14
Mara baada ya kumaliza kufundisha darasa lake, Sindi alibaki
darasani, kwenye kile kiti chake kama mwalimu, akiwa
ameegesha viwiko vyake juu ya meza iliyokuwa mbele yake na mikono yake ikiwa
imeshikana na kumfanyia egemeo la paji lake la uso. Alikuwa akilia kimya kimya.
Alipotulia na kunyanyua kichwa chake, akafuta machozi kwa
viganja vyake na kujaribu kujiweka sawa lakini huzuni ilimtembelea tena
akajikuta akijiiinamia na kuanza upya kulia.
Alilia mpaka pale alipohisi vishindo vya miguu vikisikika kuelekea
pale alipokuwa. Akanyanyua kichwa na kugeuka kutazama mlangoni, akianzia
miguuni mpaka usoni pa yule mtu aliyekuwa amesimama pale mlangoni.
Wakatazamana!
Ni kama vile ujio wa yule mtu ulimuongezea uchungu, akageuka
na kumpa mgongo, sasa akilia kwa sauti na hisia huku kwikwi za kilio zikipamba
moto na kufanya mabega yake kupanda na kushuka kufuata mirindimo ya kwikwi
zake.
Nyanza aliyekuwa mlangoni hakumsogelea, wala hakupiga hata
hatua moja kumkaribia achilia mbali kumgusa. Aliendelea kusimama pale
akimtazama Sindi alivyokuwa analia na asitamke chochote.
Akageuka taratibu na kuanza kuondoka eneo lile, Sindi
akanyamaza ghafla na kugeuka kutazama mlangoni mara tu aliposikia hatua
zikipigwa kuelekea mbali na lile darasa. Akanyanyuka kwa pupa kidogo, akigonga
meza ile iliyokuwa mbele yake na kuangusha baadhi ya vitu vilivyokuwa juu ya
ile meza, hakuokota alivyoangusha, alitoka kwa kasi na kukimbilia nje.
Alimuona Nyanza akitembea haraka akiliacha eneo lile na
kukamata njia nyembamba iliyotengenezwa na miguu na matairi ta baiskeli. Sindi akakaza
miguu Kumharakia huku akiliita jina la
Nyanza ambaye hakugeuka wala hakusimama.
Sindi alipomfikia alimkumbatia Nyanza kwa nyuma, mikono yake
ikikutana mbele ya tumbo la Nyanza. Kitendo kile kilimfanya Nyanza asipige
hatua nyingine zaidi ya kusimama kama nguzo,
akimsikilizia Sindi aliyekuwa analia nyuma yake. Nyanza akauma meno na kusigina
magego yake kwa nguvu. Machozi yalikuwa yanamlenga lakini alipigana kiume
kuyazuia kutoteremka.
Alitulia vile kwa muda tu, kabla ya kutumia nguvu kidogo
kuitanua mikono ya Sindi na kutaka kujitoa mikononi mwake, lakini Sindi
aliikaza mikono yake kwa nguvu yake na kufanya Nyanza ahairishe zoezi lake.
‘Kwanini?....hujawahi kuniambia Sindi…kwanini? Nyanza
aliongea kwa uchungu
Sindi hakujibu bado alikuwa analia. Nyanza akaushika mkono wa
kulia wa Sindi na kuuvuta kiasi cha kumleta Sindi mbele yake. Macho yake
yalikuwa yamejaa machozi na uso mzima uliloa machozi ambayo hayakukoma.
‘Sindi!...’ akamuita kwa upole huku wakitazamana
‘Ni kweli?’ akataka uhakika. ‘….nataka kusikia toka
kwako…hivi ni kweli? akauliza tena kwa msisitizo lakini hakupata jibu toka kinywani
mwa Sindi.
Lile hamaniko tu lilitosha kumfahamisha kuwa alichokuwa
amekisikia kilikuwa na ukweli ndani yake. Sindi alikuwa anaolewa na Mzee Dunia,
tajiri wa kijiji!
‘Ningeanzia wapi Nyanza….wapi?....ndoa yenyewe ya
kulazimishwa…ningeanzia wapi kukuvunja moyo?’ Sindi aliongea akilia, viganja
vyake vikibebana kifuani kana kwamba alikuwa akiuzuia moyo wake uliotaka
kuchomoka na kukimbia.
