19
Patrick Mazimbwe alisimama akiwatazama binadamu hawa wawili
kama viumbe vilivyotokea sayari nyingine. Alijikuta akitaka kuzungumza na kunyamaza
kwa wakati mmoja na pengine alitamani hata kuimba ila ndio kwa wakati ule
mifumo ya fahamu ilishatawanyika kila mfumo na njia yake, akabaki mwenyewe tu
na akili za kukodoa macho. Kufumania kipaji si kila mtu anahimilia vishindo!
Pamela alikuwa wa kwanza kumsukumia mbali Jerry, akiwa
anameza mate kwa juhudi mithili ya mtu aliyelazimishwa kumeza vipande vya mawe.
Alitaka kujiteteta kwa sauti ya kupaa lakini sauti yake ilimsaliti na ikamfanya
aachame midomo yake na kuimwemwesa pasipo kumudu hata kumuita Patrick kwa jina
lake.
Kwa kujua ameingilia shughuli ya watu, Patrick akageuka na
kuutanua mlango kisha akajitoma nje asizungumze hata neno moja kuikaripia ile
hali aliyoikuta. Pamela sasa nguvu ya kunyanyuka toka pale sofani ikamvaa
kimiujiza, akajikuta anatoka mbio almanusura ajigonge kwenye meza iliyokuwa
mbele yake. Akatoka nje akiliita jina la Patrick kwa sauti kubwa na kusihi.
Huku ndani Jerry bado alikuwa pale sofani akiwa kama mtu
aliyepigwa na bumbuwazi. Alitikisa
kichwa kulia na kushoto katika namna ya kutoamini na kushindwa kujua baada ya lile
tukio ni nini kingefuata.
Alikuwa anamjua Patrick kama mpenzi wa Pamela nay eye
mwenyewe alishatambulishwa kwa Pat kama rafiki wa karibu mwenyewe Pamela
akienda mbali na kuhitimisha utambulisho kwa cheo cha ukaka wa hiari. Kukutwa
katika hali ile kulimfanya ajione zoba kwelikweli mbele ya Patrick ambaye kwa
kuondoka bila kutia neno ndio kabisa aliwafanya wagoni wake watahayari!
Aliwasikia Pamela na Patrick wakijibizana uko nje lakini
hakuthubutu kutoka, alibaki pale sofani kama mtu aliyekalia gundi ya maji.
Wakati akiwaza na kuwazua, mlango ukatanuliwa tena na Pamela akaingia
akionekana kuchanganyikiwa zaidi ya alivyotoka. Uso wake ulikuwa umelowa
machozi na mwili ulionekana kunyong’onyea kupitiliza. Akasimama katikati ya
sebule yake akimtazama Jerry na siongee neno lolote.
‘Get out!’ akamuamrisha kwa sauti ya kinyonge, sauti
iliyoashiria kwa wakati ule alitaka kubaki mwenyewe nap engine iliashiria
hakutaka kuulizwa lolote wala kujadili lolote. Jerry aliliona hili lakini
hakutaka kulitii. Alisimama na kumsogelea Pamela
‘Nitazungumza na Partick’ akajibebesha mzigo
‘Toka nje…’ Pamela akaamrisha tena safari hii sauti akipaa
kwa ukali na mwili wake ukitetemeka
‘Pamela mimi ndio chanzo cha yote haya…’ Jerry alizidi kutaka
kuubeba ule mzigo lakini Pamela alionyesha dhahiri kutotaka kumsikiliza,
akampita na kuelekea chumbani kwake akiubamiza mlango wa chumbani kwa nguvu
zote kiasi cha Jerry kushtuka.
Mwanaume akasimama pale asijue atoke na kwenda zake ama amfuate
Pamela na kumtuliza. Kwa Sekunde kadhaa halmashauri ya kichwa chake ikamtaka
aondoke kuepusha shari zaidi lakini katibu mwenezi wa moyo wake akamshupalia na
wazo la kumfuata Pamela chumbani. Akapiga hatua mpaka mlangoni na kusimama pale
kwa sekunde kadhaa kabla ya kuamua kugeuza njia na kumfuata Pamela chumbani.
Alipoufungua mlango kwa kukinyonga kitasa na kuusukumia
mbele, alitanguliza kichwa kwanza na kumchungulia. Pamela alikuwa ameketi
kitandani akilia huku simu ikiwa sikioni, Alikuwa akimbembeleza Patrick kwa
kuzungumza huku akilia. Alikatiwa simu na akahangaikia tena kuipiga ile simu.
