N!XAU GCAO COMA..... The starring himself
hii ni mwaka 2003...mwaka aliofariki
TUMJUE KWANZA N!XAU
N!xau (matamshi yake mpaka leo ni utata but wanasema
linatamka Gcao Coma, maana unaita kisha unashangaa, (huo mshangao ni silabi
inayotamka kikao) halafu unamalizia na jina…what a name!...tried to make mine
L!?ura Lol!). N!xau alizaliwa mwaka 1943 lakini inasemekana yeye mwenyewe
alikuwa hajui umri wake halisi. Alizaliwa uko Tsumkwe, nchini Namibia
akitokea kabila la San ambalo ndilo kabila linalojulikana kama
Bushmen, jamii ya wafugaji wanaoishi maisha ya ujima.
wana sema etiiii alifanana saaana na Usher Raymond
hahahahahaaa
Kabla ya kuingia katika ulimwengu wa filamu, ulimwengu wa
kisasa uliojaa teknolojia na mambo mengine ya kizungu. N!xau alikuwa mkulima,
na katika maisha yake hakuwahi kutembelea miji mikubwa yenye magari na majumba
ya ghorofa. Alizoea kuona nyumba za nyasi kijijini kwao, alikuwa amekutana na
wazungu watatu tu lakini kali kuliko zote ni kuwa hakuwa anaijua thamani ya
pesa, kama vile alivyoigiza kuzitupa pesa katika filamu
yake…na katika maisha yake halisi N!xau hakuithamini pesa kwani alikozaliwa na
kukulia, jamii yake haikujua pesa ni ina thamani gani.
Pato lake la kwanza katika filamu yake ya kwanza The Gods
must be crazy lilipotea tu bila kufanya chochote, lakini baada ya kusaidia
kujua anaweza kufanya nini kwa kutumia pesa anayopewa. N!xau alifanya makubwa
na hapo ndipo akaanza kunegotiate mamilioni ya pesa kwa ajili ya kucheza filamu
za hao jamaa!….! kumbe hizi mbio za kukimbizia haya makaratasi a.k.a kazileta mzungu..ona sasa mbio haziishi
duniani!
N!xau alicheza filamu zipatazo saba…. The Gods Must Be Crazy (1980), The Gods Must Be Crazy II (1988), Kwacca Strikes Back (1990), Crazy Safari (1991), Crazy Hong
Kong (1993), The Gods Must be Funny in China (1994) na Sekai Ururun Taizaiki (1996)
Aliianza kazi ya uigizaji mwaka 1980 na kuhitimisha rasmi
mwaka 1994 ingawa mwaka 1996 alishiriki filamu ambayo hakuwa muigizaji mkuu
(lead actor).
Alipomaliza kazi yake ya kuigiza, N!xau alirejea Namibia
akajenga nyumba ya matofali aliyoiwekea umeme na maji, akarejea katika ukulima
sasa akimiliki ng’ombe kadhaa na mashamba, pia alikuwa na gari ambalo aliajiri
dereva wa kumuendesha. Pamoja na kupata upeo wa namna ulimwengu wa upande wa
pili ulivyo, N!xau alijifunza kunywa pombe na kuvuta sigara, mambo mabaya
aliyoyapata katika utandawazi.
N!xau aliacha wake zake watatu na watoto 12.
FILAMU YENYEWE SASA....
Nadhani wengi tunaijua hii movie aisee…. imaigiziwa Botswana ila na kampuni toka South Africa
Starring akiwa mnamibia mkulima wa jamii ya Bushmen
kama
utaiangalia mwanzo mwisho bila kucheka, mwenzangu tafuta hospitali wakacheki kama
bandamo yako bado ipo… ni stori yenye pande tatu….
Starring akiwa mnamibia mkulima wa jamii ya Bushmen
1…. N!xau au Xi kama anavyojulikana
katika movie. Siku moja rubani anadondosha chupa ya cocacola toka angani na Xi
analiona tukio hili. Kwa kutokujua chupa ni nini anaipeleka kwa jamii yake uko
kijijini. Kufika ule chupa inaleta mzozo mkali na mifarakano maana kila mtu
anataka atumie…huyu anatwangia….yule anasagia basi tafrani
hizo kazi za chupa....kwenye movie utacheka ufe.....
Ukoo unakaa na kuamua kuirudisha chupa kwa miungu(uko
ilikotoka) ili kuepusha mifarakano zaidi. Xi anatumwa akaitupe mwisho wa dunia
na safari inaanza….
2. …kuna biologist anaitwa Andrew Steyn (Marius Weyers)
hahahahaaaaa acha nicheke kwanza maana the man is real fuuuuuunnnny
kha!....huyu jamaa bwana na aibu zake anatumwa kumpokea kate Thompson (Sandra
Prinsloo)….uwiii the whole safari balaaa… unakumbuka wakati anafungua geti la
mpaka….au wakati wanafukuzwa na viboko ule usiku hahahahahaaaa…..acha hiyo
alipompelekea viatu vyake darasani kule LOL!!!.... sijamsahau Mpudi rafiki wa
Andrew…. huyu quote yake moja iliniacha hoi nab ado ipo kichwani “I know how to marry them. Nobody knows how to live
with them”
hahahahahaaa ndio safari inaanza.... hata nusu ya vituko bado
3. ….kundi la waasi likiongozwa na Sam Boga (Michael Thys).
Wakateka wanafunzi na mwalimu Kate, hapo
wameshafanya mauaji kwenye kikao cha Rais na mawaziri kisha wakakimbilia
porini. Wakawaburuta wanafunzi mpaka uko porini na kuamrisha waletewe chakula
la sivyo wanateketeza kila kitu….
Sam Boga na kundi lake.... Kuubwa la maadui
kuna matukio ya kuchekesha sana
humu ndani…. lets catch some funniest moments….
Nilicheka mpaka kichwa kinauma....
.......'amai vachauayaa amai chauyaaa...woya woya woyaa' lol! sijui lugha gani hii ila dah!
mie huo ugali unaopikwa hapo najiuliza tu ni wa mtu mmoja
hahahahahaaa....
na Movie inafikia tamati pale Xi anapofanikiwa kufika katika hili korongo
akiamini kuwa ni mwisho wa dunia...Xi anaitupa ile chupa na kurejea kwake
Apokelewa na familia yake na kuanza kuwasimulia vimbwanga vya wazungu na watu wa mjini
HOPE UMEBURUDIKA KIDOGO EEH...
UKARELAX!
nimeipenda hii kona ya filamu keep it up!
ReplyDelete