‘Pamoja na ahadi zote zile Sindi…’ Sauti ya Nyanza ilitoka kwa mtetemeko ulioashiria hasira
zilizochanganyikana na hamaki.
Hakuna aliyeongea tena, walitazama tu Nyanza akitafuta neno
la lawama la kufaa kuelezea alivyokuwa akijisikia muda ule na Sindi akitafuta
neno la kujitetea kuelezea alivyopambana na hali ile ya kushindwa kumwambia
ukweli tangu mwanzo. Nyanza akainamisha kichwa chini huku Sindi akihamanika
zaidi na kumtazama usoni akiisubiri kauli ya Nyanza
‘Nitakufa kwa ajili yako Sindi…’ akainua uso na kumudu kutoa
tamko lake lililomfanya
Sindi aachame mdomo na kutanua macho yake na hapo hapo machozi yakijazana
machoni pake na kutiririka. Nyanza alimtazama kwa jicho kali zaidi pengine
akidhani yale machozi yalikuwa ya kinafiki tu.
Akapiga hatua pembeni ya Sindi na kuanza kuondoka akimuacha
Sindi analia pasipo kugeuka. Safari hii alilia zaidi kiasi cha mwili wake
kuonekana kutetemeka. Aliumia, aliumia sana
na aliumia zaidi alipomfikiria Nyanza kuliko alivyojifikiria yeye mwenyewe.
Taarifa za ndoa yake na Mzee Dunia zilisambaa jioni ya siku
iliyopita, baada ya Mzee Dunia kukamilisha mahari jioni ile nyumbani kwa Mzee
Nalela. Tarehe ya ndoa ikatajwa siku jana hiyo na Sindi akaitwa na kuambiwa
mpoaka dakika ile alishakuwa mke halali wa Mzee Dunia, alipaswa kuisubiri siku
ya ndoa ya kimila tu kukamilisha uhalali huo.
Sindi Nalela hakuamini, hakuamini kama
siku aliyokuwa akiisikia itawadia ilikuwa imewadia ghafla vile. Mzee Dunia
aliposema Sindi angeishi kwenye nyumba ya peke yake aliyokuwa akiikarabati
kijijini hapo familia ya Nalela ilifurahi mno na taarifa za Sindi kuolewa na
Mzee Dunia na kujengewa nyumba zilisambaa kama moto wa
nyikani lakini sasa aliposema Nyumba ya Mzee Nalela pia itakarabatiwa shangwe
zilipiga hodi nyumbani kwa Nalela ikawa kama ndio Sindi
anaagwa kwao.
Asubuhi ya siku hii, aliamkia kufundisha angalau kujitoa
wahaka aliokuwa nao. haikusaidia! Alimuwaza Nyanza, aliiwaza hali atakayo kuwa
nayo, aliwaza mno.
Kauli ya Nyanza kuwa atakufa kwa ajili yake hakuielewa lakini
pia hakuipuuza kwa vile ilimuingia na ilimuumiza mno.
888888888888888888888
Jua la alasiri ilikuwa linaelekea ukingoni, kuzama kwake
kulileta manadhari ya kuvutia kwa yeyote aliyapata kukaa juu ya kilima hiki
akilitazama namna jua linavyozama. Sindi Nalela alikuwa ameketi juu ya kilima
hicho akiwa ameikunja miguu yake na kufanya magoti kugusana na kidevu. Mikono
yake iliikumbatia miguu yake hali kidevu chake kikiwa juu ya magoti.
Macho yake yalitazama mbele yakifumba na kufumbuka taratibu
huku muda mwingi yakiwa yamelikodolea
jua lililokuwa likizama wakati ule. Ndege walisikika kwa mbali wakipiga
kelele za kuvutia, utulivu ukionekana kuchukua nafasi sehemu kubwa ya eneo
lile. katika hali ya kawaida mandhari ya eneo lile ilikuwa ya kuvuta akili ya
mtu na kuituliza lakini kwa Sindi haikuwa hivyo.
Kuna mengi yalikuwa yakizunguka kichwani mwake. Aliongea na
kujijibu mwenyewe mawazoni, alibishana na akili yake na mara kadhaa alikunja
ndita chache usoni pake. Mawazo yalikuwa yamemchota mno kiasi kwamba hakumsikia
Jerry Agapela aliyekuwa amefika eneo lile kitambo na kusimama akimtazama Sindi.