Jerry akamfuata kwa kasi na kumnyang’anya ile simu. Kitendo
kile kilifanya Pamela amrushie vibao Jerry ambaye alividhibiti kwa kumkumbatia
Pamela kwa nguvu zote mpaka alipotulia na kulia kifuani pa Jerry kwa kwikwi na
hasira nyingi.
‘Pam I know how you feel…I know…. but trust me…Pat hawezi
kukusikiliza now…. pull yourself together…. Pamela!’ Jerry aliongea akiwa
ameshikilia mashavu ya Pamela na kuuinua uso wake ili amtazame. Alijisikia
vibaya mno kuona mwanmke anayempenda akilia vile kwa kuhamanika na zaidi yeye
akiwa chanzo. Alitaka kwanza kumuweka sawa Pamela ambaye aliitikia kwa kichwa
lakini machozi yakizidi kumtoka.
‘I love Pat…I love him…cant stand losing him jamani’ Pamela
alilalamika kwa uchungu bila kujua ni kiasi gani kauli ile ilimuumiza Jerry.
‘Okay…lakini ana hasira sasa…unapozidi kumtafuta ndio unazidi
kumfanya akasirike…I’m a man na najua atakavyokuwa anajisikia…. huwezi pata
suluhisho muda huu…. unanielewa’ Jerry alijaribu tena kumtoa Pamela katika ile
hali ya kuchanganyikiwa.
‘amesema nisimtafute tena…amesema hataki kuniona’ Pamela sasa
alianza kueleza alichoelezwa na Patrick, rafiki yake wa kiume wa mwaka mmoja
sasa ambaye ndiye haswa aliyekuwa ameshapanga naye kufunga ndoa. Mwanaume
ambaye moyo wake na akili zake
zilishafikia uamuzi wa kutulia naye sit u kwa mapenzi aliyokuwa anampa
bali pia kwa uwezo wake kifedha na kule kumhudumia kwa kila alichotaka. Pamela
aliona bahati yake ilikuwa imetumbukia nyongo.
Jerry alifanya kazi ya ziada kumtruliza Pamela ambaye
hatimaye alitulia na kuweka kufikiri kwa umakini bila taharuki ya kuachwa.
Wakaagana na Jerry akaondoka zake. Usiku ule Pamela alihangaika kujizuia
kutoigusa simu yake na kumtafuta Patrick, alijaribu kuufuata ushauri wa Jerry
na akaweza!
Kuna kitu walikisahau, kitu kikubwa mno!...Patrick alikuwa amemuona
Jerry Agapela ambaye alisharipotiwa kutafutwa kila kona…kwa wakati ule hamaniko
lao halikuwafanya wagundue hili haraka, wala halikuwapitia akilini haraka!
888888888888888888888888
Sindi Nalela alishapanda kitandani kulala, wakati aliposikia
Jamila akimuita mlangoni. Akaamka na kuwasha taa kisha kafungua mlango ili
kumsikiliza Jamila.
‘Umeshalala?’ Jamila akamuuliza uso ukiwa na dalili zote za
kutaka kuingia ndani ya chumba chake
‘Ndio nilikuwa najiweka kitandani…vipi kwani?’ Sindi akauliza
akiutanua mlango zaidi ili Jamila aingie ndani, naye kama mtu aliyekuwa
anangoja kuruhusiwa kuingia, akajitoma ndani na kujikaribisha kwenye sofa,
akimtazama Sindi aliyekuwa anafunga mlango wake kwa ufunguo na komeo. Akatoka
mlangoni na kuja kujiweka kwenye kitandani akipiga muhayo mrefu na kumtumbulia
macho Jamila.
‘Ndio unarudi?’ Sindi akamuuliza baada ya kugundua Jamila
alikuwa bado katika yale mavazi ya kutokea. Jamila akajibu kwa kutikisa kichwa
na hapo hapo akimkodolea macho Sindi, Umbeya ulikuwa umemkaba kupitiliza. Njia
nzima alitembea akijikwaa sababu ya kile alichokiona na alitaka sana kufika
aendako ili amuweke Sindi chini kama hivi alivyomuweka.
‘Jerry yuko wapi?’ akamuuliza Sindi kwa pupa
‘Mmm, ameenda kazini…’ Sindi akajibu akionyesha wasiwasi
‘Kazini kwake ni wapi?’ Jamila akauliza kama mtu aliyetaka
uhakika wa habari Fulani aliyokuwa nayo na ndio akazidi kumfanya Sindi
achahatike bila mpango
‘Sijui….naa vibarua vyake uko…sijui wapi kwa kweli ila ndio
ana shifti zake mara usiku mara asubuhi’ akajibu Sindi akimkazia macho Jamiala
na akitamani kumuwashia na tochi ili amuone vizuri na ile hamaki aliyoingia
nayo.
