie anasota kwenye kichumba kidogo akilala na kuamka huku akiwazia kifo
cha sumu kinachongoja saini moja na kuhitimika!
MWISHO!
SOURCE: MITANDAO MBALIMBALI
TAFSIRI: LAURA PETTIE
No comments:
Post a Comment