Jerry akaamua kwenda pembeni ya Sindi na kuketi kule ndiko
kulikomtoa Sindi mawazoni. Akageuza uso wake taratibu na kumtazama Jerry,
tabasamu la huzuni likichanua usoni na kutoweka haraka, akarejesha kichwa kule
alikokuwa akitazama, pumzi zikimshuka taratibu.
‘Pole..’ Jerry akamsemesha lakini Sindi hakujibu kitu wala
hakugeuka
‘Samahani kama nitakuudhi Sindi….ila …’ akasita kidogo kwanza
‘… umekubali kuolewa?’ Jerry akauliza sauti ikipungua kama
vile ilimlazimu kuuliza vile. Sindi hakujibu kitu, aliendelea kutazama kule
mbele kana kwamba bado alikuwa mwenyewe.
‘Najaribu kukusaidia Sindi’ Jerry akaomba kueleweka
‘Kwa misingi ipi?’ Sindi akisogeza kichwa na kutazama kando
zaidi kiasi cha kukaribia kumpa kisogo Jerry’
‘Kama rafiki!...’ Jerry akajibu na
Sindi akajikuta akigeuza kichwa chake haraka na kumtazama Jerry usoni.
‘Rafiki?!’ swali lenye mshangao ndani yake lilimtoka,
akamkazia macho Jerry mara mbili.
Jerry akatikisa kichwa kulithibitisha lile swali lililo na
jibu ndani yake. Sindi akarudisha uso
mbele. Akatulia hivyo kama mtu aliyeamriwa kufanya
hivyo.
‘Nimeuvunja moyo wa Nyanza…. nimemuumiza…. natamani kungekuwa
na njia ya kuikimbia ndoa hii…natamani sana …’
Sindi aliongea polepole na machozi yakifanya kiherehere cha kuanza kuelea
kwenye mboni za macho ya Sindi.
‘Jerry…. sikuomba kuzaliwa maskini… kwanini Mungu aniletee
mitihani kama hii wakati umaskini nilionao ni mtihani
tosha kwangu….eeh Mungu wangu’ Sindi aliongea akilia sasa akiwa ameikumbatia
miguu yake vile vile huku akiyumba kwa kwenda mbele na kurudi nyuma.
Jerry akajisikia vibaya sana ,
akahamanika na kutafuta cha kumuondoa Sindi katika hali ile. Akajilaumu kwa
kuyaanzisha mazungumzo yale. Alikuwa ameambiwa kila kitu na Maria, rafiki wa
Sindi.
‘Nikikusaidia karo ya kaka yako…si nitakuwa nimekuokoa na hii
ndoa?’ Jerry akauliza kwa huruma, akitamani kumvutia Sindi ubavuni pake na
kumbembeleza.
Macho mekundu, yaliyojaa machozi yakamtazama Jerry, ni kama
vile Sindi hakuisikia ile kauli
‘nasikia unaolewa sababu inahigtajika karo ya kaka yako….what
if nikikusaidia hiyo karo?’ Jerry alitaka Sindi aamini kuwa alikuwa ana nia ya
kumsaidia. kwa kulirudia swali lake lile
kukamfanya Sindi acheke kicehko cha kivivu katikati ya huzuni ile
‘Sio muda wa utani huu Jerry….napitia wakati mgumu sana ….nikishaolewa
hapo sina maisha ya kuwaza wala kuendeleza zaidi ya kuzaa na kulea….na hayo sio
maisha niliyomuomba Mungu’ Sindi alilalamika na Jerry akamuwahi
‘Just tell me….nikikupa karo si nitakuwa nimekuokoa?’
Sindi akauvaa uso wa umakini kidogo akiona Jerry hakuwa
anatania.
‘Utaitoa wapi karo wakati wewe mwenyewe unasaidiwa na baba
Chidi’ Sindi akamuuliza akimtaja mwenyekiti kwa kijiji kwa jina la mwanaye.
‘Nitamuomba yule rafiki yangu aliyekuja hapa’ Jerry akajibu
akimaanisha Pamela Okello. Sindi akaguna kwanza
‘Rafiki yako au mpenzi wako?’ Sindi akauliza na ile huzuni
ikisambaa na kutoweka kadiri mazungumzo yao
yalipopamba moto.
‘Nampenda ila hanipendi so anabaki kuwa rafiki’ Jerry akawa
mkweli
‘Pole!’ Sindi akajibu
akitabasamu, hakuiamini kauli ya Jerry na wala hakutaka kybishana nanye
hata kidogo.