‘Kwani vipi?’ Sindi akauliza mwenyewe akihema kwanza na akimtazama Jamila aliyekuwa
amejiinamia ghafla na kuguna.
‘Mwenzangu…. mjini hapa dada kunamambo ukiyaona unaweza
kuzimia mbele ya umati wa watu wallah’ akamfumba fumba maneno akimuacha Sindi
njia panda.
‘Kwani imekuwaje?’ Sindi sasa alitoka kitandani na kuja
kuketi kwenye lile sofa alilokalia Jamila
‘Nimemuona mtu kama Jerry akishuka kwenye gari hizi zimeingia
sana siku hizi…’ Jamila akajieleza na Sindi akashindwa kumuelewa haraka
‘Gari gani?’ akauliza Sindi utadhani alijuanaiana za magari
mjini
‘Eeh jamaini gari gani hizi sijui….zinaitwaje sijui…gari
f’lani za gharama kwelikweli…. ziko juu juu hivi’ maelezo yake wala hayakumpa
picha Sindi ya nini alitaka kuzunngumzia
‘Labda gari la bozi wake’ Sindi akajaribu kurahisisha
maongezi
‘Alikuwa nayendesha mwenyewe…na alivyokuwa amevaa….hapana
dada yaani kwanza nilitaka kusema niemmfananisha ila ni Jerry huyu huyu
jamani…alikuwa anaingia New Afrika hoteli pale…. shost huyu bwana unamjua
vizuri maana mi leo kidogo nigongwe na gari nikiyashangaa haya mambo’ Jamiala
akajieleza na Sindi akajikuta akicheka kwa sauti kwanza kama mtu aliyekuwa
akisimuliwa maajabu ya dunia.
‘Hapaba sio Jerry…kwanza hana gari, pili uko mahotelini
mmmh….’ Sindi akakanusha
‘Sindi nimemuona kwa macho yangu…. amevaa shati la mikoo
mifupi…kachomekea mkanda nje…kiatu chini na saa zile za bei… hpana ni yeye
nimemuona jamani’ Jamila akatetea alichoona lakini Sindi akampinga zaiid na
zaidi akidai duniani wawili wawili.
Mwisho wa yote Jamila akakubali kwa shingo upande kuwa
pengine alifananisha. akaga akaondoka. Sindi alipobaki mwenyewe akatulia na
kutafakari maneno ya Jamila, hakuona ukweli wowote wa kuulinganisha na Jerry
anayemjua. akapanda kitandani na kulala.
Jamila hakukosea, aliyemuona alikuwa Jerry mwenyewe, Jerry
Agapela! Muda huo aliomuona ndio muda aliokuwa akielekea New Afrika hotel
kupata chakula cha jioni na kubadilia nguo kisha kuelekea kwa Pamela, baada ya
kutoka kwa Pamela ambako aliacha sekeseke la kutosha Jerry alichoma mafuta
kurejea New Afrika hotel kulala.
Mbali na Jamila, kuna mtu mwingine alikuwa amemuona, mtu
mwingine ambaye hakutarajia kumuona Jerry eneo kama lile katika hali kama ile.
Jenifa agapela mdogo wake alikuwa amemuona kaka yake wakati akiwa nje ya hoteli
ile ndani ya gari la mwanaume aliyefika naye hapo. alimuona kaka yake akitoka
nje ya hotel na kuingia garini. Kwanza alipiga yowe kibwa mule ndani ya gari
akijaribu kumuonyesha yule boyfriend wake alichokiona lakini ikawa amechelewa
na Jerry alishaingia ndani ya gari.
Jenifa usiku huu alikuwa chumbani kwake akiwa mwenye hofu,
mwenye mtihani na mwenye kuchanganyikiwa. Alikuwa amemuona Jerry kabisa,
alishindwa kuamua amueleze baba yake kuhusu alichokiona ama amueleze mama yake
wa kambo kwanza. Alitulia akiwa amekumbatia mto wake na kukodoa macho yake
ukutani kama mtu aliyekuwa akitafuta majibu ya mtiririko wa mswali yake ukutani
hapo.
Akakata shauri kumweleza Fiona kwanza!
....TWENDE KAZI....
Dada we noma.... wapi naweza kukuona sister
ReplyDelete