Heri
ya mwaka mpya msomaji!
Haya sasa Mwaka mapya na
mambo mapya. Laura Pettie Blog sasa itakuletea kipengele cha darasa kila siku
ya ijumaa. Lengo la kipengele hiki ni kujifunza mengi kuhusu Lugha na tamaduni
za wenzetu.
Kama ambavyo Motto wa
blog yetu ni ‘KUISHI NI KUJIFUNZA’…. Hivyo tunakuletea darasa la
utu uzimani ili upate kupanua upeo zaidi na ujifunze zaidi… Mnasemaje
wadau? LIWEPO AU LISIWEPO? Mkiona halifai tutaliacha hakuna tatizo!
KWA KUANZA DARASA LEO.
TUNAANZA NA LUGHA YA KIFARANSA…
Tutajifunza salamu na
maneno machache ya kuanzia… ukitoka hapa lazima uwe nusu mfaransa hahahahaa.
Kifaransa ni lugha ya mahaba. Raha sana ukiijulia na ukitaka kuifurahia basi
upate bahati ya kuwasikia watangazaji wanaotumia kifaransa wakibubujisha maneno
yao haraka haraka… utawapenda! moja kati ya watu walionivutia nijifunze
kifaransa ni mwanadada Angelique Kidjo! wakati ule akitangaza tuzo za Kora...
Utasema wana mafua hivi,
halafu kama wanabembeleza kisha kama wanakazia maneno halafu haoooo wanateleza
tena. Ni lugha inayokadiriwa kuzungumzwa na watu karibu milioni 338
ulimwenguni!... wanasema ni lugha ya tatu barani ulaya baada ya kiingereza na
kifaransa.
Kifaransa
ni lugha rasmi Katika baadhi ya nchi za Afrika na hivi dunia imekuwa kama
kijiji kimoja. Si haba ukijua lugha tofauti tofauti. Wala huitaji kuwa mtaalamu
kile cha kuombea maji kinatosha kabisaaa!
Tunanze
na salamu kwanza na maneno madogo madogo...kisha nitakuwekea na namna ya
kutamka ili kukuwezesha kujifunza matamshi wewe mwenyewe. twende kazi.
TUNASALIMIANA....
1.
BONJOUR....
Hello, Good morning
Habari za asubuhi!
2. BON
APRES MIDI...
Good afternoon
Habari za mchana!
3.
BONSOIR
Good evening/night
Habari za usiku!
4.
SALUT!.... hii ni salamu informal ikitumiwa zaidi na watu wa rika moja au
vijana zaidi.
Hi!
Mambo!
5.
BIENVENUE!
Welcome
Karibu!
TUNAAGANA!
6.
BONNE journée ...
Good day
Siku
njema!
7. BONNE soirée
Good
evening/ night
Jioni
njema/ usiku mwema!
8. BONNE nuit
Good night
Usiku
mwema!
9. AU REVOIR
Goodbye
Kwaheri!
10. À BIENTÔT
See
you soon! see you later
Tutaonana karibuni/ baadaye!
TUNASHUKURU
11. MERCI
thank you
Asante!
ukiongeza neno
'Beaucoup' inakuwa Merci beaucoup, hii ina maana thank you so much...
Asante sana!
TUNAPONGEZA
12. FELICITATIONS
Congratulations
Hongera!
13. BONNE CHANCE
Good
luck
kila
la kheri!
SOMO LINAENDELEA....
Kumbuka ukimsalimia mtu
Bonjour naye atakujibu Bonjour!... vivyo hivyo kwa salamu zingine pia.
mfano. LAURA: Bonjour
Ndimaso
NDIMASO: Bonjour Laura!
umeelewa
hapo!...sijasomea ualimu hivyo kama hujaelewa ndio ujue sio fani yangu hii LOL!
Sasa.... katika salamu
kuna zile title za watu. huyu ni Mr. yule ni Miss na kadhalika. hebu tuone
inakuwaje.
Mr. / Bwana..... inakuwa
MONSIEUR
Miss/ Bi...... inakuwa
MADEMOISELLE usiogope utaweza tu kuitamka ni rahisi tu!
Madam.... inakuwa
MADAME!
mfano, LAURA: Bonjour
Monsieur Ndimaso!
NDIMASO: Bonjour Madame/ Mademoiselle Laura
umeona hapo! umeelewa
eeh! haya tuendelee.
sasa umesalimia bonjour
ukajibiwa bonjour. Kiswahili tunakuja na ile hujambo, mnaendeleje na
kadhalika...
COMMENT ÇA VA? ... ni kama how is it? how
are you?...
na wewe
unajibu 'ÇA VA' na kama ni mambo uko poa saaana unajibu ÇA
VA TRES BIEN! ... wakati mwingine kwa mtu wa roka moja hivi unakuwa
informal tu kwa kumuuliza ÇA VA? naye anajibu ca va...
au ca va tres bien!
au
nauliza COMMENT VAS-TU?... nikiwa na how is it going? how are you? au
unaendeleaje?
ukiulizwa hivi unajibu
...JE VAIS BIEN ... kama unaendelea poa sana basi unatupia Je vais
tres bien.... UPO? lakini pia unaweza jibu Ça va!
Mfano:
LAURA: Bonjour Monsieur
Ndimaso!
NDIMASO: Bonjour Madame/
Mademoiselle Laura
LAURA:
Comment Ça va?
NDIMASO: Ça va!/ .....Ça va tres bien!
upooooo? umeelewa
kidogo? au bado?...wapi hujaelewa sasa?
sasa ngoja nikupe
matamshi! tufunge siku ya leo.
JEDWALI LA
KWANZA......hapa kuna vowels na consonants!
JEDWALI LA PILI.... hizi ni nasal vowel. ukizitamka ni kama unazitamkia puani vile!
Mfano. BONSOIR.... ile salamu ya jioni/ usiku
UTAITAMKA BON-SWA na bon utaitamkia puani kidogo
kwasababu
1. kwenye Bon kuna 'on' ambayo ni nasal vowel...cheki jedwali la pili mstari wa chini!
2. kwenye soir kuna oi ambayo inatamkwa WA.... cheki jedwali la kwanza mstari wa pili mwishoni.
umeona?.... so umepata namna ya kutamka BONSOIR!
natumaini kuna kitu umeambulia kwenye somo la leo. kama hujaelewa kabisa basi niwie radhi ni ile mimi sio mwalimu na sina kipaji cha ualimu basi tu najaribu kukuletea kile ninachokijua au nilichokijua ili tujifunze pamoja.
i stand to be corrected...
AU REVOIR MES AMIES!!
Hongera madame, kweli kuishi ni kujifunza.
ReplyDeleteMaana hii ni ya muda ila leo imekuwa msaada kwangu.
Merci Beaucoup
Merci beaucoup madame et mei je peux parler français
ReplyDeletesafi
ReplyDeleteMerci
ReplyDelete