‘Asante !’
Jerry naye akajibu akitabasamu
‘….ulisema hivi ulisema ulipata ajali na wenzako mkiwa
mnaenda mjini kutafuta maisha?’ Sindi alibadili uelekeo wa mazungumzo, na
uelekeo ule ulikuwa wa ghafla kiasi kwamba Jerry alilazimika kukunja uso na
kuifanyisha akili yake kazi ya ziada ya kukusanya uongo wote aliomueleza Sindi
kuhusu maisha yake.
‘Yeah…’ akaitikia Jerry macho yakiwa kodo!
‘sasa msichana kama Pamela umejulia
wapi?....kwanini asikupe kazi?’ Sindi alizidi kuhoji, sasa akijigeuza mwili
mzima na kuketi bila kujikunyata akimtazama Jerry aliyejikuta akijikuna
nyuma ya shingo pasipo kuwashwa.
‘mimi naishi dar huku nilikuja tu kutafuta maisha na
wenzangu….ndio bahati mbaya nikapata ajali…. Pamela namjua siku nyingi tu
namjua…ila siwezi kumuomba msaada zaidi
ameshanisaidia vya kutosha’ Jerry alijieleza, akikwamba hapa na pale na nyakati
zingine akirudia rudia maneno.
‘kwanini hukuondoka naye alipokuja?’ Sindi akazidi kuhoji
‘Aaah…mmmh… sikuwa najisikia vema….ila karibu nitaondoka’
Jerry akajibu na Sindi akakunja uso kama mtu
anayefikiria kitu
‘wenzio mliopata nao ajali wako wapi?..... au uko kwenu
hawakutafuti?’ maswai ya Sindi yalianza kumchosha Jerry.
‘Wanajua kila kitu…. ndio maana sina wasiwasi…. sina wazazi
nina ndugu tu….unadhani nani anajali niko wapi na anafanya nini?’ naye
akamrudishia swali. Sindi akatikisa kichwa kulia na kushoto akionekana
kumuelewa angalau na akisahau habari kuhusu wale ambao Jerry aliopata nao
ajali.
Wakaongea mengine mengi, robo tatu Jerry akiongea uongo na
robo iliyobaki akisema ukweli. Alikuwa akificha utambulisho wake halisi.
Walipogeukia suala la karo ya Sega kaka yake Sindi, Sindi alikubali baada ya
ushawishi mwingi kuwa karo ingepatikana. Sindi akashukuru na kunyanyuka
akijiandaa kuonndoka eneo lile kwani giza
lilishaanza kuingia.
Alipohakikisha Sindi alikuwa ametoweka pale. Jerry alitoa
simu yake toka katika suruali aliyokuwa amevaa na kumpigia Pamela.
‘Msaada kidogo’ akatamka haraka simu ilipopokelewa
‘what is the matter honey?’ Pamela akauliza kwa sauti ya
kujali lakini lile neno Honey ndilo liliondoa tafsiri ya kujali kwa Jerry,
kwake ilikuwa kama dhihaka!
‘Nahitaji milioni mbili na nusu cash!....’ Jerry akasema kwa
sauti ya chini
‘Jay!.... two millions!?....kuna shamba unataka kununua?’
Pamela akahoji uso wake ukiwa na mikunjo ya kutosha na ilen wine iliyokuwa
kwenye glasi mkono wake wa kushoto, ikigeuka kuwa na uzito wa tani moja. Akaiweka
kwenye meza ya vinywaji iliyokuwa mbele yake na kuketi kwenye kiti hapo hapo
karibu na meza
‘nina shida nazo haraka…fanya juu chini nizipate ndani ya
siku mbili hizi please….it is urgent Pam’ Jerry akasisitiza na kumfanya Pamela
ashindwe kumuelewa zaidi
‘Umeanza lini kunificha mambo yako Jerry?....what is going on
there?’ kama mama anayemjali mwanawe, Pamela alihoji
kimashaka akitembeza macho yake huku na kule
‘Pamela please!’ Jerry akasisistiza
‘Okay!...will do so… take care’ akaaga sati yake ikionyesha
kutoridhika na kule kuamrishwa kutuma pesa bila kujua matumizi yake.
‘I’ll refund you once nikifa uko na kupata kadi….usijli hilo ’
Jerry akamhakikishia kurudishiwa hela zake
‘It is not about kurefund….ni what are you up to?.....two
millions!!...come on Jerry!’ Pamela alibebesha mguu mmoja juu ya mwingine huku
ule mkono wa kushoto ukiparaza kichwani kuanzia pajini na kuzichachafya nywele
zake kisogoni kwa kucha zake ndefu zilizonakshiwa kiustadi.
‘it is a long story’ Jerry akataka kukatisha maongezi
‘Okay… hope you are not in trouble’ Pamela akataka uhakika
kwanza
‘No!...’ Jerry akakata simu na kushusha pumzi ndefu, akicheka
pia peke yake kwani wasiwasi wa Pamela juu ya afya yake, usalama wake au
chochote kumhusu yeye ulimfanya ahisi Pamela alikuwa anampenda lakini Pamela
mwenyewe alilikana hilo kwa vitendo
vya kumuumiza!
888888888888888888888888
‘Usiniletee wazimu wako Nyanza…sikukwambia mimi?’ Mama Nyanza
alikuwa akiongea kwa jazba akiwa anafuatana na Nyanza toka ndani mpaka uani.
‘Nataka kumuoa mama…. nitamkosa Sindi bila pesa’ Nyanza
alichachatika akaongea uso ukiwa na huzuni ambayo ndani yake ilijaa hali ya
kukata tamaa
‘sasa ndio utake kuuza kibanda changu sababu ya
mwanamke?....Nyanza!’mama Nyanza aliongea kwa hasira akizungumzia nyumba ya
vyumba viwili aliyokuwa amemaliza kuijenga eneo la mbali kabisa na pale
walipokuwa wanaishi. alishachoka maisha ya kupanga na kuhangaika na kodi hivyo
aliamua kudunduliza pesa na kujenga
numba hiyo ya matofali ya kuchoma iliyoezekwa mabati yaliyotumika.
‘Nifanyeje sasa….nitoe wapi hata laki moja nikamgomboe
Sindi?..... unataka kuniambia mama nikae chini niangalie tu Sindi akichukuliwa
bila kufanya lolote?’ Nyanza alionekana kuchanganyikiwa
‘Sasa hilo lolote
ndio ukauze nguvu zangu ili uone…huyo mke utamuweka wapi?’ mama yake
hakumuelewa
‘Mama nitakujengea…. nitakufanyia mambo makubwa
mama….nisaidie angalau nizuie ndoa ya Sindi….nitampoteza’ Nyanza alimfuata mama
yake na kumbembeleza akishuka miguuni
‘Hebu ondoa huo upumbavu kichwani….baba yako nilimpenda kidogo
nilete maafa nyumbani kwetu…leo hii yuko wapi?.... yuko wapi?.....yuko wapi
huyo baba yako’ Mama Nyanza aliongea kwa hisia, akitumia sauti ya kukaripia
‘Amekufa’ Nyanza akajibu kinyonge akiwa pale miguuni pa mama
yake
‘Nimekufa naye?....amenisubiri tufe wote?.....amejali hata
kungoja niagane naye?....’ Alimporomoshea mwanaye maswali
‘Mama….Sindi yu hai…. nisaidie mama’ Nyanza alikuwa naomba
ruhusa ya mama yake ili akauze ile nyumba
na kupata mahari amabyo alihisi ingelipia deni la Mzee Dunia wakati akiwa
hajui hata hilo deni ni kiasi gani.
Kichwani mwake alitaka kuiuza nyumba ya mama yake kwa shilingi laki saba
akiamini laki 5 zingekuwa mahari na laki mbili zingekuwa za kufanyia harusi.
Wakazozana na mama yake sana ,
kiasi kwamba mama yake akaamua kuondoka pale uani na kuelekea kazini kwake.
Nyanza kama mtu aliyechanganyikiwa alitoka pale kwao na kuelekea kule bondeni
iliko nyumba ya mama yake.
Akili yake ilishaamua kuwa angeiuza ile nyumba potelea mbali,
kwake yeye alihitaji laki tano za kugomboa Sindi bila kujua mwenzake Mzee Dunia
alishagharamia kwa milioni na uchafu na Jerry Agapela alikuwa anakuja na kitita
zaidi ya wote wawili….
……..NYANZA ATAMGOMBOA SINDI WAKE…..??
Yap kazi nzuri
ReplyDeleteAsanteeee na karibu tena
ReplyDelete